Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2018

KCB kudhamini Ligi Kuu Bara

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Benki ya biashara ya Kenya (KCB) imeingia mkataba na Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) wa kuidhamini Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya shilingi Milioni 409 za Kitanzania. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini ya mkataba huo, Rais wa Shirikisho la soka nchini Wallace Karia amesema KCB imeingia mkataba wa kuidhamini Ligi Kuu Bara 2018/2019 ikiwa kama mdhamini mwenza huku jitihada zikiendelea kumpata mdhamini mkuu wa ligi hiyo. Mkataba huo ulisainiwa asubuhi katika hoteli ya Serena iliyopo mjini Dar es Salaam, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom bado haijathibitisha kama itadhamini tena ligi hiyo ama itaachana moja kwa moja na udhamini huo hasa baada ya mkataba wao kumalizika

Baada ya kipigo toka kwa Gormahia, kocha Yanga aishushia lawama TFF

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kocha msaidizi wa klabu ya soka ya Yanga SC, Mzambia Noel Mwandila amelishushia lawama Shirikisho la soka nchini TFF kwa kitendo cha kuwachukua wachezaji wao jana na kukaa nao kwa zaidi ya masaa 10 wakati wakifahamu walikuwa na mchezo mgumu dhidi ya Gor Mahia siku inayofuata. Kwa mujibu wa Mwandila, TFF iliwatoa kwenye kambi ya Yanga nyota sita wa timu ya taifa kwa ajili ya kwenda kupiga picha saa 8 mchana ambapo amesema walirejea kambini saa 7 usiku. Mwandila alikuwa akielezea umuhimu wa TFF kutoa ushirikiano kwa timu hasa zinapoliwakilisha taifa huku akisema kuwa tukio hilo linaweza kuwa limewaathiri kwavile wachezaji hawakupata muda wa kupumzika. Yanga imepoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 3-2.

KISPOTI

Picha
Mnashangaa ya Mwigulu na Yanga mnasahau ya Bakhresa kwa Simba Na Prince Hoza HIVI karibuni mbunge wa Iramba Mashariki kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dr Mwigulu Lameck Nchemba ambaye pia in kiongozi mkuu wa klabu ya soka yaSingida United inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bars aliamua kuwatunuku Yanga SC wachezaji watatu ambapo yeye mwenyewe alisema in msaada wake kwa klabu hiyo. Dr Mwigulu alianza kuwapa Yanga kiungo aliyesajiliwa na klabu take ya Singida United, Fesal Salum Abdallah "Fei Toto" katika maelezo yake Dr Mwigulu alisema aliamua kuhamisha leseni ya Fei Toto Singida United na kuipeleka kwa Yanga SC. Singida United ilimsajili Fei Toto kwa kandarasi ya miaka mitatu akitokea JKU ya Zanzibar lakini Sikh so nyingi Yanga nao wakatangaza kumsajili, Dr Mwigulu ameweka wazi kuwa gharama zote walizomlipa Fei Toto zitatumiwa na Yanga na wala hawatamdai. Pia Dr Mwigulu ambaye amewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi kabla ya Raid wa Jamhuri ya muungano wa ...

GORMAHIA YAINYUKA TENA YANGA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka nchini Kenya ya Gormahia usiku huu imeinyuka bila huruma Yanga SC ya Tanzania mabao 3-2 mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Gormahia ilitangulia kujipatia bao la kwanza lililofungwa kunako sekunde ya 23 kipindi cha kwanza na mshambuliaji George Odhiambo ambaye alifunga lingine katika dakika ya 40 na timu hizo zilienda kupumzika kwa matokeo hayo. Yanga walirejea na kasi mpya na kujipatia bao dakika ya 53 lililofungwa na Deus Kaseke likiwa pia ni goli la kwanza katika michuano hiyo ya pill kwa ukubwa Afrika, Jacques Tuyisenge aliifungia Gormahia goli la tatu na la ushindi dakika ya 64 kabla ya Raphael Saudi Lothi hajafunga bao la pill la Yanga dakika ya 80. Yanga leo watamlaumu kipa wao Youthe Rostand ambaye aliwaggharimu karibu magoli mawili na baadaye kocha wa Yanga akamtoa na kumwingiza Benno Kakolanya

UWANJA WA MAO TSE SUNG PEMBA ULIVYO SASA

Picha
Uwanja wa Mao Tse Sung ulioko Pemba kama unavyoonekana pichani jinsi ulivyo inaonekana umekamilika kwa kiwango chote, uwanja huo unafaa kwa kuchezewa nyakati zote kuanzia asubuhi, mchana, jioni au usiku. Uwanja wa Mao ni hazina nyingine kwa Tanzania katika kampeni yake ya kuandaa fainali za mataifa barani Afrika, uwanja huo ni tunu pekee visiwani Zanzibar ambapo sasa kuna viwanja viwili bomba kikiwemo cha Amaan Stadium

YANGA KULIPA KISASI KWA GORMAHIA LEO?

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga SC usiku wa leo wanatelemka uwanja wa Taiga kuumana na For Mahia ya Kenya mchezo wa kundi C kombe la Shirikisho barani Afrika. Huo ni mchezo wa nne kwa Yanga na wa pili kwa timu hizo kwani ziliumana hivi karibuni katika uwanja wa Moi Kasarani mjini Nairobi nchini Kenya na Yanga kubamizwa mabao 4-0 lakini iliemda kucheza ikiwa na mgomo wa wachezaji wake wakishinikiza kulipwa stahiki zao. Hata hivyo uongozi wa Yanga umeonekana kumalizana na wachezaji wake na mambo sasa yanekuwa shwari, kikosi kamili cha Yanga kiliingia kambini kujiandaa na mchezo huo na huenda Leo ikalipa kisasi. Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga umejinasibu kushinda I'll kufufua matumaini ya kusonga mbele Yanga pekee iko mkiani ikiwa na pointi moja wakati MC Alger ya Algeria ikiwa kileleni na pointi 7 Gor Mahia ya Kenya ina pointi 5 huku Rayon Sports ya Rwanda ikiwa na pointi 2 Kila la kheri Yanga SC

RAIS MAGUFULI AMTEUA JERRY MURO KUWA MKUU WA MKOA PIA YUMO MISS TANZANIA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli leo ameshangaza baada ya kumteua aliyekuwa msemaji wa Yanga SC Jerry Cornell Muro kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Rais Magufuli amefanya uteuzi mbalimbali wa wakuu wa mikoa na wilaya leo hasa baada ya waliokuwa wakishikilia nyadhifa hizo wengine kustaafu na wengine kupandishwa vyeo na kubadilishiwa nyadhifa. Mbali na Jerry Muro ambaye anakumbukwa vema kwa kazi yake ya usemaji pale Jangwani akishindana na hasimu wake Haji Manara, Rais Magufuli pia amemteua aliyewahi kuwa mmoja kati ya mamiss Tanzania na msanii wa filamu Jokate Mwegelo kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani. Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu leo imeonyesha mabadiliko mbalimbali ya wakuu wa wilaya na mikoa, mwanamichezo mwingine aliyekutwa na ngekewa hiyo ni Amos Makala ambaye awali alikuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na sasa amehamia Katavi

NIYONZIMA AWAZIMIA SIMU VIONGOZI WA SIMBA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kiungo wa kimataifa wa Kinyarwanda Haruna Niyonzima "Fabregas" ameamua kuikacha ziara ya Uturuki na kuzima simu yake ama kutopokea simu pindi anapopigiwa na viongozi wa klabu yake ya Simba. Niyonzima kwa sasa amerejea nyumbani kwao Rwanda na iliripotiwa angesafiri juzi na wenzake wanne ambao ni Meddie Kagere naye Mnyarwanda, Hassan Dilunga, Said Ndemla na Erasto Nyoni kuelekea kwenye kambi ya klabu hiyo iliyopo jijini Istambul, Uturuki lakini hakuweza kuungana nao. Mpaka sasa Niyonzima hajazungumza lolote juu ya kurejea kwake Simba kwani mwanzo alipozungumza na viongozi akawaambia pasipoti yake imeisha muda hivyo aliwaahidi angekuja mapema ili kushughurikia hilo na kuanza safari, lakini alipopigiwa tena simu hakupokea na pia kuna wakati akipigiwa anakata simu ama kuizima kabisa. Niyonzima alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea kwa mahasimu wao Yanga SC na tangu alipojiunga na kikosi hicho cha Msimbazi ameweza kufunga mabao mawili tu yot...

CHEGE ASHANGAA MUZIKI KUHAMIA ISTRAGRAM

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyepata kutamba na kundi la TMK Wanaume Family lililokuwa na maskani yake Temeke jijini Dar es Salaam, Said Chege Chigunda "Chege" ameshangazwa na muziki wa sasa kuhamia Istragram badala ya steji. Akizungumza jana na kituo cha Efm cha jijini Dar es Salaam amesema wasanii wanaotamba sasa wameshindwa kuusimamisha muziki huo na badala yake wamekuwa wakishindana katika mitandao badala ya stejini, Chege ameshangazwa mno kuona wasanii hao kujitamba wana viewers wengi mitandaoni. Akielezea upande wake kimuziki Chege amedai bado yuko vizuri na amewataka wale wasanii wanaojiona wana majina makubwa kwa sasa kushindana naye, amesema yuko tayari kuchuana nao na atawashinda, kulingana na maneno yake ya mafumbo ni kama amemlenga Diamond Platinum ambaye hivi karibuni alitangazwa kuongoza Istragram kwa viewers wengi kuliko msanii yeyote yule katika ukanda huu wa Afrika mashariki

CANNAVARO AWA MENEJA MPYA YANGA, HAFIDH AHAMISHIWA KWINGINE

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Nahodha wa siku nyingi wa mabingwa wa zamani nchini Yanga SC Nadir Haroub Ally "Cannavaro" ameteuliwa kuwa meneja WA timu na kustaafu rasmi mchezo wa soka. Cannavaro aliyedumu na Yanga karibu muongo mmoja na nusu ameachana na soka na kuwa meneja wa timu akichukua nafasi ya Hafidh Seleh aliyepandisha cheo na sasa anakuwa Cardnetor wa timu. Akitangaza uteuzi huo leo, kaimu katibu mkuu wa Yanga Omari Kaaya amesema Cannavaro amecheza Yanga kwa kipindi kirefu hivyo atawafaa katika nafasi hiyo, ameongeza kuteuliwa kwa beki huyo wa kati kutaleta mawasiliano mazuri baina yake na benchi la ufundi kwavile anafahamu changamoto zote. Yanga pia imetangaza kikosi chake kitakachoshiriki michuano ijayo ikiwemo Ligi Kuu Bars na safari hii imesajili wachezaji saba tu wapya na vilevile imeachana na nyota wake wawili ambao ni Geoffrey Mwashiuya na Hassan Messy

HIVI NDIVYO YONDANI ALIVYOMWAGA WINO YANGA

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Yanga Sc jana imefunga usajili kwa kumsainisha kandarasi ya mwaka mmoja beki wake kisiki Kelvin Patrick Yondani na kusalia katika kikosi hicho. Awali Yondani alikuwa akiwindwa na mahasimu wao Simba Sc lakini Abas Tarimba akaingilia kati na kumtuliza hatimaye jana wakati dirisha linafungwa beki huyo akamalizana na mabingwa hao wa zamani, hata hivyo Yanga imempoteza beki wake wa kulia Hassan Ramadhan Kessy aliyetimkia Nkana Red "Devils" ya Zambia. Yanga pia iliweza kukamilisha usajili wa nyota wawili wapya WA Kikongoman kipa Klauz Kinzi Kindoki na mshambuliaji Heritier Makambo, Yanga imesajili wachezaji sita tu ambao no Makambo na Kindoki wwngine ni Mohamed Issa Banka, Fesal Salum "Fei Toto", Deus Kaseke, Mrisho Ngasa

MWASHIUYA AIBUKIA SINGIDA UNITED, PIA MGHANA NDANI

Picha
Na Mwqandishi Wetu. Singida Klabu ya Singida United ya mkoani Singida Jana nayo imefunga zoezi la usajili kwa kunasa saini za nyota wawili mmoja wa kimataifa raia wa Ghana ambao kila mmoja amepewa mkataba wa miaka miwili. Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Geofrey Mwashiuya amesajiliwa na klabu hiyo sambamba na Mghana Hans Koffie na sasa timu hiyo inayonolewa na Mzanzibar Hemed Morocco imekamilisha usajili wake, pia Singida United itakuwa na sura mpya baada ya nyota wake wengi kutoweka. Mwashiuya alitokea Yanga ambayo yenyewe ilimsajili kutoka Kimondo FC ya mkoani Mbeya

Dakika za mwisho mwisho Simba yambakiza Ndemla, Apaa

Picha
Na Aisha Maliyaga. Dar es Salaam Dirisha la usajili limefungwa Jana usiku ambapo klabu zote 20 zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania zimetakiwa kukamilisha kila moja wapo, Simba imelifunga dirisha hilo kwa staili ya kipekee. Unaambiwa jana imemalizana na kiungo wake Said Ndemla na ikampandisha ndege kuelekea Uturuki kuungana na wenzao waliotangulia juma lililopita, Simba iliondoka na kikosi cha wachezaji 26 tu ikimwacha Ndemla asubirie kwanza kumalizana na uongozi, Ndemla pia alikuwa akiwaniwa na klabu ya AFC Eskilistuna ya Sweden. Pia Simba imemchukua kiungo wa Mtibwa Sugar Hassan Dilunga na sasa wote hao pamoja na Erasto Nyoni, Meddie Kagere na Haruna Niyonzima wamesafiri kuelekea Uturuki kuungana na wenzao, Simba pia imewaacha Jamal Mwambeleko, Ally Shomari, Said Mohamed Nduda, Moses Kitandu, Juuko Murushid na Laudit Mavugo

Yanga yapata bonge la kipa anadaka kama nyani

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Yanga SC leo imetambulisha nyota wawili wote wanatoka Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Congo (DRC) kipa anayedaka kama nyani Klauz Kinzi Kindoki na straika mwenye mashuti Heritier Makambo wwamesainishwa mkataba wa miaka miwili kila mmoja. Dirisha la usajili linafungwa usiku wa saa sita usiku Yanga imeamua kuwasainisha nyota hao wawili ikiwa kama sehemu ya kukiimarisha kikosi chake ambacho msimu uliopita kiliteteleka baada ya kushindwa kutetea taji lake lililokwenda kwa mahasimu wao Simba SC. Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji saba ambao ni Makambo na Kindoki waliotambulishwa leo, wengine ni Mohamed Issa Banka toka Mtibwa Sugar, Mrisho Ngasa wa Ndanda FC, Fesal Salum "Fei Toto", wa JKU na Deus Kaseke toka Singida United pia imemsajili Elisha Muroiwa toka Singida United ambaye aliletwa kama msaada toka kwa Mwigulu Nchemba

Danny Lyanga amwaga wino Azam FC kumrithi Chilunda

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam FC imeingia kandarasi ya mwaka mmoja na mshambuliaji Danny Lyanga wa Singida United akienda kuziba nafasi ya Shaaban Iddi Chilunda aliyeuzwa Hispania. Taarifa zilizotolewa na uongozi wa Azam FC zinasema kuwa mshambuliaji huyo aliyewahi pia kuzichezea Coastal Union ya Tanga, Simba SC na Fanja FC anajiunga na Azam FC baada ya kucheza kwa kipindi kifupi sana Singida United. Lyanga in mmoja kati ya washambuliaji bora kabisa hapa nchini ambao wana uwezo mkubwa wa kufunga na kuasist, kutua kwake Azam FC kunaweza kurudisha matumaini ya timu kufanya vema kwani tayari imeshaondokewa na nyota wake wawili ambao no tegemeo

Maguli mambo safi AS Kigali

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Elius Maguli amejiunga na klabu ya AS Kigali ya Rwanda kwa ajili ya msinu ujao wa Ligi Kuu nchini humo. Mshambuliaji huyo alikuwa akihusishwa kujiunga na mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC lakini amezima tetesi hizo na sasa anakuwa mchezaji wa timu hiyo. Maguli aliwahi pia kuzichezea Dhofal FC ya Oman, Simba SC, Ruvu Shooting na Tanzania Prisons zote za Tanzania amekuwa katika kiwango bora mpaka kufikia kuitwa kwenye timu ya taifa, Taifa Stars lakini alipotea na sasa anarejea tena kwa kujiunga na klabu hiyo

Singida United nooma, yamnyakua rasta wa Mwadui

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Klabu ya Singida United ya mkoani Singida inazidi kujiimarisha katika zoezi LA usajili baada ya jana kufanikiwa kupata saini ya kiungo mahiri wa aliyekuwa timu ya Mwadui FC ya mjini Shinyanga, Awesu Awesu. Mkurugenzj wa klabu hiyo Festo Sanga alimtambulisha mchezaji huyo mbele ya waandishi wa habari na kusema timu yake imedhamilia kufanya vema msimu ujao kwa kusajili wachezaji nyota. Juzi Sanga aliwatambulisha wachezaji wengine watatu iliowasajili, wachezaji ambao walitambulishwa kusajiliwa na klabu hiyo ni Jamal Mwambeleko kutoka Simba SC, Athamas Mdamu kutoka Alliance School na Rajabu Zahir wa Ruvu Shooting

Kagere, Niyonzima na Nyoni kuwafuata wenzao Uturuki kesho

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Wachezaji watatu wa kutumainiwa wa mabingwa wa soka nchini, Simba SC kesho watasafiri kuelekea Istanbul Uturuki kuwafuata wenzao waliosafiri mwishoni mwa juma lililopita. Simba iliondoka na wachezaji 26 ikowaacha Erasto Nyoni, Haruna Niyonzima na Meddie Kagere ambao sasa watasafiri kesho, Mkuu wa kitengo cha habari wa mabingwa hao, Haji Manara amethibitisha safari hiyo na amedai mambo yote kuhusu safari yamekamilika. Manara pia amedai kikosi kilichopo Uturuki kipo sehemu nzuri na mpaka sasa hawajacheza mchezo wowote wa kirafiki tofauti na watu wanaosambaza vibaya kuwa Simba imecheza mechi ya kirafiki na kufungwa mabao 6-0, Simba imeweka kambi katika hoteli ya Reen Park & Resort iliyopo jijini Istambul  ikiwa na viwanja vitano vya kuchezea soka

Makambo aula Yanga CAF, Ngasa atemwa

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Uongozi wa mabingwa wa zamani wa Tanzania Bars Yanga SC imeweka wazi kumuorodhesha straika Heritier Makambo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo (DRC) katika kikosi chake kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Shirikisho la Moira wa miguu barani Afrika, CAF jana lilipitisha usajili wa wachezaji wawili wa Yanga ambao awali ulishindikana, wachezaji ambao usajili ulipitishwa na kiungo mshambuliaji Deus Kaseke na mshambuliajj Matheo Antony, lakini uongozi wa klabu hiyo kwa kushirikiana na benchi la ufundi imeamua kumuongezea straika Mkongoman Heritier Makambo ambaye alisajiliwa hivi karibuni akitokea FC Lupopo. Kupitishwa kwa Makambo kunamuondoa Mrisho Ngasa katika idadi hiyo hivyo sasa Makambo atakuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga watakaotumika katika michuano hiyo ya Afrika huku Ngasa akisubiria msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoanza Agosti 22 mwaka huu

SINGIDA UNITED YAIMARISHA SAFU YAKE YA ULINZI KWA KUWANASA MWAMBELEKO NA RAJAB ZAHIR

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Klabu ya soka ya Singida United ya mkoani Singida ambayo kwa sasa ipo jijini Mwanza kwa ziara maalum ya kujiandaa na msimu, leo imetangaza kuwasajili Jamal Mwambeleko "Nando" aliyekuwa anaitumikia Simba SC na Rajabu Zahir aliyekuwa Ruvu Shooting ya Pwani wote ikiwapa mkataba wa mwaka mmoja. Mwambeleko ameachwa na Simba katika safari ya Uturuki amesajikiwa kwa mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo na sasa atakuwa miongoni mwa kikosi cha Singida United msimu ujao, Mwambeleko alijiunga na Simba akitokea Mbao FC kwa mkataba wa miaka miwili lakini wameweza kuelewana na Simba na sasa mchezaji huyo ni mali ya Singida United, Mwambeleko ni beki wa upande wa kushoto na amekuwa akipanda na kushuka. Pia kikosi hicho kimemalizana na beki wa kati wa Ruvu Shooting, Rajabu Zahir ambaye aliwahi kuzichezea Mtibwa Sugar ya Morogoro na Yanga SC ya jijini Dar es Salaam

MBAO FC YAMTAMBULISHA PASTORY ATHANAS

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Klabu ya soka ya Mbao FC ya jijini Mwanza nayo imeendelea kujiimarisha kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kumtambulisha rasmi mshambuliaji wa zamani wa Stand United, Simba SC na Singida United, Pastory Athanas kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja. Athanas aliyewahi kucheza Simba SC nusu msimu kisha kutupiwa virago amejiunga na timu hiyo ya jijini Mwanza inayonolewa na beki wa zamani wa Simba, Amri Said "Steam" na sasa kikosi hicho kinajivunia kumpata straika Hugo machachari. Tayari timu hiyo imeshafanikiwa kunasa baadhi ya mastaa mbalimbali ambao watakuja kuipa mafanikio, ujio wa Athanas ni kuondoka kwa kiungo mshambuliaji wake Habib Kiyombo aliyejiunga na Singida United

KMC YAMNASA HASSAN KABUNDA

Picha
Na Mqwandishi Wetu. Dar es Salaam Uongozi wa timu ya soka ya Manispaa ya Kinondoni ya KMC Leo imemtambulisha kiungo mshambuliaji Hassan Salum Kabunda na kumpa mkataba wa mwaka mmoja. Kabunda aliyekuwa akiichezea Mwadui FC ya mjini Shinyanga anakuwa miongoni mwa wachezaji wapya wa timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu, Kabunda amejiunga na KMC akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba. Kabunda aliyevaa kanzu akiwa na viongozi wa timu hiyo ni mtoto wa beki wa zamani wa Yanga SC, Salum Kabunda "Ninja" ama Msudani ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uchezaji wake wa kibabe na rafu nyingi

Mwigulu aipa Yanga beki Mzimbabwe

Picha
Na Aisha Maliyaga. Dar es Salaam Beki wa kimataifa kutoka Zimbabwe Erisha Muroiwa anayekipiga timu ya Singida United sasa ataitumikia Yanga SC kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa kama msaada uliotolewa na Dr Mwigulu Nchemba kwa klabu hiyo. Huo ni msaada wa pili anautoa Mwigulu kwa klabu ya Yanga ambayo kwa sasa ipo katika mdororo wa kiuchumi, jana Mwigulu aliwapa Yanga kiungo waliyemsajili kutoka JKU, Feisal Salum "Fei Toto". Hata hivyo Mwigulu aliwasilisha barua kwa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF ikiwataka kuthibitisha usajili wa Muroiwa kwa klabu ya Yanga, Mwigulu ambaye ni mbunge wa Iramba Magharibi amedai mchezaji huyo ataenda Yanga lakini fedha za usajili ililipa Singida United hivyo huo ni msaada wake na amedai timu yoyote itakayotaka msaada hatosita kuwapa

Singida United wajifua vikali Mwanza, yasalenda kwa Fei Toto

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Wakati klabu bingwa ya soka nchini Simba SC ikiweka kambi nchini Uturuki, timu ya Singida United ya mkoani Singida yenyewe imeamua kwenda kujichimbia jijini Mwanza kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bars inayotarajia kuanza Agosti 22 mwaka huu. Kikosi hicho kinachonolewa na Hemed Morocco kinafanya mazoezi kabambe asubuhi, mchana na jioni kuhakikisha wachezaji wanakuwa fiti I'll angalau kufanya vema kwenye ligi hiyo, msimu uliopita Singida United ilikomea nafasi ya tano lakini msimu huu hawataki masihara hats kidogo. Lakini kikosi hicho kikiwa na nyota wake wote iliowasajili katika kipindi hiki cha usajili, imeachana na kiungo wake mpya Fesal Salum "Fei Toto" na kuridhia akaitumikie Yanga SC, Fei Toto alisajili katika vilabu hivyo viwili hivyo ikaona vema nyota huyo acheze na akaitumikie Yanga msimu ujao, ridhaa hiyo imetolewa na mwenyekiti  wa Singida United Dr Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mbunge wa Iramba

Biashara United hawatanii aisee, yatambulisha majembe

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Klabu ya Biashara United ya Mara jana imewatangaza wachezaji wanne ambao imewasajili kutoka vilabu tofauti ili kuendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara . Wachezaji hao ni Lambele Jerome kutoka Lipuli, Yohana Moris aliyekuwa Mbeya City, Frank Sekule kutoka Dodoma FC na Daniel Manyenye kutoka Toto Africans. Biashara United imepanda Ligi Kuu bara kwa mara ya kwanza na itashiriki msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 22 tayari imeshakamilisha ujio wa kocha mpya wa kigeni na kusajili baadhi ya wachezaji pia wa kigeni ikijiandaa kutoa ushindani kwenye ligi hiyo

KMC yawaongezea mikataba nyota wake walioipandisha Ligi Kuu

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Klabu ya KMC ya Jijini Dar es salaam imewaongezea mikataba wachezaji wake Watatu ya Kuendelea Kuitumikia klabu hiyo. Beki wa pembeni Ally Ramadhani mshambuliaji Rehan Kibingu pamoja na Kiungo Mshambuliaji Cliff Buyoya . Wote hawa Wamekula kandarasi ya mwaka mmoja ya Kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Nyota mwingine Azam FC apata ulaji Afrika Kusini

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Neema imeemdelea kuwaangukia wachezaji wa timu ya soka ya Adam FC ya mjini Dar es Salaam baada ya leo kiungo mshambuliaji wake Yahya Zayed kukwea pipa na kuelekea nchini Afrika Kusini kufanya majaribio katika klabu ya Bidvest Wits inayoshiriki Ligi Kuu maarufu ABSA. Zayed aliyeisaidia Azam FC kutwaa ubingwa wa kombe la Kagame kwa kuilaza Simba SC mabao 2-1 katika fainali iliyofanyika uwanja WA Taiga mjini Dar es Salaam amesafiri kwa baraka zote na kama atafaulu majaribio ina maana Azam FC itakunja noti kwani tayari ilishamuongezea mkataba WA miaka miwili. Kuondoka kwa Zayed kunaifanya Azam FC iwe imetoa karibu wachezaji wanne kucheza soka la kulipwa, tayari Farid Musa ametangulia Hispania na kujiunga na CD Tennerife inayoshiriki Sagunda Divion, lakini Humid Mao yeye amejiunga na Petrojet ya Misri na Shaaban Iddi Chilunda akiula kwa kumfuata Farid Musa katika klabu ya Tennerife  ya Hispania, kila LA kheri Yahya Zayed

Simba wazidi kunoga huko Uturuki

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Baada ya kufanikiwa kufika salama jana huko nchini Uturuki katika mji mkuu wa Istambul na kuelekea mji wa Antaly uliopo kilometa 15 kutoka mji mkuu, wameanza mazoezi yao leo na wako tayari kwa mapambano. Wekundu hao wanafanya mazoezi makali chini ya kocha mkuu Mbelgiji Patrick Winand Aussems na msaidizi wake Irambona Masoud Djuma huku wachezaji wake wakionekana kufurahia ziara hiyo ya Uturuki. Simba itaendelea kukaa huko kwa majuma mawili na itarejea nyumbani ifikapo Agosti 5 mwaka huu ambapo pia itashuka dimbani katika hafla ya Simba Day itakayofanyika Agosti 8 ambayo huadhimishwa kila mwaka

Hatimaye Clement Sanga ajiuzuru

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Makamu mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam Clement Sanga ametangaza kujiuzuru nafasi yake leo huku akitaja sababu kubwa iliyochangia ni kuhofia maisha yake. Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Protea Courtyard mjini Dar es Salaam, Sanga amesema ameamua kujiuzuru nafasi yake kufuatia baadhi ya wanachama na wapenzi wa Yanga kutishia maisha yake pamoja na familia yake. Sanga amedai amepata clip zinazoonesha maandalizi ya watu hao ambao ni wapenzi wa Yanga wamejipanga kuvamia nyumbani kwake na kuwazuru kwa kutumia mapanga,visu nk, hivyo ameona bora ajiweke kando na kuwapisha wengine, Yanga imekuwa na mwenendo mbaya tangia iwe chini yake kaimu mwenyekiti hasa baada ya kujiuzuru mwenyekiti Yusuph Manji. Timu imetokea kuwaudhi mashabiki wake baada ya kufungwa mfululizo na kuvuliwa ubingwa wake wa bara pia ikichapwa mabao 4-0 na Gormahia katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika

KISPOTI

Picha
Simba ilipaswa kumuamini Masoud Djuma KLABU ya Simba SC imemtambulisha rasmi beki wa zamani wa kimataifa wa Ubelgiji Patrick Winand J Aussems kuwa kocha mkuu wake mpya akichukua nafasi ya Mfaransa Pierre Lechantre aliyeondoka Mei mwaka huu. Aussems aliyezaliwa Februali 6 mwaka 1965 mjini Moelingen, Ubelgiji ametambulishwa mchana katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam na Rais wa klabu hiyo Salim Abdallah "Try Again" akitokea timu ya taifa ya Nepal. Try Again amesema kwamba wana imani na Aussems kwamba atailetea mafanikio klabu yao kutokana na rekodi yake nzuri, kocha huyo ana uzoefu wa kufundisha timu kadhaa barani Asia na Ulaya lakini amewahi kufundisha KSA ya Cameroon na AC Leopards ya Dolisie nchini Kongo, hizo zikiwa pekee za Afrika. Aussems alikuwa jukwaani uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam wakati wa mchezo wa mwisho wa kundi C Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Kagame kati ya Simba SC na Singida United ulioisha kwa sare ya kufungana bao 1-...

SABABU ZA KUACHWA NDEMLA SAFARI YA UTURUKI HIZI HAPA, NDUDA NA WENGINE PIA ZIMO

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara Simba SC imesafiri alfajiri ya leo hii kuelekea nchini Uturuki ambapo itakaa huko kwa majuma mawili kabla ya kurejea kwa ajili ya tamasha lao la Simba Day litakalofanyika Agosti 8. Simba imeondoka na wachezaji wake wote iliowasajili hivi karibuni pamoja na kocha wake mkuu Mbelgiji Patrick Aussems, kikosi kilichoenda kina jumla ya nyota 26 lakini wengine imeripotiwa kuachwa katika safari hiyo. Mmoja kati ya walioachwa ni kiungo mshambuliaji Said Ndemla ambaye inasemekana amegoma kuongeza mkataba mpya na ndio maana ametoswa katika safari hiyo, pia beki Erasto Nyoni ametemwa katika safari kwakuwa ana matatizo ya kifamilia. Nyoni ataungana na kikosi hicho keshokutwa, Said Mohamed Nduda,Emmanuel Mseja, Ally Shomari, Jamal Mwambeleko wameachwa kwa vile wanapelekwa kwa mkopo kwenye klabu nyingine wakati Moses Kitandu anatarajia kujiunga na Lipuli ya Iringa

MSUVA AREJEA DAR NA KUSAINI MKATABA KMC

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji wa Mbao FC ya jijini Mwanza, James Happygod Msuva amejiunga na timu iliyopanda daraja ya KMC yenye maskani take Kinondoni jijini Dar es Salaam. Msuva (James) ambaye ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anayeichezea timu ya Difaa El Jadida ya Morocco ameripotiwa kusaini mkataba WA mwaka mmoja. Msuva anaungana na beki wa kati Yusuph Ndikumana raia wa Burundi ambao wrote hao wamemfuata aliyekuwa kocha wao wa Mbao FC Etienne Ndayiragije aliyejiunga na timu hiyo akichukua mikoba ya mzalendo Fred Felix Minziro ambaye mkataba wake ulimalizika

GARDIEL MICHAEL AAGANA NA UKAPELA

Picha
Na Mwandishi Wetu. Tanga Beki wa kushoto wa wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga SC, Gardiel Michael Mbaga amefunga ndoa na aliyekuwa mchumba wake Lovenes Haroun katika kanisa la Luthelen la usharika wa Kana jijini Tanga. Gardiel sasa anaachana na klabu ya ukapela na kuwa mwanandoa, pia anaondoa fununu kuwa in miongoni mwa wachezaji walioweka mgomo katika klabu ya Yanga kama inavgosemekana kuwa wachezaji karibu wote wamegoma.

NDANDA FC YANASA WAWILI KWA MPIGO

Picha
Na Mwandishi Wetu. Mtwara Baada ya kuondokewa karibu na nyota wake wote wa kikosi cha kwanza uongozi wa klabu ya Ndanda FC ya mjini Mtwara imefanya usajili wa kushitua baada ya kufanikiwa kuwanasa waliowahi kuwa wachezaji wao wa zamani Atupele Green na Kiggy Makassi. Uongozi WA Ndanda umethibitisha Jana kuwa imempa kandarasi ya mwaka mmoja mshambuliaji Atupele Green wa Kagera Sugar na sasa atakuwa miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo msimu ujao, pia imemnasa Kiggy Makassi aliyekuwa Singida United naye akisaini kwa mkataba wa mwaka mmoja. Kurejea kwa nyota hao kunafufua matumaini ya timu hiyo ambayo iliondokewa na washambuliaji wake tegemeo kama Omari Mponda aliyejiunga na Kagera Sugar Tibar John aliyeenda Singida United, Nassoro Kapama aliyejiunga na JKT Tanzania na Mrisho Ngasa Yanga SC

SIMBA ZIARANI UTURUKI LEO

Picha
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam JUMLA ya wachezaji 26 wa kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba SC wameondoka alfajiri ya leo kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kambi ya majuma mawili kujiandaa na msimu mpya WA Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bars. Simba ilianza safari yakr jana ambapo baadhi ya viongozi na watendaji walianza kusafiri pamoja na vifaa itakavyotumia ikiwa huko, Simba imepanga kufikia katika mji wa Antalya ambao upo kilometa 15 kutoka mji mkuu wa Istanbul. Wekundu hao watacheza mechi tatu za kirafiki na kwa mujibu wa viongozi wake wamesema kikosi chao kitarejea Agosti 5 mwaka huu na kitacheza mchezo WA kirafiki WA Simba Day kabla hakijaenda mjini Lindi kucheza mechi ya kirafiki na Namungo FC katika uzinduzi WA uwanja wa Majaliwa Stadium

SIMBA YAMALIZANA NA KIUNGO MZAMBIA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bars, Simba SC leo imeingia kandarasi ya miaka miwili na kiungo wa kimataifa WA Zambia, Clatous Chota maarufu Chama na sasa atajumuika na wachezaji wenzake watakaosafiri kesho kuelekea nchini Uturuki. Kiungo huyo alitua jana usiku akitokea kwao Zambia, Chota amesaini leo akitokea timu ya Lusaka Dynamos ya Zambia ambayo inashiriki Ligi Kuu, kocha msaidizi wa Simba, Irambona Masoud Djuma amesifu usajili huo akidai sasa Simba imemaliza ukame wa kiungo mchezeshaji. Djuma amedai Simba ilikuwa ikisumbuliwa na kiungo mchezeshaji kwa muda mrefu na ililazimika kuwatumia Shomari Kapombe au Jonas Mkude, ujio wa Chota utaifanya Simba kutimia idara zote bila shaka itatetea tena taji lake, Chota ni chaguo la Djuma ambapo yeye ndiye aliyeutonya uongoxi wa Simba kumnasa

SIMBA YAKUBALI KUZINDUA UWANJA WA MAJALIWA STADIUM

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mabingwa WA soka Tanzania Bars, Simba SC maarufu kama Wekundu wa Msimbazi, wamekubali ombi la timu ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi kucheza nayo mechi ya kirafiki ikiwa na lengo la kusherehekea uzinduzi wa uwanja wa kisasa wa Majaliwa Stadium Agosti 11 mwaka huu. Wekundu hao wa Msimbazi wamekubali maombi ya timu hiyo na sasa watashiriki kikamilifu katika uzinduzi wa uwanja huo wa mpira, Ruangwa ndiko anakotokea Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa ambaye pia ni mpenzi mkubwa wa Wekundu hao hivyo itakuwa ni burudani tosha kwa wakazi wa Ruangwa kuitazama klabu bingwa ya soka nchini. Mheshimiwa Majaliwa ndiye aliyehakikisha uwanja unajengwa na kukamilika ambapo sasa vilabu vya jimbo lake la Ruangwa na maeneo jirani vinaweza kuutumia uwanja huo kujiendeleza, Simba imeahidi kupeleka wachezaji wake wote nyota pamoja na kocha wake mpya Mbelgiji Patrick Winand Aussems, Wekundu hao kesho Jumapili wanaelekea Uturuki kujiandaa n...

Chilunda akwama kupaa Hispania

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC Shaaban Iddi Chilunda ambaye ameuzwa kwa mkopo kwa klabu ya CD Tenerife ya Ligi daraja la pili nchini Hispania, ameshindwa kuelekea huko akisubiria mambo yakae sawa kuhusu vibali vya kufanyia kazi, hayo aliyasema leo alipoulizwa juu ya safari yake baada ya kuachana na Azam FC ambao ni mabingwa wa Afrika mashariki na kati. " Kwa sasa klabu yangu mpya inashughulikia kibali cha mimi kuweza kufanya kazi Hispania na taratibu zote zikikamilika ndipo nitakuwa na uwezo wa kuondoka hapa na kwenda kuanza kazi sababu wenzetu wanazingatia sheria sana." “Sababu huwezi kwenda kule kama huna kibali cha kazi kila kitu kikikamilika ndipo nitaweza kupewa visa na kuondoka hapa nchini kwa ajili ya kuanza kazi yangu rasmi ndani ya Tenerife,” Maneno ya Shaaban Idd  Chilunda Alipoulizwa kuhusiana na safari yake ya Kwenda nchini Hispania kwa ajili ya kuanza kuitumikia klabu yake mpya ya Tenerife ambayo ameingia nayo mkatab...

AZAM FC KUELEKEA UGANDA LEO

Picha
Na Ramadhan Pilen. Klabu ya Azam FC yenye maskani yake Chamazi Jijini Dar es Salaam inatarajia kuondoka leo kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya kwenda kuweka Kambi ya wiki mbili ili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara . Kikosi hiko ambacho kitasafiri leo kitaondoka pasipo mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa toka klabu ya Yanga SC Mzimbabwe , Donald Ngoma kutokana na mchezaji huyo kuuguza majeraha . Ikiwa nchini Uganda klabu ya Azam FC itacheza mechi za kirafiki na vilabu vya Vipers SC  , KCCA, na Express FC .

COASTAL UNION KUMSAJILI ALLY KIBA

Picha
Na Mwandishi Wetu. Tanga Uongozi wa klabu ya soka ya Coastal Union ya jijini Tanga uko mbioni kumsajili mwanamuziki maarufu wa bongofleva hapa nchini Ally Saleh Kiba "Ally Kiba" na imepanga pia kumfanyia mapokezi makubwa staa Hugo. Taarifa kutoka makao makuu ya Wagosi hao wa kaya waliorejea Ligi Kuu msimu huu wamedai wameshakubaliana na nyota huyo na kinachosubiriwa kwa sasa ni mkataba tu, Ally Kiba mbali na kujihusisha na muziki pia amekuwa mmoja kati ya wachezaji mpira wenye kiwango cha kuchezea timu za Ligi Kuu. Mbali na Coastal Union ambao wamekubaliana naye, nyota huyo pia aliwahi kutakiwa na Toto Africans ya Mwanza ila walishindwana naye kutokana na mwanamuziki huyo kubanwa na shughuri sake za kimuziki lakini kwa Coastal Union mambo yatakuwa shwari, Coastal Union imejipanga kufanya vizuri kwenye ligi ijayo hivyo imeanza kujiimarisha kwa kusajili wachezaji bora Kwa habari kamili gonga www.mambouwanjani.blogspot.com

Rasmi, Tarimba awatuliza Yondani, Kessy, Yanga

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati maalumu ya mpito ya klabu ya Yanga , Abbas Tarimba amefanikiwa katika Juhudi zake za kumzuia beki Kelvin Yondani asisajiliwe na klabu ya Simba  mara baada ya kufikia makubaliano kwa beki huyo kuendelea kuitumikia klabu hiyo . Jana tena Tarimba alifanya mazungumzo na Kelvin Yondani na mchezaji huyo kukubali Kuongeza kandarasi mpya klabuni hapo . Inasemekana klabu ya Simba SC ilikuwa inamuwinda kwa hudi na Uvumba beki huyo lakini Jitihada zao zilishindwa kutokana na makubaliano kutofikiwa baina ya Simba SC na Kelvin Yondani . Tarimba ambaye amesisitiza anataka kujiondoa katika kamati maalumu ya mpito ya klabu ya Yanga pia amefikia makubaliano na Hassan Kessy ili aweze kubaki klabuni hapo .

Baba yake Mbappe asema alimpeleka mwanaye Cameroon lakini wakamkataa

Picha
"Mara ya kwanza nilipotaka mwanangu acheze timu ya taifa ya Cameroon, shirikisho la soka nchini humo lilitaka nilipe kiasi flani ( Rushwa) Ambacho nilikuwa sina. "  " Baadae nilienda katika Uongozi wa shirikisho la soka Ufaransa na hawakunitoza kiasi chochote." Maneno ya baba mzazi wa mshambuliaji Kylian Mbappe ,  mzee Wilfreid Mbappe Alipoulizwa kuhusiana na mwanawe kwanini hakuichezea timu ya taifa ya Cameroon na kwenda kuichezea Ufaransa .

Kipre Tchetche kurejea Azam FC

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Brice Herman Tchetche muda wowote kuanzia sasa anakuwa mchezaji mpya wa Azam Fc baada ya makubaliano kati ya Azam Fc na klabu anayoitumikia kwa sasa ya Terengganu Fc ya Malaysia. Taarifa za kurejea Tchetche katika kikosi cha Azam Fc ni baada ya mmoja kati ya wakurugenzi wa timu hiyo, Yusuf Bakhresa kuelekea Malaysia na kukutana na viongozi wa Terrengganu Fc ambapo wameonesha kukubali kumwachia. Mchezaji huyo amebakiza mkataba wa miezi mitatu hivyo haitaizuia Azam Fc kumrejesha nyumbani mshambuliaji huyo aliyejiunga na Azam Fc akitokea timu ya taifa ya vijana ya Ivory Coast iliyokuja nchini kushiriki michuano ya Chalenji

Ntamba Band waja na Shobo

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kundi linalobamba kwa sasa hapa jijini Dar es Salaam kwa muziki wa kizazi kipya, Ntamba Band lenye maskani yake Buza nje kidogo ya mji wameachia wimbo mpya uitwao Shobo. Wimbo huo umerekodiwa katika studio zao za Nyegera Waitu zilizopo huko huko Buza na tayari video ya wimbo huo imeachiwa katika mitandao ya kijamii mbalimbali huku ukisifiwa kwa kufanya vizuri. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Meneja wa kampuni ya Nyegera Waitu Intertainment, Prince Mawata amesema Shobo ni wimbo mzuri ambao wamepanga kuutambulisha hivi karibuni kwa mashabiki wao katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Mawata amedai wana imani kubwa wimbo huo utabamba kwenye spika za redio za mashabiki wao kutokana na maudhui yaliyomo ndani ya wimbo huo. Kundi hilo pamoja na lingine la Nyegera Waitu Band yapo chini ya tabibu Ntamba na Mungu ambaye anasifika kwa tiba mbadala ya binadamu

Kakule ruksa Simba

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Uongozi wa klabu ya soka ya Kiyovu Sports Club ya Rwanda imeridhia kiungo wake raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  (DRC) kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania Bars Simba SC. Awali klabu hiyo iliweka mgomo nyota wake huyo kujiunga na Simba kwa madai hawajafanya naye mazungumzo yoyote, lakini mchezaji huyo baada ya kufaulu majaribio yake katika klabu ya Simba alifunga safari ya Rwanda kuteta na viongozi wake. Kakule alifaulu majaribio katika mazoezi ya klabu ya Simba yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam , kocha msaidizi wa klabu hiyo Mrundi, Irambona Masoud Djuma ameridhishwa na kiwango cha kiungo huyo na kuwataka mabosi wake kumpa mkataba, Djuma alidai kiungo huyo ataisaidia sana Simba katika michuano ya kimataifa na ligi

AUSSEMS KOCHA MPYA SIMBA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Simba Sc leo imemtambulisha kocha wake mkuu Mbelgiji Patrick Winand Aussems baada ya kukubaliana kufundisha klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja. Aussems anachukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre aliyemaliza mkataba wake baada ya kuhudumu kwa miezi sita na kuipa ubingwa wa Bara iliousotea kwa misimu minne. Hafla ya utambulisho huo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ukiongozwa na kaimu Rais wa klabu hiyo Salim Abdallah "Try Again" ambapo alianza kwa kumsifu kocha huyo kwa kukubali kwake kutua Simba na kumtakia kazi njema ili aweze kuwapa mafanikio. Aussems ambaye alikuwa kocha wa Nepal ameahidi kuisaidia Simba kufika mbali kisoka, kocha huyo atasaidiwa na Masoud Djuma pamoja na kocha wa makipa Muharami Mohamed "Shilton"

BIASHARA MARA YANASA BEKI KISIKI WA SIMBA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Timu ya Biashara United ya mkoani Mara ambayo imepanda Ligi Kuu imekamilisha usajili wa beki wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc, Meshack Abel na kumpa mkataba wa miaka miwili. Beki huyo wa kati aliyewahi pia kuzichezea African Lyon na Bandari ya Mombasa nchini Kenya amejiunga na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao. Biashara United tayari imeshawasajili wachezaji wengine watatu hivyo imekuwa katika kipindi kizuri cha kujiimarisha kwani ujio wa beki huyo ni mwanzo wa kufanya vizuri msimu ujao, Meshack alitikisa alipokuwa Simba kutokana na umahiri wake

TARIMBA AZUIA USAJILI WA YONDANI SIMBA, AMBAKIZA JANGWANI

Picha
Na Asha Maliyaga. Dar es Salaam Mwenyekiti wa zamani wa kamati ya mpito wa Yanga Sc, Tarimba Abbas Tarimba jana usiku alikuwa na kikao kizito na beki kisiki Kelvin Patrick Yondani na kuweza kumshawishi abakie katika kikosi cha Yanga. Yondani alikuwa katika rada nzito za kujiunga na mabingwa wa soka nchini Simba Sc ambao inasemekana walikuwa tayari kumtumbukizia shilingi milioni 80 kwenye akaunti yake ya benki, lakini dakika za lala salama kigogo huyo akaingilia kati ma kuokoa jahazi. Pia Tarimba aliweza kumtuliza na beki mwingine Hassan Ramadhan Kessy ambaye naye alikuwa katika rada za kutoweka Yanga kwani naye aligoma kama Yondani

JUMA LUIZIO AREJEA MTIBWA SUGAR

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mabingwa wa kombe la shirikisho (Azam Sports Federation Cup) Mtibwa Sugar leo wamefanikiwa kuinasa saini ya Juma Luizio kutoka Simba Sc. Luizio aliyekuzwa na timu ya vijana ya Mtibwa Sugar na baadae kutimikia Zesco ya Zambia na baadae Simba Sc. Leo amerejea rasmi katika timu iliyomkuza Mtibwa Sugar Sc

YANGA YAKIONA CHA MOTO, YAPIGWA 4-0 NA GORMAHIA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Nairobi Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Yanga Sc usiku huu imeambulia kichapo cha mbwa mwizi baada ya kufungwa mabao 4-0 na Gor Mania ya Kenya katika mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Kasarani mjini Nairobi. Gor Mahia ilitawala eneo la katikati na kuwafanya Yanga washindwe kulishambulia lango lao hivyo ilikuwa rahisi kwao kulisakama mango LA Yanga na dakika ya 22 kipindi cha kwanza, mshambuliaji Jacques Tuyisenge aliipatia Gor Mania bao LA kwanza kabla ya Ephrahim Guikan kufunga la pili dakika ya 45. Hadi mapumziko Gor Mania walikuwa wanaongoza kwa mabao hayo mawili, kipindi cha pili Gor Mahia waliendeleza kasi yao na Mwinyi Haji WA Yanga akajifunga katika dakika ya 65 na kufanya Gor Mania kupata bao LA tatu kabla tens Guikan kufunga bao la nne dakika ya 85, kwa matokeo hayo Gor Mahia inafikisha pointi tano na kukaa kileleni huku Yanga ikiburuza mkia

MKWASA ABWAGA MANYANGA YANGA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Charles Boniface Mkwasa ametangaza kujiuzuru nafasi take hiyo lakini sababu kubwa akizitaja na kiafya ambapo amedai amejulishwa na jopo la madaktari wake kumtaka apumzike. Akizungumza Leo Mkwasa amesema amekuwa akisumbuliwa Mara kadhaa lakini anaendelea kufanya kazi ambazo zimekuwa zikimchosha, katibu mkuu huyo ambaye kitaalamu no kocha mwenye leseni A anajiweka kando huku kukiwa na lawama kubwa dhidi take. Katibu huyo anadaiwa kuihujumu Yanga katika suala la usajili ambapo mpaka sasa imeshindwa kuwasilisha majina ya wachezaji watatu waliosajiliwa kwa ajili ya michuano ya CAF, wachezaji ambao walisajiliwa ni  Mrisho Ngasa, Deus Kaseke na Mkongoman, Heritier Makambo. Wanayanga bado hawana matumaini na Mkwasa na huenda anatumia nafasi hiyo kujiweka kando ili aweze kutuliza akili zake, Mkwasa pia amewahi kuichezea klabu hiyo katika miaka ya 80, pia amewahi kuinoa Mara kadhaa kabla hajawa kocha WA Taiga Stars

PAZIA LIGI KUU BARA NI SIMBA NA PRISONS, NGAO YA JAMII SIMBA NA MTIBWA SUGAR

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Mabingwa wa Tanzania Bara Simba Sc wanatarajia kukutana na timu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ngao ya Jamii mechi itakayofanyika jijini Mwanza Agosti 18 mwaka huu. Baada ya hapo itashuka uwanjani kuumana na Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Agosti 22 huku pia  ikishuka tena dimbani Septemba 30 mwaka huu kuumana na mtani wake wa jadi Yanga Sc. Ligi hiyo itaanza rasmi Agosti 22 kwa timu zote 20 kushuka dimbani, ratiba ya ligi hiyo imetolewa leo na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF kupitia Bodi ya Ligi