Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2015

KIPA MPYA AIBEBA LIVERPOOL IKISHINDA KWA MBINDE KOMBE LA LIGI

Picha
KIPA mpya wa Liverpool, Adam Bogdan usiku wa jana alikuwa shujaa Uwanja wa Anfield baada ya kuokoa penalti tatu na kuiwezesha timu hiyo kutinga Raundi ya Kombe la Ligi England.  Liverpool ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1 na Carlisle ya Ligi Daraja la Nne England katika michuano ya Capital One. Mchezaji mwingine mpya, Danny Ings alianza kuifungia Liverpool kipindi cha kwanza kabla ya  Derek Asamoah kuisawazishia Carlisle na mchezo ukaenda kwenye dakika 30 za nyongeza. Penalti za Liverpool zilifungwa na Milner, Can na Ings wakati Lallana na Coutinho walikosa na za Carlisle zilifungwa na Dicker na Mcqueen huku Grainger, Joyce na Hery wakikosa. Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Bogdan, Clyne/Ibe dk86, Lovren, Milner, Firmino/Origi dk35, Moreno, Lallana, Can, Allen/Coutinho dk64, Ings na Skrtel. Carlisle: Gillespie, Miller, Raynes, Grainger, McQueen, Kennedy/Gillesphey dk73, Dicker, Joyce, Sweeney/Ibehre dk65, Hery na Asamoah/Gilliead dk64.

MAKALA: NI MECHI YA KUWANIA REKODI SIMBA NA YANGA

Picha
Mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi kwenye mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2015/16. Timu hizi zilianza kupambana miaka mingi iliyopita, huku mechi zao zikivuta hisia za wapenzi wa soka nchini kabla na baada ya mechi. Pamoja na kwamba timu hizi zimekutana mara nyingi, lakini kuna baadhi ya mechi ambazo zilikuwa na matukio ambayo hayawezi kusahaulika kirahisi. Ni mechi ambazo zilikuwa na matukio mbalimbali ya kuhuzunisha, kuchekesha, kushangaza na nyingine kuweka rekodi ambazo hadi leo hazijafikiwa wala kuvunjwa. Yanga ilivyoifumua Simba 5-0 Achana na ile mechi ya 2012 Simba ilipoifunga Yanga mabao 5-0. Yanga iliwahi kufanya hivyo mwaka 1968. Ilikuwa Juni Mosi mwaka 1968,Yanga ilipoifumua Simba mabao 5-0. Magoli ya washindi yalifungwa na Maulidi Dilunga alipachika mabao mawili dakika ya 18 na 43, pia Selehe Zimbwe akifunga mawili dakika ya 54 na 89, Kitwana Manara akifunga goli moja dakika ya 8

SHERMAN ANG'ARA 'BONDENI'

Picha
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga SC, Mliberia Kpah Sherman jana amecheza kwa dakika 63 timu yake mpya, Mpumalanga Black Aces ikiendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini. Aces imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini jana usiku, shukrani kwake mkongwe Collins Mbesuma aliyefunga mabao yote hayo dhidi ya Golden Arrows Uwanja wa King Zwelithini mjini Durban. Sherman alianza katika mchezo huo kabla ya kumpisha Aubrey Modiba dakika ya 63 wakati huo tayari Aces inaongoza 2-1. Deon Hotto alianza kuwafungia Arrows dakika ya 13 akimalizia pasi ya Gladwin Shitolo, lakini Mbesuma akasawazisha dakika ya 32 na kufunga la pili dakika ya 49. Sherman ametua Aces mwezi uliopita kutoka Yanga SC ambako alicheza kwa nusu msimu huu kabla ya kuamua kuondoka baada ya kuona mambo hayamuendi vizuri. Mechi nyingine za Ligi Kuu ya ABSA jana, Kaizer Chiefs imelazimishwa sare ya  1-1 University of Pretoria Uwanja wa FNB, bao lao likifungwa na Bernard Parker dakika ya 25 kabla ya  Tebogo Mony

Van Gaal:Tutanyakua ubingwa wa ligi

Picha
Ushindi wa kilabu ya Manchester United dhidi ya Southampton ni dhihirisho tosha kwamba kilabu hiyo inaweza kunyakuwa taji la ligi kuu,amesema mkufunzi wake Louis Van Gaal. Kikosi hicho cha Van Gaal kilipata ushindi wa mabao 3-2 katika uwanja wa St Mary's siku ya jumapili huku mshambuliaji Anthony Martial mwenye umri wa miaka 19 akifunga mabao mawili. Ushindi huo umeipandisha kilabu ya Manchester United hadi nafasi ya pili nyuma ya Manchester City iliopoteza mabao 2-1 nyumbani dhidi ya West Ham siku ya jumamosi.''Tumeonyesha kwamba tunaweza kupigania taji hili'',Van Gaal alisema. Huwezi kutarajia taji kama hili kupitia timu iliopo katika awamu ya mpito,lakini iwapo tuko karibu kufanya hivyo basi tutalinyakuwa''. Van Gaal alipongeza uwezo wa Martial ,aliyefunga mabao matatu kufikia sasa kwa kujaribu mara tatu tangu alipowasili katika kilabu hiyo kupitia uhamisho wa kitita cha pauni milioni 36 kutoka Monaco.

TENGA AJIWEKA KANDO CECAFA

Picha
Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) linatarajia kupata mwenyekiti mpya atakayeliongoza shirikisho hilo katika uchaguzi utakaofanyika Novemba mwaka huu jijini Addis Ababa, Ethiopia imeelezwa. Hata hivyo,  Tenga ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Rais wa zamani wa (TFF) bado hajaweka wazi kama atatetea nafasi hiyo katika uchaguzi ujao. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, alisema kuwa mwenyekiti wa sasa, Leodegar Tenga, kutoka Tanzania anamaliza muda wake wa miaka minne wa kulitumikia shirikisho hilo tangu alipochaguliwa mwaka 2011 jijini Dar es Salaam. Musonye alisema kuwa tayari nchi wanachama wa Cecafa wanafahamu taarifa za uchaguzi huo ambao utafanyika kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Chalenji ambayo mwaka huu yatafanyika Ethiopia.

KUELEKEA MPAMBANO WA WATANI, YANGA WAINGIWA MCHECHETO NA HATI TRICK YA KIIZA 'DIEGO'

Picha
HAT TRICK ya kwanza ya msimu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imetoka kwa mshambuliaji Mganda, Hamisi Friday Kiiza maarufu kama Diego. Kiiza alifunga mabao matatu jana Simba SC ikishinda 3-1 dhidi ya timu ngumu, Kagera Sugar ya Bukoba Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Na sasa Simba SC inakwenda kambini Zanzibar kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC wikiendi hii hapo hapo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tangu jana mashabiki wa Yanga SC wameanza kumuhofia Kiiza baada ya kuona na kusikia habari zake dhidi ya Kagera Sugar, hususan wakikumbuka alikuwa mchezaji wao. Kiiza aliichezea Yanga SC kwa miaka minne kabla ya kutemwa mwaka jana na kocha Mbrazil, Marcio Maximo ambaye alifukuzwa mwaka huo huo, nafasi yake ikichukuliwa na Mholanzi, Hans van der Pluijm. Mashabiki wa Yanga SC hawakuridhishwa na kitendo cha kuachwa kwa Kiiza, lakini waliamua kukubali yaishe na mchezaji huyo akarejea kwao Uganda kupumzika.

SHAW WA MAN UNITED KUPIGWA KISU

Picha
Mlinzi wa kushoto wa Man United Luke Shaw atafanyiwa upasuaji wa pili leo katika mguu wake uliovunjika. Shaw yuko katika hospital ya St Anna Ziekenhuis alikopelekwa mara baada ya kuvunjika mguu katika mchezo wa ligi ya mabigwa dhidi ya PSV. Nyota huyu aliumizwa na beki Hector Moreno dakika ya 15 ya mchezo, familia ya mchezaji huyo imekwenda Uholanzi kumuangalia chipukizi huyo. Beki huyu kisiki wa upande wa kushoto ataukosa msimu mzima wa ligi na anatarajiwa kurejea uwanja tena mwezi Machi mwakani.

NGOMA, KIIZA WATISHA KWA MABAO LIGI KUU BARA 2015/16

Picha
Yanga ilishinda 2-0 katika mechi yake ya ufunguzi wa msimu Jumapili iliyopita dhidi ya Coastal Union kupitia mabao ya Mzimbabwe, Donald Ngoma, na mzawa Simon Msuva, wakati katika mechi yao ya pili mabingwa hao walishinda 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons kupitia magoli ya beki wa Rwanda, Mbuyu Twite, Mrundi Amisi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma. Mahasimu wao, Simba, kufikia sasa wamefunga jumla ya magoli matatu, mawili yakifungwa na Mganda Hamis Kiiza na moja Mzimbabwe, Justice Majabvi. Wekundu wa Msimbazi walishinda 1-0 dhidi ya African Sports katika mechi ya ufunguzi kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kabla ya kuilaza Mgambo Shooting 2-0 juzi kwenye uwanja huohuo. Washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam FC, kufikia sasa baada ya mechi mbili za ligi hiyo ya juu zaidi nchini, wamefunga jumla ya magoli manne, mawili ya nyota wa kigeni Muivory Coast, Kipre Tchetche na Mkenya, Allan Wanga huku mengi mawili yakifungwa na Farid Mussa na Frank Domayo. Azam ilishinda 2-1 dhidi ya Prisons kw

NAHODHA SIMBA, ATAMBA KUTOIOGOPA YANGA

Picha
NAHODHA wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi amesema kwamba akili zao zipo kwenye mechi yao ya Jumapili dhidi ya Kagera Sugar na hawaumizwi kichwa hata dogo na mahasimu wao, Yanga SC. Akizungumza juzi mjini Tanga, Mgosi amesema baada ya kushinda mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara sasa wanaelekeza nguvu zao katika mchezo wa tatu dhidi ya Kagera. “Sioni sababu ya kuwazungumzia Yanga kwa sasa wakati mechi ijayo tunacheza na Kagera. Kwanza nataka nikuambie, hao Yanga hawatuumizi kichwa kabisa,”amesema. Mgosi amesema kwamba wachezaji wote wa Simba SC kwa sasa akili yao inafikiria namna gani wataifunga Kagera Sugar ili kufikisha pointi tisa ndani ya mechi tatu. Simba SC imeanza vyema Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kushinda mechi zake zote mbili za mwanzo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga 1-0 dhidi ya African Sports na 2-0 dhidi ya JKT Mgambo. Sasa Wekundi hao wa Msimbazi walio chini ya kocha Muingereza, Dylan Kerr watacheza mechi yao kwanza nyumbani mwisho

Zagreb coach thanks Bilic for Arsenal win

Picha
Slaven Bilic Dinamo Zagreb coach Zoran Mamic thanked his compatriot and West Ham manager Slaven Bilic for helping the Croatian title holders beat Arsenal 2-1 in their Champions League Group F match on Wednesday. Bilic, whose side beat London rivals Arsenal 2-0 in the Premier League's opening round, passed on valuable advice to Mamic ahead of the clash. "We scouted Arsenal well and we found information given to us by Bilic and his assistant Nikola Jurcevic very useful," Mamic told reporters. "But my players did a great job too. "I knew we could stay on the same par physically with a team uncomfortable against rivals who can keep possession." Arsenal were static when defending set pieces while they also lacked creativity in midfield and bite up front, while Dinamo's attack of El Hilal Arabi Soudani and Junior Fernandes and Marko Pjaca threatened with their

YANGA YAZIDI KUJIKITA KILELENI, SIMBA NAFASI YAKE NI YA TATU

Picha
Mabingwa wa bara Yanga wamejiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia ushindi mnono wa magoli 3-0 dhidi ya Prisons ya Mbeya, huku mahasimu wao, Simba, wakihitimisha ziara ya mkoani Tanga kwa kuzoa pointi zote sita baada ya kuifunga Mgambo 2-0 jana. Washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam, nao walishinda mechi yao ya pili mfululizo jana baada ya kuibwaga Stand United kwa magoli 2-0 na kujiimarisha katika nafasi pili. Kulikuwa na ushindi mwingine mkubwa mjini Mbeya wakati wenyeji Mbeya Ciy walipowasambaratisha JKT Ruvu kwa magoli 3-0 kwenye Uwanja wa Sokoine. Kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, beki wa kati wa kimataifa wa Yanga kutoka Rwanda, Mbuyu Twite, ndiye aliwafungia mabingwa hao watetezi bao la kwanza katika dakika ya 27 akiwahi mpira uliotemwa na kipa wa Prisons, Mohammed Yusuph. Kipa huyo alitema mpira wa ‘fri-kiki’ uliopigwa na Haruna Niyonzima. Sekunde chache kabla ya kwenda mapumziko, Mrundi, Amissi Tambwe, aliipatia Yanga bao la pili k

BONDIA AFARIKI BAADA YA KUPIGWA 'KNOCK OUT'

Picha
Mwana masumbwi mmoja wa Australia amefariki siku nne baada ya kupoteza fahamu alipopigwa 'knock out' katika pigano la kijimbo mjini Sidney. Davey Browne mwenye umri wa miaka 28 aliangushwa na Carlo Magali wa taifa la Ufilipino mwisho wa raundi ya 12 katika taji la uzani wa Feather siku ya Ijumaa. Brown ambaye ni baba ya watoto wawili alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya mitambo inayomsadia kuzimwa alipokosa kuimarika kiafya. Muungano wa wahudumu wa matibabu nchini Australia umetaka mchezo wa ndondi kupigwa marufuku nchini humo kufuatia kifo hicho.

MESSI APIGA MECHI YA 100 CHAMPIONS LEAGUE, ROMA YAIGOMEA BARCELONA

Picha
Lionel Messi amefikisha mechi 100 za Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Barcelona ikilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wao AS Roma ya Italia. ROMA (4-3-3): Szczesny (De Sanctis 50mins); Florenzi (Torosidis 85), Manolas, Rudiger, Digne; De Rossi, Keita, Nainggolan; Salah, Dzeko, Falque (Iturbe 82) Subs not used: Totti, Maicon, Vainqueur, Gervinho Goal: Florenzi 31 Booked: Nainggolan BARCELONA (4-3-3): Ter Stegen; Roberto, Pique, Mathieu, Alba; Rakitic (Rafinha 62, Mascherano 65), Busquets, Iniesta; Neymar, Suarez, Messi Subs not used: Bartra, Munir, Sandro, Adriano, Masip Goal: Suarez 21 Booked: Pique

CHELSEA YAZINDUKA NA KUPIGA MTU 4-0 ULAYA, BARCA YASHIKWA SHATI

Picha
CHELSEA inayovurunda katika Ligi Kuu ya England, usiku huu imefufua makali na kuitandika mabao 4-0 Maccabi Tel Aviv ya Israel katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Stamford Bridge, London. Mabao ya The Blues inayofundishwa na Mreno Jose Mourinho yamefungwa na Willian Borges Da Silva dakika ya 15, Oscar dos Santos Emboaba Junior kwa penalti dakika ya 49, Diego Da Silva Costa dakika ya 58 na Cesc Fabregas dakika ya 78. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Dynamo Kyiv imelazimishwa sare ya 2-2 na FC Porto Uwanja wa Olimpiki, Mabao ya Dynamo yamefungwa na Oleg Gusev dakika ya 20 na Vitaliy Buyalsky dakika ya 89 wakati ya Porto yamefungwa na Vincent Aboubakar dakika ya 23 na 81. Barcelona superstar Lionel Messi was one of the first players to congratulate Suarez after his goal against the Italian outfit Nyota wa Barcelona, Lionel Messi akimpongeza Suarez baada ya kufunga bao la kuongoza PICHA ZAIDI Arsenal imechapwa mabao 2-1 na Dinamo Zagreb katika mchezo wa Kundi H, mabao

DK SLAA AZIDI KUIPASUA UKAWA, SASA NI JUMA NATURE NA MSAGASUMU WAREJEA CCM

Picha
Wanamuziki mahiri Juma Nature na Msagasumu ambao siku ya uzinduzi wa kampeni za kumnadi mgombea wa urais wa Chadema kupitia mwamvuli wa Ukawa Edward lLowasa zilizofanyika ktk viwanja vya jangwani wametangaza kuachana na Ukawa na kutangaza kurejea CCM. Taarifa zilizotufikia hivi zinasema kuwa Nature na Msagasumu wameachana na ukawa na kurejea CCM baada ya kuchoshwa na siasa za majitaka zinazoendelea katika umoja huo wa katiba Ukawa, awali Nature alikuwa chama cha wananchi CUF na aliwahi kutangaza kugombea udiwani kupitia chama hicho lakini ikashindikana, na kuibukia kwenye kampeni za jangwani.

MAKALA: TFF ISOGEZENI MBELE MECHI YA SIMBA NA YANGA KUPISHA KAMPENI ZA UCHAGZUI MKUU

Picha
NI dhahili vuguvugu la kisiasa limepamba moto nchini, misikitini, makanisani habari ni uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, hivyo wananchi wamekuwa katika shughuri mbalimbali za kampeni. Kampeni za kuwanadi wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani zimepamba moto kila mahari, watu wako bize na siasa, kubwa zaidi ni nafasi ya mgombea wa urais, vyama mbalimbali vinajaribu bahati yao kwa kuzunguka nchi nzima kuwanadi wagombea wao. Vyama vikuu CCM, Chadema kupitia mwamvuli wa Ukawa vinachuana vikali kuisaka dola, CCM yenyewe imeamua kumsimamisha mgombea wake wa urais Dk John Pombe Magufuli wakati Ukawa imemsimamisha mgombea wake Edward Ngoyai Lowassa. Mchuano umekuwa mkali, kila mgombea anakubalika na watu wake hivyo kwa sasa habari inayozngumzwa kila sehemu ni uchaguzi mkuu, watu wameamua kuacha shughuri zao na kuwafuata wanasiasa wanaojinadi majukwaani wakiomba kura. Siasa inatawala akili zetu kwa sasa, kuanzia kwenye daladala au vijiweni hata mahospitalini stori i