Kagere, Niyonzima na Nyoni kuwafuata wenzao Uturuki kesho
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Wachezaji watatu wa kutumainiwa wa mabingwa wa soka nchini, Simba SC kesho watasafiri kuelekea Istanbul Uturuki kuwafuata wenzao waliosafiri mwishoni mwa juma lililopita.
Simba iliondoka na wachezaji 26 ikowaacha Erasto Nyoni, Haruna Niyonzima na Meddie Kagere ambao sasa watasafiri kesho, Mkuu wa kitengo cha habari wa mabingwa hao, Haji Manara amethibitisha safari hiyo na amedai mambo yote kuhusu safari yamekamilika.
Manara pia amedai kikosi kilichopo Uturuki kipo sehemu nzuri na mpaka sasa hawajacheza mchezo wowote wa kirafiki tofauti na watu wanaosambaza vibaya kuwa Simba imecheza mechi ya kirafiki na kufungwa mabao 6-0, Simba imeweka kambi katika hoteli ya Reen Park & Resort iliyopo jijini Istambul ikiwa na viwanja vitano vya kuchezea soka