Ntamba Band waja na Shobo
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Kundi linalobamba kwa sasa hapa jijini Dar es Salaam kwa muziki wa kizazi kipya, Ntamba Band lenye maskani yake Buza nje kidogo ya mji wameachia wimbo mpya uitwao Shobo.
Wimbo huo umerekodiwa katika studio zao za Nyegera Waitu zilizopo huko huko Buza na tayari video ya wimbo huo imeachiwa katika mitandao ya kijamii mbalimbali huku ukisifiwa kwa kufanya vizuri.
Akizungumza na Mambo Uwanjani, Meneja wa kampuni ya Nyegera Waitu Intertainment, Prince Mawata amesema Shobo ni wimbo mzuri ambao wamepanga kuutambulisha hivi karibuni kwa mashabiki wao katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mawata amedai wana imani kubwa wimbo huo utabamba kwenye spika za redio za mashabiki wao kutokana na maudhui yaliyomo ndani ya wimbo huo.
Kundi hilo pamoja na lingine la Nyegera Waitu Band yapo chini ya tabibu Ntamba na Mungu ambaye anasifika kwa tiba mbadala ya binadamu