HIVI NDIVYO YONDANI ALIVYOMWAGA WINO YANGA
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Yanga Sc jana imefunga usajili kwa kumsainisha kandarasi ya mwaka mmoja beki wake kisiki Kelvin Patrick Yondani na kusalia katika kikosi hicho.
Awali Yondani alikuwa akiwindwa na mahasimu wao Simba Sc lakini Abas Tarimba akaingilia kati na kumtuliza hatimaye jana wakati dirisha linafungwa beki huyo akamalizana na mabingwa hao wa zamani, hata hivyo Yanga imempoteza beki wake wa kulia Hassan Ramadhan Kessy aliyetimkia Nkana Red "Devils" ya Zambia.
Yanga pia iliweza kukamilisha usajili wa nyota wawili wapya WA Kikongoman kipa Klauz Kinzi Kindoki na mshambuliaji Heritier Makambo, Yanga imesajili wachezaji sita tu ambao no Makambo na Kindoki wwngine ni Mohamed Issa Banka, Fesal Salum "Fei Toto", Deus Kaseke, Mrisho Ngasa