MWASHIUYA AIBUKIA SINGIDA UNITED, PIA MGHANA NDANI
Na Mwqandishi Wetu. Singida
Klabu ya Singida United ya mkoani Singida Jana nayo imefunga zoezi la usajili kwa kunasa saini za nyota wawili mmoja wa kimataifa raia wa Ghana ambao kila mmoja amepewa mkataba wa miaka miwili.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Geofrey Mwashiuya amesajiliwa na klabu hiyo sambamba na Mghana Hans Koffie na sasa timu hiyo inayonolewa na Mzanzibar Hemed Morocco imekamilisha usajili wake, pia Singida United itakuwa na sura mpya baada ya nyota wake wengi kutoweka.
Mwashiuya alitokea Yanga ambayo yenyewe ilimsajili kutoka Kimondo FC ya mkoani Mbeya