Maguli mambo safi AS Kigali
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Elius Maguli amejiunga na klabu ya AS Kigali ya Rwanda kwa ajili ya msinu ujao wa Ligi Kuu nchini humo.
Mshambuliaji huyo alikuwa akihusishwa kujiunga na mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC lakini amezima tetesi hizo na sasa anakuwa mchezaji wa timu hiyo.
Maguli aliwahi pia kuzichezea Dhofal FC ya Oman, Simba SC, Ruvu Shooting na Tanzania Prisons zote za Tanzania amekuwa katika kiwango bora mpaka kufikia kuitwa kwenye timu ya taifa, Taifa Stars lakini alipotea na sasa anarejea tena kwa kujiunga na klabu hiyo