KISPOTI

Mnashangaa ya Mwigulu na Yanga mnasahau ya Bakhresa kwa Simba

Na Prince Hoza

HIVI karibuni mbunge wa Iramba Mashariki kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dr Mwigulu Lameck Nchemba ambaye pia in kiongozi mkuu wa klabu ya soka yaSingida United inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bars aliamua kuwatunuku Yanga SC wachezaji watatu ambapo yeye mwenyewe alisema in msaada wake kwa klabu hiyo.

Dr Mwigulu alianza kuwapa Yanga kiungo aliyesajiliwa na klabu take ya Singida United, Fesal Salum Abdallah "Fei Toto" katika maelezo yake Dr Mwigulu alisema aliamua kuhamisha leseni ya Fei Toto Singida United na kuipeleka kwa Yanga SC.

Singida United ilimsajili Fei Toto kwa kandarasi ya miaka mitatu akitokea JKU ya Zanzibar lakini Sikh so nyingi Yanga nao wakatangaza kumsajili, Dr Mwigulu ameweka wazi kuwa gharama zote walizomlipa Fei Toto zitatumiwa na Yanga na wala hawatamdai.

Pia Dr Mwigulu ambaye amewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi kabla ya Raid wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli hajatengua uteuzi wake na kumpa mbunge wa jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, aliwapa tens Yanga kiungo mshambuliaji Deus Kaseke.

Kaseke ameenda Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao ulisalia akiwa na Singida United, Kaseke alijiunga na Singida United mwaka Jana akitokea Yanga SC ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili, na mpaka sasa ametumikia mwaka mmoja na kwa mujibu wa Dr Mwigulu, Kaseke atamalizia mwaka mmoja Yanga badala ya Singida United na wala hawatadai fedha yao.

Pia waziri Hugo wa zamani wa mambo ya ndani akawapa tens beki WA kati raia wa Zimbabwe Elisha Muroiwa ambaye naye alikuwa amebakiza nkataba wa mwaka mmoja, kwa mujibu wa Mwigulu alifafanua kuwa Muroiwa ataenda kumalizia mkataba wa mwaka mmoja Yanga, hats hivyo Yanga walimkataa beki Hugo dakika za mwisho na kurejea tena Singida united.

Baada ya kukamilisha kuwapa nyota hao wawili Yanga, Dr Mwigulu alisema aliamua kuwasaidia Yanga kama mdauntu kwani ikumbukwe yeye in kiongozi WA Singida United na amedai kama kuna timu nyingine yoyote itahitaji msaada kutoka kwake hatosita kusaidia.

Mbali na kujitolea msaada huo, hakuna mtu asiyejua kama Dr Mwigulu ni mpenzi na mkereketwa wa Yanga SC, na tunajua kuwa hakuna mtu anayejua kupenda kama shabiki aka mkereketwa, hao ndio wanaoguswa, Yanga kwa sasa inapitia majaribu na tayari karibu viongozi wake wakuu wameshajiuzuru.

Hivyo imejikuta katika kipindi kigumu, ikishindwa kufanya usajili, pia kuwabakisha nyota wake, Yanga ilijikuta ikishindwa kuwasajili wachezaji iliowatangaza kuwahitaji kiasi kwamba mtani wake Sumba SC ikaamua kati na kuwasajilii.

Yanga ilitaka kumsajili Adam Salamba lakini Simba wakamuwahi, pia ikataka kumsajili Paschal Wawa, Simba nao wakachangamkia fulsa na kumnasamwishoni ikataka kumsajili Meddie Kagere kama kawaida Simba wakasikia na kumsajili.
Yanga ikajikuta ipo kwenye migomo na wachezaji wake mpaka ikajikuta ikipoteza mwelekeo katika michuanno ya kombe la Shirikisho barani Afrika, katika Sikh za karibuni Yanga imefungwa jumla ya mabao 7 kwa moja na Gormahia, ilianza kuchapwa 4-0 Moi Kasarani jijini Nairobi nchini Kenya, kisha Jana ikachapwa 3-2 uwanja wa Taiga Dar es Salaam.

Mbali na Dr Mwigulu kuguswa hadi kuhamisha mikataba ya wachezaji wakenwawili na kuwapeleka Jangwani, mwekezaji mpya wa Klabu ya Simba ambaye in mfanyabiashara maarufu hapa nchini Mohamed Dewji "Modewji" naye aliguswa baada ya kusikika akiiombea Yanga ivuke salama katika kipindi hiki kigumu inachopitia, lakini baada ya Dr Mwigulu kuwapa Yanga wachezaji wawili baadhi ya wadau wa soka nchini wameonekana kushangazwa na aina hiyo ya kupeana wachezaji na kuhusisha undugu kati ya Yanga SC na Singida United.

Wanajiuliza iweje Singida United iwape Yanga wachezaji wake, kuna wengine tayari wamezihusisha timu hizo na undugu wa damu, lakini wadau hao wamesahau anayofanya Said Salim Awadh Bakhresa kwa klabu ya Simba.

Ikumbukwe Bakhresa ndiye mmiliki wa makampuni ya Azam Group ambayo inamiliki klabu ya soka ya Azam FC, Bakhresa amewahi kuwa mweka hazina wa klabu ya Simba miaka kadhaa iliyopita. Akiwa kama mmiliki wa Azam FC ameisaidia sana wachezaji Simba SC.

Ingawa kila mmoja ana njia yake ya kusaidia, lakini msaada no msaada tu, Azam FC iliwahi kuwapa Simba kiungo mahiri asiye na mfano Patrick Mafisango ambaye kwa sasa ni marehemu, msaada wa Mafisango uliwapa faida Simba kwani iliweza kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2011/12, na baada ya Simba kupotea kwa misimu minne bila ubingwa wa bara, Bakhresa tena akaamua kuwasaidia Simba kivingine.

Mwanachama huyo mtiifu wa Simba SC akawapa tena Simba kipa Aishi Manila, mabeki Shomari Kapombe na Erasto Nyoni pia mshambuliaji John Bocco "Adebayor" ujio wa nyota hao uliwasaidia Simba kupata ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Wachezaji hao kutoka Azam FC wanafanya vizuri kwa sasa na wamekuwa msaada muhimu kwenye timu hiyo, huo ni ukumbusho tu anayofanya Dr Mwigulu kwa Yanga pia yamefanywa sana na Bakhresa , tofauti iliyopo kwamba watu wamesahau

Alamsiki

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA