Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2017

NGOMA AOTA MBAWA CHALENJI

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Ndoto za mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, Donald Ngoma kucheza katika michuano ya kombe la Chalenji sasa imeota mbawa kufuatia nchi yake ya Zimbabwe kujitoa katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba tatu mwaka huu nchini Kenya. Taarifa kutoka nchini Zimbabwe jana zinasema wameamua kujitoa kwa sababu hali ya usalama nchini Kenya si nzuri hivyo wao wakiwa kama timu mwalikwa wameamua kujitoa. Chama cha soka Zimbabwe (ZIFA) kimesema kwamba usalama nchini Kenya ni mdogo kufuatia uchaguzi wao ambao umeleta mzozo kati ya Rais Uhuru Kenyatta na mshindani wake Raila Odinga. Zimbabwe ilipangwa pamoja na Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini na Burundi hivyo kujitoa kwake kunasababisha timu zibakie nne kwenye kundi lake, Watanzania walitarajia kumtazama Ngoma kupitia michuano hiyo lakini ameota mbawa Kikosi cha Zimbabwe kimejitoa Chalenji

Lipuli yaweka ngumu kwa Asante Kwasi kwenda Simba

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Uongozi wa timu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa, umemzuia kiungo wake Mghana, Asante Kwasi kujiunga na vinara wa Ligi Kuu bara, Simba SC kama ilivyodaiwa hivi karibuni. Simba iimteka Kwasi kwa masaa manne ili kuteta naye ikitaka kumpa mkataba lakini Lipuli wameshituka na kudai mchezaji huyo haendi kokote na bado ana mkataba wa kuitumikia timu yao. Asante Kwasi alimtungua kipa wa Simba, Aishi Manula kwa shuti la mbali na kufanya matokeo yawe 1-1 mchezo wa Ligi Kuu bara uliofanyika Jumapili iliyopita uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Simba na Yanga zimenogewa na mchezaji huyo aliyejiunga na Lipuli mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mbao FC ya jijini Mwanza. Asante Kwasi anatakiwa na Simba

Kill Stars kupaa zao usiku wa leo

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars kinatarajia kusafiri leo usiku kuelekea Kenya tayari kwa kushiriki michuano ya mataifa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Chalenji, kikosi hicho kilikuwa kikijifua chini ya kocha Amme Ninje na jana kimeongeza nyota wengine watatu ili kukipa makali na ikiwezekana kurejea na kikombe. Kocha wa kikosi hicho ameamua kuongeza nyota wengine watatu na kufanya jumla ya wachezaji walioteuliwa kujiunga na kikosi hicho kufikia 22, waliojumuhishwa jana ni kipa wa Yanga SC, Ramadhan Kabwili, Aman Kiata wa Nakuru All Stars ya Kenya na mshambuliaji chipukizi wa Azam FC, Yahaya Yazed. Kill Stars imepamgwa pamoja na wenyeji Kenya, Libya, Zanzibar na Rwanda ambapo michuano hiyo inatazamiwa kuanza kutimua vumbi Jumapili ijayo na viwanja viwili vimepangwa kutumika Wachezaji wa Kill Stars wakijifua kwa mara ya mwisho kabla ya safari

DEGE LA TP MAZEMBE LAZUIWA KUTUA DRC

Picha
Rais wa jamuhuri wa kidemokrasia ya Congo, (DRC) Joseph Kabila amezuia ndege iliyobeba wachezaji wa TP Mazembe ambao walikuwa wakitokea nchini Afrika Kusini walikotoka kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika. Kabila ameingiza masuala ya siasa, baada ya kuzuia ndege inayomilikiwa na timu hiyo isitue DRC na badala yake ikatua Ndola, Zambia na baadaye kuchukua usafiri wa basi na kuelekea Lubumbashi. Kabila amekuwa na uhasama wa kisiasa na mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Katanga na pia aligombea urais wa DRC kisa kilichopelekea ashikiliwe na baadaye kukimbia nchi Wachezaji wa TP Mazembe wakishuka kutoka kwenye ndege yao iliyozuiliwa kutua DRC

Waziri Mwakyembe azuia Simba kukabidhiwa kwa mwekezaji Jumapili

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Waziri wa habari, michezo, sanaa na utamaduni, Dk Harrison Mwakyembe, amesema kwa mujibu wa sheria za jamuhuri ya muungano wa Tanzania, hairuhusu klabu yoyote ya michezo inayomilikiwa na wanachama kuuza Hisa kwa asilimia zaidi ya 49. Mwakyembe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na chombo kimoja cha habari ambapo amefafanua kuwa klabu inayomilikiwa na mtu binafsi ndiyo inaruhusiwa kuuza hisa zaidi ya 49 na kumilikiwa na mwekezaji. Kwa maana hiyo Mwakyembe amezuia mchakato wa kumkabidhi mwekezaji aliyeshinda zabuni ya kununua Hisa asilimia 50 za klabu ya Simba, ambapo Jumapili ya Desemba 3 itamtambulisha kwa wanachama na kupewa klabu aiendeshe. Waziri Mwakyembe amezuia Simba isiuzwe kwa asilimia 50

ZFA YAKANUSHA KUANIKA RATIBA YA KOMBE LA MAPINDUZI

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Chama cha soka Zanzibar, (ZFA) imesema hawaitambui kabisa ratiba iliyotolewa jana ya kombe la Mapinduzi ambayo inasema michuano hiyo itaanza Desemba 30 huku timu 10 zikitajwa katika makundi mawili, Katibu mkuu wa ZFA ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati ya mashindano hayo, Sheikh Khamis Abdallah,  amesema ile ratiba iliyotolewa jana na kusambazwa mirandaoni ni feki. Sheikh Abdallah amedai ni kweli michuano hiyo itashirikisha timu 10 na wameialika URA ya Uganda lakini ratiba iliyotangazwa si yao ometengenezwa na watu wachache wanaotaka kuharibu mambo yao, pia katika mashindano hayo timu ya Shaba ya Pemba hawajaialika isipokuwa kwenye ratiba feki imejumuhishwa. Ratiba hiyo iliyotolewa jana ilisema kuwa kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza rasmi visiwani Zanzibar kuanzia Desemba 30 mwaka huu na kumalizika Januari mwakani, ambapo jumla ya timu 10 zinarajiwa kushiriki huku timu moja ikiwa ni mwalikwa. Chama cha soka Zanzibar (ZFA) kimezitaja timu za URA

Himid Mao awa mchezaji bora wa mwezi, Azam FC

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kiungo Himid Mao Mkami "Ninja" ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi inayotolewa na klabu yake ya Azam FC, kiungo huyo amewashinda nyota wenzake watatu alioshindanishwa nao kupitia ukurasa wa facebook wa klabu hiyo, Ninja ambaye pia ni nahodha msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars atapewa zawadi yake ya uchezaji bora. Nahodha wa Azam FC, Himid Mao, anakuwa mchezaji wa tatu msimu huu kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Azam FC (NMB Player Of The Month) baada ya Yakubu Mohammed kufanya hivyo Agosti-Septemba na mshambuliaji Mbaraka Yusuph aliyeibeba Septemba-Oktoba. Tuzo hiyo inadhaminiwa na Wadhamini wakuu wa Azam FC, Benki ya NMB, ambayo kwa sasa ndio bora kabisa Tanzania ikikuhakikishia usalama wa fedha zako na ikiwa na matawi mengi yaliyosambaa kote hapa nchini Himid Mao awa mchezaji bora wa mwezi Azam FC

Uganda ipo kamili kwa Chalenji, Okwi atemwa

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, Moses Basena, ameita kikosi cha wachezaji 24 watakaochujwa hadi kubakia 22 watakaosafiri Jumamosi ijayo kuelekea Nairobi Kenya tayari kwa kushiriki michuano ya kombe la Chalenji inayoanza kutimua vumbi Desemba 3 mwaka huu. Katika kikosi kilichotangazwa na Basena ambaye amewahi kuinoa klabu ya Simba ya Tanzania, amemtema kinara wa mabao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Emmanuel Okwi anayeichezea Simba lakini akamjumuhisha beki kisiki anayekipiga Simba, Jjuuko Murushid, Okwi amefunga mabao manane huku klabu yake ikiwa kileleni. Michuano ya chalenji itafanyika mwaka huu baada ya kukosekana kwa muda wa miaka miwili na Uganda ndio mabingwa watetezi, hivyo Basena amekiandaa vema kikosi chake Emmanuel Okwo hayupo The Cranes

KOMBE LA MAPINDUZI KUANZA DESEMBA 30, SIMBA NA YANGA NDANI

Picha
Na Mwandishi Wetu. Zanzibar Michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza rasmi visiwani Zanzibar kuanzia Desemba 30 mwaka huu na kumalizika Januari mwakani, ambapo jumla ya timu 10 zinarajiwa kushiriki huku timu moja ikiwa ni mwalikwa. Chama cha soka Zanzibar (ZFA) kimezitaja timu za URA ya Uganda  ambayo imepangwa kwenye kundi A lenye timu za Simba SC, Azam FC, Jamhuri ya Pemba, Taifa Jang' ombe na URA ya Uganda wakati kundi B lina timu za Yanga SC, JKU, Zimamoto, Mlandege na Shaba ya Pemba. Azam FC ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kuifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa fainali, michuano hiyo kwa sasa imekamata chti katika ukanda huu Simba na Yanga zitashiriki kombe la Mapinduzi

Kapuya asema Simba ikizubaa tu, Yanga bingwaa VPL

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Aliyekuwa waziri wa elimu, utamaduni na michezo katika awamu ya tatu ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Profesa Juma Othman Kapuya, ambaye ni mpenzi na mwanachama wa klabu ya Simba, amesema kama timu yake anayoishabikia itazubaa kama ilivyokuwa misimu iliyopita, watani zao Yanga SC watabeba tena ndoo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Kapuya aliyasema hayo juzi Jumapili wakati Simba ilipocheza na Lipuli ya Iringa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba ilitoshana nguvu na Lipuli kwa kufungana bao 1-1 na alipoitazama vema Simba,  Kapuya akatikisa kichwa na kutamka Simba ikizubaa tu, Yanga bingwa. Waziri huyo hivi karibuni alitembelea makao makuu ya klabu ya Yanga na kupokelewa na katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ambapo alitembezwa hadi maktaba na kuonyesha makombe mbalimbali iliyotwaa klabu hiyo. Kapuya alikabidhiwa kombe la Ligi Kuu ya Bara ambalo Yanga imelitwaa mara tatu mfululizo, mdau huyo mkubwa wa soka nch

Kevin Sabato atia mchanga kitumbua cha Azam, usiku huu

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Klabu bingwa Afrika mashariki kati , Azam FC usiku huu imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliomalizika usiku huu katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mchezo ulikuwa mgumu na mkali huku mashambulizi yakielekezwa kila lango, hadi mapumziko timu zote zilikuwa hazijafungana hata bao, kipindi cha pili Azam walianza kulishambulia lango la Mtibwa na kufanikiwa kupata kona iliyoleta sekeseke langoni mwa Mtibwa. Dakika ya 56 Azam FC waliandika bao la uongozi lililofungwa na mchezaji wake wa kimataifa raia wa Ghana, Enock Atta Agyei aliyeunganisha pasi ya Mbaraka Yusuf, lakini katika dakika ya 75 Mtibwa Sugar walisawazisha goli hilo kupitia kwa Kevin Sabato "Kiduku". Kwa matokeo hayo Azam imefikisha pointi 23 ikiendelea kukaa katika nafasi ya pili huku Simba ikiendelea kuongoza ligi hiyo na Mtibwa wakishuka hadi

Mtangazaji Clouds ampeleka Singano Yanga

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mtangazaji wa kipindi cha michezo cha kituo cha matangazo cha Clouds Fm, Issa Maeda amelitaka benchi la ufundi la mabingwa wa soka nchini, Yanga SC kumsajili kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano Messi ili aweze kuisaidia timu hiyo katika kutetea taji lao pamoja na uwakilishi wa nchi mwakani. Maeda aliyesema hayo juzi katika kipindi chake cha michezo kinachoanzia saa 3:00 hadi saa 4:00 usiku, mtangazaji huyo amedai Yanga inahitaji winga mwenye kasi kama ilivyokuwa kwa Simon Msuva ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa Morocco katika klabu ya Difaa El Jadida. Singano anafaa kuisaidia Yanga hivyo uongozi wa Yanga unapaswa kumtazama kwani kwa sasa winga huyo aliyelelewa na kukuzwa na timu ya Bom Bom ya Kariakoo kisha akajiunga na Simba SC, anaichezea Azam FC lakini amekuwa hapati nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza Ramadhan Singano "Messi" amepigiwa chapuo aende Yanga na mtamgazaji wa Clouds

KISPOTI

Picha
NENO LA HANSPOPPE KWA KAPOMBE, NDIO MANENO YA VIONGOZI WETU. Na Prince Hoza HIVI karibuni mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe aliibuka kwenye vyombo vya habari na kusema mchezaji wao Shomari Kapombe achague moja kati ya kucheza au kuondoka. Hanspoppe amedai klabu ya Simba imechoka kumlipa mshahara mchezaji asiyecheza hivyo njia nzuri iliyomchagulia ni moja tu, kucheza au kuondoka, kiongozi huyo aliendelea kusema akidai Kapombe ameshapona majeraha yake yaliyokuwa yakimsumbua. Kapombe alikuwa majeruhi  na tayari alishapona hivyo anatakiwa aanze kucheza, Hanspoppe alitanabaisha kuwa daktari wa klabu ya Simba, Yassin Gembe alianika ukweli kuwa Kapombe amepona ila hataki kucheza, Simba ilimsajili Kapombe mwanzoni mwa msimu huu akitokea Azam FC ambapo mkataba ulimalizika, na alisaini Simba kwa miaka miwili. Moja kati ya usajili uiofurahiwa na Wanasimba wengi ambao waliamini ujio wake ungeleta faraja, Simba iliamua kumtema Mkongoman, Janviel Besala Bokun

Yohana Mkomola amfuata Kabwili Yanga

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana ya chini wa umri wa miaka 23, Yohana Mkomola ambaye pia alikuwemo kwenye kikosi cha Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za mataifa ya Afrika zilizofanyika Gabon mwaka huu. Mkomola amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga jana timu ambayo pia anaichezea kinda mwenzake Ramadhan Kabwili. Mkomola alienda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa Tunisia katika klabu ya Esperance, anajiunga na Yanga timu ambayo jana ilimsainisha Mkongoman, Fiston Kayembe kwa mkataba wa miaka miwili. Hussein Nyika ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usajili amesema Yanga bado inaendelea kuimarisha kikosi kwakuwa imeandamwa na majeruhi wengi. Yohana Mkomola amejiunga na Yanga SC

Simba nao kama Yanga, washikwa na 'Wanapaluhengo'

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC nao kama Yanga, baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare na 'Wanapaluhengo', Lipuli FC ya Iringa ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu bara uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Simba walikuwa wa kwanza kujipatia bao la uongozi lililofungwa na kiungo wake mkongwe Mwinyi Kazimoto lakini Lipuli wakasawazisha kupitia Asante Kwasi na kufanya mchezo huo kuamuliwa kwa sare. Sare hiyo inafanana na ile ya watani wao Yanga ambao jana walilazimishwa na Prisons ya Mbeya ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Simba sasa imefikisha pointi 23 ikiendelea kukaa kileleni ikiwa imecheza mechi 11, kesho Azam FC itakuwa na kazi nyepesi ya kukamata kiti cha uongozi itakapoialika Mtibwa Sugar katika uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex uliopo Chamazi, Azam ina pointi 22 na ikishinda tu itakaa kileleni Mwinyi Kazimoto ameinusuru Simba leo

IBRAHIM CLASS ATETEA MKANDA WA DUNIA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Class au King Class, jana mchana ameitoa kimasomaso Tanzania baada ya kufanikiwa kuutetea mkanda wake wa dunia wa Global Boxing Council (GBC) kwakumchapa kwa pointi mshindani wake Cosilia kutoka Afrika Kusini katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Class ambaye alishinda ubingwa huo nchini Ujerumani katika mji wa Berlin kwa kumshinda bondia wa Panama, aliweza kuonyesha kiwango kizuri na kuibuka na ushindi aliopewa bila shaka na majaji, pambano hilo liliudhuriwa na Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii, Mhe Dk Harrison Mwakyembe ambaye hata hivyo alimsifu. Class anakuwa bondia pekee nchini kwa mwaka huu kuitoa kimasomaso Tanzania kutokana na ushindi wake huo ambao unakuwa wa pili kwa ngazi ya mashindano, pambano lake la kwanza lilikuwa Agosti mwaka huu ambalo lilimpa ubingwa wa mkanda huo Ibrahim Class ametetea mkanda wake jana

YANGA YANOGEWA NA WAKONGOMAN, YAMPA MIAKA MIWILI KAYEMBE

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mlinzi wa kati toka nchini Congo ( DRC )Finston Festo Kayembe asajiliwa na Yanga SC baada ya majaribio ya muda mrefu! . Yanga imeanza kusuka kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi, ASFC na klabu bingwa Afrika. Kayembe amesaini kandarasi ya miaka miwili. Kayembe alikuwa na kikosi hicho kwa kipindi kirefu na kiwango chake kimeweza kuwashawishi viongozi wa klabu hiyo pamoja na wanachama, wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo, kwa usajili huo wa Kayembe ambaye ni beki wa kati, unaondoa uvumi urejeo wa Vincent Bossou raia wa Togo ambaye alitajwa kurejea. Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Dissmas Ten, amesema Yanga imemsajili beki huyo ili kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwani wao walikuwa na wachezaji sita. Kuhusu wachezaji wa ndani, Ten amedai hilo kwa sasa ni jukumu la kocha na mambo yakiwa tayari atawajulisha Finston Kayembe amesaini miaka miwili Yanga

TP MAZEMBE WABEBA NDOO YA SHIRIKISHO AFRIKA

Picha
Timu ya soka ya TP Mazembe ya jamuhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo (DRC) jana usiku imetawazwa kuwa mabingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika,baada ya kulazimisha sare tasa 0-0 ya ugenini dhidi ya Supersport ya Afrika Kusini katika uwanja wa Lucas Moripe mjini Tshwane. TP Mazembe wanakuwa mabingwa kufuatia ushindi wake wa mabao 2-1 ilioupata mjini Lubumbashi wiki iliyopita, huo unakuwa ubingwa wa pili mfululizo kwa timu hiyo ambapo pia ni rekodi nyingine kwa kocha wake Pamphile Mihayo ambapo sasa anakuwa kocha wa 10 Mwafrika kubeba taji hilo. Ubingwa huo wa pili mfululizo kwa TP Mazembe kunarejesha heshima ya timu hiyo inayoonekana kupotea hasa baada ya kuondolewa katika hatua za mwanzoni za Ligi ya Mabingwa barani Afrika TP Mazembe wametetea ubingwa wa Shirikisho Afrika

Simba kuwateketeza Lipuli leo

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, jioni ya leo inawakaribisha "Wanapaluhengo", Lipuli FC kutoka mkoani Iringa, mchezo wa Ligi Kuu bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Simba ambao ni vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 22 sawa na Azam isipokuwa wana mabao mengi ya kufunga, watajihakikishia kukaa kileleni leo endapo watailaza timu hiyo inayonolewa na mchezaji na kocha wa zamani wa Simba, Seleman Matola. Hata hivyo Lipuli inajivunia kwa kikosi bora na Simba inatakiwa isiwadharau Lipuli kwani lolote linaweza kutokea. Simba itaiteketeza Lipuli leo

NDEMLA AFUZU MAJARIBIO SWEDEN

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, Said Hamisi Juma (Ndemla) amefuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweden katika klabu ya AFC Eskilistuna ambayo pia anaichezea Mtanzania mwingine Thomas Ulimwengu ambaye kwa sasa ni majeruhi. Ndemla aliondoka majuma mawili yaliyopita kuelekea Sweden na taarifa zilizotolewa na Klabu hiyo aliyofanyia majaribio zinasema amefuzu, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara amefurahishwa na kufuzu huko kwa Ndemla na amesema klabu yao haitasita kumuuza endapo wataafikiana na Eskilistuna. Manara amesema Simba haina kawaida ya kuwazuia nyota wake wasicheze Ughaibuni hivyo watafanya biashara endapo tu wataafikiana, kesho uongozi wa Simba unakutana kuzungumzia mambo mbalimbali likiwemo hilo ka Ndemla, nyota huyo anatazamiwa kurejea nchini Jumatatu. Said Ndemla (Kushoto) akiwa Sweden, amefuzu majaribio

Yanga yakwama kwa Prisons, Simba washindwe wenyewe

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Licha ya kucheza pungufu, vijana wa Tanzania Prisons jioni ya leo wamefanikiwa kuwabana mbavu wakongwe Yanga SC na kutoka nao sare ya kufungana bao 1-1 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dares Salaam, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Endapo Yanga ingeibuka na ushindi leo ingefanikiwa kukamata kiti cha usukani wa ligi kwani ingefikisha pointi 23 ikiziacha nyuma Simba na Azam zenye pointi 22 kila moja, hata hivyo sare hiyo imewapa pointi moja sasa wamefikisha pointi 21 wakiendelea kukaa katika nafasi yao ya tatu. Prisons walikuwa wa kwanza kupata bao la uongozi likifungwa kipindi cha kwanza dakika ya 10 na mshambuliaji wake Eliud Mpepo lakini Yanga wakachomoa kupitia Raphale Daudi. Prisons walionekana kuelemewa zaidi na kupelekea wachezaji wake kujiangusha hovyo na kupoteza muda, Ligi hiyo iliendelea katika viwanja vingine tofauti ambapo Ruvu Shooting ilishinda 2-1 dhidi ya Majimaji ya Songea uwanja wa Mabatini Mla

Ni zamu ya Yanga kukaa kileleni leo

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa wa soka nchini, Yanga SC jioni ya leo wana nafasi kubwa ya kurejea kileleni endapo wataifunga Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaofanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Na kwa bahati nzuri Yanga leo itakuwa imetimia hasa baada ya kurejea kwa mastaa wake Thabani Kamusoko na Amissi Tambwe ambao walikuwa majeruhi. Lakini pia kinara wake wa magoli, Obrey Chirwa pamoja na kiungo mshambuliaji mbunifu Ibrahim Ajibu watakuwa chachu ya ushindi katika mchezo huo. Prisons nao siyo wa kubeza kwani wana washambuliaji wao hatari Mohamed Rashid na Eliuta Mpepo ila wanaweza kutulizwa na Kevin Yondan na Vincent Andrew. Yanga ina pointi 20 ikiwa imecheza mechi 10 na leo utakuwa mchezo wake wa 11 na kama itashinda itafikisha pointi 23 ambapo zitakuwa nyingi zikiwaacha nyuma Simba na Azam zenye pointi 22 kila moja ila zenyewe zitazidiwa mchezo mmoja. Simba wao watacheza kesho na Lipuli katika uwanja wa U

Ndanda FC yalazimishwa sare nyumbani

Picha
Na Albert Babu. Dar es Salaam Timu ya Ndanda FC ya Mtwara jioni ya leo imeshindwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Nangwanda Sijaona, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Njombe Njombe FC ya mkoani Njombe, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Hadi timu hizo zinaenda kupumzika zilikuwa hazijafungana yaani 0-0, lakini kipindi cha pili kilionekana kuwa kizuri kwa wageni Njombe Mji ambao wananolewa na Mrage Kabange ambapo walikuwa wakilishambulia lango la Ndanda kama nyuki, Ndanda ilirangulia kupata bao kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa kistadi na William Lucian "Gallas" na Njombe wakasawazisha baada ya kufanya shambulizi kali langoni kwa Ndanda na kuzama kimiani. Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumamosi ambapo Yanga SC wataialika Prisons uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Mechi nyingine ni Singida United vs Mbeya City, Namfua, Mbao FC vs Mwadui FC, CCM Kirumba, Mwanza, Kagera Sugar vs Stand United, Kaitaba Stadium. Nyingine ni Ruvu Shooting vs Ma

Dida mbioni kurejea Simba

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kuna uwezekano mkubwa klabu ya Simba ikamrejesha aliyekuwa kipa wake wa zamani, Deogratus Munishi "Dida" ambaye kwa sasa anakipiga na klabu ya daraja la pili ya Pretoria University ya nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa ripoti ya kocha wa vinara hao wa Ligi Kuu bara, Mcameroon, Joseph Omog inaonyesha kwamba wanatakiwa wachezaji watatu muhimu ambapo mmoja wa kimataifa anayecheza nafasi ya ushambuliaji na mwingine kipa, Omog pia anamuhitaji kiungo mshambuliaji mzawa ambao mipango ya kuwanasa imeanza. Taarifa ambazo Mambo Uwanjani imezipata na wala hazina shaka yoyote zinasema kipa Dida ambaye amewahi kuichezea Simba miaka kadhaa iliyopita kabla hajaenda Mtibwa Sugar kisha Azam ambapo baadaye akajiunga na Yanga na kung' ara nayo kisha msimu uliopita kutimkia Afrika Kusini anafaa katika kikosi cha Simba ambao kwa sasa wanahitaji kipa mwingine wa kumpa changamoto Aishi Manula kufuatia Said Mohamed Nduda kuumia. Hata hivyo alipoulizwa msemaji

Staa Wetu:

Picha
MRISHO KHALFAN NGASA. ANAPOTEA AU ANARUDI? Na Prince Hoza NIMEMUONA kwenye mechi zote mbili ambazo timu yake ya Mbeya City ilipocheza na miamba Simba na Yanga, mechi ambazo zilifuatana, ama kweli Mrisho Ngasa alicheza vizuri ingawa kikosi chake kilipoteza michezo yote hiyo. Mbeya City ikicheza uwanja wa nyumbani wa Sokoine dhidi ya Simba SC iliyosheheni kikosi cha Shilingi Bilioni 1.3 za Kitanzania na kuonyesha ushindani mkubwa lakini Shiza Kichuya aliweza kuwalaza kwa goli lake la utatanishi ambalo inadaiwa lilikuwa la kuotea, katika mchezo huo Simba ilishinda bao 1-0. Vijana hao wa Mbeya City walisafiri hadi Dar es Salaam kuwafuata mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara, Yanga SC mchezo uliofanyika uwanja wa Uhuru, Mbeya City ilifungwa mabao 5-0 ambayo yamezua mshangao mkubwa kwa mashabiki wa soka, wengi hawakuamini kipigo hicho hasa kwakuwa wanaifahamu fika Mbeya City. Mbeya City ni moja kati ya timu zilizokuwa zikionyesha ushindani mkubwa hasa zinapokutana na Simba na Yanga, si ra

Tanzania yazidi kutota FIFA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Tanzania imeendelea kuporomoka kwenye viwango vya ubora wa kandanda duniani vinavyotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA), Shirikisho hilo jana lilitangaza viwango vipya ambapo Tanzania imezidi kushuka kutoka nafasi ya 136 hadi ya 142 ikionekana kudondoka kwa nafasi sita zaidi. Licha ya kulazimisha sare ya ugenini dhidi ya Benin ya kufungana bao 1-1 lakini bado haikuweza kuishawishi FIFA kuipandisha juu Tanzania, katika mchezo huo Tanzania ilicheza vizuri na kuweza kuwabana wenyeji ambao walitangulia kupata bao la kuongoza ambalo lilikuwa la utatanishi. Goli hilo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti kipindi cha kwanza lakini mwamuzi wa mchezo huo ni kama aliwapa penalti hiyo kwa dhumuni la kuibeba Benin kwani mchezaji wa Benin ndiye aliyeunawa mpira lakini penalti ikaelekezwa langoni kwa Tanzania. Elius Maguri aliisawazishia Tanzania na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare, katika viwango hivyo, Senegar imekuwa kinara kwa hapa Afrika na Ug

SIMBA NA LIPULI YARUDISHWA UHURU

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya vinara Simba SC na Lipuli FC ya Iringa uliokuwa ufanyike katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi siku ya Jumapili, sasa umerudishwa katika uwanja wa Uhuru. Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema mchezo huo utapigwa uwanja wa Uhuru kwakuwa wamiliki wa uwanja huo serikali haitautumia siku hiyo kwani matumizi ni yanaishia Jumamosi tu ambapo mchezo kati ya Yanga na Prisons utachezewa Azam Complex. Simba wamepokea kwa mikono miwili mchezo huo kurudishwa uwanja Uhuru wakiamini ndio uwanja wao wa nyumbani na utawapa matokeo mazuri, akizungumza jioni ya leo, Haji Manara ambaye ni msemaji wa vinara hao amesema ni uamuzi mzuri kurudisha mechi hiyo Uhuru Simba SC sasa watacheza mechi na Lipuli uwanja wa Uhuru

Ndanda na Njombe Mji FC kazi ipo kesho Nangwanda Sijaona

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara itaendelea kesho kwa mchezo mmoja ambapo Ndanda FC itawakaribisha Njombe Mji FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi ambapo Yanga wataialika Prisons uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Mechi nyingine ni Singida United vs Mbeya City, Namfua, Mbao FC vs Mwadui FC, CCM Kirumba, Mwanza, Kagera Sugar vs Stand United, Kaitaba Stadium. mechi nyingine Ruvu Shooting vs Majimaji FC, Mabatini Stadium, Mlandizi na Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Simba na Lipuli uwanja wa Uhuru Wachezaji wa Ndanda wakijifua kwa ajili ya mchezo wao na Njombe Mji

Prisons yajivunia washambuliaji wake, Yanga itakufa mapemaa

Picha
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya Timu ya soka ya Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya, imejiweka mguu sawa kuumana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga SC Jumamosi ijayo katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Kocha mkuu wa timu hiyo Mohamed Abdallah amesema hana presha kabisa kuelekea mchezo huo kwani kikosi chake kina washambuliaji wake hatari ambao ni Mohamed Rashid na Eliuta Mpepo ambapo wanaweza kuiua Yanga mapema. Kocha huyo ametoa ufafanuzi juu ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba katika uwanja wa Sokoine Mbeya ambapo amedai wamefungwa kimchezo lakini Simba ilitegemea bahati zaidi ila watawanyoosha Yanga kwani haiwatishi kabisa na amewataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia soka safi toka kwa vijana wake ambao wanakamata nafasi ya sita. Washambuliaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid na Eliuta Mpepo

Azam FC yamnasa Mghana mwingine hatari

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Baada ya kuachana na straika wake Yahaya Mohamed ambaye ni raia wa Ghana, uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unayofuraha kuwajulisha kuwa imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji Bernard Arthur, akitokea Liberty Professional ya Ghana. Taarifa kamili zinasema kwamba Mghana huyo amepewa mkataba wa miaka miwili ingawa msemaji wa klabu hiyo yenye maskani yake Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Jaffar Idd Maganga amekataa kuzungumzia usajili huo na kudai kesho ndio wataanika kila kitu. Azam inaonekana imenogewa na wachezaji wanaotokea Ghana, kwani mbali na kuachana na Mghana, Yahaya Mohamed ambaye ameshindwa kuushawishi uongozi wa timu hiyo lakini ikaamua kumnasa Mghana mwingine na kufanya kikosi hicho kutawaliwa na nyota wa kigeni kutoka Ghana nchi iliyoko ukanda wa Afrika magharibi Benard Athur (Kushoto) akitambulishwa rasmi kusajiliwa na Azam FC

KAMUSOKO, TAMBWE WAREJEA MAZOEZINI YANGA, PRISONS MJIPANGE MSIJE KUPIGWA MKONO KAMA NDUGU ZENU

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Nyota wa kigeni wa mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC, Mzimbabwe, Thabani Scara Kamusoko na Mrundi, Amissi Joselyin Tambwe leo wameanza mazoezi rasmi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya kukosekana kwa kipindi kirefu. Kamusoko aliumia na kukosa mechi kadhaa za klabu yake na Amssi Tambwe alishindwa kabisa kuitumikia Yanga tangu inaanza msimu mpya naye akiwa na majeraha, lakini nyota hao wawili leo wameungana na wenzao na kurudisha matumaini mapya kwa mabingwa hao ambao Jumamosi ijayo watashuka kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi kucheza na Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Yanga iliichabanga Mbeya City mabao 5-0 katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam wikiendi iliyopita bila kuwepo mastaa wake hao, hivyo kwa uwepo wao, Prisons inaweza kuchabangwa zaidi ya mabao hayo kama haijagangamala Thabani Kamusoko (Kushoto) amerejea mazoezini leo, (Kulia) ni kocha George Lwandamina

Chalenji Cup, Stars kuanza na waarabu

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Michuano ya mataifa Afrika mashariki na kati, (Cecafa- Chalenge Cup) yamatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 3 hadi 17 mwaka huu katika miji mitatu nchini Kenya. Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki tayari limetanga makundi mawili ambapo kila kundi lirashirikisha timu tatu huku timu mbili zikiwa mwalikwa, akitangaza makundi hayo ya A na B, katibu mkuu wa Cecafa, Nicolaus Musonye amedai timu zinazoshiriki ni kumi ambapo Kundi A zipo Kenya, Rwanda, Tanzania bara, Zanzibar na Libya. Kundi B lina timu za Burundi, Ethiopia, Uganda, Sudan Kusini na Zimbabwe, mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya Tanzania bara na Libya ambao ni waalikwa, kwa mujibu wa Musonye, michuano ya Chalenji imerejea rasmi ya kukosekana miaka miwili iliyopita na amedai sasa itakuwa ikichezwa kila mwaka. Tanzania Bara itaanza na Libya, Chalenji Cup

GARDIEL MICHAEL KUREJEA AZAM FC

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam. Beki wa kushoto wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga SC, Gardiel Michael Mbaga anatazamiwa kurejea katika klabu yake ya Azam FC siku ya Jumamosi pale ambapo atakaposhuka katika uwanja wa Azam Complex kwa mara ya kwanza tangu alipoihama klabu hiyo. Mbaga kwa sasa anaichezea Yanga SC na Jumamosi mabingwa hao wa bara watautumia uwanja huo kucheza na Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara badala ya kuutumia uwanja wa Uhuru ambao umefungwa kupisha shughuri nyingine za kitaifa. Mlinzi huyo wa kushoto anayemweka benchi Mwinyi Haji Mngwali, atacheza katika uwanja huo ambao alikuwa akiuchezea alipokuwa na kikosi cha Wana lambalamba Azam FC hivyo ni sawa kama anarejea tena katika klabu yake ya zamani lakini kivingine kwa maana atavaa uzi wa kijani na njano unaovaliwa na watoto wa Jangwani Gardiel Michael, anarejea tena katika uwanja wa Azam Complex

Bocco asema ataendeleza kufunga

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mshambuliaji wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, John Bocco "Adebayor" amesema ataendeleza moto wake wa kufunga kila mchezo kama alivyofanya dhidi ya Tanzania Prisons mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Bocco amesema amepania kuingia katika orodha ya wanaowania kiatu cha dhahabu kwa kufunga kwani uwezo anao na ameshawahi kufanya hivyo, mshambuliaji huyo aliifungia Simba goli pekee la ushindi na kuifanya iendelee kusimama kileleni mwa msimamo wa ligi kwakufikisha pointi 22. Mshambuliaji huyo kwa sasa amefunga jumla ya magoli mawili na yote amefunga kiustadi mkubwa, Bocco ameahidi kufunga katika michezo inayofuatia ambapo Simba itacheza na Lipuli Jumapili katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi John Bocco ameahidi kuendeleza moto wake wa kufunga

Bossou arejea Yanga kiaina

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Beki wa kimataifa wa Togo, Vincent Bossou ametangaza kurejea Yanga baada ya kuikacha msimu huu akitaka kuongezewa donge nono pamoja na mshahara lakini kwa bahati mbaya aliyekuwa akitoa pesa hizo aliingia matatizoni na Yanga hakuna pesa na kuamua kutimkia kwao. Lakini baada ya kusikia mambo yameanza kuwa safi na umuhimu wake bado unahitajika akaamua kumtwangia simu kocha mkuu, Mzambia George Lwandamina na kwa bahati nzuri Lwandamina anamuelewa akaamua kuliorodhesha jina lake katika nyota anaowahitaji na tayari viongozi wa Yanga wameweka wazi kuwa beki huyo lazima wamnase ili kuimarisha kikosi chao. Bossou amewahi kuichezea Yanga kwa misimu miwili na kuiongoza kutwaa ubingwa wa Tanzania bara mara mbili mfululizo, na akaamua kutimka zake baada ya kushindwana na viongozi juu ya kusalia katika kikosi hicho. Hata hivyo Bossou ameamua kurejea kufuatia mipango yake ya kucheza soka nchini Vietnam kukwama na kuiomba klabu yake ya zamani ya Yanga impe tena nafasi i

Kocha Mbeya City aizimia Yanga, adai ni kiboko

Picha
Na Exipedito Mataruma. Mbeya Kocha mkuu wa Mbeya City, Mrundi, Ramadhan Nsanzurwimo amesema kwamba mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga SC walistahili kuwashindilia mabao 5-0 kwani wana kikosi bora na hatari msimu huu kuliko timu yoyote inayoshiriki ligi hiyo. Nsanzurwimo ameyasema hayo alipozungumza na Mambo Uwanjani ambapo amedai kikosi cha Yanga kilicheza vizuri na kuwazidi idara zote wachezaji wake wa Mbeya City. Lakini kocha huyo aliyechukua mikoba ya Mmalawi Kinnah Phiri, amesema wanajipanga kufanya vizuri katika mchezo ujao dhidi ya Singida United ambao amedai nao utakuwa mgumu. Amedai Yanga iliwazidi mbinu na maarifa na kupelekea kupata ushindi huo mnono, katika mchezo huo Yanga ilipata mabao yake kupitia kwa Obrey Chirwa aliyefunga matatu (Hat trick) na Emmanuel Martin aliyefunga mawili Ramadhan Nsanzurwino ambaye ni kocha wa Mbeya City, ameukubali mziki wa Yanga

Chanongo arejea kuipa nguvu Mtibwa

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mambo yameanza kuwa mazuri kwa Mtibwa Sugar baada ya kurejea tena uwanjani kwa kiungo mshambuliaji wake Haroun Chanongo kufuatia kupona majeraha yake ya goti yaliyomweka benchi kwa kipindi cha miezi sita. Chanongo aliyejiunga na wakata miwa hao wa Manungu akitokea Stand United ambayo alijiunga nayo akitokea Simba SC, anaweza kuwa msaada kufuatia kikosi hicho kupoteza mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Manungu Complex, Morogoro. Meneja wa mchezaji huyo Said Ibrahim amesema kwamba, Chanongo amerejea katika kikosi hicho kuhakikisha anakisaidia ili kuweza kufanya vema katika ligi inayoendelea ambayo mpaka sasa Mtibwa Sugar inakamata nafasi ya nne ikiwa na pointi 17 katika mechi kumi ilizocheza Haruna Chanongo amerejea tena Mtibwa baada ya kupona majeraha yake ya goti

Duh Maguri kimeeleweka Yanga

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC, wanaelekea kukamilisha dili ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Tanzania Prisons, Ruvu Shooting na Simba, Elius Maguri ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Dhofar ya Oman aliyojiunga nayo misimu miwili iliyopita. Uongozi wa Yanga umeweka bayana kumuhitaji Maguri kwakuwa atawasaidia kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani, Maguri ana uwezo mkubwa wa kufunga na amekuwa akifanya hivyo katika timu ya taifa, Taifa Stars. Katika mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania na Benin, Maguri aliifungia Tanzania goli la kusawazisha na kufanya matokeo yawe 1-1, Na Yanga wameamua kumnasa Maguri wakitaka ushirikiano wake na akina Ibrahim Ajibu, Obrey Chirwa na Raphael Daudi kwenye safu ya ushambuliaji Elius Maguri anaelekea kumwaga wino Yanga

Kispoti:

Picha
WAAMUZI WANAHARIBU UTAMU WA SOKA. Na Prince Hoza MCHEZO wa soka ndio unaoongoza kwa kupendwa zaidi hapa duniani, mashabiki wake wamekuwa wengi zaidi kuliko wanaopenda michezo mingineyo kama vile ndondi, riadha, basketiboli, netiboli nk na hiyo ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanyika. Lakini mchezo huo unaharibiwa na watu wachache sana ambao wanatibua utamu wake, kwa mfano pale dunia iliposhuhudia maajabu ya goli la mkono lililofungwa na Diego Maradona kwenye fainali za kombe la dunia. Maradona alifunga goli hilo dhidi ya timu ya England mwaka 1986 mechi ilikuwa ya Nusu fainali, mwamuzi katika mchezo huo alikuwa Aly Bennoceur raia wa Tunisia ambaye inadaiwa hakuona goli hilo hivyo akapuliza kipyenga kuashiria goli halali. Achana na goli hilo la Diego Armando Maradona ambalo lilichangia kumpa umaarufu mkubwa duniani, bado mchezo wa soka umeendelea kupendwa duniani kote. Kwa hapa nyumbani yaani Tanzania mchezo wa soka nao unapendwa na inasadikika ndio unaokamata namba moja,

Kagera Sugar yaizima Mtibwa, Azam nayo jino kwa jino na Simba

Picha
Na Saida Salum. Morogoro Goli lililofungwa na Christophee Edward "Edo" limetosha kabisa kuipa ushindi wa bao 1-0 Kagera Sugar "Wanamkulukumbi" kutoka Misenyi Bukoba jioni ya leo katika uwanja wa Manungu Complex na kuzima ndoto za Mtibwa Sugar kurejea kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Mtibwa Sugar wakicheza nyumbani wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo ili kuzidi kuipa presha Yanga ambao walikuwa sawa kwa pointi lakini wamejikuta wakifia kwa ndugu zao hao wanaotengeneza sukari. Kipigo hicho kinaifanya Mtibwa Sugar kubaki katika nafasi yao ya nne, Azam FC nayo imeendelea kuifukuzia Simba baada ya kuwalaza wenyeji Njombe Mji bao 1-0  katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, goli lililofungwa na Agrey Morris kwa mkwaju wa penalti, Azam sasa imefikisha pointi 22 sawa na Simba lakini ikizidiwa kwa magoli ya kufunga Kagera Sugar wakishangilia magoli yao

YANGA 'INAPENDEZA ZAIDI' YAIUA MBEYA CITY 5-0, CHIRWA ATUPIA MATATU

Picha
Na Albert Babu. Dar es Salaam Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC jioni ya leo imependeza zaidi baada ya kuilaza Mbeya City mabao 5-0 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Mbeya City iliingia uwanjani kwa lengo la kuiuzia Yanga baada ya mchezo wake uliopita kulala nyumbani 1-0 na Simba SC hivyo hawakutaka kupoteza tena leo. Yanga nao wametoka kulazimishwa sare tasa 0-0 na Singida United hivyo leo ilipania kushinda ikiingia uwanjani bila nyota wake wanne Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Papy Kabamba Tshishimbi na Amissi Tambwe lakini imeweza kunawili. Magoli ya mabingwa hao watetezi yalifungwa na Obrey Chirwa aliyefunga matatu peke akiondoka na mpira wake na mengine mawili Emmanuel Martin

Kilimanjaro Stars yatangaza kikosi cha Chalenji Cup

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Timu ya taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars imetangaza kikosi chake ambacho kitashiriki michuano ya mataifa Afrika mashariki na kati (Cecafa Chalenge Cup) ambayo kwa mwaka huu yatafanyika nchini Kenya kuanzia Desemba 3 hadi 17. Kocha mkuu wa kikosi hicho, Amme Ninje ametangaza kikosi huku akimtema winga Simon Msuva anayeichezea Difaa El Jadida ya Morocco na kumjumuhisha Danny Lyanga anayeichezea Fanja FC ya Oman. Akitangaza kikosi hicho jana, Ninje ambaye amewahi kuichezea Stars miaka iliyopita ameita wachezaji 20. Ambao ni makipa: Aishi Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United), mabeki: Boniface Maganga (Mbao FC), Gardiel Michael (Yanga SC), Kevin Yondan (Yanga SC), Erasto Nyoni (Simba SC), Mohamed Hussein "Tshabalala", (Simba SC) na Kennedy Wilson. Viungo: Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Tusker, Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Raphael Daudi (Yanga SC), Jonas Mkude (Simba SC), Shiza Kichuya (Simba SC), Ibrahim Ajibu

PROFESA JAY AMWANGUSHA MR TWO SUGU

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Msanii mkongwe na mbunge wa jimbo la Mikumi kupitia Chadema, Joseph Haule "Profesa Jay" leo amemwangusha nguli mwenzake wa hip hop na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi au Mr Two "Sugu" katika shindano la Nani zaidi. Shindano hilo lililoratibiwa na kituo cha matangazo cha Radio One Stereo chini ya mtayarishaji na mtangazaji mkongwe Abubakar Sadik, Jay ameshinda kwa kura 16 kati ya 2 za Mr Two. Wawili hao wote ni wabunge wa Jamuhuri ya muungano na pia wamepata kutamba katika medani ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini, akizungumzia pambano hilo, Abubakar Sadiki amesema lilikuwa pambano la aina yake ikizingatiwa wote ni wanasiasa kwa sasa Profesa Jay amemshinda Mr Two Sugu leo

Matokeo yote Ligi Kuu Bara haya hapa

Picha
Tz Prisons 0-1 Simba SC, (Sokoine Stadium, Mbeya. Ruvu Shooting 1-0 Ndanda FC, (Mabatini Stadium, Mlandizi) Stand United 0-0 Mwadui FC (Kambarage Stadium, Shinyanga) Majimaji FC 2-1 Mbao FC (Majimaji Stadium, Songea) Novemba 19 J,pili Yanga SC vs Mbeya City, (Uhuru Stadium, Dar es Salaam) Mtibwa Sugar vs Kagera Sugar (Manungu Complex, Morogoro) Njombe Mji FC vs Azam FC, (Sabasaba Stadium, Njombe) Kikosi cha Ruvu Shooting leo kimechomoza na ushindi kwa mara yao ya kwanza tangu kuanza msimu huu

BOCCO AZIMA NGEBE ZA WAJELAJELA

Picha
Na Exipedito Mataruma. Mbeya Goli lililofungwa kunako dakika ya 85 na mshambuliaji John Rafael Bocco "Adebayor" limetosha kabisa kuipa pointi tatu Simba SC baada ya kuilaza Tanzania Prisons bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Mchezo huo uliomalizika jioni hii ulikuwa mkali na wa kusisimua na kila timu ilijaribu kupeleka mashambulizi langoni kwa mwenzie, mechi hiyo ngumu imefanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Edward Moringe Sokoine jijini Mbeya na Simba kuweza kujizolea pointi sita na sasa ikifikisha pointi 22 ikiwa imeshuka uwanjani mara kumi. Mchezo wa leo umekumbushia ule wa msimu uliopita uliofanyika katika uwanja huo huo wa Sokoine ambapo vijana wa Prisons waliweza kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Victor Hangaya ambaye kwa sasa amejiunga na Mbeya City John Rafael Bocco amezima ngebe za Prisons leo

Profesa Jay na Mr Two kupambanishwa kesho

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Wasanii mashuhuri wa Hip Hop waliopata mafanikio makubwa hapa nchini, Joseph Haule "Profesa Jay" na Joseph Mbilinyi "Mr Two" wanatazamiwa kupambanishwa kesho Jumapili katika kituo cha Radio One Stereo kupitia kipindi chake cha Nani Zaidi kinachoanza kusikika kuanzia saa 8 kamili mchana hadi saa 10 jioni. Akizungumza na Mambo Uwanjani, mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi hicho Abubakar Sadik "Kwa fujo" amesema hilo ni pambano kubwa na kali ambalo litawasisimua wengi. Wawili hao kwa sasa wote ni wabunge wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakichaguliwa katika majimbo yao ya Mikumi (Haule) na Mbeya mjini (Mbilinyi) kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Joseph Haule (Kulia) akiwa na Joseph Mbilinyi (Kushoto) wanapambanishwa kesho na Radio One

Tutaichakaza Prisons- Djuma

Picha
Na Exipedito Mataruma. Mbeya Kocha msaidizi wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, Mrundi,Masoud Djuma amesema kikosi chake leo kitachomoza na ushindi dhidi ya Wajelajela Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Masoud Djuma amesema ana kila sababu ya kukiongoza kikosi chake kushinda leo kwakuwa kimeimarika vya kutosha. Simba ilipotoka kuichapa Mbeya City 1-0 ikaenda Katavu kisha Sumbawanga kujiandaa na mchezo huo hivyo ushindi ni lazima, amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kushangilia mwanzo mwisho kwani matokeo ni jambo la kawaida kwao Masoud Djuma (Kushoto) amesema Simba itashinda leo

KOCHA WA PRISONS AIDHARAU SIMBA NA KUWAAMBIA KIPIGO KIPO PALEPALE

Picha
Na Exipedito Mataruma. Mbeya Kocha mkuu wa timu ya Tanzania Prisons, Mohamed Abdallah, ameielezea mechi ya leo dhidi ya Simba na kusema ushindi kwa timu yake upo palepale akikumbushia ushindi wa mabao 2-1 walioupata msimu uliopita dhidi ya Simba. Leo jioni katika uwanja wa Kumbukumbu ya Edward Moringe Sokoine jijini Mbeya kutapigwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania baina ya Wajelajela na Wekundu wa Msimbazi ambapo wenyeji Prisons wamedai Simba si timu kubwa ila ni timu kongwe hivyo watawahenyesha na ukongwe wao. Kocha huyo anajiamini kuliko maelezo hasa kutokana na kikosi chake kuwa na pointi 14 huku kikionyesha ushindani wa hali ya juu, Prisons inamtumainia mshambuliaji wake Mohamed Rashid ambaye mpaka sasa amefunga mabao matano

AFANDE SELE AMPONDA MAMA KANUMBA, ADAI SIYO MAMA BORA

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Msanii wa muziki wa kizazi kipya Afande Sele, amesema anashangzwa na kitendo cha Mama Kanumba kushukuru kufungwa kwa Lulu wakati mtoto wake ndiye alikuwa na makosa kwa kuwa na mahusiano na binti mdogo. Afande Sele amesema mama Kanumba ni mama ambaye hana vigezo vya kuwa mzazi kwani hana uchungu na mtoto wa mwenzake kwenda jela akiwa mdogo, huku ambaye alistahili kuhukumiwa ni mtoto wake Kanumba . "Mama Kanumba nimeshangaa kusikia anashukuru kwamba Lulu kafungwa, mama ambaye hana uchungu hana sifa ya kuwa mzazi, anashukuru kwamba mtoto mdogo anafungwa kwa ajili ya ubazazi wa mtoto wake, ujinga wa mwanae, upuuzi wa mwanae, mkubwa anambaka mtoto mdogo kama yule”, amesema Afande Sele. Afande Sele ameendelea kwa kusema kwamba yeye kama mzazi mwenye mtoto wa kike anatamani hata maiti ya Kanumba ingefukuliwa ichomwe moto ili kuwa fundisho kwa wanaume wengine wenye matendo kama yake. . Afande Sele

Singida United yaibamiza Lipuli na kupaa

Picha
Na Mwandishi Wetu. Singida Timu ya Singida United jioni ya leo imeutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Namfua baada ya kuilaza Lipuli ya Iringa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara raundi ya 10. Bao pekee lililoipa pointi tatu Singida United lilifungwa na mshambuliaji wake Danny Usengimana raia wa Rwanda aliyepokea pasi toka kwa Salum Chuku, kwa ushindi huo Singida United inafikisha pointi 17 na ikikamata nafasi ya tano hivyo inakuwa imeishusha Tanzania Prisons ambayo kesho itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Simba. Ligi hiyo inayoongozwa na Simba SC yenye pointi 19 itaendelea tena kesho kwa mechi nne kupigwa kwenye viwanja tofauti, Stand United itaialika Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga, wakati Majimaji itakuwa mwenyeji wa Mbao FC katika uwanja wa Majimaji mjini Songea. Pale katika uwanja wa Sokoine Mbeya, Simba itakuwa mgeni wa Prisons na uwanja wa Mabatini, Mlandizi Pwani, Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara Singida Uni