Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2023

TANESCO YAOKOA JAHAZI UMEME KUKATIKA KWA MKAPA YANGA VS RIVERS LEO

Picha
Shirika la Umeme (TANESCO) limesema baada ya Majenereta ya Uwanja wa Taifa kushindwa kufanya kazi katikati ya mechi ya Yanga vs Rivers United ya Nigeria na taa kuzimika, umeme wa TANESCO ndio ulianza kutumika na mchezo ukaendelea. “Tunasikitika kwa kadhia iliyojitokeza na tutashirikiana na wenzetu kwa siku za usoni jambo hili lisijirudie, Uwanja wa Taifa unahudumiwa na vyanzo viwili vya umeme ambavyo ni TANESCO na Majenereta ya uwanja, mechi ya leo uwanja ulikuwa unahudumiwa na majenereta ya uwanja”

Tusker, Gor Mahia zamuwania Yacouba Sogne

Picha
Vilabu vya Tusker na Gor Mahia vimeingia vitani kuisaka saini ya kiungo wa ushambuliaji wa klabu ya Ihefu raia wa Burkina Faso Yacouba Songne, Kandarasi ya Yacouba Songne na Ihefu inatamatika mwishoni mwa msimu huu 2022-2023.

Nusu fainali ni Yanga vs Marumo Gallants ya Afrika Kusini

Picha
Yanga imefuzu kucheza hatua hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuiondoa Rivers United ya Nigeria baada ya matokeo ya 0-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar Yanga imesonga mbele kwa matokeo ya jumla ya magoli 2-0 ambayo iliyapata katika mchezo wa ugenini wakati #MarumoGallants imeingia hatua hiyo kwa kuitoa #Pyramids ya Misri kwa jumla ya magoli 2-1 Mechi za Nusu Fainali ni Mei 10, 2023 na marudio ni Mei 17, 2023

KOZI YA MAKOCHA CAF KUCHUKUA DIPLOMA B YAENDELEA TANGA

Picha
Washiriki wa kozi ya CAF B diploma wakiendelea na mafunzo ya vitendo kwenye kituo cha ufundi cha TFF kilichopo Mnyanjani, Tanga

MASHABIKI SIMBA WAMIMINIKA LEO KUIPOKEA TIMU YAO IKITOKA MOROCCO

Picha
Na Shafih Matuwa Mashabiki wa waliokuwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, Simba SC, lwameweka historia ya kwenda kuipokea timu yao iliyotokea nchini Morocco. Simba juzi iliondolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 4-3 na timu ya Wydad Casablanca yaliyopatikana kwa changamoto ya penalti hasa baada ya kutoka sare 1-1 ndani ya dakika 180. Mashabiki wa Simba waliamua kujitokeza kwa wingi uwanja wa ndege wa JK Nyerere jijini Dar es Salaam kuwapokea wachezaji wao na kuwapa moyo. Wachezaji wa Simba wanastahili mapokezi hayo kwani walipambana vya kutosha na kuwabana wenyeji wao kiasi kwamba waliambulia ushindi kiduchu wa 1-0 na kupelekea changamoto ya penalti tano kwa tano. Simba nayo ilipata ushindi kiduchu jijini Dar es Salaam wa bao 1-0

Fountain Gate walia na Kitayonce, wadai inatoa rushwabkupanda Ligi Kuu

Picha
Baada ya mchezo kati ya Fountain Gate FC dhidi ya Kitayosce FC kutamatika, mmoja wa kiongozi wa klabu ya Fountain Gate alizungumza na waandishi wa habari huku akiushutumu uongozi wa klabu ya Kitayosce kuhusika na vitendo vya rushwa Katika hatua nyingine aliwaambia waandishi wa habari kwamba kabla ya mchezo huo mmoja wa kiongozi wa Kitayosce alituma kiasi cha fedha Kwa wachezaji wa Fountain Gate FC ili kurahisisha matokeo ya mchezo huo. Alisema pia kama viongozi wameripoti tukio hilo polisi huku tayari mchakato wa kuripoti tukio hilo Shirikisho la Soka nchini TFF ili kuona haki inatendeka

YANGA KUTINGA NUSU FAINALI LEO?

Picha
Na Salum Fikiri Jr WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Dar Young Africans, maarufu Yanga SC usiku wa saa moja watashuka dimbani kuikaribisha timu ya Rivers United ya Nigeria kucheza mechi ya marudiano ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.  Katika mchezo huo utakaofanyika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga inahitaji sare yoyote ama kufungwa goli moja ili iweze kutinga hatua ya nusu fainali hasa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Nigeria.  Hata hivyo mechi hiyo itakuwa ngumu kwani Rivers hawatakubali  kutolewa kwenye hatua hiyo ya robo fainali na watapambana ili kulipiza kisasi na kushinda zaidi ya magoli mawili ili waweze kuingia nusu fainali.  Lakini Yanga nao wanaonekana kukamia vikali na kupata ushindi ili wawape furaha mashabiki wake, mshambuliaji hatari wa timu hiyo Mkongoman Fiston Mayele ambaye katika mchezo wa kwanza uliofanyika Nigeria aliweza kufunga magoli yote mawili, hivyo leo atataka kuendeleza maka

NABI AFURAHIA MORALI KWA WACHEZAJI WAKE IKO JUU

Picha
“Nafurahi kuona morali ya wachezaji iko juu sana kuelekea mchezo wetu wa kesho tofauti na huko nyuma naweza kusema morali hii ni kama ile tulipocheza na TP Mazembe hapa, kila mchezaji anaonyesha yuko tayari kupewa nafasi hili ni muhimu sana kwa timu yetu,” -" Nimewambia wachezaji kazi yote tulioifanya katika mechi ya kwanza haitokuwa na maana kama atutashinda mchezo huu. Pia nashabiki waache tabia ya kunipangia kikosi kwa sababu kila mechi ina Plan zake mfumo wake na aina haina ya wachezaji ambao unapaswa kuwatumia".

Kibu, Baleke na Salim kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki Simba SC

Picha
Orodha ya nyota watatu (3) ambao wameingia katika kinyang'anyiro cha kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) kwa mwezi Aprili, 2023. 👤 Jean Othos Baleke 👤 Denis Kibu Prosper 👤 Ally Salim Juma (GK)

Mayanga atupiwa virago vyake Mtibwa Sugar

Picha
Imefahamika na sasa ni rasmi klabu ya Mtibwa Sugar FC ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro, imemfuta kazi kocha wake mkuu Salum Shaban Mayanga kutokana na mwenendo wa matokeo mabovu ya timu hiyo katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara. Baada ya kuachana na kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mtibwa Sugar kwa sasa itakuwa chini ya kaimu kocha mkuu, Awadhi Juma 'Maniche' ambaye Ataoiongoza timu hiyo Katika mechi zilizosalia mpaka mwishoni mwa msimu huu.

MAMELOD SASA USO KWA USO NA WYDAD

Picha
Klabu ya Mamelodi Sundowns imetinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia ushindi wa jumla wa 6-2 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria. FT': Sundowns 🇿🇦 2-1 🇩🇿 CR Belouizdad (Agg 6-2) ⚽ Zwane 45' ⚽ Morena 49' ⚽ Bouchar 24' Mamelodi Sundowns itachuana na Wababe wa Simba SC, Bingwa mtetezi Wydad Casablanca kwenye nusu fainali. BAADAE LEO: #CAFCL 22:00 Esperance 🇹🇳 🆚 🇩🇿 JS Kabylie (Agg 1-0) 22:00 Raja CA 🇲🇦 vs 🇪🇬 Al Ahly (Agg 0-2)

ASEC MIMOSAS YAUA 30-0

Picha
TIMU ya Wanawake ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast imeifunga timu ya wanawake ya SABA Queens FC leo katika mchezo wa kirafiki. Halafu hapo aliyepigwa 30-0 yupo nyumbani kwake,

Mayele anawania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa CAF

Picha
Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga SC Fiston Mayele ameingia kwenye orodha ya wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi April wa Afrika ambapo anashindanishwa na mastaa mbalimbali wanaocheza barani. Orodha hiyo imetolewa na mtandao wa @foot_africa mpaka sasa Mayele anashika nafasi ya pili kwa wachezaji waliopogiwa kura nyingi na zoezi bado linaendelea kwenye website ya Foot-Africa.com na zoezi bado halijafungwa mpaka sasa. Msimamo hupo hivi ⚽🇨🇲 Vincent Aboubakar: (27%) ⚽🇨🇩 Fiston Mayele: (22%) ⚽🇩🇿 Riyad Mahrez: (18%) ⚽🇸🇳 Iliman Ndiaye: (14%) ⚽🇪🇬 Mohamed Salah: (9%) ⚽🇲🇦 Youssef En Nesyri: (7%)

AZAM FC WAJINASIBU KUFANYA VIZURI MSIMU UJAO AFRIKA

Picha
Uongozi wa klabu ya Azam FC ‘Wanalamba lamba’ umesema, watahakikisha msimu ujao wa mwaka 2023-24 wanafanikiwa kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa kwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ ameiambia EATV kuwa, mpaka sasa wameshajihakikishia nafasi ya ushiriki wa kombe la shirikisho barani Afrika hivyo wanaendelea kuweka mipango ya kuboresha benchi la Ufundi na wachezaji.

Simba yaanza safari ya kurejea nyumbani

Picha
Baada ya jana usiku kuondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, kikosi cha wachezaji wa Simba SC kimeanza safari ya kurejea nchini Tanzania. Simba jana ilitupwa nje ya michuano hiyo ilipofungwa na Wydad Casablanca kwa changamoto ya penalti 4-3 hasa baada ya kutoka sare ya mabao 1-1 ndani ya muda wa dakika 180. Katika mchezo wa jana Simba ilifungwa bao 1-0 goli lililofungwa na mshambuliaji Bouly Sambou raia wa Senegal, mchezo uliofanyika uwanja wa Mohamed wa 5 mjini Casablaca. Lakini Simba ilikuwa ya kwanza jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Mkapa kuifunga Wydad pia 1-0 likifungwa na mshambuliaji wake Jean Baleke raia wa DR Congo, Simba sasa inaenda kushiriki Ligi Kuu bara, kombe la FA na michuano ya Super League pekee baada ya kuondoshwa Ligi ya mabingwa.

Baloteli ajutia makosa yake hadi Messi na Ronaldo kushinda Ballon d'Or nyingi

Picha
Ni kosa langu Messi na Ronaldo kuwa na Ballon d'Or nyingi- Balotelli Mtukutu Super Mario Balotelli amedai kuwa ni makosa yake Messi na Ronaldo kuwa na wingi wa Ballon d'Or. Kupitia Muschio Selvaggio, Balotelli amesema wakala wake wa zamani, Mino Raiola alimwambia anauwezo mkubwa uwanjani kiasi kwamba kuwazidi Messi na Ronaldo na hata kuvunja utawala wao wa miaka 12 wa tuzo za Ballon d'Or. Mshambuliaji huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 32 anaamini kama sio utukutu na ukorofi wake basi angekuwa na mafanikio makubwa na kuleta ushindani mkali mbele ya Messi na Ronaldo. "Raiola mara zote amekuwa akiniambia jambo moja tu, kama Messi na Cristiano Ronaldo wanakuwa na tuzo nyingi za Ballon d'Or ni makosa yako,” amesema Balotelli ambaye kwa sasa anakipiga FC Sion. Balottelli ameongeza kuwa "Wakala Raiola alikuwa sahihi, nilikuwa nacheza asilimia 20 tu ya uwezo wangu.” Mwishoni mwa mwaka 2000 Mshambuliaji huyo alikuwa wamoto kweli kweli akiitumikia Inter Milan na kuhes

Kiwango cha Djuma Shabani kimeshuka

Picha
“Ukiachana na Injury, performance ya Djuma imekuwa too flat msimu huu, hajawa yule wa msimu uliopita, msimu uliopita ulikuwa ukizungumzia right back ulikuwa unamtaja Djuma Shaban over hata Kapombe. “Lakini kwa msimu huu unaweka question mark nyingi sana, kwenye mechi nyingi performance yake imekuwa flat sana nadhani anahitaji kuongeza juhudi. “Kuna wakati alikuwa anazungumziwa uzito akapungua lakini bado hajarudi kwenye kiwango au ubora wake ambao watu wengi walikuwa wanauzungumzia,”

Ndanda yajitoa Ligi daraja la kwanza bara

Picha
NDANDA WAKUBALI YAISHE Klabu ya Ndanda ya Mtwara imetangaza kujitoa katika Ligi Daraja la Kwanza (Championship), huku sababu ikielezwa ni ukata kiasi Cha kushindwa kumudu gharama za kujiendesha. Timu hiyo ilipaswa kusafiri kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili mchezo dhidi ya COPCO Veteran lakini walikosa fedha za kugharamia safari hiyo. Baada ya hali hiyo Uongozi umetangaza kujitoa rasmi kwenye Ligi hiyo huku ukisisitiza walijaribu kuwashirikisha wadau mbalimbali ili wapate msaada lakini ilishindikana. Ndanda inakuwa ni timu ya pili msimu huu kujitoa katika Ligi Daraja la Kwanza (Championship) baada timu ya Gwambina kufanya hivyo katikati ya Msimu wa Ligi.

Familia ya Mwakalebela yadai bondia huyo hakuwa mgeni kwenye ngumi

Picha
Familia ya Bondia Ibrahim Mwakalebela aliyefariki jana Hospitalini Dodoma alikowaishwa baada ya kuanguka akipigana ulingoni, imesema Marehemu hakuwa Mchezaji mpya sana ulingoni kwani hili lilikua pambano lake la tatu. Mwakalebela alikua akishiriki pambano la utangulizi katika pambano (Main Card) kati ya bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo na Kuvesa Katembo kutoka nchini Afrika Kusini lililofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma weekend iliyopita. Mwakalebela alishindwa kuendelea na pambano katika round ya tatu na kuanguka wakati akipigana na Laurent Segubo “SEGU Jr” na kukimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambapo siku ya pili alionekana ana shida eneo la kichwani na kutakiwa kufanyiwa upasuaji. “Tulistuka sana baada ya kudondoka nilikuwa naangalia kwenye TV lakini nashukru kwa yote na kupanda ulingoni hii ni mara ya tatu hakuwa Mgeni sana na sio mzoefu sana” ———amesema Juma Mwakalebela kaka wa marehemu Bondia Ibrahim Mwakalebela.

WYDAD CASABLANCA YAITOA SIMBA NA KUTINGA NUSU FAINALI

Picha
Na Prince Hoza Mabingwa watetezi wa Ligi ya mabingwa barani Afrika, Wydad Casablanca ya Morocco usiku huu imefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuifunga Simba SC ya Tanzania mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti kutokana na sare ya 1-1 ndani ya dakika 180. Katika mchezo wa leo Wydad ilipata ushindi wa bao 1-0 na kufanya timu hizo kufungana 1-1 kwani Simba nayo ilipata ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wake wa nyumbani wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Mchezo wa leo umefanyika katika uwanja wa Mohamed wa 5 uliopo mjini Casablanca ambapo Bouly Sambou alifunga goli pekee la ushindi lililopelekea timu hizo kupigiana penalti. Shomari Kapombe na Clatous Chama ndio wachezaji wa Simba waliopoteza mikwaju ya penalti, Simba sasa wameshindwa kufika nusu fainali na kama kawaida yao kutolewa kwenye hatua ya robo fainali

Rivers yawasili kuivaa Yanga

Picha
Klabu ya Rivers United ya Nigeria imewasili salama, Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa mkondo wa pili wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga SC Katika mchezo wa kwanza Yanga SC aliibuka na ushindi wa goli 2 -0 dhidi ya Rivers pale Nigeria.

Rais wa Wydad atinga mazoezini kuwapa hamasa wachezaji

Picha
Rais wa Klabu ya Wydad Casablanca, Said Naciri alihudhuria mazoezi ya mwisho ya Wydad kabla ya kumenyana na Simba SC Siku ya Ijumaa Katika Dimba la Mohammed