SINGIDA UNITED YAIMARISHA SAFU YAKE YA ULINZI KWA KUWANASA MWAMBELEKO NA RAJAB ZAHIR
Na Paskal Beatus. Mwanza
Klabu ya soka ya Singida United ya mkoani Singida ambayo kwa sasa ipo jijini Mwanza kwa ziara maalum ya kujiandaa na msimu, leo imetangaza kuwasajili Jamal Mwambeleko "Nando" aliyekuwa anaitumikia Simba SC na Rajabu Zahir aliyekuwa Ruvu Shooting ya Pwani wote ikiwapa mkataba wa mwaka mmoja.
Mwambeleko ameachwa na Simba katika safari ya Uturuki amesajikiwa kwa mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo na sasa atakuwa miongoni mwa kikosi cha Singida United msimu ujao, Mwambeleko alijiunga na Simba akitokea Mbao FC kwa mkataba wa miaka miwili lakini wameweza kuelewana na Simba na sasa mchezaji huyo ni mali ya Singida United, Mwambeleko ni beki wa upande wa kushoto na amekuwa akipanda na kushuka.
Pia kikosi hicho kimemalizana na beki wa kati wa Ruvu Shooting, Rajabu Zahir ambaye aliwahi kuzichezea Mtibwa Sugar ya Morogoro na Yanga SC ya jijini Dar es Salaam