GORMAHIA YAINYUKA TENA YANGA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Klabu bingwa ya soka nchini Kenya ya Gormahia usiku huu imeinyuka bila huruma Yanga SC ya Tanzania mabao 3-2 mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Gormahia ilitangulia kujipatia bao la kwanza lililofungwa kunako sekunde ya 23 kipindi cha kwanza na mshambuliaji George Odhiambo ambaye alifunga lingine katika dakika ya 40 na timu hizo zilienda kupumzika kwa matokeo hayo.
Yanga walirejea na kasi mpya na kujipatia bao dakika ya 53 lililofungwa na Deus Kaseke likiwa pia ni goli la kwanza katika michuano hiyo ya pill kwa ukubwa Afrika, Jacques Tuyisenge aliifungia Gormahia goli la tatu na la ushindi dakika ya 64 kabla ya Raphael Saudi Lothi hajafunga bao la pill la Yanga dakika ya 80.
Yanga leo watamlaumu kipa wao Youthe Rostand ambaye aliwaggharimu karibu magoli mawili na baadaye kocha wa Yanga akamtoa na kumwingiza Benno Kakolanya