Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2016

JUMA ABDUL AISOGEZA YANGA KARIBU NA UBINGWA

Picha
Na Ikram Khamees, MWANZA BAO lililofungwa na beki wa kulia Juma Abdul Mnyamani limetosha kabisa kuisogeza Yanga Sc jirani na ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya jioni ya leo kuichapa Toto Africans mabao 2-1 uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Wakicheza vizuri kabisa chini ya kocha wao John Tegete, Toto Africans walionekana kuidhibiti Yanga idara zote na dakika ya 39 kipindi cha kwanza walijipatia bao la kuongoza lililofungwa na William Kimanzi. Hadi mapumziko Toto walikuwa mbele kwa bao hilo moja, kipindi cha pili Yanga walirejea kwa kasi ya aina yake na dakika ya 8 Amissi Tambwe aliisawazishia timu yake, Yanga waliongeza bao la pili lililofungwa na Juma Abdul Mnyamani kufuatia makosa ya mabeki wa Toto. Kwa ushindi huo wa leo, Yanga sasa imefikisha pointi 65 na mechi 26 hivyo ikizidi kupaa kileleni, mechi nyingine tatu zimechezwa leo ambapo mjini Shinyanga Mwadui imewaalika majirani zao Stand United, Prisons wameialika JKT Ruvu na jijini Tanga Africans Sports wamekipiga

MAPYA YAIBUKA KIFO CHA PAPA WEMBA, YADAIWA ALIWEKEWA SUMU KWENYE MIC PHONE

Picha
Na MITANDAO MAPYA yameibuka kufuatia kifo cha mwanamuziki gwiji barani Afrika Papa Wemba raia wa DRC aliyeanguka jukwaani na kufariki dunia huko Abidjan Ivory Coast imefahamika kuwa mwanamuziki huyo aliuawa kwa kuwekewa sumu. Kwa mujibu wa taarifa moja iliyoenea mitandaoni ikionyesha video ya msanii huyo akiwa jukwaani alibadilishiwa Microphone nyingine ambayo ina sumu, kwani mkongwe huyo hakuweza kudumu nayo na alianguka ghafla ya kupoteza maisha. Ripoti hiyo si nzuri sana kwani inasema kuzusha uhasama mwingine ambao unaweza kulipeleka mahakamani, Papa Wemba muasisi wa muziki wa kizazi kipya wa Soukous alifariki dunia Aprili 14 Abidjan baada ya kuanguka jukwaani akitumbuiza. Mwili wake uliwasili DRC juzi na anatarajia kuzikwa Jumanne ijayo, marehemu Papa Wemba atakumbukwa kwa nyimbo zake nzuri ikiwemo Shomy the Way Marehemu Papa Wemba enzi za uhai wake

YANGA NA TOTO LEO HATUMWI MTOTO DUKANI

Picha
Na Ikram Khamees, MWANZA MTANANGE wa ligi kuu bara maarufu kama VPL unaendelea jioni leo ambapo jumla ya viwanja vinne vitatimka vumbi, Uwanja wa CCM Kirumba wenyeji Toto Africans wataikaribisha Yanga Sc. Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wengi wa kandanda hapa nchini, licha kwamba Yanga na Toto zina udugu wa karibu lakini makocha wa timu hizo mbili wamekataa na kudai hawana udugu wa ujamaa. Kocha wa Yanga Mholanzi Hans Van der Pluijm amesema katika mchezo wa mpira hakuna kitu kinachoitwa udugu, amedai Yanga haiwezi kusimama uwanjani na ikapata ushindi bila kucheza eti sababu ni udugu. Amedai vijana wake watapambana kwa kushambulia lango la Toto na kupata magoli, anataka kushinda ili aendelee kukalia usukani, Naye kocha wa Toto John Tegete amesema hana udugu na Yanga na leo lazima wautumie vema uwanja wa nyumbani. Mechi nyingine leo ni kati ya African Sports na Coastal Union zote za Tanga uwanja wa Mkwakwani na Mwadui Fc na Stand United nazo za Shinyanga uwanja wa M

STAA WETU: HASSAN KABUNDA, MTOTO WA NINJA WA YANGA ANAYEING' ARISHA MWADUI FC

Picha
Na Paskal Beatus, SHINYANGA JINA la Hassan Kabunda linaonekana kama geni masikioni mwa watu, lakini wapo wanaomkunbuka beki wa zamani wa Tukuyu Stars, Yanga Sc na timu ya taifa ya Tanzania bara Kakakuona Salum Kabunda 'Ninja' ukipenda Msudan. Beki huyo alijulikana kwa kucheza kibabe sana uwanjani mpaka ikafikia washambuliaji kuanza kumuogopa, Hassan Kabunda ni mtoto wa Salum Kabunda, lakini iko tofauti kidogo. Hassan Kabunda yeye ni mshambuliaji na si beki kama ilivyokuwa kwa baba yake, kijana huyu amekuwa katika kiwango kizuri na kuwa msaada mkubwa kwenye timu yake ya Mwadui Fc ya Shinyanga. Kabunda ni mshambuliaji wa timu hiyo na anakumbukwa vizuri hasa pale alipoifungia Mwadui mabao yote mawili dhidi ya Coastal Union mchezo wa ligi kuu bara Nwadui ikishinda ikishinda mabao 2-1. Nyota huyo aliibukia katika mashindano ya Copa Cocacola akiwa na timu ya Mkoa wa Ilala, Kabunda akiwa na ndugu yake Ally Kabunda wote washambuliaji, walitamba katika michuano hiyo na baadaye waka

KOCHA AZAM AIGWAYA YANGA FAINALI YA FA CUP

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM KOCHA mkuu wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Muingereza Stewart Hall amesema Yanga Sc haikustahili kucheza fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup kwani imebebwa na TFF. Akizungumza na vyombo vya habari, Hall amesema aliutazama mchezo wa Nusu fainali kati ya Yanga na Coastal Union uliofanyika uwanja wa Mkwakwani Tanga ambapo Yanga ilishinda mabao 2-1 na mchezo huo ukavunjika kutokana na vurugu. Muingereza huyo aliyeiwezesha Azam kutwaa kombe la Kagame amedai Yanga ilibebwa na waamuzi kwani magoli yote iliyofunga hayakuwa halali, Stewart amesema kwamba upendeleo huu wa waamuzi hauvumiliki. TFF chini ya kamati yake ya mashindano iliamua kuipa ushindi Yanga hasa baada ya kujiridhisha Coastal walifanya vurugu kupitia kwa mashabiki wake na pia waamuzi waliboronga kwani iliwaadhibu. Kwa kauli hiyo ni sawa kama anaigwaya Yanga kwani atakutana nayo kwenye mchezo wa fainali itakayopigwa Mei mwaka huu

TCHETCHE FITI KUIVAA SIMBA J,PILI

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam Fc Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast huenda akawepo katika kikosi cha timu hiyo kitakachoivaa Simba Sc uwanja wa Taifa Dar ea Salaam. Tchetche alikosa mechi kadhaa za mashndano matatu tofauti akisumbuliwa na misuli, Simba na Azam zinakutana Jumapili ya keshokutwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Mshambuliaji tegemeo alikosa mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia ambapo Azam iliondolewa kwa jumla ya mabao 4-2. Aidha mshambuliaji huyo alikosa mchezo wa Nusu fainali kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup dhidi ya Nwadui Fc ya Shinyanga ambapo Azam ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-3. Pia aliukosa mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Majimaji ambao Azam ilishinda 2-0, kurejea kwa mshambuliaji huyo kunaongeza joto la mchezo huo Kipre Tchetche fiti kuivaa Simba

AZAM FC YAIPASHIA MISULI SIMBA, NGOMA KUPIGWA JUMAPILI, SIMBA WATUA JANA KIMYAKIMYA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM WAKATI klabu ya Simba ikiwasili Dar es Salaam jana kimya kimya, wapinzani wao Azam Fc wao wameendelea na mazoezi yao kabambe katika uwanja wao wa Azam Complex Chamazi. Azam Fc inacheza na Simba Sc mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Taifa Dar ea salaam, Simba wao walienda Zanzibar kuweka kambi kujiandaa na mchezo huo na juzi usiku waliichapa Mafunzo mabao 3-0 yaliyofungwa na Awadh Juma kama sehemu ya kujiandaa na mchezo huo. Hadi sasa Azam Fc inashika nafasi ya pili wakiwa nyuma ya vinara Yanga Sc na wana pointi 58 na mechi 25 sawa na Simba anbayo yenyewe inashika nafasi ya tatu na pointi 57, Yanga iko kileleni ikiwa na pointi 62 na mechi 25. Mchezo wa Azam na Simba utakuwa mgumu kwakuwa kila timu inataka kuibuka na ushindi ili kulisogelea taji la ubingwa wa bara ambalo linashikiliwa na Yanga, Simba inanolewa na Jackson Mayanja raia wa Uganda wakati Azam yenyewe inanolewa na Stewart Hall raia wa Uingereza, Nani ataibuka Wacheza

MICHANO: HUSSEIN MACHOZI, BAADA YA KUVIMBA KICHWA, AKAKIMBILIA KENYA AKAWASAHAU MASHABIKI WAKE BONGO

Picha
Na Mkola Man, TANGA YAP....Yap...yap...Michano yangu ya leo inamchana Mmasai wa Singida ajulikanaye kwa jina la Hussein Machozi mkali wa bongofleva aliyeiibukia jijini Mwanza chinj ya meneja wake Kid Bway. Mbali na muziki pia ni mwanasoka mzuri na kwa mara ya kwanza nilikutana naye Tanga katika studio za Motika Record chini ya marehemu Mr Ebbo. Mimi nilienda kurekodi wimbo wangu uitwao "Utajiri hewa",niliomshirikisha Mr Ebbo kwenye kiitikio, toka hapo hatujaonana tena ila kwa sasa yupo nchini Kenya. Alifahamika sana kwa nyimbo zake za mikasa kama vile 'Kafia gheto', 'Jela' na nyimbo nyinginezo ambazo zilimfanya avimbe kichwa hadi kupasuka. Kupotea kwenye gemu ya muziki kwa Hussein Machozi ni kutokana na kuachana na meneja wake akiamini atajiendesha mwenyewe akisahau kuwa thamani ya kidole ni pale kinapoondoka, kiufupi kwa sasa kaishiwa pumzi. Jamaa ilifikia hatua hadi anataka kurudia tena kucheza soka, akaenda kufanya mazoezi Kagera Sugar timu aliyowahi

MWILI WA PAPA WEMBA WAWASILI DRC

Picha
Na Mwandishi Wetu, DRC MWILI wa aliyekuwa mwanamuziki gwiji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Papa Wemba aliyefariki jukwaani akitumbuiza mjini Abidjan umewasili leo na kupokewa uwanja wa ndege wa Kinshasa. Mamia ya waombolezaji walijitokeza kwa wingi kushuhudia jeneza lililobeba mwili wa muasisi huyo wa miondoko ya kizazi kipya ya Soukous, Papa Wemba alifariki jukwaani Aprili 14, 2016 akiwa kwenye shoo zake za muziki. Mke wa marehemu aliyeambatana na wasaidizi wake aliudhuria uwanja wa ndege wa Kinshasa kushuhudia mwili wa mumewe, baadhi ya watu waliofurika uwanjani hapo walionekana kuwa na hisia na kutokwa na machozi hasa pale jeneza lake lilipotelemshwa kutoka kwenye ndege. Rais wa DRC Joaeph Kabila alituma ndege nchini Ivory Coast kufuata mwili wa gwiji huyo wa muziki aliyeitangaza nchi hiyo nje ya mipaka, Papa Wemba atazikwa hivi karibuni Mwili wa marehemu Papa Wemba ulipowasili Heshima ya mwisho ikitolewa na maafisa walioupokea mwili uwanja wa ndege

FARID MUSSA KIMEELEWEKA HISPANIA, BAKHRESSA AMPANDIA NDEGE KUMALIZANA NAO

Picha
Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM WINGA kinda wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam Sc, Farid Mussa Mariki anaelekea pazuri katika majaribio yake na huenda akafuzu hasa baada ya kuwashangaza kwenye mchezo wa kirafiki kati ya CD Tanarife timu anayoichezea kwa sasa na UD Diabora. Kinda huyo atakayefanya majaribio ya mwezi mmoja na timu hiyo ameonyesha kiwango kizuri na tayari uongozi wa timu hiyo umeshaanza kuwasiliana na mabosi wa Azam ambapo Yussuf Bakhressa ameshapanda pipa kufuatilia dili. Farid atakuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza soka la kulipwa miaka hii sasa mara baada ya kuanzishwa soka la kulipwa, winga huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars amekuwa msaada kwenye klabu yake ya Azam kwani ndiye muuaji wa bao dhidi ya Esperance ya Tunisia, Azam ikishinda 2-1 uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam

YANGA WAWASILI MWANZA KIBABE

Picha
Na Paskal Beatus, MWANZA YANGA ya Dar es Salaam imewasili asubuhi ya leo hapa jijini Mwanza ikitokea Dar es Salaam ambako jana jioni iliichapa Mgambo JKT ya Tanga mabao 2-1 uwanja wa Taifa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Kikosi cha Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wametua na wachezaji wao wote mapema na kulakiwa na mashabiki wake waliojitokeza uwanja wa ndege. Jumamosi ijayo Yanga itakuwa mgeni wa Toto Africans "Wanakishamapanda" uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, tayari Yanga inaongoza ligi ikiwa kibindoni na pointi 62 mechi 25 na inahitaji pointi tatu muhimu ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa bara. Vijana wa Toto nao wanataka kudhihirisha kuwa hawakubahatisha kuwafunga Simba Sc bao 1-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam hivyo kulufabya pambano hilo kuwa kali na  la kuvutia

YANGA YAPEWA USHINDI DHIDI YA COASTAL UNION, SASA KUKIPIGA NA AZAM FC FAINALI FA CUP

Picha
Na Feisa Baba, DAR ES SALAAM Coastal Union imepoteza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga baada ya washabiki wake kuwa chanzo cha Mwamuzi kuvunja mchezo huo uliofanyika Aprili 24, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Aprili 27, 2016) jijini Dar es Salaam kwa kuzingatia Kanuni ya 28(2) ya Kombe la Shirikisho. Wakati mechi hiyo inavunjwa, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1. Pia Coastal Union imepigwa faini ya sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kuzingatia Kanuni ya 42(26) ya Ligi Kuu kutokana na vitendo vya vurugu za washabiki wake wakati wa mechi hiyo. Pia TFF haitasita kufungiwa uwanja huo iwapo vitendo hivyo vya vurugu za washabiki havitakoma. Mwamuzi wa mchezo huo Abdallah Kambuzi amefungiwa mwaka mmoja wakati Mwamuzi Msaidizi namba mbili Charles Simon ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi. Adhabu hizo zimetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(

AZAM FC YAISHUSHA SIMBA, YAICHAPA MAJIMAJI 2-0

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM AZAM FC jioni ya leo katika uwanja wake wa Azam Complex Chamazi imewafumua Wandengeleko kutoka Ruvuma Majimaji mabao 2-0 mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Shujaa wa Azam katika mchezo huo alikuwa Mudathili Yahya aliyefunga magoli yote mawili, kwa matokeo hayo Azam imechupa hadi nafasi ya pili ikiiondoa Simba ambayo sasa imeangukia nafasi ya tatu. Majimaji licha ya kucheza kandanda zuri na la kuvutia lakini ilijikuta ikinyukwa mabao hayo yaliyoifanya Azam ifikishe pointi 58 na mechi 25 ikiwa nyuma ya mabingwa watetezi Yanga wenye pointi 62 baada ya leo hii kuichapa Mgambo JKT mabao 2-1. Jumapili ijayo uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Azam Fc itakutana na Wekundu wa Msimbazi Simba Sc mchezo wa ligi kuu bara ambao utaamua nani ataingia kwenye vita ya kuwania ubingwa wa bara Azam Fc imeishusha Simba hadi nafasi ya tatu

KASEKE AING' ARISHA YANGA KILELENI

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM DEUS Kaseke ameifungia Yanga mabao mawili muhimu jioni ya leo uwanja wa Taifa Dar es Salaam ikiifunga Mgambo JKT ya Tanga mabao 2-1 mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Mgambo JKT ilitangulia kupata bao la kuongoza dakika ya nne likifungwa na Nassoro Gumbo, Yanga walipambana kuhakikisha wanasawazisha bao na walifanikiwa kusawazisha lililofungwa na Deus Kaseke. Hadi mapumziko timu hizo zilienda sare ya 1-1, kipindi cha pili kilianza kwa kasi nyingine huku Yanga ikijaribu kuwaingiza nyota wake wanaotamba  kama Donald Ngoma na Thabani Kamusoko. Yanga waliongeza bao la pili lililofungwa na yule yule Deus Kaseke, hadi mpira unakwisha matokeo ndio hayo, Yanga sasa imefikisha pointi 62 na mechi 25 ikiendelea kung' ara kileleni Yanga Sc yazidi kuchanua kileleni

KIZUGUTO NJE, ALFRED LUCAS AFISA HABARI MPYA TFF

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limemteua Alfred Lucas kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa shirikisho hilo kuanzia leo Aprili 27, 2016. Lucas mwandishi wa habari wa siku nyingi nchini wa magazeti mbalimbali likiwemo la Dimba anachukua nafasi ya ndugu Baraka Kizuguto aliyehamishiwa ofisi nyingine. Kizuguto anakwenda kuwa Afisa mashindano na meneja mifumo Pepe ya usajili kwa TMS, Alfred ana uzoefu kutoka kwenye vyombo vya habari mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri likiwemo gazeti la Dimba ambalo lilimuinua kabla hajaenda magazeti mengine. Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari na uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na lugha Baraka Kizuguto amehamishiwa ofisi nyingine

ANAYEKUMBUKWA: ABDALLAH KIBADENI, MUUAJI WA MABAO MATATU PEKEE SIMBA NA YANGA

Picha
Na Ikram Khamees, DAR S SALAAM HAKIKA kabisa miaka ya 70 gwiji la soka wakati huo alikuwa Abdallah Seif Athuman, Wangoni wakampachika jina la Kibadeni na wakamuongezea lingine la King Mputa. Kibadeni alikuwa mfanisi wa soka uwanjanj, kwa wale waliobahatika kumuona akisakata kandanda hawana shaka naye, kwakweli alikuwa fundi wa mpira. Ingawa historia zinaonyesha alikuwa klabu ya Simba na alitamba na klabu hiyo, lakini yeye mwenyewe aliweka bayana kuwa ilikuwa kidogo aichezee Yanga, anasema alianza kujiunga na Yanga lakini akakataliwa. Kisa cha kukataliwa kwanza kilikuwa kimo chake kidogo lakini pili bangili, anadai yeye hupendelea kuvaa bangili mkononi hivyo Yanga walimtaka avue akakataa na ndipo alipoamua kuachana nao na kupelekwa Simba. Alivuma na Simba pamoja na Taifa Stars kabla ya kujiunga na Majimaji ya Songea alikopachikwa jina la Kibadeni, alirejea Simba na kuendeleza makali yake. Kibadeni ana rekodi yake moja ambayo bado inashindwa kuvunjwa, mshambuliaji huyo akiwa Simba

VIPORO VYA 'WAKUDA', YANGA NA AZAM LEO DAR

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM YANGA SC na Azam Fc jioni ya leo wote kwa pamoja wanataraji kushuka dimbani kukamilisha viporo vyao, katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mabingwa wa bara Yanga Sc wataialika Mgambo JKT ya Tanga. Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili izidi kujiweka katika mazingira mazuri, mabingwa hao wa bara wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 59 na mechi 24 wakifuatiwa na Simba yenye pointi 57 mechi 25. Mgambo JKT vijana wa Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga  nao hawatakubali kupoteza mchezo huo kwani wapo sehemu mbaya ya kushuka daraja. Mtanange mwingine upo uwanja wa Azam Complex ambapo wenyeji  "Wauza Ice Cream wa Bakhressa" Azam Fc wanawaalika "Wapiganaji wa vita ya Majimaji" kutoka Songea, Azam inahitaji ushindi ili iweze kukwea hadi nafasi ya pili ikiwashusha Simba. Azam hadi sasa ina pointi 55 mechi 24 ikishinda mchezo huo itafikisha pointi 58 na kuiacha Simba kwa tofauti ya pointi moja Waikato Jumapili miamba hiyo Azam na Simba

SIMBA KUMREJESHA OKWI, KUACHANA NA KIIZA

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM IMEBAINIKA klabu ya Simba ipo katika mipango ya mwisho ya kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani Mganda Emmanuel Okwi na pia ikitaraji kuachana na Mganda mwenzake Hamisi Kiiza 'Diego'. Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kipo karibu na klabu hiyo kimesema tayari viongozi wa timu hiyi wameshakubaliana kumrejesha nyota huyo kipenzi cha mashabiki wa Simba. Okwi aliuzwa na Simba mwishoni mwa msimu uliopita kwa klabu ya Sonderjyske ya Denmark inayoshiriki ligi kuu lakini maendeleo yake si mazuri ndani ya timu hiyo na imetangaza kumpiga bei. Uongozi wa timu hiyo umewasiliana na Simba na kukubalina kwamba Okwi atauzwa kwa hela ileile iliyotumika kumnunua, kwa maana hiyo Simba sasa itafufua matumaini yake ya kufanya vizuri msimu ujao kwani mshambuliaji huyo ana msaada mkubwa ndani ya klabu hiyo. Wakati Okwi anarejea Simba, mshambuliaji Hamisi Kiiza huenda akatupiwa virago, Kiiza aliyebakisha miezi michache kumaliza mkataba, anapigiwa hesabu za kuachwa

KWA WAPENZI WA FILAMU, MSIKOSE MZIGO MPYA UNAKUJA

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM SOKO la filamu nchini linazidi kuongezeka kufuatia wasanii mbalimbali nchini kuzidi kutengeneza filamu zenye ubora wa kipekee na wa hali ya juu. 'The Dead Samson' ni moja kati ya filamu inayosubiriwa kutoka hivi karibuni na tayari imeshaanza kuwa gumzo ambayo ndani yake yupo mwanadada anayeibukia kwa sasa kwenye tasnia hiyo Rachel Bithulo 'Recho'. Mwanadada anayetokea Mwanza, amezidi kujipatia umaarufu kutokana na kazi zake na kufanya vizuri, Ector huyo wa kike pia ni Video Queen wa bongofleva na wimbo uliompa saluti ni ule wa PNC uitwao 'Yule yule', ambao alikubalika vilivyo na kuwavutia wengi. Mbali na kutamba kwenye filamu hiyo, Recho pia amewahi kutamba kwenye filamu ya 'Craritha' ambayo ilimtangaza kama msanii wa kike anayefanya vizuri, msanii huyo alipata bahati kuingia kwenye tuzo za Nyambago Award 2016 lakini hakubahatika kupata tuzo na hasa mchakato wenyewe kudaiwa kuwa na upendeleo kwa wasanii wa kanda ya ziwa

STARS KUJIPIMA NA HARAMBEE STARS MEI 29

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM TIMU ya taifa ya Tanzanja Taifa Stars inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars ifikapo Mei 29 mjini Nairobi Kenya. Mchezo huo unatosha kuzipa mazoezi tosha timu zote mbili za ukandaa huu wa Afrika mashariki na kati ambapo Juni mwaka huu zitakuwa na vibarua vya kufuzu fainali za mataifa Afrika. Stars inayonolewa na mzalendo Charles Boniface Mkwassa itakuwa na mtihani mgumu wa kuipiku Misri "Farao" katika kuipata tiketi ya kufaulu kwenye kundi lake. Hadi sasa Stars na Misri ndizo zenye nafasi ya kufuzu fainali za AFCON kutokana na mazingira yenyewe, Stars ina pointi moja iliyopata dhidi ya Nigeria ambayo imeshatolewa tayari, Misri wanapointi 5 na wamesaliwa na mechi moja, wakati Stars imebakiza mechi mbili na ikishinda zote itafikisha pointi 7 na moja kwa moja itafuzu kwenda Gabon mwakani. Misri na Tanzania zitaumana Juni mwaka huu jijini Dar es Salaam, imepita miaka kadhaa Stars na Harambee hawajakutana k

YANGA WATAKIWA KUFANYA UCHAGUZI JUNI 5

Picha
Na Mwandishi Wetu  DAR EA SALAAM SHIRIKISHO la soka nchini TFF limeitaka klabu ya Yanga kuitisha uchaguzi wake ifikapo Juni 5 kulingana na agizo lilikotolewa na BMT na wizara. Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi TFF, Aloyce Komba amesema mchakato mzima wa uchaguzi wa Yanga utakuwa ndani ya siku 33. Komba ambaye pia ni Wakili, amesema mchakato rasmi wa uchaguzi wa Yanga utaanza Mei 3, 2016, Komba amesema jukumu lao TFF kusimamia na kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali ya demokrasia. Wakili Komba ameongeza kuwa kamati yake itatangaza mchakato mzima wa uchaguzi huo wa Yanga na kubandika tangazo kwenye mbao za matangazo na kutangaza nafasi zitakazogombaniwa. Mei 4-9, 2016 kuchukua fomuza wagombea na mwisho wa kurudisha kwa wagombea, Mei 10, 2016 kamati ya uchaguzi TFF itakaa kikao cha mchujo wa awali wa wagombea na kuandika barua za kuwajulisha wagombea juu ya mchujo huo wa awali. Mei 11, 2016 kamati ya uchaguzi ya TFF itachapisha na kubandika

SIMBA KAZI MOJA TU, YAPIGA MAZOEZI YA HATARI, AZAM KAZI MNAYO

Picha
Na Salum Fikiri Jr, ZANZIBAR KLABU ya Simba imejichimbia Zanzibar wakiweka kambj kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu bara na Azam Fc uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Vijana wa Simba wameendelea na mazoezi makali chini ya kocha wake Jackson Mayanja raia wa Uganda ambayo yanawafanya wachezaji wa Simba kuwa fiti zaidi. Simba inacheza na Azam Fc Mei Mosi mwaka huu mchezo utakaotoa majibu nani anaweza kugombania ubingwa wa bara, Simba inakamata nafasi ya pili nyuma ya Yanga ikiwa na pointi 57 mechi 25, wakati Azam inashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 55 mechi 24 Wachezaji wa Simba wakijifua Zanzibar

YANGA WATUA DAR NA KUFIKIA TIFFANY HOTEL KUWANGOJA MGAMBO JKT

Picha
Na Ikram Khamees, DAR EA SALAAM YANGA SC imewasili Dar es Sala leo ikitokea mkoani Tanga ambako jana iliwalaza Coastal Union ya Tanga mabao 2-1 mchezo wa Nusu fainali michuano ya FA Cup na kutinga fainali. Mabingwa hao wa bara Jumatano ya keshokutwa wanashuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwakaribisha Mgambo JKT mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Yanga  ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 59 wakicheza mechi 24 wakifuatiwa na Simba wenye pointi 57 wenye mechi 25, endapo Yanga itashinda mchezo huo itazidi kujikita kileleni Yanga wakiwa njiani kuja Dar es Salaam

MPYA KUHUSU COASTAL UNION, YADAIWA AZAM INATIA MKONO KUIUA, KISA BIASHARA

Picha
Na Mkola Man, TANGA MPYA nadhani hakuna yeyote anayefahamu taarifa hiyo ni kwamba klabu ya Coastal Union ya Tanga inahujumiwa na Azam ambao ndio wadhamini wa mashindano ya Azam Sports  Federation Cup maarufu FA Cup. Habari za uhakika ambazo Mambo Uwanjani imezinyaka kuwa hata katika mchezo wa jana kati ya Yanga na Coastal Union uwanja wa Mkwakwani Tanga, Azam imehusika kwa namna moja ama nyingine ingawa ni ngumu kuamini. Ishu iko hivi, mdhamini mkuu wa Azam Fc ni kampuni ya Azam Food Production watengenezaji wa bdhaa mbalimbali ukiwemo unga wa ngano na sembe, wakati mdhamini mkuu wa Coastal Union ni kampuni ya Pembe watengenezaji wa unga bora wa ngano na sembe. Ushindani wa makampuni unaweza kuwa mkubwa endapo tu Coastal itapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, kwa sasa Coastal imepote,a mwelekeo kwenye ligi hivyo nafasi walikuwa nayo kupitia FA Cup. Inadaiwa Azam imetia mkono ili Coastal isipate nafasi ya kuonekana kimataifa kwani itaathili biashara ya Azam, lakini kiko

MAONI: HAYA YOTE WAMEYATAKA TFF YA MALINZI, NUSU FAINALI YA FA CUP KUCHEZWA "UCHOCHORONI"

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM KAMA ingetokea mwamuzi aliyechezesha pambano la kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup Nusu fainali kati ya Yanga Sc na Coastal Union uliofanyika uwanja wa Mkwakwani Tanga angepoteza maisha basi lawama zote zinngeelekezwa TFFna rais wake Jamal Malinzi kwa kupeleka mechi hiyo "Uchochoroni". Mechi hiyo yenye uzito wake ilipaswa kuchezwa uwanja mkuu wa Taifa, mechi ya Nusu fainali inahitaji usalama wa kutosha lakini kwa jana ni kichekesho tupu. Pambano kati ya Yanga na Coastal lilivunjika kunako sakika ya 110, ina maana zilisalia dakika kumi kumalizika mchezo huo huku Yanga Sc ikiwa mbele kwa mabao 2-1, mashabiki wa Coastal Union walianza vurugu kwa kurusha mawe uwanjani na kusababisha wachezaji wa Yanga kutoka nje kuogopa kuumia. Mwamuzi namba mbili Charles Simon alijeruhiwa vibaya maeneo ya usoni na kupelekea kupatiwa matibabu ya haraka, mbali na kuumia vurugu hizo zilisababisha pambano hilo kuvunjika na kuwaacha watu wengi na msha

AZAM FC YATINGA FAINALI YA FA CUP, YAWACHAPA MWADUI KWA PENALLTI 5-3

Picha
Na Paskal Beatus, SHINYANGA AZAM FC jioni ya leo imetinga fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup baada ya kuilaza Mwadui Fc kwa mikwaju ya penalti 5-3 baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya 2-2 uwanja wa Mwadui Complex mchezo wa Nusu fainali. Kwa matokeo hayo Azam Fc imeingia fainali na sasa inaweza kukutana na Yanga ambayo ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union uwanja wa Mkwakwani Nusu fainali nyingine, mchezo huo ulivunjika zikiwa zimebaki dakika 10. Azam walipata magoli ya Azam yaliwekwa kimiani na Hamisi Mcha "Vialii" wakati yale ya Mwadui yalifungwa na Jabir Aziz "Stima" na Kevin Sabato. Timu hizo zilienda kwenye mikwaju ya penalti baada ya muda wa nyongeza dakika 30 kukamilika, Azam walipata penalti zao kupitia kwa John Bocco "Adebayor", Waziri Salum, Himid Mao Mkami, Allan Wanga na Agrey Morris aliyefunga ya ushindi. Mwadui nao walipata penalti zao tatu kupitia kwa Malika Ndeule, Iddi Mobby na Jabir

YANGA WATANGULIA FAINALI FA CUP, MAWE YAVULUMISHWA MKWAKWANI

Picha
Na Mkola Man, TANGA MABINGWA wa soka Tanzania bara Yanga Sc jioni ya leo imefanikiwa kuchomoza na ushindi katika uwanja wa Mkwakwani Tanga baada ya kuilaza Coastal Union mabao 2-1 mchezo wa Nusu fainali kombe la FA. Licha kwamba mchezo huo haukumalizika kutokana na muda wake hasa mashabiki wa Coastal Union kuwapiga mawe wachezaji wa Yanga wakianza na kipa wake Deogratus Munishi 'Dida'. Mchezo huo ilibidi uende kwenye muda wa nyongeza yaani dakika 30 baada ya kumaliza dakika 90 wakifungana 1-1, Coastal walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Yousef Sabo raia wa Cameroon. Goli hilo lilipatikana kipindi cha pili baada ya kumaliza dakika 45 za kwanza 0-0. Yanga nao wakacharuka na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa Donald Ngoma raia wa Zimbabwe. Yanga tena walipata bao la pili katika muda wa nyongeza kupitia kwa Amissi Tambwe raia wa Burundi aliyepokea krosi ya Juma Abdul Mnyamani. Kwa maana hiyo Yanga wanaingia fainali na sasa watakutana na Azam Fc ambayo iliwa

PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA IVORY COAST

Picha
Na Mwandishi Wetu, KIMATAIFA MWANAMUZIKI maarufu barani Afrika Papa Wemba raia wa DRC amefariki dunia ghafla mjini Abidjan akiwa anafanya maonyesho yake ya kimuziki na ghafla alipatwa na maradhi na kupelekea kifo chake. Mwanamuziki huyo aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa miondoko yake ya muziki wa Kikongo huku akipata mialiko mbalimbali katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji. Marehemu pia atakumbukwa na wapenzi wa muziki nchini Tanzania nao wanamkumbuka vilivyo kwani aliwahi kuitembelea nchi hiyo na kufanya maonyesho kadhaa. Papa Wemba alizaliwa Juni 14, 1949 katika mji wa Lubefu, Belgian DRC Congo na alipata kuhudumu katika bendi za Zaiko Langa Langa na Viva la Musica, marehemu Papa Wemba ndio jina lililovuma sana lakini jina halisi ni Jules Shungu Pene Wembadio Kikumba Marehemu Papa Wemba

HANSPOPPE AMRUKA BASENA, ASEMA SIMBA HAWANA MPANGO NAYE

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM BAADA ya kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kwamba kocha wa zamani wa Simba Moses Bassena raia wa Uganda anawasili nchini tayari kabisa kwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba. Lakini mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Wekundu hao wa Msimbazi Kapteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Zacharia Hanspoppe amesema hawana mpango wa kumuajili kama kocha mkuu wa Simba Mganda huyo. Hanspoppe amekiri ni kweli Simba iko mbioni kutafuta kocha mpya atakayeiongoza timu hiyo msimu ujao lakini si Bassena, amedai uwezo wa Bassena hautofautiani na ule wa Jackson Mayanja hivyo wao wanasaka kocha wa matawi ya juu. Mayanja alichukua jukumu la kuiongoza Simba kama kocha wa muda baada ya Muingereza Dylan Kerr kutupiwa virago, Simba kwa sasa inakamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 nyuma ya Yanga yenye pointi 59 ila imecheza mechi 26 wakati Yanga imecheza mechi 25

MITANANGE MIWILI FA CUP KUPIGWA LEO, NANI KUCHEZA FAINALI

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM MICHUANO ya Azam Sports Federation Cup inatarajia kuendelea jioni ya leo katika viwanja viwili tofauti hatua ya Nusu fainali ambapo timu mbili zitafuzu fainali itakayopigwa mwezi Mei mwaka huu. Tukianzia pambano linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka katika miji ya Dar es Salaam na Tanga, mabingwa watetezi wa ligi kuu bara Yanga Sc watakuwa wageni wa Coastal Union ya Tanga uwanja wa CCM Mkwakwani. Timu hizo zinakutana leo katika michuano hiyo inayofahamika zaidi kama FA Cup, Yanga inataka kulipiza kisasi kwani ilibutuliwa mabao 2-0 na vijana hao wa Wana Mangushi, Yanga ilifungwa kwenye mchezo huo wa ligi kuu bara. Hivyo mchezo huo utakuwa mkali ikitaka kulipiza kisasi, pia ina machungu ya kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 3-2 na Al Ahly ya Misri, Coastal nao kwa sasa wako vizuri hasa baada ya kupata ushindi wa mara mbili mfululizo. Coastal iliifunga Simba Sc mabao 2-1 mchezo wa Robo fain

HATIMAYE MWANZA WAPATA TIMJ YA PILI LIGI KUU

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la kandanda nchini TFF limeipandisha ligi kuu timu ya Mbao Fc ya Mwanza na kuufanya mkoa huo kuwa na timu mbili zitakazoshiriki ligi kuu bara kwa pamoja na kuwa historia. Mkoa wa Mwanza haukuwahi kuwa na timu mbili kwa pamoja kwa muda mrefu tangia Pamba Fc pia ya Mwanza iliposhuka daraja na kuiacha Toto Africans ikiendelea kutesa hadi sasa. TFF imeamua kuipandisha Mbao Fc ligi kuu kufuatia kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo kuzishusha daraja timu nne kwa mkupuo za Geita Gold, Polisi Tabora, JKT Kanembwa na JKT Oljoro kwa kupanga matokeo. Geita Gold iliifunga mabao 8-0 timu ya JKT Kanembwa ya Kigoma na Polisi Tabora nayo ikaichapa mabao 7-0 timu ya JKT Oljoro ya Arusha na baadaye kuibuka mgogoro mkubwa kuwa timu hizo zimepanga matokeo ambapo TFF ikaamua kuzishusha daraja na baadhi ya wachezaji, viongozi na marefa wakafungiwa miaka kumi hadi maisha. Mbao Fc ilikamata nafasi ya nne kwenye kundi lake la C lililojumuhisha timu hizo zilizoshush

STAA WETU: JUMA ABDUL JAFFARI, MPISHI WA GOLI LA NGOMA, WAARABU WAMZIMIA

Picha
Na Exipedito Mataruma, ALIYEKUWA MISRI. JUMA Abdul Jaffari ukiongeza lingine Mnyamani ni jina linalochomoza kwa sasa kwenye medani ya soka hapa nchini na kwingineko. Anacheza nafasi ya ulinzi wa pembenj hasa akimudu upande wa kulia na akisaidia kupandisha mashambulizi, Abdul amekuwa na uwezo mkubwa wa kusababisha mashambulizi na timu yake kung' ara. Akiwa katika kikosi hicho cha mabingwa wa soka nchini Yanga Sc, Abdul ameisaidia hadi kukamata usukani wa ligi kuu na kuweka hai matumaini yake ya kutetea ubingwa wa bara. Nyota huyo pia amekuwa mpigaji mzuri wa mipira iliyokufa kwa maaba faulo, Abdul amejaaliwa nguvu za miguu na amekuwa akipiga mashuti makali hatimaye kuifungia timu yake magoli. Anakumbukwa kwa magoli yake ya mashuti moja dhidi ya Azam Fc, ambapo alisawazisha makosa yake baada ya kujifunga kisha akapanda na kupiga bunduki kali na kufunga la kusawazisha, katika mchezo huo timu hizo zenye ushindani zilifungana mabao 2-2. Abdul pia akafunga bao lingine dhidi ya APR

SIMBA HAOOOO ZANZIBAR KUIWINDA AZAM MEI MOSI

Picha
Na Salum Fikiri Jr, ZANZIBAR SIMBA SC imewasili Zanzibar jioni ya leo ikitokea jijini Dar es Salaam ikiwa tayari kabisa kuiwinda Azam Fc mchezo wa ligi kuu bara Mei mosi mwaka huu uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Simba ikiwa na mechi ngumu hutumia kambi ya Zenji kujiwinda zaidi, mchezo wake na Azam utakuwa mkali kutokana na kila timu kutaka kumaliza kwenye nafasi za juu. Klabu hiyo yenye maskani yake mtaa Msimbazi ina pointi 57 na mechi 25 ikikamata nafasi ya pili nyuma ya Yanga inayoongoza ikiwa na pointi 59 lakini imecheza mechi 24, Azam inashika nafasi ya tatu ikiwa imecheza mechi 24. Meneja wa Simba Abbas Ally amesema vijana wake watakuwa imara zaidi wakiwa Zanzibar kwani kuna utulivu wa hali ya juu tofauti na Dar es Salaam, Ally amewataka mashabiki wa Simba kuwa watulivu katika kipindi hiki na ushindi utapatikana tu. Simba ilipoteza mechi mbili mfululizo moja ikifungwa na Coastal Union mabao 2-1 mchezo wa Robo fainali kombe la FA na nyingine ilifungwa na Toto Africans mchezo wa

YANGA NAO WAWASILI TOKA MISRI NA KUELEKEA TANGA

Picha
Na Exipedito Mataruma, DAR ES SALAAM. Mabingwa wa Tanzania bara Yanga Sc wamewasili leo kutokea nchini Misri ambako waliondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na Al Ahly kwa jumla ya mabao 3-2. Yanga ilitua leo na moja kwa moja kuanza safari ya kuelekea jijini Tanga ambapo Jumapili ijayo itaumana na Coastal Union mchezo wa Nusu fainali kombe la FA. Kikosi cha Yanga kilichopata mapokezi makubwa uwanja wa Mwl Nyerere kinapewa nafasi kubwa kulipiza kisasi katika mchezo huo kwani zilipokutana ligi kuu bara Yanga ilichapwa 2-0. Coastal wameonekana kubadilika katika siku za karibuni na hawatakubali kirahisi kupoteza mchezo huo na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika

BAADA YA KUTUA KUTOKA TUNISIA, AZAM WAIFUATA MWADUI

Picha
Na Exipedito Mataruma, DAR ES SALAAM KLABU bingwa Afrika mashariki na kati Azam Fc wamewasili leo na moja kwa moja kuunganisha ndege kuelekea Mwanza tayari kabisa kuwavaa Mwadui ya Shinyanga mchezo wa FA Cup Jumapili ijayo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, mtendaji mkuu wa Azam, Saad Kawemba amedai vijana wake wako sawasawa kushinda. Bingwa wa michuano ya kombe la FA anapata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Azam imewasili leo kutoka Tunis, Tunisia ilikokwenda kurudiana na Esperance ambapo iliondoshwa kwa jumla ya mabao 4-2, Katika mchezo huo Azam ililala 3-0 na mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam, Azam ilishinda 2-1

MICHANO: PHILIPO NYANDINDI "O TEN", ALISAHAU MSEMO HUU, UKIMUONA KOBE JUU YA MTI UJUE KAWEKWA

Picha
Na Mkola Man, TANGA YAP....yap....yap Michano yangu ya leo inamchana Philipo Nyandindi "O Ten" kutoka mji kasoro bahari yaani Morogoro ila safari yake kimuziki ilianzia Upanga jijini Dar es Salaam katika kundi la East Coast Team. Lakini kabla hajatua kundi hilo, O Ten alikuwa msanii wa kujitegemea huko Morogoro na siku moja wakati msanii Inspekta Haroun akitamba na 'Mtoto wa geti kali' alivutiwa na msanii huyo jukwaani na kuamua kumleta Dar es Salaam. Inspekta ndiyo msanii wa kwanza kurekodi studio na O Ten wimbo unaojulikana kwa jina la "Siku za Hukumu ya mwisho'. na hapo ndipo safari ya O Ten ilipoanza. KWANINI ALIINGIA EAST COAST O Ten alijiunga na East Coast Team baada ya kutelekezwa na Inspekta ambaye alimuahidi kumsaidia kimuziki ndipo alipotua kundi hilo lililotamba sana, mwaka 2004 alitoka na nyimbo iitwayo 'Nicheki' iliyotengenezwa vizuri na prodyuza P Funk Majani iliyompa heshima ndani ya kundi lake na nje pia. Kisha nyota yake ikaanza

CAF YAWAPA YANGA WAANGOLA

Picha
Na Exipedito Mataruma, CAIRO SHIRIKISHO la kandanda barani Afrika CAF limeipangia klabu ya Yanga ya Tanzania kucheza na Segrada Esperance ya Angola (Pichani) mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga na Esperance zimeangukia kombe la Shirikisho baada ya kuondoshwa kwenye ligi ya mabingwa Afrika, Yanga ilifungwa mabao 2-1 jana usiku na Al Ahly ya Misri uwanja wa Borg Al Arab mjini Alexandria. Mechi za mchujo kombe la Shirikisho kuelekea kwenye makundi zinataraji kuchezwa kati Mei 6-7 na marudiano kuchezwa kati Mei 17-18, hiyo ni nafasi nyingine kwa Yanga kuandika rekodi kwani ikivuka hatua hiyo itaingia Robo fainali

FARID MUSSA ATIMKIA HISPANIA KUJARIBU BAHATI

Picha
Na Salum Fikiri Jr, TUNISIA Farid huyooo Malaga, Las Palmas -------------------------------------------------------- WINGA chipukizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Farid Mussa, kesho Ijumaa anatarajia kuondoka nchini hapa Tunisia kuelekea Hispania kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa. Farid atakuwa huko kwa takribani mwezi mmoja na atafanya majaribio katika timu za Malaga na Las Palmas zinazoshiriki Ligi Kuu ya nchini humu na atarejea jijini Dara es Salaam May 19 mwaka huu msimu wa ligi ukiwa umeisha. Farid amekuwa katika kiwango cha juu akiwa na klabu yake ya Azam na akawa miongoni mwa wachezaji walioifungia magoli timu hiyo ya bilionea Said Salim Awadh Bakhressa na familia yake ilipoiduwaza 2-1 Esperance ya Tunisia katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam Farid Mussa (Kulia) akichanja mbuga

YANGA KUANGUKIA MIKONONI KWA WAARABU

Picha
Na Prince Hoza, DAR E SALAAM YANGA SC ya Tanzania inaweza kuangukia tena mikononi mwa timu za waarabu endapo Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF litaamua kufanya hivyo leo. Yanga ambayo jana usiku iliondolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly ya Misri katika uwanja wa Borg Al Arab mjini Alexandria. Jumla Yanga imefungwa mabao 3-2, na kutolewa kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika, kwa maana hiyo Yanga imeangukia kombe la Shirikisho barani Afrika na inaweza kukutana tena na timu za uarabuni. Timu ambazo zinaweza kukutana na Yanga ni Kawkab Marakech ya Morocco, Mounana ya Gabon, Misr Makkassa ya Misri, Medeanna ya Ghana, FAR Rabbat ya Morocco, Esperance ya Tunisia, Sagrade Esperance ya Angola au Stade Gabesien ya Tunisia. Yanga vilevile inaweza kuangukia mikononi mwa timu za ES Sahel ya Tunisia, Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, Al Ahly Benghazi ya Libya, TP Mazembe ya DRC, El Merreikhy ya Sudan, MO Bejala ya Algeria

YANGA YAKARIBIA KUMREJESHA HAMISI KIIZA

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TAYARI jina la mshambuliaji wa Simba Hamisi Kiiza "Diego" limeshafika mikononi mwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga bilionea Yusuf Manji na muda wowote wanaweza kumasajili. Mahambuliaji huyo raia wa Uganda anaelekea kumaliza mkataba wake na amekuwa haelewani na kocha wake Mganda mwenzake Jackson Mayanja. Yanga wanataka kumpa kazi moja ya kusaidiana na Mzimbabwe Donald Ndombo Ngoma baada ya Mrundi Amissi Tambwe kuonekana kushuka kiwango katika siku za hivi karibuni. Lakini mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Sc Zacharia Hanspoppe yeye amesema Kiiza ni mali yao na hawana mpango wa kumwachia kwa sasa, Hanspoppe amedai mchezaji huyo ataendelea kukipiga Msimbazi hadi msimu utakapomalizika na wamepanga kumuongeza mkataba mwingine Hamisi Kiiza mwenye jezi namba tano mgongoni akikumbatiana na kocha wa Yanga Hans Pluijm, Kiiza anarudi Yanga msimu ujao

YANGA YAFA KISHUJAA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YAPIGWA 2-1 YAANGUKIA SHIRIKISHO

Picha
Na Exipedito Mataruma, ALEXANDRIA MABINGWA wa Tanzania bara Yanga Sc wameondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika bada ya kufungwa kishujaa mabao 2-1 na Al Ahly ya Misri mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa Borg Al Arab mjini Alexandria usiku ya Jumatano. Katika mchezo huo Yanga ilixheza vizuri muda wote na kulisakama lango la Al Ahly kiasi kwamba mwamuzi wa mchezo huo alipopuliza kipyenga kuashiria mpira umemalizika mashabiki wa Al Ahly walishangilia kama wametwaa ubingwa wa Afrika. Kwa sasa unaweza kutamka kuwa Yanga na Al Ahly ni kama wapinzani wa jadi katika soka la Afrika kutokana na ushindani ulioonyeshwa usiku huu, Al Ahly walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Hossam Ghaly. Bao lilipatikana kipindi cha pili dakika ya 52 baada ya kuunganisha kwa kichwa kona ya Ahmed Fathi, Yanga walitulia na kucheza soka la kitabuni na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia mshambuliaji wake Mzimbabwr Donald Ngoma kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Juma Abdul.

BUNDI AENDELEA KULIA MSIMBAZI, HASSAN KESSY ATUPIWA VIRAGO, BANDA NAYE ASUSA

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM BAADA ya juzi kutangaza kujitoa kwenye kikosi cha Simba, beki Hassan Ramadhan Kessy ametupiwa virago vyake na uongozi wa Simba leo huku beki mwenzake wa kati Abdi Banda akijifukuzisha mwenyewe. Kamati ya utendaji ya Simba iliketi leo makao makuu ya klabu mtaa wavMsimbazi ambapo ilipitia suala la Kessy na kuona mchezaji huyo alimfanyia rafu mbaya ya makusudi mshambuliaji wa Toto Africans Edward Christopher na kupewa kadi nyekundubiliyoigharimu timu. Kessy amekuwa mtovu wa nidhamu na hii ni mara ya pili, mara ya kwanza Kessy alijitoa kambini akishinikiza alipwe fedha zake wakati timu ikiwa katika maandalizi ya mchezo wa ligi msimu uliopita. Hajji Manara ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Habari wa Simba amefafanua kuwa klabu ya Simba imemsimamisha Kessy kucheza mechi tano, ina maana Kessy atakosa mechi zote za msimu. Naye kocha wa Simba Jackson Mayanja amewataka mashabiki wa Simba kutokata tamaa kwani bado wanayo nafasi ya kutwaa ubingwa, pia ameelezea kuj

ANAYEKUMBUKWA LEO: SAIDI MWAMBA "KIZOTA". MSHAMBULIAJI ALIYETAMBA YANGA NA SIMBA

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM MIAKA ya mwishoni na 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90 Saidi Nassoro Yusuph Mwamba ama Kizota alichomoza kwenye soka na kutamba katika vilabu vya Yanga, Simba na timu ya taifa, Taifa Stars. Kizota alikuwa na uwezo mkubwa wa kusakata kandanda na alisifika kwa magoli ya vichwa, kuna wakati mchezaji huyo alikuwa akicheza kama mshambuliaji na wakati mwingine alicheza kama beki wa kati. Amewahi kupata heshima akiwa na Yanga ambayo itamfanya asisahaulike kamwe, kwa sasa ni marehemu na alifariki Februali 11 mwaka 2007 kwa ajali ya gari maeneo ya Temeke Vetenary. Kizota alikuwa anatoka uwanja wa Taifa kuangalia pambano la kombe la Washindi barani Afrika (Sasa Shirikisho) kati ya Simba na Chapungu ya Msumbiji, akiwa njiani aligongwa na gari na kufariki papo hapo. Kona yetu imeanza kumkumbuka Kizota ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tabora aliyepata kuzichezea Tindo ya Tabora na CDA ya Dodoma, je wiki ijayo tutakuja na nani? ni jambo la kusubiri Saidi Mwamba "

NAFASI KWA YANGA USIKU HUU NA AL AHLY

Picha
Na Exipedito Mataruma,  ALEXANDRIA WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga Sc wanashuka uwanjani muda si mrefu leo hii kukwaruzana na Al Ahly ya Misri mchezo wa marudiano uwanja wa Borg Al Arab mjini Alexandria Misri. Katika mchezo wa leo Yanga wanahitaji ushindi wa aina yoyote ama sare inayoanzia mabao 2-2 ili isonge mbele, Al Ahly wanahitaji sare isiyo na .mabao ili wavuke hatua ya makundi. Timu hizo zilifungana mabao 1-1 mjini Dar es Salaam zilipokutana juma lililopita, kocha mkuu wa Yanga Mholanzi Hans Van der Pluijm ameelezea mchezo huo na kusema vijana wake wana kila sababu ya kuibuka na ushindi. Nahodha wa Yanga Nadir Haroub maarufu Cannavaro amewatoa wasiwasi wapenzi wa Yanga na Watanzania kwa ujumla kuwa ni lazima wapate ushindi hii leo Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi

ESPERANCE YAIFURUSHA AZAM KOMBE LA SHIRIKISHO

Picha
Na Salum Fikiri Jr, TUNISIA AZAM FC imeaga michuano ya kombe la Shirikisho la soka barani Afrika  baada ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Esperance katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 bora usiku wa leo Uwanja wa Olympique de Rades mjini Tunis. Matokeo hayo yanaifanya Azam Fc inayomilikiwa na bilionea Said Salim Bakhressa na familia yake itolewe kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam. Ikicheza mchezo wa kujihami kwa kutumia viubgo watano na mshambuliaji mmoja tu, Nahodha John Raphael Bocco, Azam ilifanikiwa kuwabana vizuri wenyeji dakika 45 za kwanza na kumaliza bila kuruhusu bao. Timu hiyo ya kocha Muingereza Stewart Hall ilikuwa ikifanya mashambulizi ya kushitukiza kwa kumpelekea mipira mirefu Bocco, ambaye hata hivyo alidhibitiwa, ukuta wa Azam ukifanya kazi ya ziada ya kuzuia mashambulizi ya Esperance muda mwingi wa kipindi hicho huku kipa wake Aishi Manula akiokoa michomo zaidi ya minne ya hatari langoni mwake. Hata hivyo, bao la mapema kipindi cha

YANGA WAFANYA MAZOEZI MAKALI MCHANA NA USIKU, TAYARI KABISA KUWAMALIZA WAARABU KESHO

Picha
Na Exipedito Mataruma, MISRI WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga Sc, wanaendelea kujifua vikali katika uwanja wataochezea mechi yao ya marudiano na Al Ahly ya hapa Misri kesho. Kocha wa Yanga Mholanzi Hans Van der Pluijm ameiambia Mambo Uwanjani kwamba vijana wake wanafanya mazoezi makali ya kuwamaliza kabisa Waarabu hiyo kesho. Yanga inahitaji sare ya mabao zaidi ya moja ama mawili ili iweze kusonga mbele lakini amedai hawezi kupoteza mchezo huo. Timu hizo zinarudiana kesho baada ya mchezo wa kwanza kutoka sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam, Al Ahly itakuwa na kazi nyepesi kwani tayari ina bao la ugenini ililolipata Dar es Salaam. Endapo itatokea Yanga kushinda mchezo huo itakuwa imeingia hatua ya makundi, na kama bahati mbaya imetolewa itaangukia kombe la shirikisho barani Afrika Yanga wakiwa mazoezini

AZAM TV KURUSHA LIVE MECHI YA AZAM NA ESPERANCE SAA 3 USIKU

Picha
Na Salum Fikiri Jr, TUNISIA MPAMBANO unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini Tanzania kati ya Azam na Esperance sasa utarushwa live na Azam Tv. Mpaka sasa ni asilimia 100 kuwa mechi kati ya Azam FC na Esperance ya Tunisia itakayofanyika leo saa 3.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, itarushwa moja kwa moja kupitia Kingamuzi cha Azam TV (Azam TWO). Hivyo mashabiki wa Azam FC pamoja na Watanzania kwa ujumla kaeni mkao wa kula kutazama mpambano huo, kama ulikuwa ujalipia Kingamuzi cha Azam TV, tafadhali lipia haraka ili uweze kushuhudia mchezo huo. Kama hiyo haitoshi, ukurasa huu utakuwa ukikupa matokeo 'live' kwa kila kinachojiri ndani ya Uwanja wa Olympique de Rades. Azam wakijifua leo katika uwanja wa Olympique de Rades Wachezaji wa Azam wakiendelea na mazoezi