CANNAVARO AWA MENEJA MPYA YANGA, HAFIDH AHAMISHIWA KWINGINE

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Nahodha wa siku nyingi wa mabingwa wa zamani nchini Yanga SC Nadir Haroub Ally "Cannavaro" ameteuliwa kuwa meneja WA timu na kustaafu rasmi mchezo wa soka.

Cannavaro aliyedumu na Yanga karibu muongo mmoja na nusu ameachana na soka na kuwa meneja wa timu akichukua nafasi ya Hafidh Seleh aliyepandisha cheo na sasa anakuwa Cardnetor wa timu.

Akitangaza uteuzi huo leo, kaimu katibu mkuu wa Yanga Omari Kaaya amesema Cannavaro amecheza Yanga kwa kipindi kirefu hivyo atawafaa katika nafasi hiyo, ameongeza kuteuliwa kwa beki huyo wa kati kutaleta mawasiliano mazuri baina yake na benchi la ufundi kwavile anafahamu changamoto zote.

Yanga pia imetangaza kikosi chake kitakachoshiriki michuano ijayo ikiwemo Ligi Kuu Bars na safari hii imesajili wachezaji saba tu wapya na vilevile imeachana na nyota wake wawili ambao ni Geoffrey Mwashiuya na Hassan Messy

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA