Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2017

Straika wa Stand United aula Zimbabwe

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam. Mshambuliaji wa kimataifa wa  Stand United, raia wa Nigeria, Chidiabere Abaslim hatimaye amefuzu vipimo vya afya na kusajiliwa na mabingwa wa soka nchini Zimbabwe, Caps United kwa kandarasi ya miaka miwili. Chidiabere aliyewahi pia kuichezea Coastal Union ya Tanga ambayo akashuka nayo daraja kabla ya kurejea Stand United timu ambayo ilimuibua kisoka tangu alipojiunga nayo mwaka 2014. Mshambulizi huyo alikuwa na mwanzo mzuri msimu wake wa kwanza akiwa Stand United ambapo aliweza kuchuana na vinara wa magoli Ligi Kuu Bara, Coastal Union waliamua kumchukua ili awasaidie lakini kwa bahati mbaya Chidiabere aliumia na akashindwa kuisaidia timu hiyo isishuke daraja. Kwa maana hiyo Chidiabere atakuwepo kwenye kikosi cha mabingwa hao watakaposhiriki michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani kwani timu hiyo ndio mabingwa wa Zimbabwe

Waarabu wamfuata Msuva, Sauzi

Picha
Na Exipedito Mataruma. Rustenburg. Matajiri wa Morocco wamempandia ndege winga wa kimataifa wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simon Msuva na kumfuata Afrika Kusini ambapo yupo na timu ya taifa, Taifa Stars ambayo inashiriki michuano ya Cosafa Castle Cup. Msuva ameivusha Taifa Stars kutinga robo fainali ya kombe la Cosafa likiwa ni goli la kusawazisha dhidi ya Mauritius mchezo uliofanyika jana ukimalizika kwa sare ya 1-1. Jana vigogo wa timu ya Difaa El Jajida ya Morocco wameamua kutua Afrika Kusini na inasemekana wako tayari sasa kumnasa winga huyo aliye katika kiwango cha juu kwa sasa. Taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo zinasema kuwa Msuva alikataa mshahara wa Wamorocco hao ambao tayari wameshampata Ramadhan Singano 'Messi' wa Azam FC

Ronaldo siyo kwenye soka peke yake, apiga hat trik ya watoto

Picha
Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amebahatika kupata watoto wawili kwa mpigo baada ya mkewe kujifungua kwa mpigo. Sasa Ronaldo anakuwa baba wa watoto watatu na kumfanya adhihirishe makali yake kuwa yeye siyo kwenye mchezo wa soka pekee hata kunako familia anatisha. Ronaldo ametoka kushiriki kombe la mabara ambapo timu yake ya Ureno imeondoshwa kwa mikwaju ya penalti na Chile, mwanasoka huyo bora wa dunia ametishia kuihama Real Madrid ili kukwepa kodi Hispania

Tambwe asaini miaka miwili Yanga

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC wamezidi kuendelea kuwabakiza nyota wake baada ya usiku huu kuthibitisha kumuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wake Amissi Jocelyin Tambwe. Tambwe aliyejiunga na mabingwa hao misimu miwili iliyopita akitokea kwa mahasimu Simba, amesaini mkataba mpya leo ambao utamfanya aendelee kusalia hapo hadi mwaka 2019. Msimu wake wa kwanza Tambwe amekuwa mfungaji bora akifikisha mabao 21 na vilevile bado amekuwa katika kiwango kizuri na kufikia Yanga kunogewa naye na kumuongezea mkataba

TANZANIA YATINGA ROBO FAINALI COSAFA CUP

Picha
Na Exipedito Mataruma. Rustenburg. Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya Mataifa ya ukanda wa kusini mwa Afrika, Cosafa Castle Cup baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Mauritius. Mchezo huo uliokuwa mkali na wa kuvutia, Stars ilisawazisha bao kupitia kwa winga wake Simon Msuva aliyeingia kipindi cha pili. Kwa matokeo hayo Tanzania inaungana na Botswana, Zambia, Namibia, Lesotho, Swaziland na Afrika Kusini kucheza robo fainali huku zikisubiria timu nyingine moja kutoka kundi B. Katika mchezo mwingine wa kundi A, Angola ililazimishwa suluhu 0-0 na Malawi na kuifanya Tanzania isonge hatua nyingine kirahisi, Stars itakutana na mwenyeji Afrika Kusini, Bafana Bafana

Aveva, Kaburu nao kusota rumande

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam. Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake  Geofrey Nyange 'Kaburu' wote wawili wamewekwa rumande Kisutu hadi Julai 13 mwaka huu baada ya kukutwa na makosa ya utakatishaji fedha. Aveva na Kaburu wakishikiliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mchini (Takukuru) wakidaiwa kutumia vibaya madaraka yao, wawili hao walipandishwa mahakamani leo na kusomewa mashitaka yao. Wote wawili wamekutwa na hatia na kwakuwa makosa yao hayaruhusu dhamana wametupwa rumande hadi Julai13 mwaka huu watakapopandishwa tena mahakamani. Kwa mujibu wa Takukuru kupitia kwa Afisa habari wake, Musa Misalaba alisema Aveva na Kaburu wamekutwa na makosa ya utakatishaji fedha na kubwa ni usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye aliuzwa kwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia na ilidaiwa Simba ilipata zaidi ya milioni 600 lakini vigogo hao wakawadanganya Simba kwa kusema walimuuza kwa milioni 600 wakati si kweli

Malinzi kwishinei, atupwa rumande hadi Julai 3

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi na katibu mkuu wa Shirikisho hilo Celestine Mwesigwa wamekutwa na hatia ya utakatishaji fedha na wote wamewekwa rumande hadi tarehe 13 ya mwezi Julai watakapopelekwa tena mahakamani. Kwa maana hiyo Jamal Malinzi ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo atakuwa amejiengua rasmi kwenye nafasi hiyo kulingana na vigezo na masharti ya kugombea. Malinzi, Mwesigwa na Nsiana wamesomewa mashtaka 28... Kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa EXCOM imeridhia kubadilishwa kwa Signatories wa Bank hii inamhusu Malinzi na Mwesigwa pia, Kufoji risiti za kuwa Malinzi anaidai TFF (risiti zipo zaidi 20 zinazodaiwa kufojiwa) hii inamhusu Malinzi pekee Na Mwisho ni shtaka la kutakatisha fedha dola za kimarekani 375418 hii inamhusu Malinzi, Mwesigwa na Nsian

Mario Balotelli akubali yaishe, kuongeza mkataba mpya Nice

Picha
Mshambuliaji wa zamani wa Inter Milan, Man City na Liverpool, Mario Balotelli raia wa Italia, amekubali yaishe baada ya kukubali kusaini kandarasi nyingine katika klabu yake ya Nice ya Ufaransa inayoshiriki Ligue 1. Balotelli alikuwa katika mvutano mkubwa na timu yake hiyo aliyoitumikia baada ya kuihama Inter Milan ya Italia ambayo ilimchukua baada ya kuachana na Liverpool. Hivi karibuni Mario Balotelli alivumishwa kutaka kurejea tena Uingereza ambapo vilabu kadhaa vilitaka kumnyakua ikiwemo Arsenal, pia alipokea ofa mbalimbali barani Ulaya ambapo ilisalia dakika chache kutimka kikosini hapo. Lakini mabosi wa Nice wakafanya naye mazungumzo ambayo yameweza kumbakisha tena straika huyo mtukutu

OKWI AWAPONZA KABURU, AVEVA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini, (Takukuru), inawashililia Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange 'Kaburu' kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. Inadaiwa Aveva na Kaburu kwa pamoja walijipatia pesa za mauzo ya kiungo mshambuliaji wa kimataifa raia wa Uganda Emmanuel Okwi (Pichani kulia) kwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia. Aveva na Kaburu walijipatia zaidi ya dola 300,000 sawa na shilingi milioni 600,000 lakini wakawadanganya Wanasimba na kusema walimuuza kwa kiasi hicho cha pesa ambacho ni dola 300,000. Hata hivyo fedha hizo za mauzo ziliingizwa kwenye akaunti binafsi na si ya klabu, Takukuru imewahoji viongozi hao kila mmoja na imefahamika kuwa itawafikisha mahakamani, Taasisi hiyo pia inawashikilia viongozi wa TFF, Jamal Malinzi na Celestine Mwesigwa

Kimeeleweka, Ngoma asaini miwili Jangwani

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Baada ya kuzuka kwa taarifa kwamba mshambuliaji wa kimataifa raia wa Zimbabwe, Donald Ndombo Ngoma amesaini mkataba wa miaka mitatu katika timu ya Polokwane City ya Afrika Kusini, hatimaye amemaliza ubishi baada ya mchana wa leo kusaini mkataba wa miaka miwili na timu yake ya Yanga SC. Ngoma pia alikuwa akihitajika na mahasimu Simba, lakini ameamua kumalizana na timu yake aliyoitumikia misimu miwili kwa mafanikio makubwa akiipa ubingwa wa bara mara mbili, kombe la FA, Ngao ya Hisani pamoja na kuiwezesha kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika. Ngoma alisajiliwa na Yanga akitokea FC Platinum ya kwao Zimbabwe amekuwa mmoja kati ya washambuliajj nyota ambao waliweza kutolewa udenda na vilabu mbalimbali barani Afrika

MALINZI ADAKWA NA TAKUKURU

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam. Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (Takukuru) leo imemkamata Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (Tff) Jamal Malinzi pamoja na katibu mkuu wa Shirikisho hilo Mwesigwa Celestine kwa tuhuma mbalimbali za rushwa. Ukweli wa kukamatwa kwao haujawekwa wazi licha kwamba Takukuru imethibitisha kuwashikilia watu hao kwa mahojiano zaidi na kama ikithibitika ni kweli wana hatia watafikjshwa mahakamani. Kukamatwa kwa Malinzi kunatishia nafasi yake ya kurejea tena madarakani katika uchaguzi ujao unaotaraji kufanyika Agosti 12 mwaka huu mjini Dodoma, hata hivyo Mambo Uwanjani imejulishwa kuwa Malinzi anahusika kwa ufujaji wa fedha

Uingereza yasikitishwa na Tanzania kumpoka mtaa Wanyama

Picha
Vyombo vya habari tena vile vikubwa nchini Uingereza vimelaani vikali kitendo cha Tanzania kumpora mtaa mwanasoka wa kimataifa anayeichezea klabu kubwa duniani ya Tottenham Hotspurs inayoshiriki Ligi Kuu ya Premia, Victor Wanyama. Wanyama ambaye ni raia wa Kenya ana uhuru wa kuchagua nchi yoyote kwenda kupumzika na katika mapumziko yake akaichagua Tanzania katika jiji la Dar es Salaam kama sehemu yake ya mapumziko baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Uingereza. Akiwa jijini Dar es Salaam, Wanyama alitembelea Ubungo Shekilango kwenda kutazama Ndondo Cup ambapo pia alikutana na mbunge wa Ubungo, Boniface Jacob na kumpa mtaa, Wanyama alipewa mtaa wa Viwandani na kuitwa jina lake Victor Wanyama Street. Lakini kesho yake uongozi wa serikali ya mtaa huo ukang' oa bango lililowekwa likielekeza mtaa huo, pia serikali ya mtaa huo ikasema wameamua kufuta jina la mtaa kwa maana hazikufuatwa taratibu. Uingereza imelaani kitendo ikisema haijamtendea haki Wanyama na itambue kuwa mwanasoka huy

STARS YAKOMAA KILELENI SAUZI

Picha
Na Exipeditor Mataruma. Afrika Kusini. Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeilazimisha sare tasa 0-0 dhidi ya Angola mchezo wa kundi A michuano ya Cosafa Castle Cup Uwanja wa Royal Bafokeng mjini Rustenburg, Afrika Kusini. Mechi hiyo ilipigwa usiku kuanzia saa 2:30 ilishuhudiwa kiungo wake Muzamiru Yassin Selembe akiibuka Man of the Match akionyesha kiwango kikubwa. Kwa maana hiyo Stars imefikisha pointi 4 ikiongoza kundi A kwa wingi wa mabao dhidi ya Angola ambao nao wana pointi 4 kama Stars ila wao wana bao moja wakati Stars inayo mawili, keshokutwa Stars itacheza na Mauritius mechi ikipigwa jioni

YANGA MAFIA, WAMSHUSHA NGOMA USIKU HUU

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam. Yanga jeuri bwana, usiku huu wamemshusha mshambuliaji wao Mzimbabwe Donald Ngoma anayedaiwa kumwaga wino katika timu ya Polokwane City ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu. Awali katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa aliwahakikishia Wanayanga kwamba ni lazima wampe mkataba mpya mshambulizi wao Donald Ngoma. Lakini jioni ya leo kumezuka taarifa kuwa mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu katika timu ya Polokwane City ya bondeni kwa Jacob Zuma, Mambo Uwanjani inajulishwa usiku huu Ngoma ametua Airport ya Dar es Salaam tayari kwa kusaini mkataba mpya. Huo ni umafia mkubwa kuwahi kufanywa na mabingwa hao kwani Ngoma pia alitajwa kujiunga na Simba ambao ni mahasimu wa Yanga

Mengi atajwa kuifadhili Yanga

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Inaelezwa kuwa mpenzi na mwanachama wa Yanga na mfanyabiashara mkubwa hapa nchini, mmiliki wa makampuni ya IPP, Reginald Abrahamu Mengi anatajwa kutaka kuisaidia timu hiyo baada ya kukimbiwa na aliyekuwa mwenyekiti wake Yusuf Manji. Mengi na Manji walikuwa hawaivi chungu kimoja na kutajwa kwake kunahusisha mpango wa kujitolea kama mshabiki wa timu hiyo, bado Mambo Uwanjani haijajulishwa kama lini kibopa huyo ataanza kumwaga mamilioni. Mengi inadaiwa ni mpenzi na mwanachama wa Yanga lakini hakuwahi kujitokeza hata mara moja wakati timu hiyo inafadhiliwa na Yusuf Manji kwakuwa hawakuwa wakielewana ingawa wote ni wamiliki wa makampuni na Mengi ndiye mwenyekiti wao

NGOMA ASAINI POLOKWANE CITY MIAKA MITATU

Picha
Na Mwandishi Wetu. Afrika Kusini. Hatimaye maisha ya mshambulizi wa kimataifa raia wa Zimbabwe katika klabu ya Yanga SC ya Tanzania yamefikia tamati baada ya leo kusaini kandarasi ya miaka mitatu kwa klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu ya Absa. Ngoma amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na Yanga na alikuwa katika mvutano mkali na uongozi wa timu hiyo, mapema leo katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa  aliwahakikishia Wanayanga kuwa wamejipanga kumuongezea mkataba straika huyo aliyekuwa katika kiwango kizuri. Ngoma amefuzu vipimo vyake vya afya na Polokwane City wakaamua kumpa mkataba wa miaka mitatu, akiwa na Yanga, Ngoma aliipa ubingwa wa bara mara mbili mfululizo, kombe la FA, na kuiwezesha kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika

RASHID MANDAWA HAENDI KOKOTE

Picha
Na Albert Babu. Morogoro Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, umesema mshambulizi wake Rashid Mandawa "Chididebe" haendi kokote na wamepanga kumwongezea mkataba mpya. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Tobias Kifaru amesema Mandawa hawezi kuihama Mtibwa kwakuwa bado wanamuhitaji. Ameongeza kuwa tetesi za usajili kwa nyakati hizi ndiyo wakati wake lakini ukweli unabaki palepale, anasema Mandawa ni mshambuliaji mahiri hivyo haiwezi kuwa rahisi kumwachia aende. Mtibwa Sugar ilimchukua Mandawa kutoka Stand United na tangu atue hapo ameweza kuisaidia timu hiyo na kuendelea kusalia katika nafasi za juu, pia Mtibwa imesema itaendelea kuwabakiza karibu nyota wake wote hasa baada ya beki wake Ally Shomari kujiunga na Simba ya Dar es Salaam

Ni vita ya Tanzania na Angola leo

Picha
Na Exipedito Mataruma. Afrika Kusini. Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jioni ya leo kitashuka uwanjani kwa mara ya pili kukwaruzana na Angola katika mchezo wa michuano ya kombe la COSAFA Castle Cup. Tanzania inahitaji ushindi katika mchezo huo ili iweze kutinga robo fainali ya michuano hiyo inayoshirikisha mataifa 13, Tanzania ikishiriki kama nchi mwalikwa, ilianza vema katika fainali hizo baada ya kuilaza Malawi mabao 2-0. Mabao yote ya Tanzania yalifungwa na winga wake Shiza Kichuya, kuelekea katika mchezo wa jioni, kocha wa Tanzania Salum Mayanga amesema vijana wake wapo tayari kwa mchezo huo na amewaahidi Watanzania zawadi nzuri ya sikukuu ya Iddi El Fitr

Yanga yamwandalia mkataba mpya Ngoma

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Mabingwa wa soka nchini, Yanga SC imejipanga kumwongezea mkataba mpya mshambuliaji wake wa kimataifa, raia wa Zimbabwe, Donald Ndombo Ngoma. Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema leo kuwa klabu yake imejipanga kumbakiza Ngoma na itampa mkataba mpya. Mkwasa amedai jukumu hilo la kuhakikisha Ngoma anabaki Yanga na kuondoa uzushi unaozagaa kuwa straika huyo anaenda upande wa pili, Mkwasa ambaye aliwahi kuichezea na kuinoa Yanga miaka iliyopita, amedai Yanga haiko tayari kuona nyota wake wa kikosi cha kwanza wanatoweka. Juma lililopita, Yanga ilimpoteza kiungo wake wa kutumainiwa, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda waliyeshindwana naye huku taarifa zikionyesha kuwa ataelekea upande wa pili baada ya kumtengea mamilioni ya shilingi

OKWI ASAINI SIMBA MIAKA MIWILI

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi raia wa Uganda amesaini kandarasi ya miaka miwili kujiunga na Simba SC msimu ujao huku akifunguka mengi na kudai atauwasha moto kwenye ligi kuu. Okwi anajiunga na Simba kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo akitokea SC Villa ya kwao Uganda aliyojiunga nayo akitokea Denmark katika klabu ya Sonderjyske inayoshiriki Ligi Kuu. Mshambuliaji huyo alivunja mkataba na timu hiyo baada ya kudaiwa kushuka kwa kiwango chake lakini Okwi amesema wasibiri ligi ianze auwashe moto, Naye mfadhili wa Simba, Mohamed Dewji "Mo" amesema yeye ndiye aliyefanikisha usajili huo na amedai ni zawadi kwa mashabiki wa Simba. Okwi amesaini mkataba huo mbele ya makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange "Kaburu", Okwi alitua nchini jana usiku akitokea kwao Uganda

Mtaa wa Wanyama wafutwa

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Watu wasiojulikana wameling' oa bango lililopachikwa rasmi jana na meya wa Ubungo Mhe Boniface Jacob likitambulisha jina la mtaa mpya wa Victor Wanyama Street maeneo ya Ubungo Shekilango. Victor Wanyama nyota wa Tottenham Hotspurs ya Uingereza ambaye ni raia wa Kenya jana alizuru maeneo hayo ya Shekilango njia na madhumuni kucheki michuano ya Ndondo Cup ndipo alipolakiwa na meya Jacob wa Ubungo. Meya huyo akaamua kumpa heshima mchezaji huyo wa kimataifa wa Kenya na kuubadili mtaa wa Viwandani jina ambapo akaupa jina la Victor Wanyama na bango likawekwa, lakini haijajulikana ni nani aliyekwenda kung' oa bango hilo

Mtanga awa bingwa wa draft Tabata Mtambani

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Hatimaye michuano ya kumsaka bingwa wa mchezo wa draft imemalizika usiku huu huko Tabata kwa kupigwa mchezo mmoja wa fainali ambapo kijana Michael Mtanga alimgalagaza mpinzani wake Charles Chinguile kwa bao 1-0. Fainali hiyo haikuwa nyepesi kwa Michael Mtanga, kwani ilimchukua raundi ya pili kupata bao ambalo limekuja kuwa la ushindi, hadi mwisho kijana Michael Mtanga ameweza kuwa bingwa. Michael Mtanga alikabidhiwa kuku wake jogoo na mmoja wa waratibu wa mashindano hayo Mussa Benjamin, naye mshindi wa pili Charles Chinguile alikabidhiwa mchele kilo tano akiwa kama mshindi wa pili wa mashindano hayo yaliyoanza Jumapili iliyopita kwa kushirikisha watu 18. Hata hivyo Mratibu msaidizi wa mashindano hayo Mussa Kibichwa amesema kutaanza ligi nyingine ambapo bingwa atapatiwa mchele kilo kumi wakati mshindi wa pili atapewa kilo tano na wa tatu kilo tatu Michael Mtanga akichuana na Chinguile fainali ya draft leo Tabata Mtambani Mussa Benjamin (Kulia) akim

Nyamlani ashituka, ajitoa mbio za urais TFF

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mgombea wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, (TFF) Athuman Nyamlani amejitoa katika kinyang' anyiro hicho leo. Kwa mujibu wa Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema Nyamlani amewaandikia barua ya kujitoa kwenye mbio za kuwania Urais wa Shirikisho hilo na hakuweza kuwapa sababu zilizopelekea kujitoa kwake. Lakini kwa taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo inafahamu fika kuwa Nyamlani ameshitukia hujuma zinazofanywa na mmoja wa washindani wake wakuu (Jina tunalo). Kujitoa kwa Nyamlani sasa kunaongeza joto kwa washiriki waliosalia kwenye mbio hizo, Nyamlani aliwahi kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho hilo likiwa chini ya Leodegar Tenga

Kichuya aibeba Stars, Cosafa

Picha
Na Exipeditor Mataruma. Afrika Kusini. Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jioni ya leo imefanikiwa kuanza vema michuano ya Cosafa baada ya kuilaza timu ya taifa ya Malawi kwa mabao 2-0 mchezo wa kwanza kundi A. Stars ilijipatia mabao yote mawili katika kipindi cha kwanza yote yakifungwa na Shiza Ramadhan Kichuya kipindi cha kwanza mabao ambayo yaliipa ushindi Stars na kuanza vema michuano hiyo tofauti na mwaka jana ilipoondolewa mapema. Mchana kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga alisema lazima kikosi chake kitachomoza na ushindi kwakuwa Malawi anawafahamu vizuri, Stars itashuka tena dimbani Jumanne kukwaruzana na Angola ambao leo wanachuana na Mauritius

Taifa Stars yaapa kuilaza Malawi

Picha
Na Exipedito Mataruma. Afrika Kusini. Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inajitupa uwanjani hapa Afrika Kusini kukwaruzana na timu ya taifa ya Malawi mchezo wa michuano ya COSAFA kundi A. Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema vijana wake wapo tayari kwa mchezo huo na wataweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo, michuano hiyo inaanza leo na michuano hiyo inajumlisha karibu timu ,13. Tanzania, Angola, Mauritius na Malawi zenyewe zimepangwa kundi A wakati kundi B lina timu za Shelisheli, Msumbiji, Madagascar na Zimbabwe, timu za Afrika Kusini, Zambia, Botswana, Namibia na Lesotho zitacheza mechi za mtoano

OKWI AMETUA JANA TAYARI KWA KAZI

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi amewasili nchini jana usiku majira ya saa nne akitokea kwao nchini Uganda tayari kwa kusaini mkataba wa miaka miwili. Ujio wa Okwi unadhihirisha kuwa Simba hawataki mchezo na wamejipanga kisawasawa kukiboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao, Okwi anajiunga na Simba kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 2010 akitokea SC Villa ya nyumbani kwao Uganda. Okwi aliuzwa kwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia mwaka 2013 na baadaye akavunja mkataba wake na kurejea tena kwao Uganda na kujiunga na SC Villa, kisha Villa wakawauzia Yanga SC kwa mkataba wa miaka miwili. Lakini Okwi alitumikia Yanga miezi sita tu na kuvunja mkataba wake na kujiunga tena kwa mara ya pili Simba, mwaka 2015 Okwi aliuzwa tena nchini Denmark katika klabu ya Sonderjsky ambapo nako hakudumu akavunjiwa mkataba wake na kurudi tena nyumbani kwao Uganda. Okwi akarejesha makali yake hadi kuitwa kwenye ti

Wanyama apewa mtaa Dar

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs ya Uingereza, Victor Mugubi Wanyama raia wa Kenya, leo amekabidhiwa mtaa wenye jina lake. Wanyama yupo nchini tangu majuzi na ana ziara ya mapumziko kabla hajarejea kazini Uingereza kwenye timu yake inayoshiriki Ligi Kuu ya Premia, akiwa hapa nchini Wanyama ametembelea maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam. Leo Wanyama alitembelea Ubungo ambapo alilakiwa na meya wa Manispaa hiyo Boniface Jacob na kutembelea mtaa wa viwandani uliopo Shekilango, kwa heshima, meya Jacob aliamua kuupa jina la Victor Wanyama mtaa wa viwandani. Kwa maans hiyo Wanyama anakuwa mwanasoka wa kwanza kupewa mtaa kwa hapa nchini, heshima hiyo ni kubwa kwake, pia Wanyama alitembelea Azam Tv ambapo alizungumza na waandishi wa habari

Yassar awa mshindi wa tatu michuano ya draft Tabata

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kijana aliyefahamika kwa jina la Yassar usiku huu amefanikiwa kupata ushindi wa tatu katika michuano ya kumtafuta bingwa wa draft Tabata Mtambani baada ya kumfunga bao 1-0 mpinzania wake Mroka. Ushindi huo haukuja bure ni baada ya kucheza michezo mitatu na miwili walitoka suluhu huku wa mwisho aliweza kuibuka na ushindi, Yassar alifikia kucheza mechi hiyo ya mshindi wa tatu baada ya kuondoshwa kwenye nusu fainali na mpinzani wake Charles Chinguile. Yassar alifungwa bao 1-0, wakati Mroka naye alifungwa na Michael Mtanga pia bao 1-0, fainali itapigwa kesho kati ya Charles na Michael na bingwa atapata kuku jogoo.

Sportpesa kusitisha ufadhili wake Kenya

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kampuni ya michezo ya kubahatisha Sportpesa ya nchini Kenya imetishia kujiondoa ufadhili wake kwa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) baada ya serikali ya nchi hiyo kuwaongezea ongezeko la kodi la asilimia 35. Ofisa wa Sportpesa nchini Kenya, Ronald Karauri amesema kampuni yake itaacha kudhamini Ligi Kuu ya Kenya kwa sababu ya ongezeko hilo la kodi. Endapo Sportpesa itaacha kufadhili ligi ya Kenya litakuwa anguko kubwa kwa soka la nchi hiyo, Sportpesa inadhamini pia vilabu vya Gor Mahia, AFC Leopards, Nakuru All Stars na Tusker FC. Naye Afisa wa Kampuni ya Ligi Kuu (KPL) Jack Aduga amesema kujitoa kwa Sportpesa ni pigo kubwa kwao, kampuni hiyo imekuwa ikijitolea mamilioni ya shilingi kufadhili shughuri za soka hivyo kama wataondoka hakuna atakayeweza kubeba mzigo wa soka la Kenya

Mshahara wamwondoa Singano, Azam FC

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Dau nono litalotolewa na klabu ya Difaa El Jajida ya Morocco inadaiwa kumwondoa kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano "Messi" aliyekataa kuongeza mkataba mwingine. Messi kama anavyofahamika na wengi, amekataa kusaini mkataba mpya na Azam ambayo imempunguzia dau na kuamua kugeukia dili ya Morocco ambapo ametamgaziwa mshahara mnono wa Dola 2000 kwa mwezi sawa na shilingi Milioni 4.4. Uzushi unaoenea mitaani kuwa winga huyo wa zamani wa Simba na Taifa Stars kuhusishwa na mpango wa kurejea Simba si kweli, Messi hana mpango wa kurejea Simba isipokuwa amegomea mkataba mpya wa Azam na anataka kupaa zake majuu

Nusu fainali ya Draft kupigwa kesho Tabata

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mashindano ya kumsaka bingwa wa mchezo wa Draft kesho yanafikia hatua ya nusu fainali baada ya hii leo kuchezwa mechi nne za robo fainali na washindi wanne kupatikana. Musa Kibichwa mratibu msaidizi wa michuano hiyo ameuambia mtandao huu kuwa kesho zitachezwa mechi mbili za robo fainali. Kibichwa amewataja watakaochezwa nusu fainali ni Charles Chinguile 'Paparazi' atakayekipiga na Yassar wakati nusu fainali nyingine ni kati ya Michael Mtanga na Mroka. Jioni ya leo zilipigwa mechi za robo fainali ambapo Athuman Mpemba alifungwa bao 1-0 na Mroka, Charles Chinguile alimnyanyasa Geofrey Mbawala mabao 2-0 wakati Yassar alimtungua Richard Ted kwa bao 1-0 huku Michael Mtanga alimchapa Cosmas mabao 2-0, bingwa atapata kuku jogoo

Raphael Daudi injini mpya Jangwani

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC nao wanazidi kujiimarisha kwa kuziba mapengo yaliyopo, baada ya kuachana na kiungo wake wa Kinyarwanda Haruna Niyonzima, hatimaye Wanajangwani hao wamefikia makubaliano mazuri na kiungo wa Mbeya City, Raphael Daudi. Daudi kiungo mshambuliaji wa Mbeya City ameonyesha nia ya kujiunga na mabingwa hao wa Bara na inasemekana atasaini mkataba wa miaka miwili, endapo Yanga itamsainisha kiungo huyo atakuwa mchezaji wa pili baada ya Abdallah Shaibu 'Ninja' aliyesajiliwa hivi karibuni. Pia Wanajangwani hao wanakaribia kumtambulisha kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Ajibu Migomba ambaye naye anadaiwa kusaini mkataba wa miaka miwili

Singida United yamnasa mbaya wa Yanga, Azam

Picha
Na Saida Salum. Singida Timu ya Singida United ya mkoani Singida imeendelea kutikisa kwenye usajili baada ya kufanikiwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili beki wa kushoto na kulia, Miraji Adam. Kikosi hicho kilichopanda ligi kuu mwaka huu, imemalizana na mlinzi huyo ambaye amewahi kuzichezea Simba na Coastal Union, Miraji Adam aliyekuwa akiichezea African Lyon iliyotelemka daraja atavaa uzi mpya wa Singida United. Huu ni usajili wa nane kwa Singida United smbayo imeamua kukiboresha kikosi chake kilichoungana na Njombe mji na Lipuli ya Iringa kucheza Ligi Kuu, Miraji anakumbukwa vema na vilabu vya Yanga na Azam kwani vyote alivitungua

HIMID MAO AITOSA YANGA

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami 'Ninja' amesema alishakataa dili ya kujiunga na Yanga kwakuwa bado ana mkataba na Azam FC. Mao alisema hayo jana akiwa Uwanja wa ndege wa kimataifa Mwl Nyerere tayari kwa safari ya kuelekea nchini Afrika Kusini. Amesema ni kweli Yanga walimtafuta lakini aliwakatalia waziwazi mpango wao wa kumuhitaji katika kikosi chao, alisema kiungo huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. "Yanga nimewakatalia, kwa sasa siwezi kucheza tena Tanzania endapo nitamaliza mkataba wangu, matarajio yangu ni kucheza nje", amesema Mao ambaye ni mtoto wa kiungo wa zamani wa Pamba FC ya Mwanza. Hivi karibuni kiungo huyo alienda kufanya majaribio nchini Denmark katika klabu ya Randers inayoshiriki Ligi Kuu, haijajulikana kama alifaulu au amefuzu

Sarah avunja rekodi ya usajili Liverpool

Picha
Timu ya Liverpool ya Uingereza imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa AC Roma ya Italia, Mohamed Salah kwa kumpa kandarasi ya miaka mitano kwa kuvunja rekodi ya mauzo Paundi Milioni 39. Rekodi ya mauzo ya usajili iliwekwa na Andre Carol ya Paundi Milioni 35, kwa maana hiyo Sarah, raia wa Misri anakuwa mchezaji ghali kwenye kikosi hicho kitakachoshiriki Ligi ya mabingwa barani Ulaya. Hata hivyo Sarah amefurahia usajili wake wa kutua Anfield aliamini ataipa mafanikio timu hiyo iliyotwaa taji la ligi ya premia mara 18. "Nimefurahia kujiunga Liverpool, nitaitumikia kwa moja mmoja, naamini tutatwaa mataji", alisema Sarah alipotambulishwa rasmi

Maelfu wajitokeza kumzika Ally Yanga

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Watu mbalimbali wakiwemo wapenzi na mashabiki wa soka wamejitokeza kwa wingi kumzika shabiki maarufu wa klabu ya Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars, Ally Mohamed maarufu Ally Yanga aliyezikwa mjini leo mjini Shinyanga. Ally Yanga alifariki katika ajali ys gari aina Rover Four iliyopinduka na kupondekapondeka vibaya Mpwapwa mkoani Dodoma akiwa kwenye harakati za mbio za Mwenge. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliwakilishwa na ndugu Mpogolo ambaye ni naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania Bara, marehemu Yanga anakumbukwa kwa staili yake ya ushangiliaji iliyomfanya ajulikane. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ametuma salamu zake za rambirambi akionyesha kuguswa na msiba huo mzito kwa Wanayanga na wanamichezo kwa ujumla

MAVUGO APATA TIMU RWANDA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Klabu ya Simba, Laudit Mavugo raia wa Burundi amepata timu nchini Rwanda ambayo iko tayari kumnunua akitokea Simba SC ya Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa moja kutoka nchini Kenya, inasema kuwa Klabu ya AC Kigali ya Rwanda inayoshiriki Ligi Kuu Bara imetenga kumchukua straika huyo na kumpa kandarasi ya miaka miwili. Mavugo alifunga mabao 10 akiwa Simba iliyomaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Yanga SC, pia ameiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa kombe la FA. Simba sasa itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani na imeanza kuboresha kikosi chake ambapo tayari nyota mbalimbali wanatajwa kutua wakiwemo John Bocco, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma na Waltel Bwalya

Yanga yaibomoa Azam FC, yampa miaka miwili Gadiel Michael

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania Bara  Yanga SC nao wameibomoa Azam FC ambayo hivi karibuni iliwanyang' anya wachezaji wake watatu iliotaka kuingia nao mikataba. Yanga imemnasa beki wa kushoto wa Azam na timu ya taifa, Taifa Stars, Gadiel Michael kwa kumpa kandarasi ya miaka miwili. Taarifa zenye uhakika kabisa zinasema mchezaji huyo ameridhia kutua Yanga lakini atalazimika kufanya siri ili mkataba wake umalizike na ndiyo ajiunge na Yanga. Mkataba wa Gadiel unaishia Desemba mwaka huu hivyo atalazimika kuitumikia Azam katika mzunguko wa kwanza, na mzunguko wa pili ataanza kuitumikia Azam, Azam FC nao wameanza kuachana na wachezaji wake na inasemekana mishahara mikubwa inawashinda kwa sasa

Stars kupaa bondeni usiku

Picha
Na Salum Fikiri Jr Timu ya taifa, Taifa Stars, inaondoka leo usiku wa saa moja na nusu kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo itashiriki michuano ya kombe la Cosafa ikiwa kama mwalika. Alfred Lucas Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini (TFF) amesema kikosi cha timu ya taifa kinaondoka usiku wa saa moja na nusu hii leo kuelekea Afrika Kusini ambapo itashiriki michuano ya Cosafa. Lucas amedai kikosi kikitoka Afrika Kusini kitarejea nchini kisha kitaanza maandalizi dhidi ya Rwanda kusaka tiketi ya kufuzu fainali za kombe la CHAN, hata hivyo Lucas amedai kikosi cha Stars kinachonolewa na Salum Mayanga kitafanya vizuri katika mashindano hayo

Manara amnanga Mbolembole

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Afisa Habari aliyesimamishwa wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara amemvaa blogger wa tovuti ya Shafih Dauda, Baraka Mbolembole na kumwambia aache kuiandika vibaya Simba kila anapokurupuka. Manara amesema kuwa Mbolembole ana tabia ya kuiandika vibaya Simba hata kama inafanya vizuri, Akiandika jana kwenye ukurasa wake wa Twitter, Manara amefunguka mengi akianza kumsifu Shafih Dauda anayefanya kazi yake Clouds Media kupitia redio na televisheni. Shafih Daud ni mmoja ktk watu wa soka hapa nchini,ni rafiki yangu tunaoongea muda mrefu hususan masuala ya mchezo huu murua,uliyobeba maisha yangu,pia ni kijana mwenzangu tunaoheshimiana sana,kiasi cha kwamba sijawahi kwa namna yoyote ile kukwazana nae,hata kama tunatofautiana kimtazamo ktk baadhi ya mambo, hususan ya Soka. Wengi mnakumbuka sakata la Ramadhan Singano,jinsi lilivyokaribia kuvunja uhusiano wetu,kwa jinsi alivyolivalia njuga bila kuujua ukweli,lakini mwishoe ni yy juzi tu aliandika kuwa Singano a

Kaburu kujiuzuru umakamu wa Rais Simba

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kwa mujibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limesisitiza kuwa ili uchaguzi mkuu wa TFF ufanyike ni lazima wagombea wote watambue kuwa endapo uchaguzi utaisha na ukapata viongozi wake ni lazima wasalie na nafasi moja tu. Mohamed Kiganja kaimu katibu mkuu wa Baraza hilo alisisitiza masharti hayo yafanye kazi, hiyo inakuja kufuatia viongozi wa Shirikisho hilo kuwa na nafasi ya madaraka zaidi ya moja. Makamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange "Kaburu" anayegombea umakamu wa rais wa TFF yuko hatarini kujiuzuru nafasi yake ya umakamu wa rais katika klabu yake ya Simba endapo atachaguliwa. Siyo Kaburu peke yake hata Jamal Malinzi ambaye ni rais wa Shirikisho hilo, atalazimika kuachia ngazi nafasi ya mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Kagera kama atafanikiwa kutetea kiti chake

Ajibu sasa rasmi Yanga, mkataba wake wawekwa hadharani

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Yanga SC imeamua kuweka hadharani usajili wa mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu Migomba 'Kadabla' na imeuanika mkataba wake wa miaka miwili. Uongozi wa Yanga kupitia kwa katibu mkuu wake Charles Boniface Mkwasa aliwaambia Wanayanga kuwa wameshamslizana na Ajibu na kinachosubiriwa kwa sasa ni kumalizika kwa mkataba wake na Simba mwishoni mwa mwezi huu. Ajibu aligomea kuongeza mkataba mpya na Simba lakini akalainika kusaini mkataba wa miaka miwili Jangwani na inaaminika kuwa ana mapenzi makubwa na Yanga na sasa atavaa uzi wa kijani na njano, Ajibu aliibuliwa na Simba akipitia timu ya vijana, Simba B

Musa Kisocky akalia kuti kavu Sputanza, mbinu chafu kumuondoa zasukwa

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Imefahamika kuwa mwenyekiti wa chama cha wanasoka, (SPUTANZA) Musa Kisocky yuko hatihati kung: olewa katika nafasi hasa baada ya katiba ya chama hicho kuwekewa mkazo kuwa mwenyekiti lazima awe amecheza soka tena Ligi Kuu. Marekebisho ya katiba huenda yakafanywa hivi karibuni na inadaiwa ina njama za kumtoa mwenyekiti huyo aliyekaa madarakani kwa kipindi kirefu sasa. Baadhi ya wanachama wa Sputanza wanasema Kisocky anakiongoza chama hicho lakini hana sifa kwakuwa hakucheza Ligi Kuu ingawa yeye mwenyewe amekuja juu. Kisocky slipoulizwa alikiri ni kweli yeye hakucheza Ligi Kuu lakini amewahi kucheza ligi ambayo kwa miaka hiyo ilikuwa kuu, "Nimecheza mpira zamani kwenye timu ya Asante Tololi ya Dar es Salaam, zamani kulikuwa na ligi iliyojulikana kama klabu bingwa", alisema Kisocky ambapo aliwashangaa wanaompinga ambapo amedai kucheza Simba au Yanga ndiyo kunakowaaminisha watu

RASMI: YANGA YANAWA MIKONO KWA NIYONZIMA, NJIA NYEUPE MSIMBAZI

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Katibu mkuu wa klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa, leo amewaambia Wanayanga kuwa mchezaji wao Haruna Niyonzima wameshindwana katika suala la kuongeza kandarasi nyingine baada ya kumalizika kwa ule wa miaka miwili Julai mwaka huu. Mkwasa amewaambia Yanga kuwa Niyonzima walikuwa naye kwa misimu sita kwa mafanikio lakini sasa umefika mwisho na wanamruhusu kwa mikono miwili aende huko anakotaka kwenda. Niyonzima alifunguka jana kuwa bado yeye ni mchezaji wake wa Yanga hadi Julai mwaka huu, lakini bado hajasaini kokote licha ya kuenezwa taarifa kuwa amesaini Simba miaka miwili, Mkwasa amemtakia kheli kiungo huyo raia wa Rwanda aliyetua Yanga akitokea APR ya Rwanda

Ronaldo amgomea Perez, anarudi Man Utd

Picha
Mshambuliaji wa kimataifa Cristiano Ronaldo raia wa Ureno amekataa kusalia Real Madrid ya Hispania na anataka kurejea Manchester United ya Uingereza. Licha ya Rais wa Real Madrid Fiorentin Perez  kuwahahakishia mashabiki wa timu hiyo kuwa atambakisha Ronaldo ambaye hivi karibuni alihusishwa na kashfa ya ukwepaji kodi. Ronaldo alituhumiwa na mamlaka za Hispania kuwa alikwepa kodi mwaka 2011 hadi 2014 hivyo anadaiwa jumla ya Dola Milioni 16.5 kitendo kilichopelekea kuamua kutangaza msimamo huo wa kutoweka. Ronaldo amewaambia rafiki zake kuwa anarejea katika klabu chake cha zamani cha Manchester United kitendo kinachoamsha furaha kwa mashabiki wa Old Trafford kumuona mfalme wa soka duniani akitua kwao

Kiemba mbioni kutua Mtibwa Sugar

Picha
Na Saida Salum. Morogoro Kiungo wa zamani wa Kagera Sugar, Yanga, Simba na Taifa Stars, Amri Ramadhan Kiemba anakaribia kujiunga na Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro tayari kabisa kwa ajili ya msimu ujao. Kiemba aliyekuwa akiichezea Stand United anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Mtibwa Sugar timu ambayo imekuwa ikifanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara, miamba hiyo ya mjini Morogoro imethibitisha kumnasa kiungo huyo. Akiwa Simba, Kiemba aling' ara mno mpaka kuitwa timu ya taifa, Taifa Stars na aliachwa na mabingwa hao wa kombe la FA na kuelekea Shinyanga kujiunga na Stand United ambayo nayo akaachana nayo

Kagera Sugar wamefoji mkataba wa Mbaraka Yusuf

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Inadaiwa kuwa timu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera imefoji mkataba wa aliyekuwa mchezaji wake Mbaraka Yusuf Abeid ambaye kwa sasa ni mali ya Azam FC. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Azam FC leo baada ya kulalamikia kitendo kinachofanywa na viongozi wa Kagera Sugar kudai Mbaraka Yusuf ni mchezaji wao na wana mkataba naye wa miaka miwili si kweli. Azam wanadai wamezungumza vizuri na Mbaraka na kugundua kuwa mkataba wake alioingia na Kagera Sugar ni wa mwaka mmoja ambao tayari umemalizika, leo Azam pamoja na Mbaraka waliongozana hadi TFF na kukuta mikataba miwili mmoja ukiwa umefojiwa ambao unaonyesha Mbaraka amesaini miaka mitatu. Azam wanaituhumu Kagera kwa kuwafanyia kauzibe juu ya kumpata Mbaraka lakini wamesema haki itendeke kwani Mbaraka ni mali yao kihalali na ataitumikia Azam msimu ujao