RAIS MAGUFULI AMTEUA JERRY MURO KUWA MKUU WA MKOA PIA YUMO MISS TANZANIA
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli leo ameshangaza baada ya kumteua aliyekuwa msemaji wa Yanga SC Jerry Cornell Muro kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Rais Magufuli amefanya uteuzi mbalimbali wa wakuu wa mikoa na wilaya leo hasa baada ya waliokuwa wakishikilia nyadhifa hizo wengine kustaafu na wengine kupandishwa vyeo na kubadilishiwa nyadhifa.
Mbali na Jerry Muro ambaye anakumbukwa vema kwa kazi yake ya usemaji pale Jangwani akishindana na hasimu wake Haji Manara, Rais Magufuli pia amemteua aliyewahi kuwa mmoja kati ya mamiss Tanzania na msanii wa filamu Jokate Mwegelo kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu leo imeonyesha mabadiliko mbalimbali ya wakuu wa wilaya na mikoa, mwanamichezo mwingine aliyekutwa na ngekewa hiyo ni Amos Makala ambaye awali alikuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na sasa amehamia Katavi