COASTAL UNION KUMSAJILI ALLY KIBA
Na Mwandishi Wetu. Tanga
Uongozi wa klabu ya soka ya Coastal Union ya jijini Tanga uko mbioni kumsajili mwanamuziki maarufu wa bongofleva hapa nchini Ally Saleh Kiba "Ally Kiba" na imepanga pia kumfanyia mapokezi makubwa staa Hugo.
Taarifa kutoka makao makuu ya Wagosi hao wa kaya waliorejea Ligi Kuu msimu huu wamedai wameshakubaliana na nyota huyo na kinachosubiriwa kwa sasa ni mkataba tu, Ally Kiba mbali na kujihusisha na muziki pia amekuwa mmoja kati ya wachezaji mpira wenye kiwango cha kuchezea timu za Ligi Kuu.
Mbali na Coastal Union ambao wamekubaliana naye, nyota huyo pia aliwahi kutakiwa na Toto Africans ya Mwanza ila walishindwana naye kutokana na mwanamuziki huyo kubanwa na shughuri sake za kimuziki lakini kwa Coastal Union mambo yatakuwa shwari, Coastal Union imejipanga kufanya vizuri kwenye ligi ijayo hivyo imeanza kujiimarisha kwa kusajili wachezaji bora
Kwa habari kamili gonga www.mambouwanjani.blogspot.com