Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2014

ORIGI ASAJILIWA RASMI LIVERPOOL

Picha
Divorc Origi katika mojawapo ya mechi za Ubelgiji Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji Divorc Origi hatimaye amejiunga na timu ya Liverpool. Baba yake Origi, Mike Okoth, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu taifa ya Kenya Harambee Stars amethibitsha mwanawe Divorc amesaini mkataba na Liverpool ambao walifurahishwa na mchezo wake mzuri alipoiwakilisha Ubelgiji kwenye kombe la dunia.

AKINA BALOTELLI WACHAPWA 5-1 NA MAN CITY

Picha
MANCHESTER City imeitandika mabao 5-1 AC Milan katika mchezo wa kujiandaa na msimu mjini Pittsburhg usiku wa kuamkia leo, huku mshambuliaji Stevan Jovetic akifunga mabao mawili dakika za 12 na 58.

UINGEREZA YAIZUIA URUSI KUANDAA KOMBE LA DUNIA

Picha
FIFA yaikabidhi Urusi haki za kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018. Naibu waziri mkuu nchini Uingereza Nick Clegg ametoa wito wa Urusi kupokonywa haki za kuandaa mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2018.

SIRI YA KUTEMWA BIN KLEB YANGA HII HAPA....

Picha
WAKATI kukiwa kuna sintofahamu juu ya Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC, Yussuf Manji kuunda Kamati mpya ya Utendaji ya klabu hiyo akiwaweka nje Wajumbe kadhaa, akiwemo Abdallah Bin Kleb, imefahamika kiongozi huyo aliomba mwenyewe kujitoa. Ingawa sababu haswa ya Bin Kleb kujitoa haijulikani, lakini chanzo cha karibu na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, kimesema kwamba sababu za kupata muda wa kutosha kwa ajili ya biashara zake. “Abdallah kwa muda mrefu alikuwa anaomba udhuru ili kushughulikia biashara zake ambazo zilikuwa zinakosa usimamizi wa uhakika kutokana na muda wake mwingi kufanya kazi za Yanga,”.

SHILOLE ATANGAZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA IGUNGA 2015

Picha
Muigizaji wa filamu na mwanamuziki Shilole ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Igunga anakotokea katika uchaguzi mkuu ujao 2015. Shilole ameyasema hayo kupitia kipindi cha Sizi za Kitaa cha Clouds TV huku ile collabo yake na Jennifer Lopez wa Marekani ikiwa bado inasubiriwa na mashabiki wake."Baada ya Dr. Dalali Kafumu anayefuata ni mimi, mimi nadhani napenda jimbo langu na napenda wakazi wangu wa Igunga wananiona toka nakua mpaka sasa hivi, kwahiyo wanafurahi, sasa wananiambia sisi hatutaki kumpa mtu mwingine kiti hiki sasa wananipa changamoto.

YANGA YATHIBITISHA KUSHIRIKI KAGAME

Picha
Uongozi wa klabu ya Yanga umekanusha taarifa kwamba umejitoa katika Kombe la Kagame la klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati nchini Rwanda kama ambavyo imeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini. Yanga imesema itashiriki michuano hiyo ya kila mwaka, baadaye mwezi ujao, endapo itaarifiwa rasmi na Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambao ndiyo waandaaji.

NIGERIA KUTETA NA STEPHEN KESHI

Picha
Shirikisho la kandanda la Nigeria NFF limesema kuwa linaanda mikakati ya kufanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wa timu ya taifa Super Eagles Stephen Keshi wakimtaka aendelee kuhudumu kama mkufunzi mkuu. 

CHEGE: WAUWE NI VIDEO BORA LAKINI WATANZANIA WAMEROGWA

Picha
Chege na Temba mwanzoni mwa mwezi huu wali release video kali ya Wauwe ambayo director Adam Juma alitumia red camera – camera ambayo inasemekana kuwa ni bora katika kupata picha bora za video.Sasa ndani ya Burudani Chegge amefunguka kuwa bajeti ya video hiyo ilikuwa kubwa kidogo zaidi ya Milioni 10 kutokana na tathmini aliyopewa na Meneja wake, Saidi Fela. Pia Chegge alifunguka kuwa anaamini wauwe ni video kali sana, kwa video ambazo zimefanywa ndani ya nchi, hadhani kama kuna video ya kuweza kuifananisha nayo.

MALINZI AWASUTA MAREFA WA TANZANIA, ADAI WAMESHAMIRI RUSHWA

Picha
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kwamba sekta ya marefa nchini inatia aibu kwa sababu ipo chini mno na amewataka viongozi wa sekta hiyo kuhakikisha wanaiinua juu. Akizungumza wakati wa kufunga semina ya marefa wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Malinzi amesema kwamba ipo haja ya jitihada kubwa kufanyika kuinua sekta hiyo.

USAJILI ULAYA WAZIDI KUPAMBA MOTO

Picha
Manchester United wamerejea tena kumfuatilia winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 26, baada ya jaribio la kwenda Paris Saint Germain kugonga mwamba kuhusiana na ada ya uhamisho ya pauni milioni 45 (Sun) Southampton wanataka kubaki na kiungo wao Morgan Schneiderlin, 24, na watawaambia Tottenham na Arsenal watahitaji kutoa zaidi ya pauni milioni 27 kama wanamtaka (Guardian) Boss mpya wa Southampton, Ronald Koeman amekataa pauni milioni 3.25 kutoka Cardiff kumsajili beki Jose Fonte, 30 (Daily Mirror)

DROGBA AREJEA DARAJANI

Picha
Mshambuliaji wa Garatasalay ya Uturuki na Ivory Coast Didier Drogba amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga tena na Chelsea ya England. Drogba, 36, alishinda makombe 10 akiwa na Chelsea kuanzia mwaka 2004 hadi 2012, na alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka klabu ya Galatasaray ya Uturuki. Meneja Jose Mourinho, mapema alisema Stamford Bridge ni kama "kwake" mchezaji huyo, Mourinho ameonyesha kufurahishwa kwa kurejea mshambuliaji huyo ambaye anaamini anaweza kuisaidia timu hiyo katika kupachika mabao .

STRAIKA WA IVORY COAST AMALIZANA NA SIMBA

Picha
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Taifa ya Burundi, Pierre Kwizera, ambaye alikuwa nchini akifanya mazungumzo na uongozi wa Simba, ameondoka juzi usiku kurejea Ivory Coast kwa lengo moja la kwenda kuvunja mkataba na klabu yake ya Afad Abdijan. Mchezaji huyo anayecheza nafasi zaidi ya mbili uwanjani, amewaambia viongozi wa Simba kwamba atahakikisha anamalizana na Afad Abdijan na kurejea jijini Dar es Salaam kuitumikia klabu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. "Kuna mambo naenda kumalizia huko, ila nitarudi Tanzania kucheza Simba," alisema kwa kifupi mchezaji huyo. Habari kutoka uongozi wa Simba zinaeleza kuwa mchezaji huyo atarejea jijini Agosti 28, mwaka huu tayari kuanza mazoezi na wachezaji wenzake wa timu hiyo.

EVRA AENDA JUVENTUS

Picha
Patrice Evra amekamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United kwenda Juventus.

GERRARD ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA

Picha
Nahodha wa timu ya taifa ya England Steven Gerrard, 34, amestaafu kucheza soka la kimataifa baada ya kuitumikia nchi yake katika kombe la dunia iliyomalizika hivi karibuni nchini Brazil na kuondoshwa katika hatua za awali.

MATS HUMMELS HUYOOOO MAN UNITED, VAN GAL NOOMA

Picha
BEKI Mats Hummels yuko mbioni kujiunga na Manchester United wiki hii akitokea Borussia Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 16, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania. Klabu hizo mbili bado hazijafanya mazungumzo kwa ajili ya uhamisho huo, lakini timu ya Old Trafford inajiamini mno inaweza kumpata beki huyo hodari. Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 25 aling'ara kwenye Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani iliyoibuka bingwa nchini Brazil, kiasi cha kumvutia hadi kocha mpya wa United, Louis van Gaal.

MTUNISI ADAIWA KUMVISHA PETE YA UCHUMBA VJ PENNY, MWENYEWE AKANUSHA

Picha
Latest buzz is about Mtunisy kumvisha pete ya uchumba VJ Penny hivi juzi kati. Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilicho karibu na Penny kikizungumza na burudani. kilisema kuwa Mtunisy amemvisha Penny pete hiyo kwa siri kubwa na wamekuwa karibu kwa muda sasa bila hata watu wao wa karibu kujua. Habari zaidi zinadai kuwa Penny yupo tayari kuolewa na Mtunisy kama mke wa pili ndiyo maana kwa muda sasa amekuwa akivaa ushungi licha ya kuwa mkristu ili akubalike ukweni ambapo Mtunisy ni muislamu. "Mtunisy kamvisha VJ Penny pete ya uchumba mna taarifa? ilitokea hivi juzi walifanya siri sana hata mimi nilijua baadaye, wapo karibu siku hizi hata Penny anavaa ushungi ili akubalike kwa wakwe zake, Penny amechoka na upweke tangu aachane na Diamond"

MAPROO SIMBA WAZIDI KUTUA

Picha
KIUNGO wa kimataifa wa Kenya, Paul Mungai Kiongera anatarajiwa kutua nchini kesho kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam. Mchezaji huyo wa KCB ya Ligi Kuu ya nchini, anakuja nchini kwa mazungumzo ya mwisho baada ya mazungumzo ya awali kwa simu na kama yatakwenda vizuri, atasaini Mkataba. Aidha, kiungo Mrundi Pierre Kwizera baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa Simba SC anarejea Ivory Coast kumalizana na klabu yake, Afad Abidjan ili aje kusaini Mkataba.

BRAZIL KUTAMBULISHA KOCHA MPYA

Picha
Aliyekuwa mkufunzi wa timu ya soka ya Brazil Luiz Felipe Scolari Brazil inatarajiwa kumtangaza mkufunzi wake mpya katika mkutano na wanahabari siku ya jumanne kufuatia kujiuzulu kwa kocha wa timu hiyo Luiz Felipe Scolari.

LILE BONGE LA KIPA LA CLOMBIA MBIONI KUTUA ARSENAL

Picha
KLABU ya Arsenal imekubali kutoa Pauni Milioni 3.2 kwa ajili ya kumnunua kipa wa Nice, David Ospina. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 aling'ara na Colombia wakati wa Kombe la Dunia na anatarajiwa kumpa changamoto Wojciech Szczesny. Ospina amekataa ofa ya Valencia. Ospina alikuwa mmoja wa makipa waliokuwa kivutio kikubwa katika Kombe la Dunia, hakiiwezesha Colombia kufika Robo Fainali, ambako ilitolewa na wenyeji Brazil.

VJ PENNY KUTANGAZA FILAMU ZA KITANZANIA KATIKA TV YA KIMATAIFA

Picha
Vipindi vya TV kuhusu filamu za kitanzania vinazidi kuongezeka kila siku katika harakati za kuzidi kuitangaza tasnia ya filamu Swahiliwood. Habari mpya ni kuwa mtangazaji maarufu nchini VJ Penny soon ataonekana katika kipindi kipya kinachohusu filamu za kitanzania ambacho kitaonekana katika kituo cha kimataifa kinachoonekana nchi za Afrika mashariki na kati.

STARS YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI

Picha
TANZANIA, Taifa Stars imeanza vibaya hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco, baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Msumbiji. Katika mchezo huo, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana, mabao ya Stars inayofundishwa na Mholanzi Mart Nooij yalifungwa na kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa.

GOTZE ASEMA, LILE LILIKUWA BAO LA NGEKEWA TU KWAKE.

Picha
Shujaa wa Ujerumani, Mario Gotze amesema kufunga bao pekee na la ushindi katika fainali ya Kombe la Dunia ni kama bahati na zawadi yake katika msimu wake mgumu akiwa Bayern Munich. Gotze (22), mwenye sura ya kitoto, alituliza kifuani mpira wa krosi ya Andre Schuerrle kabla ya kupiga shuti kufunga bao katika dakika ya 113, na kuipa Ujerumani ushindi 1-0 dhidi ya Argentina kwenye Uwanja wa Maracana, Rio de Janeiro, Brazil.

DEMBA BA KWENDA BESITKAS KWA PAUNI MILIONI 8

Picha
Mshambuliaji wa Chelsea Demba Ba anakaribia kuhamia klabu ya Besitkas ya Uturuki baada ya klabu hizo mbili kukubaliana.

VJ PENNY, WEMA SEPETU WAMALIZA BIFU LAO LILILOTOKANA NA PENZI LA DIAMOND PLATINUMZ

Picha
Wema Sepetu na VJ Penny wamemaliza beef lao lililokuwepo kwa muda mrefu sasa baada ya Penny kuingilia uhusiano wa Wema na Diamond. Hata hivyo Wema ameamua kumsamehe Penny wakati huu wa mwezi  mtukufu wa Ramadhani "Kwa moyo mweupe, nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye kama kawaida', alisema na kuongeza. 'Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu." alisema Wema wakati akizungumza na mwandishi wetu.

LIVERPOOL YAMSAJILI MARKOVIC KWA PAUNI MIL 20

Picha
Liverpool imetumia £20m kumsajili Markovic Pauni millioni 20 ndicho kima imekitumia Liverpool kumhamisha Lazar Markovic kutoka Benfica. Mserbia huyo aliiwezesha Benfica kutwaa taji la Ureno msimu uliopita na anasema anamatumaini makubwa ya kuwaridhisha mashabiki na mwenye club hiyo.

MBWANA SAMATTA, THOMAS ULIMWENGU WAWASILI DAR TAYARI KUIKABILI MAMBAZ

Picha
WASHAMBULIAJI tegemeo wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wamewasili Dar es Salaam asubuhi ya leo kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Msumbiji ‘Mambas’ mwishoni mwa wiki. Washambuliaji hao wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wote wamewasili wakiwa fiti tayari kwa mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Pili na ya mwisho kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco.

IVO MAPUNDA AMUHOFIA CASSILAS

Picha
Kipa chaguo la kwanza wa timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Ivo Mapunda, amesema kwamba anamhofia kipa mpya aliyetua kwenye kikosi hicho, Hussein Shariff 'Casillas' kutoka Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro. Casillas alisaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kuitumikia Simba mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza na gazeti hili, Mapunda, alisema kwamba Casillas ndiye kipa bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita hivyo atajipanga kufanya mazoezi ili kulinda kiwango chake na kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza.

NI SHANGWE NA NDEREMO UJERUMANI

Picha
Timu ya taifa imewasili nchini humo kwa kishindo Timu ya taifa ya soka ya Ujerumani imewasili nchini humo kwa kishindo wakiwa na kombe lao la ushindi walilolinyakua katika mashindano ya kombe la dunia ambyo yalikamilika juzi nchini Brazil. Maelfu ya mashabiki wa soka wamekuwa wakisubiri tangu asubuhi na mapema mjini Berlin kuwakaribisha wachezaji hao.

MAXIMO AMREJESHA NSAJIGWA YANGA

Picha
KOCHA mpya wa Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo amemrejesha beki wa zamani wa timu hiyo, Nsajigwa Joel Shadrack Mwandemele ‘Fusso’ katika timu hiyo. Maximo alifanya kazi na Nsajigwa katika miaka yake minne ya kuifundisha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na alimpa Unahodha katika miaka yake miwili ya mwisho. Hiyo ilifuatia kustaafu kwa Manahodha wake wawili wa awali, kwanza Mecky Mexime na baadaye Salum Swedi ‘Kussi’ na Nsajigwa aliendelea kuwa Nahodha wa Stars mbele ya kocha aliyemfuatia Maximo, Jan poulsen kabla ya kustaafu mwaka jana.

BLATTER ASHANGAZWA NA TUZO YA MESSI

Picha
Rais wa Fifa Sepp Blatter amesema ameshangazwa kuwa Lionel Messi alishinda tuzo ya mchezaji bora - Golden Ball Award- katika Kombe la Dunia.

BREKING NEWS ZA USAJILI BARANI ULAYA

Picha
Kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, amewapa matumaini zaidi Manchester United baada ya kukiri kuwa "angependa kuichezea moja ya klabu kubwa duniani" ingawa amesema hatolazimisha uhamisho wake (Independent) United pia wamepata matumaini baada ya winga wa Real Madrid, Angel Di Maria, 26, kukataa kwenda Paris St- Germain (Daily Mirror), beki wa Atlètico Madrid, Filipe Luis, 28, anajiandaa kufanya vipimo vya afya kabla ya kuhamia Chelsea kwa ada ya pauni milioni 20 (Daily Express)

MCHUMBA WA DIAMOND APATA MUME

Picha
Mtangazaji maarufu nchini VJ Penny ambaye alikuwa mpenzi wa Diamond Platnumz amechumbiwa !...well kupitia Instagram Penny ameweka picha akiwa amevaa pete ya uchumba. Pia juzi ilisikia kuwa penny amechumbiwa ingawa hatukupata habari kwa kina mpaka Penny mwenyewe alipoweka picha Instagram inayoonyesha ameshachukuliwa tayari ingawa haijajulikana amechumbiwa na mwanaume gani. Vj Penny ameandika "Road trip..........site here we come....Cc @HalimaKimwana1"

UJERUMANI MBABE ZAIDI YA ARGENTINA HISTORIA HIYO

Picha
Mara ya mwisho Argentina kukutana na Ujerumani katika Fainali 1986. Argentina na Ujerumani zitachuana kwa mara ya 3 katika fainali ya kombe la dunia. Je wajua itakuwa mara ya 8 kwa timu hizo kuchuana katika kombe la dunia ? Ukinzani wa jadi kati ya Brazil-Argentina unaweza kumithilishwa tu na uhasama baina ya Ujerumani na Uholanzi.

MAKALA: HUSSEIN SHARRIF CASSILAS KUSAJILIWA KWAKE SIMBA NA NDOTO YA KUWA TANZANIA ONE

Picha
Na Prince Hoza JANA Simba SC ilifanya usajili wa wachezaji watatu kwa mkupuo, wamo walinda milango wawili ambao ni Hussein Sharrif 'Cassilas' na Peter Manyika mtoto wa kipa wa zamani wa Yanga na timu ya taifa Manyika Peter Manyika. Usajili huo ulienda sambamba na mchezaji mwingine aitwaye Hajibu, lakini usajili wa Cassilas ndio ulioweza kushtua zaidi hasa kutokana na ubora wake awapo uwanjani.

MBWANA SAMATTA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA BRAZIL

Picha
Straika wa kimataifa Mbwana Samata wa Tanzania, amesema atatua nchini Julai 16 (Jumatano ijayo) ili kuongeza nguvu katika kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kuikabili Msumbiji kuwani tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Mataifa ya Afrika (AFCON). Samata ambaye alikuwa na majeraha yaliyomfanya akose mechi ya marudiano ya Taifa Stars dhidi ya Zimbabwe mwezi uliopita, amesema kwa sasa yupo fiti japo hajacheza mechi yoyote tangu apone. “Nitakuja kambini tarehe 16, inshallah panapo majaliwa, ninaendelea vizuri kwa sasa japokuwa sijacheza mchezo wowote tangu nilipotoka katika maumivu,” alikaririwa Samata jana na moja ya mitandao ya michezo nchini.

NEYMAR AKESHA AKILIA KWA KIPIGO CHA MABAO 7-1, ADAI YEYE NI MBRAZIL DAMU

Picha
NYOTA wa Brazil, Neymar alishindwa kuyazuia machozi wakati akisema ilibaki kidogo tu apooze. Neymar, alifanya Mkutano wa kwanza na Waandishi wa Habari baada ya kutoka hospitali alipokuwa amelazwa baada ya kuumizwa mgongo katika mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia Brazil ikiitoa Colombia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 pia amesema kwamba beki wa Colombia, Juan Zuniga amempigia simu kumuomba msamaha kwa kumpiga kwa goti mgongoni kwenye mechi hiyo.

HUU NDIO MKOKO ALIOZAWADIWA MAMA YAKE DIAMOND PLATINUMZ

Picha
Gari la kifahari linaloonekana pichani ndilo alilozawadiwa jana mama mzazi wa mwanamuziki nyota nchini Naseeb Abdul au Diamond Platinumz ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani, gari hilo alipewa wakati akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

IRENE UWOYA, JAGUAR WADAIWA KUKUTANA FARAGHA NAIROBI, MINONG'ONO YAANZA!

Picha
Latest news zinasema kuwa star wa filamu nchini Irene Uwoya amekutana faragha Nairobi, Kenya na star mwenzake wa muziki toka nchini humo Jaguar. Chanzo kimoja kilicho karibu na Uwoya kikizungumza na Swahiliworldplanet  kimesema kuwa wawili hao kuna deal wanafikiria kufanya pamoja lakini hana uhakika mpaka sasa ni deal gani "Uwoya na Jaguar wamekutana faragha kuna issue zao wana-talk ila sijui ni deal gani hizo, nitakupa updates" kilisema chanzo hicho jana Hata hivyo chanzo kingine kutoka Kenya kimesema kuwa kimewaona Uwoya na Jaguar katika hotel moja jijini Nairobi wakiwa katika mikao ya kimahaba a.k.a zero distance " Hi, I have seen Irene Uwoya with Jaguar in a hotel in Nairobi they looked like an item, hawa celebs sio predicted" kilisema chanzo hicho

SIMBA YAIFANYIA UMAFIA MKUBWA YANGA, YAMPORA STRAIKA NA KUMWAGA WINO.

Picha
Katika kuhakikisha kikosi cha Simba kinarejesha makali yake kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, uongozi wa timu hiyo umefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars), Paul Kiongera. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jijini kutoka katika kamati ya usajili ya timu hiyo, Kiongera, ambaye ni mchezaji wa KCB inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka ya Kenya, amesaini mkataba wa miaka miwili. Chanzo hicho kilisema kuwa kwa sasa Kiongera ni mmoja wa washambuliaji wanaoaminiwa na kocha mkuu wa Harambee Stars, Adel Amrouche na vile vile Kocha Mkuu wa Simba, Mcroatia Zdravko Logarusic, anatambua uwezo wake.

WEBB KUCHEZESHA FAINALI KOMBE LA DUNIA

Picha
Referii muingereza anayefahamika kwa ukakamavu wake Howard Webb ni miongoni mwa waamuzi 15 walioteuliwa kusalia Brazil kushiriki mechi zilizosalia za kombe la dunia.

DUDUBAYA AFUKUZWA NYUMBANI KWA MPENZI WAKE KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

Picha
Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mary "Mama wa Kinyakyusa" amedai kuwa eti amekua akiishi kinyumba na msanii wa Bongo Flava Dudubaya kwa muda mrefu lakini hivi karibuni eti alimfukuza nyumbani msanii huyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vyake viovu ikiwemo ubakaji na unyanyasaji, hayo aliyasema kupitia HekaHeka ya Leo Tena (Cloudsfm) Mama wa Kinyakyusa anadai alikua anamnyima unyumba Bwana ake wa zamani (DuduBaya) kwa sababu eti Dudu akishalewa pombe anakua mtata matusi kwa wingi na eti DuduBaya anauwezo wa kuishi Bar siku tatu mfululizo huku akitandika kilauri.

TUTAISHINDA UJERUMANI- SCORARI

Picha
Mlinzi wa Brazil Thiago Silva hatocheza katika mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani Jumanne .Hii ni baada ya juhudi za shirika la soka la Brazil kukata rufaa kwa shirikisho la soka duniani FIFA kutaka kadi ya pili ya njano iliyompelekea kupigwa marufuku mechi hiyo muhimu kuambulia patupu. Fifa imepuzilia mbali ombi la BFA la kuitaka ibatilishe kadi ya njano ambayo imemlazimu kocha Luiz Felipe Scolari kutafuta mlinzi mbadala kuziba pengo la nahodha huyo.

MAXIMO, MART NOOIJ WANUNIANA

Picha
KOCHA mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars Mholanzi Mart Nooij na Mbrazil Marcio Maximo anayeinoa Yanga wameingia vitani kila mmoja akitaka kuona taifa lake linaibuka mbabe wa soka duniani, Brazil na Uholanzi zipo katika kombe la dunia linalofanyika nchini Brazil. Huku timu hizo zote mbili zikifanikiwa kuingia nusu fainali, wakati kesho Brazil ikicheza na Ujerumani, Uholanzi itakuwa na shughuri pevu itakaposhuka uwanjani kukabiliana vikali na Argentina siku inayofuata yaani Jumatano.

DJOKOVIC AMZIMA FEDERAR WIMBLEDON

Picha
Djokovic ndiye bingwa wa Wimbledon Mchezaji tenis wa Serbia Novak Djokovic ndiye bingwa wa mwaka huu wa kombe la Wimbledon. Djokovic alimlaza Mswisi Rodger Federer seti tatu kwa mbili za alama 6-7 (7/9), 6-4, 7-6 (7/4), 5-7, 6-4 katika fainali hizo za wanaume..

LIVERPOOL KUWANUNUA ORIGI NA MARKOVIC, SUAREZ ANAKWENDA BARCELONA

Picha
Liverpool ya Uingereza imekubaliana na klabu ya Lille kumsajili mshambulizi wa Ubeljiji ambaye ni mzaliwa wa Kenya Divock Origi .

UONGOZI WA SIMBA WAVAMIA BUNJU

Picha
UONGOZI wa juu wa klabu ya Simba ukiongozwa na makamu wa rais Gofrey Nyange 'Kaburu' leo umetembelea uwanja wa klabu hiyo uliopo Bunju ambao bado unaendelea na ujenzi wake, Kaburu na sekretalieti nzima ya Simba ilivinjali uwanjani hapo na kushuhudia maendeleo ya ujenzi ya uwanja huo. Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Kaburu amesema jitihada zao zinahitajika ili kuumalizia uwanja huo na kuanza kutumika, wachezaji wa Simba huenda wakaana kuutumia uwanja huo, endapo Simba itaanza kuutumia uwanja wake huo itakuwa imewapiga bao Yanga ambao wanaendelea kukodi viwanja vya kufanyia mazoezi.

BALOTELLI AFANYA MATANUZI YA 'SIJALI LOLOTE' MAREKANI

Picha
BAADA ya matokeo mabaya katika Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa, Italia, mshambuliaji Mario Balotelli amepigwa picha akivuta sigara na kufanya matanuzi na mpenzi wake Fanny Neguesha mjini Miami, Marekani. Mshambuliaji huyo wa Milan, ambaye alipigwa faini na klabu yake kwa kuvuta sigara kwenye treni mwaka jana, haonekani kabisa kuwa na dalili za kuacha sigara baada ya kupigwa picha akiwa kwenye korido la hoteli anavuta.

MADEMU WA HOLLYWOOD WAJIGONGA KWA DIAMOND, KARRUACHE ATAKA NAMBA YA SIMU,WEMA SEPETU APEWA ONYO

Picha
This is hot gossip...! latest news zinasema kuwa Diamond amekuwa "Diamond" kwa mademu wa Hollywood akiwemo Karruache Tran ambaye ni demu wa Chris Brown ! juzi zilifanyika tuzo za BET Awards 2014 ambapo Diamond alikuwa nominated katika best international act Africa na kuhudhuria tuzo hizo Los Angels. Sasa basi kwa mujibu wa chanzo kimoja toka Tanzania kilichopo Marekani kwasasa kikichat na Swahiliworldplanet kimesema kuwa yeye alihudhuria tuzo hizo na rafiki yake mnigeria ambaye alikuwepo kuwapa support Tiwa Savage.

AVEVA AMTEUA DEWJI KUMSAIDIA KAZI HANS POPPE, AUNDA KAMATI ‘NZITO’ YA MASHINDANO, HUKUMU YA WAMBURA AGOSTI 3

Picha
RAIS mpya wa Simba SC amemteua Zacharia Hans Poppe kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, huku Makamu wake akiwa ni Kassim Mohammed Dewji.

ORIGI APIGIWA CHAPUO KUCHEZA LIGI KUU YA ENGLAND

Picha
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Gor Mahia na timu ya taifa ya Kenya Haraambee Stars, Austin Oduor, amesema mshambuliaji matata wa timu ya taifa ya Ubelgiji Divorc Origi ameiva kucheza katika ligi kuu ya England.