Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2014

KWA KAULI HII, T.I.D ANAMCHOKOZA TENA ALLY KIBA.

Picha
Bifu lilikuwepo huko nyuma kati wasanii wa bongofleva Khaleed Mohamed T.I.D na mwenzake Ally Kiba limeibuka upya na safari hii ni hatari zaidi ya mwanzo. Nyota hao walikuwa katika bifu zito na kufikia hatua ya kuchafuana mitandaoni- jana T.I.D alipost picha ya Diamond Platinum katika ukurasa wake wa Instragram ikimtaka arejee na tuzo na aachane na mafala. Kwa kauli yake na wadadisi wa mambo wanasema T.I.D amemnanga Ally Kiba na mashabiki wake ambao katika siku za hivi karibuni walikuwa wakimuandama Diamond kiasi kwamba walimpoteza kisaikolojia. Diamond alizomewa jukwaani na mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Ally Kiba katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni Dsm. Mashabiki hao walimtaka Diamond ashuke jukwaani huku wakitaka Ally Kiba arudi tena jukwaani. T.I.D ambaye alikuwa ktk bifu kubwa na Ally Kiba

BAYENR MUNICH WANA NJAA YA KUFUZU

Picha
Jerome Boateng  Beki wa kushoto wa Bayern Munich, David Alaba amekariri kuwa magitu hao wa Ujerumani hawatapuuzilia kibarua chao dhidi ya klabu cha Italia, AS Roma kwenye ngoma ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya Jumatano licha ya kuwaadhibu kichapo kikali jijini Roma hivi majuzi.  Bayern walilupua waitaliano hao 7-1 majuma mawili yaliopita kuhifadhi utawala wa kundi lao na alama zote tisa baada ya michuani mitatu huku wakiweka rekodi ya ushindi mkubwa sana ugenini ya mabingwa hao wa ligi ya Bundesliga ya Ujerumani katika shindano hilo la hadhi kuu. Kiungo hatari wa Uholanzi, Arjen Robben, alifunga magoli mawili kuweka Bayern kwenye usukani wa Kundi E alama tano mbele ya Roma. Vigogo hao watafuzi raundi ya 16-bora ikiwa watawakunguta tena wageni wao kwenye mechi ya marudiano itakayotandazwa ugani Allianz Arena kwa mara saba mtawalia.

SUNDERLAND YAINYUKA CRYSTAL PALACE 3-1

Picha
Steven Fletcher amefunga mabao mawili na kuisaidia timu yake ya Sunderland kuinyuka Crystal Palace 3-1 kwenye dimba la Selhurst Park na kujitoa kwenye shimo la kushukia daraja la ligi kuu ya England. Katika mchezo huo pekee wa jana usiku Fletcher aliifungia timu yake bao la kuongoza kabla ya mlinzi wake Wes Brown hajaisawazishia Palace kwa bao la kujifunga mwenyewe. Sunderland waliongeza mapigo pale Jordi Gomez alipoutia wavuni mpira kwa kombora la chini kabla ya Mile Jedinak hajatolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya njano ya pili kutokana na mchezo mbaya.

RONALDO KUIFIKIA REKODI YA RAUL LEO?

Picha
NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anahitaji bao moja tu ili kulingana na mfungaji mabao anayeongoza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa miaka yote, Raul. Real Madrid itakutana na Liverpool kwenye mchezo mkali wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi leo Jumanne na Ronaldo ana nafasi kubwa ya kufikisha mabao 71 ambayo yalitundikwa na Raul au hata kupita zaidi atakapokuwa mbele ya mashabiki wa Santiago Bernabeu. Madrid inaweza kufika katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa kama watawafunga Liverpool kwenye mchezo huo wa Kundi B Ronaldo ambaye anatabiriwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara nyingine hajapungua kasi. Amefunga katika mechi 12 mfululizo alizocheza katika siku za karibuni. Vile vile bao lake kwenye mechi dhidi ya Granada la Jumamosi ambapo walishinda mabao 4-0 lilimfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufunga katika mechi nane mfululizo katika La Liga.

MAKALA>>>NANI APEWE MECHI MBILI, PHIRI AU ALIYEMSAJILI KWIZERA!

Picha
Na Frank Sanga BAADHI ya wachezaji wa Simba wanamaliza mikataba Desemba mwaka huu na wengine wamebakiza miezi sita hivyo wanaweza kufanya mazungumzo na klabu yoyote. Tunaambiwa kuwa hata Jones Mkude, ambaye ni tegemeo lao kuu yupo ndani ya miezi sita kumaliza mkataba wake katika mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam. Najua mashabiki wa Simba wasingependa kusikia habari hizi, wala wasingependa kusoma habari ya aina hii, lakini huo ndio ukweli ambao ni lazima ukubaliwe. Ni kama uongozi wa Simba umechanganyikiwa, haujui ufanye nini na ndio maana tunashuhudia mambo mengi yakitokea katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara. Uongozi hauelewi ufanye nini? Kuna uwanja ambao tuliambiwa uko Bunju, lakini ilikuwa ni mbwembwe tu hakuna unaloweza kujivunia mpaka sasa katika mradi huo.

MAXIMO AKIRI KAGERA WALIWAZIDI UJANJA YANGA

Picha
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amesema kikosi chake kilizidiwa mbinu na Kagera Sugar katika mechi yao ya raundi ya sita ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu ambayo Wanajangwani hao walipoteza kwa bao 1-0 ugenini mjini Bukoba, Kagera juzi. Kikianza na wachezaji wanne wa kimataifa, Warwanda Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima na Wabrazil Andrey Coutinho na Geilson Santos Santana 'Jaja', kikosi cha Yanga kilijikuta kikipoteza mechi yake ya pili kati ya tatu ugenini baada ya mshambuliaji, Paul Ngwai kuwafungia wenyeji bao kali dakika nane baada ya kuanza kwa kipindi cha pili ikiwa ni mpira wake wa kwanza tangu aingie kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba akitokea benchi.

LUHENDE AZUSHIWA ZENGWE MTIBWA.

Picha
Siku moja baada ya beki wa Mtibwa Sugar David Luhende kukosa penalti dhidi ya Simba, mashabiki wanaodhaniwa kuwa wa Mtibwa Sugar wamemshutumu beki huyo kwa kitendo chake cha kuinyima ushindi timu yao. Wakizungumza kwa mtandao huu kwa njia ya simu, mashabiki hao wamemshutumu beki huyo kwa madai ya kuinyima ushindi Mtibwa ambao wameishia kutoka sare ya 1-1 na wekundu wa msimbazi. Simba ilitangulia kupata bao ktk kipindi cha kwanza lililofungwa na Joseph Owino baada ya kupata pasi murua toka kwa Emmanuel Okwi. Kabla ya kuelekea mapumziko Mtibwa Sugar walipata penalti iliyokwenda kupigwa na David Luhende ambapo iliokolewa na mlinda mlango chipukizi Peter Manyika Jr. Manyika alitumia udhaifu wa Luhende kwa kumsoma miguu yake wakati akijiandaa kupiga. Hata hivyo Luhende alikosa penalti hiyo baada ya kipa kuiokoa, Mtibwa walichomoa bao hilo ktk kipindi cha pili likifungwa na Mussa Hassan Mgosi.

CITY YAITAMBIA UNITED, AGUERO SHUJAA

Picha
Manchester City imeendeleza ubabe wake dhidi ya majirani zao Manchester United kwa kuwachapa goli 1-0 katika mchezo mkali uliofanyika katika uwanja wa Etihad, Jumapili. Goli hilo la kumi kwa Aguero katika msimu huu wa ligi kuu ya England liliivunja Manchester United iliyokuwa na ngome iliyosambaratika baada ya Chris Smalling kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza cha mchezo na Marcos Rojo kutolewa nje katika machela baada ya mapumziko kutokana na kuumia bega. Ushindi huu wa Manchester City pia unatoa mwanga wa matumaini kwa kocha Manuel Pellegrini ambaye wiki iliyopita, timu yake ilipoteza kwa West Ham katika mchezo wa ligi kuu na kisha kutolewa katika kombe la Capital One baada ya kufungwa nyumbani na Newcastle.

ENTENTE SETIF MABINGWA WAPYA BARANI AFRIKA

Picha
Klabu ya Entente Satif kutoka Algeria imeshinda ubingwa wa kilabu bora barani Afrika kwa mara ya kwanza katika miaka 26 baada ya kuishinda kilabu ya AS Vita Club kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutokana na mabao ya ugenini kufuatia sare ya 3-3 siku ya jumamosi. Raundi ya pili ya fainali katika uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida ilikamilika kwa sare ya 1-1,siku sita baada ya sare ya 2-2 katika mechi ya kwanza iliochezwa mjini Kinshasa.

JONAS MKUDE MBIONI KUTUA YANGA, AZAM NAYO YAMTAKA NDEMLA

Picha
SIMBA huenda wakapata pigo kubwa kama hawatafanya jitihada za kukaa chini na wachezaji wao muhimu ambao mikataba yao iko ukingoni. Miongoni mwa wachezaji hao ni Jonas Mkude na Said Ndemla ambao kwa sasa wanaruhusiwa kufanya mazungumzo ya awali na klabu yoyote. Gazeti hili linajua kuwa Simba walianza mikakati jana Jumapili ya kuweka mambo sawa lakini wapinzani wao Yanga na Azam wameshashtukia dili na ndio wanafanya mikakati ya chinichini kuwanasa wachezaji hao muhimu kwa Simba. Habari za uhakika kutoka Yanga ambazo gazeti hili inazo ni kwamba wameelekeza nguvu zao kwa Mkude huku wakisisitiza kwamba ndiye mchezaji pekee wa Simba kwa sasa mwenye hadhi ya kuichezesha na kusukuma mashambulizi kwenye mzunguko wa pili wa ligi na Kombe la Shirikisho ikielezwa kwamba hata mfumo wa Marcio Maximo unambeba.