Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2014

TUTAIUA AL AHLY KAMA KOMOROZINE- OKWI

Picha
Na Fikiri Salum Kama walivyotoa ahadi ya mabao kwenye mchezo wa ligi kuu bara kati yao na Ruvu Shooting ambapo wachezaji wa Yanga waliahidi kuifunga magoli mengi timu hiyo, ndivyo itakavyokuwa katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika kati ya mabingwa wa Tanzania bara na wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa Yanga dhidi ya mabingwa watetezi wa Afrika Al Ahly ya Misri. Yanga na Al Ahly ya Misri zitakutana kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wachezaji wa mabingwa hao wa bara wameahidi kuishushia kichapo kitakatifu Al Ahly kama waliofanyia Komorozine ya Comoro. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Emmanuel Okwi raia wa Uganda amesema ana usongo mkubwa katika michuano ya kimataifa na hasa mechi iliyo mbele yake, Okwi ametamba kutoka na magoli si zaidi ya mawili katika mechi hiyo kwani wapinzani wao ni timu ya kawaida kama nyingine, Naye Simon Msuva amedai Al Ahly ni timu ya kawaida na inafungika.

WENGER AWASHAMBULIA WAKOSOAJI WA ARSENAL

Picha
Arsene Wenger Arsene Wenger amesema “hahitaji kutetea” uamuzi wake wa kuwapa wachezaji wa Arsenal siku mbili za mapumziko wiki hii na kushambulia ukosoaji “wa kushangaza” ambao hatua hiyo imeibua. “Si lazima iwe ni uchovu, sioni ni kwa nini hili ghafla limekuwa tatizo,” Wenger alisema Alhamisi. “Tumecheza bila kupumzika tangu Desemba, si lazima tueleze sababu, ni jambo la kushangaza. “Tuko katika jamii ambalo kila mmoja anataka kudhibiti kila kitu; sielewi hili hata kidogo. “Tuna haki ya kufanya mambo yasiyo ya kawaida. Tumetoka kucheza kipindi cha mechi ngumu. Tulichukua siku mbili za kupumzika, ni hayo tu. “Wakati mwingine huwa si mwili tu, pia akili, unakabiliwa na presha kila wakati, hakuna jambo la ajabu hapa,” Mfaransa huyo alieleza. “Wakati mwingine unapokabiliwa na presha ya aina hii, ni vyema kupumzika.

MALINZI KUMLIPA POULSEN ILI AONDOKE

Picha
Rais  wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amesema atalipa nusu ya gharama zilizotokana na shirikisho hilo kuvunja mkataba wa aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen. Hata hivyo, Malinzi na Kim hawakutaka kuweka wazi hatua walizofikia baada ya kuamua kuvunja mkataba zaidi ya kueleza kuwa walifikia makubaliano ya pamoja. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema sehemu nyingine ya gharama ya fedha zilizobakia zitalipwa na shirikisho hilo na waliamua kusitisha mkataba wa Kim ili wasake kocha mpya ambaye moja ya sifa zake ni kuwahi kuipeleka timu mojawapo ya Afrika kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON.

NYOTA YANGA WATEMWA STARS.

Picha
Na Boniface Wambura, Dar es Salaam KAIMU Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri. Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba. Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union). Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.

ADEBAYOR AZIDI KUTAKATAKA ENGLAND

Picha
KOCHA Tim Sherwood aliwataka vijana wake wafanye kazi na Emmanuel Adebayor ameiongoza vizuri kazi hiyo usiku wa kuamkia leo baada ya kuifungia Tottenham Hotspur mabao mawili katika ushindi wa 3-1 Uwanja wa White Hart Lane katika mchezo wa Europa League. Matokeo hayo yanaifanya Spurs iliyofungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza,ipate ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Dnipro na kutinga 16 Bora ya Europa League ambako itakutana na Benfica. Christian Eriksen alianza kufunga dakika ya 56 kabla ya Mtogo Emmanuel Adebayor kumaliza kazi dakikaza 65 na 69 katika mchezo ambao wageni walimpoteza mchezaji wao, Zozulya aliyetolewa nje kwa nyekundu dakika ya 62, akitoka kuifungia timu hiyo bao dakika ya 48.

UCHAGUZI TASWA KUMEKUCHA,PINTO,GEROGE JOHN KUCHUANA

Picha
WAOMBAJI 27 kati ya 28 wamerejesha fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TASWA, Boniface Wambura amesema leo kwamba, mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ilikuwa leo Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri. Waliorejesha kwa nafasi ya ujumbe ni Arone Benedict Mpanduka, Elizabeth Rashid Mayemba, Emmanuel Augustino Muga, Hassan Maulid Bumbuli, Ibrahim Mkomwa Bakari, Masau Kuliga Bwire, Mbozi Ernest Katala, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa, Salum Amiri Jaba, Tullo Stephen Chambo na Urick Chacha Maginga.

OKWI, KIIZA WAULA UGANDA, OWINO WA SIMBA ATOSWA

Picha
KOCHA Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ amewaita wote washambuliaji wa Uganda waliopo kwenye kikosi cha Yanga SC ya Dar es Salaam, Emmanuel Arnold Okwi Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’ kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Zambia, Chipolopolo ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) utakaofanyika Machi 5, mwaka huu Uwanja wa Ndola, Zambia. Katika taarifa aliyotumwa mapema jana, Micho amewachunia beki wa Simba SC, Joseph Owino na washambuliaji Brian Umony wa Azam FC na Yayo Lutimba wa Coastal Union, Waganda wengine wanaocheza Tanzania. Kikosi kamili kwa ajili ya mechi hiyo alichoteua Micho ni makipa; Onyango Dennis wa Bidvest Wits ya Afrika Kusini, Odonkara Robert wa Saint George ya Ethiopia na Watenga Ismail wa Vipers. Mbakei ni Iguma Denis wa Victoria University, Wadada Nicholas wa Vipers, Walusimbi Godfrey wa Gor Mahia ya Kenya, Kakuba Alex wa Covilha ya Ureno, Kalungi Henry wa Richmond Kickers ya Marekani, Isinde Isaac wa Saint George, Mwesigwa Andrew wa Ordab

MAYWEATHER AFANYA KUFURU YA PESA.

Picha
BONDIA Floyd Mayweather amewaonyesha mamilioni ya wafuasi wake kwenye Twitter namna alivyosherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwake mwishoni mwa wiki kwa kupanda ndege binafsi na rafiki zake na timu ya walinzi wake kwenda kufanya 'kufuru'.

AL AHLY YAIHOFIA YANGA, YATISHWA NA 7 ZA KOMOROZINE, RUVU SHOOTING

Picha
Kocha Msaidizi wa Al Ahly, Ahmed Ayoub ameichambua Yanga kwa kusema ni timu bora katika kushambulia, lakini si nzuri kwenye safu ya ulinzi. Yanga itaivaa Al -Ahly Jumamosi hii katika pambano la raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mahojiano na mtandao wa klabu hiyo, Ayoub alisema, ushindi wa jumla ya mabao 12-2 ilioupata Yanga dhidi ya Komorozine ni uthibitisho kwamba safu yake ya ushambuliaji ni moto wa kuotea mbali.

MAPENZI YA JINSIA MOJA HARAMU UGANDA.

Picha
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini muswada wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki mapenzi ya jinsia moja. Rais Museveni alitia saini mswada huo nyumbani kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na maafisa wakuu wa serikali pamoja na wandishi wa habari. Mswada huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa wale watakaopatikana na hatia ya kuhusika na mapenzi ya jinsia moja. Muswada huo pia umeharamisha wanaharakati kutangaza misimamo yao hadharani kuhusu au kuwasaidia wanapenzi wengine wa jinsia moja kujitangaza hadharani.

ENGLAND YAAJIRI MWANASAIKOLOJIA

Picha
kocha_wa_uingereza_roy_hodgson Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amesajili huduma za daktari wa akili ama ilikuwasaidia wachezaji wake kuimarisha uwezo wao wa kupiga penalti katika kampeini yake ya fainali za kombe la dunia litakaloandaliwa huko Brazil baadaye mwaka huu. Hodgson tayari amemsajili afisa wa shirikisho la uendeshaji baiskeli Sir Dave Brailsford kusaili kikosi chake. Brailsford anasifika kwa kuongoza ufanisi wa timu ya mbio za uendashi baiskeli ya Uingereza na Hogdson amemwalika kuzungumza na wachezaji

WAPINZANI WA YANGA VINARA WA MAKOMBE DUNIANI

Picha
Mashabiki wa timu ya Al-Ahly ya Misri Miamba wa soka barani Afrika, Al-Ahly ya Misri wameipiku timu ya AC Milan ya Italia, timu ambayo inatambuliwa kutwaa makombe mengi kimataifa. Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya mabingwa barani Afrika, wameweza kuipiku AC Milan kufuatia ushindi wao dhidi ya CS Sfaxienya Tunisia pale ilipowachabanga magoli 3-2 Alhamisi iliyopita mjini Cairo, wakifikisha mataji 19, moja zaidi ya mataji 18 ya AC Milan.

TUTU AMSIHI MUSEVENI ASISAINI MUSWADA WA MASHOGA

Picha
Askofu mstaafu wa Cape Town, Desmond Tutu, amemsihi Rais Museveni wa Uganda asitie saini mswada ulioleta utatanishi kuhusu wapenzi wa jinsia moja. Akofu Tutu, aliyewahi kupata tuzo ya amani ya Nobel, alisema amevunjika moyo kuwa Rais Yoweri Museveni anaonesha kubadilisha msimamo wake, kwa vile awali alisema kuwa hataruhusu mswada huo kuwa sheria. Desmond Tutu alisema haistahiki kuwa na ubaguzi kama huo, na alitoa mifano ya mfumo wa zamani wa ubaguzi wa rangi uliokuwako Afrika Kusini na ubaguzi wa Wa-Nazi wa Ujerumani. Alisema hiyo ni mifano mibaya kabisa.

REAL MADRID HAIKAMATIKI HISPANIA.

Picha
TIMU ya Atletico Madrid jana ilikula ngwala katika mbio zake za ubingwa wa La Liga baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Osasuna, hivyo kuwaacha Real Madrid wajinafasi kileleni kwa pointi tatu zaidi. Mabingwa Barcelona na vinara Real walilazimishwa sare kwenye Uwanja wa Osasuna, El Sadar mjini Pamplona mapema msimu huu na Atletico ikadondoka jana.

ASKARI WA JKT WAUA SIMBA TAIFA, LAMBALAMBA YALAMBWA NA ASKARI MAGEREZA.

Picha
SIMBA SC imelambwa mabao 3-2 na JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Azam FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Prisons ya Mbeya Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Matokeo hayo yanamaanisha, Yanga SC iliyoshinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting jana Uwanja wa Taifa, inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 38, Azam ya pili 37 na Mbeya City ya tatu 35 na Simba SC ya nne 32. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi mapumziko JKT Ruvu walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na Hussein Bunu dakika ya 14 na Emmanuel Swita dakika ya 44 kwa penalti, baada ya Henry Joseph kumuangusha Amos Mgisa kwenye eneo la hatari.

PRINCE HOZA AANZA KAMPENI ZAKE

Picha
Mgombea nafasi ya katibu uchumi na fedha wa CCM tawi la Mtambani kata ya Tabata jijini Dar es Salaam Prince Hoza akizindua kampeni zake za kuwania kiti hicho hivi karibuni, Hoza anachuana na wanachama wenzake watatu, uchaguzi rasmi utafanyika Jumatano ijayo, (Picha na Charlse Chinguile)

YANGA ILIPOILIPUA RUVU SHOOTING 7-0

Picha
Kikosi cha Yanga.

FLAMINI AZICHAPA KAVUKAVU NA WILSHERE

Picha
KIUNGO Jack Wilshere ameposti picha inayomuonyesha akipigana na mchezaji mwenzake Mathieu Flamini baada ya mazoezi jana kwenye basi la timu. Viungo hao wawili walipigwa picha wakionekana kutofautiana kwenye mazoezi ya timu hiyo saa 24 kabla ya Arsenal kuwakaribisha Black Cats katika mchezo wa Ligi Kuu. Nipishe: Jack Wilshere amehusishwa na kutofautiana na mchezaji mwenzake Mathieu Flamini kwenye mazoezi ya Arsenal jana na Bacary Sagna anaonekana kwenda kusuluhisha. Sakata la wachezaji hao wawili wa Arsenal linakuja siku kadhaa baada ya Flamini kutaka kugombana hadharani na Mesut Ozil wakifungwa mabao 2-0 na Bayern Munich Uwanja wa Emirates.

ROONEY AONGEZA MKATABA MWINGINE MAN UNITED

Picha
Wayne Rooney Wayne Rooney believes his decision to commit his long-term future to Manchester United can help the spluttering Premier League champions get back on track. United are in the midst of one of their worst seasons in recent memory and face the devastating possibility of missing out on qualification for the Champions League. Less than 12 months after Alex Ferguson bowed out as United manager by winning his 13th Premier League title, the Old Trafford outfit are a pale shadow of the side that dominated the English game. Ferguson's hand-picked successor David Moyes has been unable to make a smooth transition since arriving from Everton and, incredibly, United are languishing in seventh place, 15 points behind leaders Chelsea and 11 adrift of fourth placed Liverpool. Yet England striker Rooney is adamant the possibility of missing out on Champions League qualification never threat

UHURU SELEMAN AINYIMA UBINGWA SIMBA

Picha
Uhuru Suleiman amesema timu yake ya Simba ina mazingira magumu ya kutwaa ubingwa kutokana na ushindani mkali iliopo kwenye ligi kuu ya Bara  ugumu uliopo katika duru la pili. Lakini, kiungo huyo amesema, Simba bado ina nafasi ya kutwaa taji hilo kama itarekebisha makosa yaliyojitokeza nyuma na kufanya vizuri katika mechi zilizosalia. Akizungumza na Nipashe katikati ya wiki, Uhuru ambaye hakuambatana na Simba jijini Mbeya ambako ilitoka sare ya 1-1 na Mbeya City Jumamosi iliyopita alisema ligi imekuwa gumu kutokana na timu kukamiana na ndiyo maana timu yake haifanyi vema. "Ligi katika duru la pili imekuwa ngumu mno," alisema Uhuru nyota wa zamani wa Mtibwa Sugar na Coastal Union.

OKWI KUONGOZA MAUAJI YANGA LEO

Picha
Yanga leo inashuka kwenye Uwanja wa Taifa kucheza na Ruvu Shooting huku kocha mkuu wa timu hiyo, Hans Van der Pluijm akipanga kumtumia mshambuliaji Emmanuel Okwi kwa mara ya kwanza kwenye michezo ya ligi kuu ya Bara. Okwi hajaichezea timu hiyo mchezo wowote wa ligi tangu alipotua timu hiyo katika dirisha dogo la Januari kutokana na utata uliokuwapo kwenye usajili wake. Afisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, alisema Pluijm anaweza akamtumia Okwi leo kulingana na mahitaji yake. "Suala la Okwi kucheza au kutocheza hilo lipo mikononi mwa kocha kulingana na kikosi chake atakachokipanga kesho," alisema Kizuguto kwa sababu "kocha kwa sasa yupo huru kumtumia na kutokana na mazoezi ya leo (jana) asubuhi ni wazi atamtumia."

MKOLA MAN ATOBOA SIRI YA KUJIUNGA FREEMASON, ADAI WASANII 20 TANZANIA WAMO KWENYE DINI HIYO.

Picha
Na Prince Hoza TANGIA ilipoanza kupa kufahamika miongoni mwa wanadamu dini ya kishetani ya freemason imeanza kupata wanachama wengi, idadi kubwa ya watu hasa katika bara la Afrika imezidi kuongezeka. Nchini Tanzania kundi kubwa la vijana wanaoamini ukijiunga na dini hiyo ya kishetani unafanikiwa kimaisha, dini hiyo iliyoingia nchini miaka michache iliyopita ikitokea nchi jirani za Kenya na Uganda ambapo ndipo ilipoanza kupokelewa na kusambaa katika mikoa ya kaskazini mwa Tanzania. Lakini freemason Lakini freemason ilikuwepo tangia kuanzishwa kwa kanisa la Roma katoliki, chimbuko la imani hiyo inatokana na watoto wawili wa nabii Nuhu (Noa) Mashindano ya kwanza kufanyika duniani ya Olimpiki ni sehemu ya kusambaa kwa dini hiyo ya kishetani ambapo waumini wake hudiriki kusali wakiwa uchi. Baada ya kutapakaa sehemu mbalimbali duniani freemason iliingia nchini na baadaye ilianza kukubalika, Freemason uligeuka mtandao mkubwa na watu mbalimbali walijiunga kwa malengo  ya kufanikiwa haraka, u

TFF YAPANGUA TENA RATIBA LIGI KUU BARA, MECHI YA AZAM NA PRISONS YASOGEZWA MBELE

Picha
Na Boniface Wambura, Dar es Salaam LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaingia Raundi ya 19 kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na Arusha. Yanga itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting ya mkoani Pwani katika mechi itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Nayo Kagera Sugar inaikaribisha Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Uwanja wa Manungu uliopo Turiani mkoani Morogoro ndiyo utakaotumika kwa mechi kati ya Mtibwa Sugar na Ashanti United, wakati Coastal Union itaumana na Mbeya City katika mechi itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kutoka Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Maafande wa Oljoro JKT watakuwa nyumbani kupambana na Mgambo Shooting katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.

FUFA KUIVURUGA TENA YANGA KWA OKWI.

Picha
YANGA SC itacheza mechi ya marudiano na Al Ahly ya Misri mjini Cairo kati ya Machi 7 na 9 katika Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mchezo wa kwanza Dar es Salaam Machi 1, mwaka huu. Na kikosini mwake ina wachezaji wawili tegemeo wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes ambao ni washambuliaji Emmanuel Okwi na Hamisi Kiiza. Uganda imetangaza itacheza mechi ya kirafiki na Zambia, Chipolopolo iliyo katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Machi 5, mwaka huu Uwanja wa Ndola, Zambia. Hiyo imethibitishwa na Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Edgar Watson baada ya kufikia makubaliano na wenzao, Chama cha Soka Zambia (FAZ). Kocha Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ bado hajataja kikosi ambacho kitacheza na Zambia, lakini wakati wote amekuwa hawaachi Okwi na Kiiza na bila shaka ataendelea na utamaduni huo.

KOCHA SPURS ALALAMIKIA UWANJA UKRAINE BAADA YA KUFUNGWA

Picha
Kocha mkuu wa Tottenham hotspurs ya Uingereza ,Tim Sherwood amesema uwanja wa FC Dnipro ya Ukraine haufai kabisa. Sherwood alilaumu uwanja huo kwa kichapo cha bao moja kwa nunge katika mraundi ya kwanza ya mchuano wa ligi ya Europa huko Ukraine . Spurs ilishindwa mechi yake ya kwanza baada ya kucheza mechi 16 . Hata hivyo, Spurs itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kufunga mabao fursa yao nzuri ikipotezwa na Roberto Soldado.

BRAZIL YAZINDUA MPANGO MPYA WA KUJILINDA

Picha
Maafisa wa usalma nje ya Uwanja wa Mineirao Brazil imetangaza kwamba wameongeza maafisa wa kulinda usalama 70,000 zaidi watakao toa huduma za usalama katika fainali ya Dimba la Kombe la Dunia mwaka huu. Idadi hii iliyoongezwa ni katika jitihada za kukabiliana na tishio la usalama na maandamano . Idadi iliyopendekezwa hapo mbeleni ya maafisa 100,000 . Kwa ujumla maafisa wa usalama wapatao 170,000 watatumika katika miji 12 itakayoandaa mashindano hayo. Jumatano wiki hii Rais wa Brazil Dilma Rouseff alisema kwamba jeshi litajumuishwa kwenye mpango huo dhabiti wa usalama iwapo kutaibuka wimbi lingine la maandamano.

MBEYA CITY WAPIGA KAMBI MOMBASA KUIUA COASTAL UNION KESHO

Picha
Na Salum Fikiri Jr Kikosi cha Mbeya City kimeweka kambini jijini Mombasa, Kenya kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kesho. Msemaji wa Mbeya City, Fred Jackson alisema jana kuwa, kikosi chao kinachonolewa na kocha mzawa, Juma Mwambusi kitakuwa kikijifua jijini Mombasa hadi kesho asubuhi kitakaposafiri kwa basi kwenda jijini Tanga kuwakabili Coastal Union jioni. "Tulianza safari yetu kuelekea Kenya jana (juzi), tumelala Dar es Salaam. Asubuhi hii tunaunganisha ndege kwenda Mombasa ambako timu itakaa hadi Jumamosi asubuhi," alisema Jackson.

KOCHA WA YANGA AAPA KUIUMALIZA MAPEMA AL AHLY

Picha
Na Regina Mkonde, Bagamoyo Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm, amesema atahakikisha anatumia mbinu zote alizo nazo ili kuiondoa Al Ahly ya Misri kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuifanya ajira yake iendelee kuwapo ndani ya Wanajangwani hao. Akizungumza juzi jioni baada ya timu hiyo kufika Bagamoyo mkoani Pwani, Pluijm alisema aliufahamu 'mtihani' huo wa kukabiliana na Al Ahly mapema kabla ya kuja nchini kukubali ajira ya kuifundisha Yanga. Pluijm alisema katika soka hakuna kitakachoshindikana na akaongeza dakika 180 ndizo zitakazoamua nani atasonga mbele. Mholanzi huyo alisema katika dunia ya sasa kwenye soka hakuna mechi rahisi au mashindano mepesi na kwamba kila upande unajiandaa kufanya vizuri na kuweka rekodi.

TWIGA STARS, ZAMBIA KUUMANA MACHI 2

Picha
Na Boniface Wambura MECHI ya pili ya raundi ya kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo) itachezwa Machi 2 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Twiga Stars tayari imeingia kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi za bandia kama ulivyo ule wa Azam Complex. Shepolopolo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.

MASIKINI EMMANUEL OKWI! TFF YAMKANDAMIZA TENA KWENYE SAKATA JINGINE,IKIBAINIKA KUFUNGIWA MAISHA.

Picha
Sakata la uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi limeanza kuwatafuna vigogo wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakidai kushughulikia suala hilo kiushabiki badala ya kufuata taratibu. Taarifa ya Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura jana ilisema kuwa kiongozi wa idara ya Takwimu, Sabri Mtulla analalamikiwa na  shirikisho hilo kwa madai ya kuidanganya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi  dhidi ya  usajili wa Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si kweli. “Kamati ilikutana mara ya kwanza, ikahoji kama kuna pingamizi lolote dhidi ya Okwi, lakini Mtulla alidanganya kuwa hakuna, kamati ilivyokutana kwa mara ya pili ikabaini pingamizi lilikuwepo, ila kiongozi huyo alificha wakati alijua wazi kuwa Simba walikuwa wameweka pingamizi  wakipinga Okwi kusajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.

PSG YAICHAKAZA BAYER LEVERKUSEN

Picha
Zlatan Ibrahimovic aifungia PSG dhidi ya Bayer Leverkusen Zlatan Ibrahimovic alifunga mabao mawili na kuisaidia Paris St-Germain kusajili ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Bayer Leverkusen katika mchuano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya. Blaise Matuidi ndiye aliyefungua mvua hiyo ya mabao alipotikisa wavu kunako dakika ya tatu ya ya kipindi cha kwanza na kumwacha kipa Bernd Leno amezubaa.

MAN CITY YAFUNGWA NYUMBANI NA BARCELONA

Picha
Kipa Joe Hart na mshambulizi wa Barcelona Messi Matumani ya timu ya Manchester City kunyakuwa taji la ligi ya mabingwa ulaya yalipata pigo baada ya wachezaji wa Barcelona Lionel Messi na Dani Alves kufunga jumla ya mabao mawili katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Etihad. Messi alikuwa wa kwanza kufunga kupitia penalty katika dakika ya 54 alipoangushwa na difenda Martin Demichelis aliyepewa kadhio nyekundu. Licha ya Manchester City kuwa kasoro mchezaji mmoja walijizatiti kukabiliana na timu hiyo ya Uhispania ila Dani Alves alizima matumaini yao mbele ya mashabiki wao alipofunga bao la pili mwisho mwisho wa kipindi cha pili.

MAKALA: RAGE ANAMALIZA UENYEKITI WAKE SIMBA, BILA MAKAMU MWENYEKITI.

Picha
Na Salum Fikiri Jr SASA hivi hatuna haja ya kuangalia maigizo ya vichekesho kwenye luninga, siyo dili tena, ndio maana wasanii wa vichekesho wameanza kuipa kisogo fani hiyo, eti wanasema hailipi, ila hawajagundua kitu. Kama inavyoelewa, Tanzania kila mtu msanii, mambo yote yanaenda kisanii tu, ukienda kwenye majukwaa ya kisiasa utavunjika mbavu mwenyewe, kiongozi tena waziri anahutubia wananchi na kuwaambia 'kama hamtaki kuleni nyasi, lazima ndege ya rais inunuliwe', maneno anayatoa baada ya wananchi kumuomba waziri asiidhinishe manunuzi ya ndege ya rais ambayo inagharimu mamilioni ya fedha. Tuachane na hiyo, waziri mwingine aliwahi kuwaambia wananchi waogelee kwenye maji baada ya kushindwa kuwaletea kivuko kipya alichowaahidi, hiyo ni moja kati ya vunja mbavu ambazo tulikuwa tunazipata kwenye sanaa ya vichekesho pekee. Msishangae kauli ya msanii mkongwe wa vichekesho nchini Amri Athuman 'King Majuto' kwamba anataka kuachana na maigizo na kwenda kujikita kwenye

ROONEY KUONGEZA MKATABA MAN UNITED

Picha
Wayne Rooney   Wayne Rooney anatarajiwa kutia saini mkataba mpya wiki hii ambao utaweka straika huyo wa Uingereza katika Manchester United hadi mwisho wa msimu wa 2018-2019, vyombo vya habari nchini humo viliripoti Jumatatu. Mchezaji huyo wa miaka 28 huenda atie saini mkataba huo Old Trafford Jumatano au Alhamisi, Chama cha Wanahabari kilisema. Kumekuwepo na shaka kuhusu mustakabali wa Rooney katika miamba hao wa Ligi Kuu ya Uingereza hasa baada ya Chelsea kujaribu kumshawishi ajiunge nao kabla ya kuanza kwa msimu huu. Licha ya masaibu ya United kwa sasa mbele ya meneja mpya David Moyes – ambayo yamepelekea wao kukwama nambari saba, alama 15 nyuma ya viongozi Chelsea – Rooney anadaiwa kutulia Old Trafford.

LEO NDIO LEO, MAN CITY VS BARCELONA.

Picha
Yaya Toure Manchester City and Barcelona's Uefa Champions League round of 16 first leg will be their first competitive encounter, but there are unlikely to be too many surprises for either side given the hosts' Spanish connections. Watch the action live on SS3, SS3HD and live streaming on supersport.com from 9pm (CAT, GMT +2). City's squad features four Spaniards – Javi García, Jesús Navas, Álvaro Negredo and David Silva – along with four more players also signed from Spain's top flight including Yaya Touré, who joined from Barcelona in 2010. Additionally they have in Manuel Pellegrini a coach well acquainted with the Spanish game, and in director of football Txiki Begiristain a man who knows Barcelona better than most. Pellegrini's City reached this stage by finishing second in Group A where they took 15 points – two more than Gerardo Martino's Barcelona managed in wi

NGASA AMFUNIKA OKWI YANGA.

Picha
BAADA ya mechi 20 za kuichezea klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam tangu arejee msimu huu, Mrisho Khalfan Ngassa amedhihirisha klabu hiyo haikukosea kumrejesha Jangwani. Jumapili Ngassa alicheza mechi ya 20 tangu arejee Yanga SC msimu huu akitokea kwa mahasimu, Simba SC alikocheza msimu mmoja akitokea Azam FC, waliomtoa Jangwani mwaka 2009. Ngassa alifunga mabao matatu katika ushindi wa 5-2 mjini Moroni, Comoro dhidi ya wenyeji, Komorozine katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali, Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika mechi hizo 20, Ngassa ametimiza mabao 15 na kuwapiku wachezaji kadhaa waliomtangulia, huku kukiwa kuna kila dalili atampiku Mrundi Didier Kavumbangu, mchezaji mwenye mabao mengi kati ya nyota waliojiunga na timu hiyo ndani ya misimu hii miwili.

RATIBA KAMILI RAUNDI YA KWANZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA HII HAPA

Picha
Yanga SC (Tanzania) Vs Al Ahly (Misri) Berekum Chelsea (Ghana) Vs Ahli Benghazi (Libya) Gor Mahia (Kenya) Vs Esperance (Tunisia) Enyimba (Nigeria) Vs AS Real (Mali) Astres de Douala (Cameroon) Vs TP Mazembe (DRC) B.Y.C (Liberia) Vs Sewe Sport (Ivory Coast) Dedebit (Ethiopia) Vs CS Sfaxien (Tunisia) Horoya (Guinea) Vs Raja Casablanca (Morocco) Flambeau de l’Est (Burundi) Vs Coton Sport (Cameroon) Entente Setif (Algeria) Vs ASFA Yennenga (Burkina Faso) Stade Malien (Mali) Vs El Hilal (Sudan) AC Leopards (Congo) Vs Primeiro de Agosto (Angola) Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) Vs Liga Muçulmana (Msumbiji) Dynamos FC (Zimbabwe) Vs AS Vita Club (DRC) Zamalek (Misri) Vs Kabuscorp (Angola)

JANUZAJ AITWA KOSOVO KUIVAA HAITI.

Picha
KINDA Adnan Januzaj amepigiwa simu na Naibu Waziri Mkuu wa Kosovo kuombwa aichezee mechi ya kwanza ya kimataifa nchi hiyo. Behgjet Pacolli, bilionea mmiliki kampuni za ujenzi anayekadiriwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 550, anajaribu kumshawishi Januzaj acheze dhidi ya Haiti mwezi ujao. Januzaj, mwenye umri wa miaka 19, bado hajaamua acheze nchi gani soka ya kimataifa, lakini familia yake ilikuwa moja ya wanaharakati wa uhuru wa nchi hiyo. Pamoja na hayo, Kosovo bado haijapata uanachama wa FIFA, wameruhusiwa kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Haiti mwezi ujao.

BAADA YA KUHOJIWA, MEMBE ADAI, URAIS MCHUNGU KAMA SHUBIRI

Picha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amesema aliulizwa maswali mazito na Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Phillip Mangula kuhusu mbio za urais 2015. Akizungumza jana mjini Dodoma muda mfupi baada ya kuhojiwa na kamati hiyo, Membe alisema kamati hiyo inauliza maswali magumu kuhusu wanayoyafanya pamoja yanayofanywa na mashabiki wao. “Kamati inauliza maswali mazito na magumu yanayohusiana na uvunjaji wa maadili ya uongozi wa chama chetu… Kamati ya maadili imejipanga vizuri sana wala msidanganyike, wanauliza maswali mazito,” alisema Membe. Membe aliongeza kusema aliulizwa mambo makubwa matatu, kubwa likiwa ni kuibuka ghafla kwa makundi makubwa ambayo yanazaliwa kila wakati chama hicho kinapokaribia kwenye uchaguzi wa Rais.

AZAM YAHAMISHIA HASIRA ZAKE LIGI KUU BARA.

Picha
AZAM FC sasa inaelekeza nguvu zake katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jana kutolewa mapema katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika. Timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake, yenye maskani yake Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, jana ilifungwa mabao 2-0 na wenyeji Ferroviario Beira kwenye Uwanja wa Ferroviario Beira mjini Beira Msumbiji katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho. Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ amesema kwamba matokeo hayo yamewaumiza, lakini wanalazimika kukubaliana nayo kwa sababu huo siyo mwisho wa maisha.

LIVERPOOL SI LOLOTE KWA ARSENAL, YADUWAZWA 2-1

Picha
BAO la Alex Oxlade-Chamberlain na pasi ya bao vimetoa mchango mzuri kwa Arsenal kutinga Raundi ya sita ya Kombe la FA baada ya kuifunga Liverpool mabao 2-1 Uwanja wa Emirates. Kiungo huyo kinda wa England alifunga bao la kwanza dakika ya 16 akimalizia pasi ya Lukas Podolski, aliyefunga bao la pili dakika ya 47. Refa Howard Webb aliwapa penalti Liverpool baada ya Podolski kumchezea faulo Luis Suarez, na Steven Gerrard akaenda kufunga dakika ya 59.

OBAMA AMUONYA MUSEVENI.

Picha
Rais wa Marekani Barrack Obama amemwonya rais wa Uganda,Yoweri Musuveni, kwamba ikiwa atasaini mswada wa sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja basi uhusiano kati ya Uganda na Marekani utatatizika. Chini ya sheria hiyo iliyopendekezwa, watu watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ushoga watakabiliwa na hukumu kali, ikiwemo kifungo cha maisha jela. Marekani ni mojawepo wa mataifa ya kigeni yanayotoa kiwango cha juu zaidi cha msaada kwa Uganda, na mwaka 2011 idadi ndogo ya wanajeshi wa Marekani walitumwa kulisaidia jeshi la Uganda kupanda na kundi la waasi wa Lords Resistance Army, LRA.

AMISSI TAMBWE, HAWEZEKANIKI TENA KWA MABAO.

Picha
Na Salum Fikiri Jr KAMA kuna kosa kubwa lilifanywa na uongozi wa Simba ni pale ulipoamua kumuuza mshambuliaji wake ghali na wa kimataifa Mganda Emmanuel Okwi kwa waarabu wa Etoile Du Sahel ya Tunisia na kuibua maswali kadhaa kwa mashabiki wa soka. Simba ilifanya kosa hilo ambalo mpaka sasa limeweza kuiatihili, Simba ilipoteza mwelekeo baada ya kuondoka mshambuliaji huyo ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa timu pinzani hasa Yanga. Yanga hawatamsahau Okwi kwa vile ndiye aliyeandikisha rekodi ya ushindi wa mabao 5-0 ambao mpaka sasa bado unawatesa, katika ushindi huo wa kihistoria Okwi aliweza kufunga magoli mawili huku akisaidia kutengeneza mengine matatu. Bosi wa Yanga Yusuf Manji alitumia kila njia kuhakikisha anampata Okwi, ni kweli yametimia kwa licha ya uongozi wa Simba kumuuza kwa Etoile Du Sahel ya Tunisia, Yanga ilitumia njia ya mkato na kumnasa mshambuliaji huyo.

PISTORIUS AJUTIA KIFO CHA MPENZI WAKE

Picha
Oscar Pistorius DUNIA leo inaadhimisha siku ya wapendanao yaani Valentine Day, Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amezungumzia masikitiko na majuto yake kuhusu mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp, mwaka mmoja uliopita. Katika taarifa kwa mtandao wake, alisema: ''Kumpoteza Reeva kulinipa huzuni mkubwa sana siku hiyo na nitaubeba maisha yangu yote.'' Kesi ya mauaji dhidi ya Pistorius inatarajiwa kuanza mjini Pretoria mnamo mwezi Machi. Oscar anasema kuwa alimpiga risasi Reeva kwa bahati mbaya baada ya kudhani kuwa alikuwa jambazi ndani ya nyumba yake alipompiga risasi kupitia mlango wa bafu yake mwaka 2013. Mwendesha mkuu wa mashitaka anadai kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kupangwa baada ya wawili hao kuzozana.

YAMETIMIA, OKWI NI MALI YA YANGA YAKIRI TFF, FIFA.

Picha
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limemuidhinisha mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi kuchezea klabu ya Yanga ya Dar es Salaam. Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa amesema kwamba, FIFA imewaandikia barua ikiwaambia Okwi ni halali kuchezea Yanga SC. “Suala la Okwi limekwisha, ila siwezi kuzungumza zaidi kwa sasa naingia kwenye kikao, tutatuma taarifa kwa vyombo vya habari baadaye,”alisema Mwesigwa. Januari 22 mwaka huu ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilisimamisha usajili wa Mganda huyo Yanga ili kwanza upatikane ufafanuzi kutoka FIFA juu ya uhalali wake kucheza timu hiyo ya Jangwani akiwa anatambulika kama mchezaji wa Etoile du Sahel ya Tunisia. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Januari 22, mwaka huu kupitia masuala mbalimbali, ilisema imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC V

LIONEL MESSI AANDIKISHA REKODI NYINGINE BARCA

Picha
MSHAMBULIAJI Lionel Messi ameweka rekodi nyingine ya mabao wakati Barcelona ikitinga fainali ya Kombe la Hispania kuelekea mechi na Manchester City wiki ijayo Ligi ya Mabingwa Ulaya. Messi alifunga katika sare ya 1-1 na Real Sociedad na kufikisha mabao 335 hivyo kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika klabu hiyo ya Hispania. Barca imeingia fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1 baada ya awali kushinda 2-0 na sasa itakutana na Real Madrid katika mechi ya kuwania Kombe.

MAKALA; WIMBI HILI LA VIGOGO WA SIMBA NA YANGA KUJAZANA TFF LINAASHIRIA NINI?

Picha
Na Prince Hoza WAKATI Watanzania wakijiandaa kutimiza miaka 53 ya muungano huku kukiwa na mafanikio hafifu kwenye ekta muhimu, upande wa michezo nao si lolote, Kilio kikubwa ni ukosefu wa viwanja pamoja na uduni wa kiwango cha soka kinachoonyeshwa na timu ya taifa, Taifa Stars. Taifa Stars imeonyesha kuwakera wadau wa soka nchini na kuamua kuhamishia mapenzi yao kwa timu za mataifa mengine, uzalendo umetoweka kabisa, mwaka 2006 rais wa TFF wakati huo Leodegar Tenga alitangaza mikakati kabambe ya kurejesha hamasa ya soka nchini. Tenga alitangaza kutengeneza misingi imara ya soka nchini, jitihada za Tenga ziliungwa mkono na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete .

MMAREKANI ANYAKUA TUZO YA FIFA 2014 WORLD CUP SUPER SONG COMPETETION.

Picha
Na Regina Mkonde Msanii kutoka marekani anayefahamika kwa jina la Elijah King, juzi aliibuka mshindi kwa kunyakua tuzo ya Super Song iliyoandaliwa na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. Nyimbo iliyompa ushindi mwanamuziki huyo ni nyimbo ya VIDA, Nyimbo ambayo mashairi yake yamesimama na ya kuvutia kiasi kwamba ikazifunika nyimbo nyingine zote zilizokuwa zinashindania tuzo hiyo. Kutokana na ubora wa nyimbo hiyo iliwaweka majaji hao katika wakati mgumu kuchuja na nyimbo nyingine, Na kuzidi kuipa nafasi nyimbo hiyo kwa kura nyingi hatimaye juzi kuibuka mshndi wa nyimbo bora ya FIFA 2014 WORLD CUP SUPER SONG COMPETETION. Mashindano hayo ambayo juzi yalikuwa fainali ambapo staa Ricky Martin, alipomtangaza rasmi Mmarekani huyo kuwa ni mwanamuziki bora wa FIFA mwaka 2014.Na wimbo wake kuwa ni wimbo bora katika mashindano hayo.

CHELSEA YAKABWA KOO NA WEST BROM 1-1

Picha
Wachezaji wa West Brom Chelsea imepoteza nafasi ya kuhakikisha kuwa imesalia kileleni mwa ligi kuu ya Premier ya Uingereza, mbele ya mahasimu wao Arsenal, baada ya kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na West Brom, katika mechi iliyochezewa katika uwanja wa Hawthorns. Victor Anichebe aliifungia West Brom bao hilo muhimu kunako dakika ya 87 Na kuinyima Chelsea alama mbili ambazo zingeihakikishia Chelsea hakikisho la uongozi wa ligi hiyo hadi juma lijalo. Branislav Ivanovic aliiweka Chelsea mbele dakika ya 45, bao ambalo lilikuwa limeipa vijana hao wa Jose Mourinho kuwa alama nne mbele ya Arsenal ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya pili.

TFF KUMRUHUSU OKWI KUKIPIGA YANGA.

Picha
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema linajipanga kulipigia simu Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kusaka ufafanuzi wa uhalali wa usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kwa klabu ya Yanga. Januari 22 mwaka huu ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilisimamisha usajili wa Mganda huyo katika klabu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi Fifa. Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema jana mchana jijini hapa kuwa baada ya kusubiri kwa muda mrefu pasipo kupewa ufafanuzi wowote, wameamua kulitwangia simu shirikisho hilo la kimataifa.