SIMBA YAMALIZANA NA KIUNGO MZAMBIA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bars, Simba SC leo imeingia kandarasi ya miaka miwili na kiungo wa kimataifa WA Zambia, Clatous Chota maarufu Chama na sasa atajumuika na wachezaji wenzake watakaosafiri kesho kuelekea nchini Uturuki.
Kiungo huyo alitua jana usiku akitokea kwao Zambia, Chota amesaini leo akitokea timu ya Lusaka Dynamos ya Zambia ambayo inashiriki Ligi Kuu, kocha msaidizi wa Simba, Irambona Masoud Djuma amesifu usajili huo akidai sasa Simba imemaliza ukame wa kiungo mchezeshaji.
Djuma amedai Simba ilikuwa ikisumbuliwa na kiungo mchezeshaji kwa muda mrefu na ililazimika kuwatumia Shomari Kapombe au Jonas Mkude, ujio wa Chota utaifanya Simba kutimia idara zote bila shaka itatetea tena taji lake, Chota ni chaguo la Djuma ambapo yeye ndiye aliyeutonya uongoxi wa Simba kumnasa