Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2015

KIBADEN ATAKA USHINDI MECHI YA KESHO NA ETHIOPIA

Picha
Kocha Mkuu wa Kili Stars, Abdallah Kibadeni amesema pamoja na kuwa wamepanga kushinda mechi zote za hatua ya makundi katika michuano ya Chalenji. Kibadeni amesema pamoja na kuwa mchi ya mwisho ya makundi watamaliza na wenyeji Ethiopia, bado wanataka kushinda mchezo huo. “Itakuwa mechi ngumu zaidi kwa kuwa tunakutana na wenyeji. Lakini lazima tushinde na tumepania kufanya hivyo. “Kushinda mechi zote za makundi kuna faida mbili, kwanza kupata nafasi kwa uhakika hatua ya robo fainali. “Pili imani ya kikosi kwa maana ya kujiamini kutokana na kushinda. Hali ambayo itasaidia katika mechi zijazo,” alisema.

HOZA ATOBOA SIRI YA MAKUNDI YA PANYA ROAD NA WAASI DAR ES SALAAM

Picha
Mdau wa michezo jijini Dar es Salaam  Prince Salum Hoza amesema wakati wake alipokuwa mratibu wa michuano ya soka kwa vijana chini ya miaka 20 Hozaboy cup kwenye uwanja wa shule ya msingi Tabata jijini makundi ya kihuni kama ya Panya road na waasi hayakuwepo. Hoza aliyasema hayo akizungumza na mtandao huu ambapo amedai vijana wa kihuni walikuwepo tena wengi ila walishiriki ipasavyo kwenye soka. 'Zamani tuliandaa mashindano mengi ya soka nikishirikiana na mwalimu Kenny Mwaisabula 'mzazi', alisema Hoza ambaye kwa sasa ni mchambuzi katika gazeti la Msimbazi. Hoza amewataka wadau wa soka jijini

DROGBA ANATAKA KUMRITHI MOURINHO CHELSEA

Picha
Mshambulizi wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba amesema kuwa atarejea Stamford Bridge kuwa kocha. Drogba, ambaye kwa sasa anasakata soka ya kulipwa huko Canada, aliifungia the Blues mabao 164 katika enzi yake huko Stamford Bridge. "Ningependa kuihudumia klabu hiyo hata baada ya kukamilika kwa kipindi changu cha uchezaji'' ''Tayari nimekubaliana na wakurugenzi wa klabu hiyo kuwa ninaweza kurejea kuwa mkufunzi kwa sababu klabu hiyo ilinifaa sana nilipoanza'',alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 37. ''Kwani siwezi kuwa meneja ? kwani siwezi kuwa mkurugenzi wa kiufundi,mkufunzi wa chuo cha mafunzo ya wachezaji ama hata mshauri wa washambuliaji ?

ZIARA YA PAPA AFRIKA MASHARIKI: Papa Francis: Dini isitumiwe kuvuruga amani

Picha
Papa Francis ameongoza ibada ya misa ambayo imehudhuriwa na maelfu ya watu uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi ambapo amesisitiza umuhimu wa familia katika jamii. Awali katika mkutano na viongozi wa dini mbalimbali, alisema dini haifai kutumiwa kuvuruga akisema “Mungu ni Mungu wa amani.” "Jina lake takatifu halifai kutumiwa kutetea chuki na mauaji. Ninajua kwamba mashambulio ya Westgate, Chuo Kikuu cha Garissa na Mandera bado hayajasahaulika. Na sana, vijana wamekuwa wakiingizwa na kufunzwa itikadi kali kwa jina la dini kupanda woga na kuvunja umoja katika jamii,” alisema. "Ni muhimu sana tuwe manabii wa amani, watu wa amani wanaokaribisha wengine kuishi na amani, umoja na kuheshimiana. Mungu na akaguse nyoyo za wanaohusika katika mauaji na ghasia, na azipe imani familia na jamii zetu."

MAKALA: UNAMKUBUKA LUCAS NKONDOLA? MCHEZAJI ALIYEWEZA KUCHEZA NAFASI NYINGI UWANJANI

Picha
MICHUANO ya mataifa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Chalenji inaendelea kushika kasi nchini Ethiopia katika miji ya Adis Ababa na Awassa City, Tanzania inawakilishwa na timu za taifa mbili Kilimanjaro Stars kwa upande wa bara na Zanzibar Heroes kwa upande wa Zanzibar. Kilimanjaro Stars ilikuwa timu ya kwanza kujikatia tiketi ya kucheza robo fainali baada ya kushinda mechi zake mbili mfululizo za mwanzo, ikumbukwe michuano ya Chalenji ndiyo michuano mikubwa kuliko yote katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati. Lakini pia ndiyo michuano mikongwe kuliko yote barani Afrika, michuano ya Chalenji inasadikika ilianzishwa mwaka 1924, na kwa mara ya kwanza Tanzania bara baada ya uhuru ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka 1974 ikiwa na kikosi bora kabisa ambacho kinatajwa hakijawahi kutokea. Kikosi hicho golini alisimama Omari Mahadhi Bin Jabir (sasa marehemu), beki wa kulia alicheza Zaharani Makame, wakati beki wa kushoto alicheza Mohamed Chuma (sasa marehemu), namba nne al

WACAMEROON WATUA MSIMBAZI

Picha
Wachezaji wawili wa kimataifa kutoka Cameroon, wamewasili nchini juzi usiku kwa ajili ya kufanya majaribio na timu ya Simba ya Dar es Salaam. Akizungumza na gazeti hili jana kiongozi mmoja wa Simba (jina tunalihifadhi) alisema kuwa wachezaji hao wanacheza nafasi ya ushambuliaji. Kiongozi huyo alisema wachezaji hao wameletwa na wakala mmoja aliyegharamia safari za wachezaji hao na mahitaji mengine kwa siku zote watakazokuwa nchini kufanya majaribio. “Wakala aliyemleta Doumbie Ernest, ndiye jana (juzi) usiku, amewapokea wachezaji hao wawili kwa ajili ya kufanya majaribio Simba,” kilisema chanzo chetu. Doumbie aliyewahi kuichezea Leopard FC inayoshiriki Ligi daraja la pili nchini Cameroon, mwishoni mwa wiki alionekana kwenye mazoezi ya Simba yanayofanyika kwenye fukwe ya Coco pamoja na winga Mganda, Brian Majwega.

BLATTER ASEMA ALINUSURIKA KIFO

Picha
Rais aliyepigwa marufuku wa shirikisho la soka duniani,FIFA,Sepp Blatter amesema alinusurika kifo kufuatia matatizo ya kiafya yaliyomkumba majuzi. Suspended Fifa president Sepp Blatter has said he feared he was dying during a recent health scare. Blatter, 79, ambaye anatumikia marufuku ya siku 90 kutoka kwenye maswala yeyote ya kandanda alilazwa kwa siku 6 hospitalini akiwa amezongwa na msukumo wa maisha. ''nilikuwa katikati ya malaika walokuwa wakiimba kwa furaha na sheitan aliyekuwa akiwasha moto lakini malaika ndio walioimba'' alisema Blatter. 'Nilikaribia kufa.' 'Wakati mmoja ulifika ambao mwili ulikubali kushindwa' Image copyright Reuters Image caption Blatter, na Platini wanatumikia marufuku ya siku 90 kufuatia malipo yaliyoihujumu FIFA

KAVUMBAGU AWAITA SIMBA MEZANI

Picha
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Didier Kavumbangu amesema amekuwa akisikia sikia tu habari za kutakiwa na Simba SC, lakini hajawahi kuzungumza na kiongozi yeyote wa klabu hiyo. Akizungumza mjini Addis Ababa, Ethiopia mwishoni mwa wiki, Kavumbangu amesema kwamba na wala klabu yake, Azam FC haijawahi kumpa taarifa zozote za kuhamishwa kwa mkopo. “Nasikia Simba SC wananitaka kwa mkopo. Nasikia sikia tu, lakini sijawahi kuambiwa na klabu yangu, wala Simba SC hawajawahi kunifuata,”amesema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC na TP Mazembe ya DRC. Alipoulizwa iwapo Simba SC wana nia kweli ya kumchukua, Kavumbangu anayechezea Burundi kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge amesema; “Siwezi kuzungumza hadi Simba wakinifuata ndiyo nitawajibu, lakini kwa sasa mimi ni mchezaji wa Azam FC na nina Mkataba,”amesema. Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva mwishoni mwa wiki alisema kwamba hawajawahi kufanya mazungumzo na Kavumbangu, lakini wanasikia nao kwamba Azam FC inataka

ERICK MAJALIWA: Alisababisha mgogoro mkubwa wa kiuongozi Simba, inadaiwa ni mtoto wa waziri mkuu

Picha
HISTORIA imeandikwa katika soka la Tanzania hasa baada ya Rais wa jamhuri ya muungano Mhe John Pombe Magufuli kumteua mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi Majaliwa Kasimu Majaliwa kuwa Waziri mkuu wa 11 wa Tanzania. Uteuzi huo ulipokelewa kwa hisia tofauti toka kwa Watanzania, wapo walioshangazwa na uteuzi huo ambao waliamini huenda lingetangazwa jina kubwa lililozoeleka masikio mwao, na wengine walishangaa tu kuona Naibu waziri TAMISEMI wa serikali ya Awamu ya nne anakuwa waziri mkuu serikali ya Awamu ya tano.

YANGA KUWAALIKA HEARTS OF OAK YA GHANA KUCHEZA KIRAFIKI

Picha
Katika kudhihirisha tambo za msemaji wao, Jerry Muro kwamba 'wao ni wa kimataifa', Yanga wamewaalika mabingwa wa Ligi Kuu ya Ghana, Hearts of Oak, kuja nchini kwa ajili ya mechi ya kirafiki. Tangu aingie madarakani Januari, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga (Muro) amekuwa akitamba kuwa klabu hiyo ya Jangwani ni ya kimataifa. Ili kufanya vyema katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwakani, Yanga wameanza kusaka mechi za kimataifa za kirafiki, safari hii wakikimbilia Ghana alikokuwa anafanyia kazi kocha mkuu wao, Hans van der Pluijm. Jonas Tiboroha, Katibu Mkuu wa Yanga, aliliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana kuwa tayari walishapeleka barua ya maombi katika klabu hiyo kongwe inayoshiriki Ligi Kuu ya Ghana na wanaamini wataukubali mwaliko wao. Tiboroha alisema programu ya benchi la ufundi, imeelekeza timu yao ipate mechi mbili za kirafiki kabla ya ligi haijaendelea na wanaamini watapata mechi hizo ili kukiimarisha zaidi kikosi chao.

Timu tano zasonga hatua ya makundi

Picha
Timu za Uganda, DR Congo, Morocco, Guinea na Gabon zimesonga mbele katika hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya Kombe la Dunia. Uganda, wakicheza nyumbani katika uwanja wa Mandela waliifunga Togo 3-0 na hivyo wakawa wameshinda kwa jumla ya mabao 4-0 ambapo mchezo wa kwanza walishinda kwa bao 1-0. Gabon nao wakasonga mbele katika hatua ya makundi kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Msumbiji. Nao Zambia, wakawachapa Sudan kwa 2-0 na kufuzu kwa makundi kwa jumla ya mabao 3-0 huku mabao ya jana yakifungwa na Lubambo Musonda na Winston Kalengo. DR Congo walitoka sare ya 2-2 na Burundi huko kwao lakini wamesonga mbele baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-2 huko Bujumbura.

KERR ATISHIA KUBWAGA MANYANGA SIMBA IWAPO.......

Picha
Baada ya kupita siku kadhaa tangu Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, atangaze kuacha kukinoa kikosi hicho, kocha mkuu wa timu hiyo, Muingereza, Dylan Kerr, ameibuka na kusema na yeye anaondoka klabuni hapo huku akidai mechi yake ya mwisho inaweza kuwa dhidi ya Azam FC, Desemba 12. Matola aliamua kuachana na Simba kwa kile alichoeleza kuwa ni kutoelewana na Kerr, kwani kocha huyo amekuwa mtu asiyependa kushauriwa. Ikumbukwe kuwa, wakati Matola anatangaza hivyo, Kerr alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mapumziko baada ya Ligi Kuu Bara kusimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa, Taifa Stars, iliyokuwa ikijiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia.  Kerr alisema Matola hakupaswa kufanya hivyo, kwani hajui kama uhusiano wake na yeye haupo sawa huku akisema tangu tukio hilo litokee, vyombo vya habari vimekuwa vikimtupia lawama. “Vyombo vya habari vimekuwa havinitendei haki, vimekuwa vikiniandama sana tangu Matola atangaze kuachia ngazi, sasa nimechoka na mimi nitaondoka.

MAKALA: JUSTUCE MAJABVI: Kutoka Bundesliga hadi VPL

Picha
SI kazi rahisi kumnyang'anya namba Jonas Mkude mtoto wa 'Don Town', alishindwa Mrundi Pierre Kwizera aliyekuwa akicheza soka la kulipwa Ivory Coast, Mkude alimwachia nafasi wakati yeye akijiuguza majeraha yake ya goti, lakini alirejea kwenye nafasi yake baada ya Kwizera kushindwa kumshawishi kocha wa Simba wakati huo Mzambia Patrick Phiri. Kwizera hakumridhisha kabisa kocha wa Simba Patrick Phiri ambaye aliamua kuachana naye na kuendelea kumtumia Mkude, Mkude anamudu kucheza namba sita na kwa kipindi kirefu hajatokea wa kumzidi. Mwanzoni mwa msimu huu uongozi wa Simba uliamua kumsajili Mzimbabwe Justuce Majabvi aliyekuwa kicheza soka la kulipwa nchini Vietnam katika timu ya Vicem Hai Phong FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo. Ujio wake umechagizwa na kocha mkuu wa Simba Muingereza Dlan Kerr ambaye naye alikuwa akiifundisha timu hiyo, Kerr anamfahamu vizuri Majabvi na ndiyo maana akapendekeza asajiliwe haraka, lakini kocha huyo hakutambua kama Simba inaye kiungo matata

WACHEZAJI WA UJERUMANI WANUSURIKA KIFO UFARANSA, WATU 120 WAMEUAWA

Picha
Watu 120 wauawa katika mashambulio Paris Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 120 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris. Watu 120 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris. Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi. Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa ikiendelea. Wasimamizi wa mji wa Paris wamewataka raia kusalia manyumbani na wanajeshi 1,500 wametumwa kushika doria Paris. Shambulio mbaya zaidi linaonekana kuwa hilo la Bataclan, ambako ripoti zinasema watu waliokuwa wamehudhuria tamasha ukumbini walipigwa risasi na kuuawa baada ya kushikwa mateka.

KERR MBISHI NA HASHAURIKI- MATOLA

Picha
Ilianza kama utani, lakini hatimaye juzi usiku  ikawa kweli baada ya Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba, Selemani Matola kutangaza rasmi kutema kibarua hicho. Matola, beki wa zamani wa klabu hiyo, amesema amefikia uamuzi huo baada ya kushindwa kuelewana na bosi wake, Kocha Mkuu, Dylan Kerr. Akizungumza muda mfupi baada ya kujiondoa Simba usiku wa kuamkia jana, Matola alisema tabia ya ubishi na kutoshaurika kwa Kocha  Kerr ndiyo sababu iliyom kimbiza Msimbazi. Alisema uongozi wa Simba una taarifa za kuondoka kwake, kwani alifanya hivyo baada ya kikao kilichoongozwa na Rais wa Simba, Evans Aveva juzi usiku. “Nimeamua kukaa pembeni, mambo yalikuwa yanazidi kuwa magumu, nilikutana na Evans tangu saa mbili usiku (juzi usiku), tumeongea lakini, msimamo wangu ulikuwa palepale,” alisema Matola,  kiungo  wa zamani wa RTC Kagera na Super Sport ya Afrika Kusini. Aliongeza: “Msimamo wangu ni kujiondoa kabisa kufundisha Simba kwa sasa, sitaki hata kwenda timu B.” Alisema mara kadhaa amekuwa akiripo

KINNAH PHIRI AJA KUMRITHI MWAMBUSI MBEYA CITY

Picha
NI takribani mwezi mmoja sasa tangu aliyekuwa kocha mkuu wa Mbeya City Fc (timu ya kizazi kipya) Juma Mwambusi alipotangaza rasmi kuachana na timu hii ili kwenda kujiunga na Young African ya Dar es Salaam ambayo pia inashiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara kama ilivyo City. Kujiunga na Yanga, safari ya Mwambusi aliyedumu ‘kikosini’ takribani miaka mitano na kupatia mafanikio makubwa, ni wazi imekuwa na baraka tele kutoka kwa uongozi, wadau na mashabiki wa hasa kwa yote aliyoyafanya ndani ya timu hii, ndiyo maana mpaka leo hajawahi kukutana na kadhia yoyote kuhusu kuondoka kwake kikosini. Kwa wadau wa soka, kuhama kutoka timu moja kwenda nyingine kunakowakuwata wachezaji, makocha na kwa uchache viongozi ni jambo la kawaida ambalo linafanyika kwa lengo moja tu kuongeza mafanikio kwa pande zote zinazohusika, huku maslahi yakiwa ‘chagizo kuu’ kwa upande mwingine. Safari ya kocha Mwambusi kutoka kwenye timu aliyoshiriki kuianzisha na kudumu nayo kwa miaka mitano kwenda timu nyingine haki