Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2024

CHASAMBI APEWA ONYO SIMBA

Picha
INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Simba, Ladack Chasambi ambaye ni kiungo mshambuliaji amepewa onyo mapema kutofikiria atafanya makubwa ndani ya timu hiyo kwa kuwa bado anahitaji muda zaidi. Chasambi kasajiliwa Simba akitokea Mtibw Sugar ya Morogoro alipokuwa ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila. Shiza Kichuya nyota anayetumia zaidi ya mguu wa kushoto amesema kuwa ni muhimu kwa Chasambi kuwa makini na kujifunza zaidi baada ya kupata changamoto mpya. "Namtambua Chasambi ni mchezaji mzuri na amepata nafasi ya kujiunga na Simba ambayo ni timu kubwa. Anahitaji muda ili kufanya vizuri asifikirie kwa wakati huu anaweza kufanya makubwa bado atajiongezea presha kubwa ikiwa ataanza kuwaz hivyo,". Simba kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa raundi ya pili dhidi ya Tembo FC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Januari 31, Uwanja wa Azam Complex. saa 1:00 usiku. Ladack Chasambi amepewa onyo

SIMBA YAMLA TEMBO MARA 4

Picha
Wekundu wa Msimbazi , Simba SC jioni ya leo imedhihirisha kwamba wao ni wakubwa mbele Tembo baada ya kuilaza mabao 4-0 katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup, ASFC maarufu kombe la FA. Wekundu hao waliandika bao la kwanza kupitia kwa Luis Miquissone dakika ya 11 kabla ya Saido Ntibanzokiza kupiga la pili dakika ya 31. Lakini Wekundu hao waliandika bao la tatu kupitia kwa Omar Jobe daiika ya 81 kabla ya Saleh Karabaka kuhitimisha ushindi wa Wekundu hao daoika ya 83

MUBARAK AMZA AJIUNGA KAGERA SUGAR

Picha
Kiungo Mshambuliaji wa Zamani wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga, Mubarak Amza Ngamchiya raia wa Cameroon amejiunga na Klabu ya Kagera Sugar ya hapa mkoani Kagera kwa mkataba wa iiaka miwili akitokea klabu ya Ihefu SC kwa uhamisho huru baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na klabu hiyo kutoka wilayani Mbarali Jijini Mbeya. Mubarak Amza amejiunga Kagera Sugar

WINGA SENEGAL AISHUTUMU CAF

Picha
Winga wa timu ya Taifa ya Senegal, Krepin Diatta ameibua hoja ya rushwa akiwatuhumu waandaaji wa mashindano ya AFCON Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwadhulumu haki yao kwenye mchezo wa hatua ya (16) Bora dhidi ya wenyeji wa Mashindano hayo Ivory Coast na kuwapa upendeleo wenyeji. “Mmetudhulumu, mashindano yamejaa rushwa bakini na Kombe lenu” alisema Diatta, Hii ni baada ya Ivory Coast kupata penati dakika za mwishoni ,penati iliyoamuliwa na VAR, Hata hivyo mchezaji huyo anaweza kukutana na adhabu kutoka CAF kwa kuwatuhumu kuendesha mashindano kwa rushwa. Diatta

DJIGUI DIARRA AWEKA REKODI LIGI KUU BARA

Picha
Mlinda mlango bora nchini kwa kipindi cha misimu miwili Djigui Diarra wa Yanga na Malia ameweka rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kutoka Ligi Kuu ya kuanza michezo 4 mfululizo katika michuano ya AFCON 2023. Pia Diarra anaungana na walinda milango wengine Afrika ambao wamecheza mechi 4 mfululizo katika Afcon akiwemo Edouard Mendy wa Senegal,Llyod Kazapua wa Namibia,Stanley Nwabali wa Nigeria na Yahia Fofana wa Ivory Coast. Djigui Diarra

MALI YATINGA ROBO FAINALI AFCON

Picha
Hatimaye timu ya taifa ya Mali usiku huu imeingia robo fainali ya michuano ya mataifa Afrika, AFCON nchini Ivory Coast baada ya kuilaza Burkina Faso mabao 2-1. Kwa matokeo hayo sasa Mali imeingia robo fainali na inamngoja mshindi kati ya Morocco au Afrika Kusini watakaokutana saa 5 usiku. Mabao ya Mali yamefungwa na Edmond Tapsoba dakika ya 3 na Lassine Sinayoko dakika ya 47 wakati la Burkina Faso limefungwa na Bertrand Traore, pia jana usiku Senegal ilivuliwa ubingwa na wenyeji Ivory Coast baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 9-8 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Mali wameingia robo fainali AFCON

MZIZE APIGA HAT TRICK, YANGA IKIICHAPA HAUSING FC 5-1

Picha
Mabingwa watetezi wa kombe la Azam Sports Federation Cup, maarufu ASFC au kombe la FA, Yanga SC usiku huu imeichapa Housing FC ya mkoani Njombe mabao 5-1 katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. Yanga walitangulia kupata bao kupitia kwa Jonas Mkude kynako dakika ya 19 kabla ya Skudu Makulubela kuandika la pili dakika ya 25. Lakini Clement Mzize alifunga mabao yote matatu kunako dakika ya 27, 33 na 57, Tony Jailos aliifungia Housing bao LA kufuta machozi dakika ya 70, kesho Simba wataumana na Tembo ya Tabora Yanga wakishangilia mabao yao

ADAM ADAM WA MASHUJAA AMHOFIA BACCA WA YANGA

Picha
Mshambuliaji wa Mashujaa FC, Adam Adam amesema Ligi Kuu Tanzania Bara ina mabeki wengi wa kati lakini beki wa Young Africans, Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ ndiye anayempa wakati mgumu wanapokutana uwanjani. Adam amesema kuwa timu kubwa zinaenda mbali kusajili lakini zikitulia hapa nyumbani kuna wachezaji wengi wazuri na viwango vyao vinalingana na hao wa nje ya nchi, akimtolea mfano Bacca ambaye ndio muhimili wa safu ya ulinzi ya Young Africans. “Bacca ni mchezaji mzuri na mtulivu anayeweza kukabiliana na mshambuliaji wa aina yoyote ile ndio maana hata mimi ninapokutana naye huwa Napata wakati mgumu kutokana na ubora wake. “Upande wa nyota chipukizi anayenifurahisha ni Clement Mzize kwa staili yake ya uchezaji, ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee ambaye kama akiendelea hivi atafika mbali,” amesema Adam. Katika hatua nyingine Adam amesema kuwa katika mchezo ujao dhidi ya Simba SC, wao hawaangalii ukubwa wao wanachoangalia ni kucheza mpira. Adam Adam “Tukikutana na Simba SC tutawaheshimu ni

MGOSI AIANGUKIA TFF

Picha
Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’ ameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuangalia uwezekano wa kurekebisha ratiba ya ligi hiyo kutokana na kupitia changamoto mbalimbali zinazowasababishia kukosa muda wa kupumzika. . “Tumetoka Dar kwenye mechi na JKT Queens, tukasafiri kwenda Iringa kucheza na Amani, kisha Musoma dhidi ya Bunda halafu tumecheza tena Dar na Bunda kisha tutarudi tena Dodoma hivyo kuna haja ya TFF kuangalia hilo,” alisema na kuongeza; . “Licha ya changamoto hiyo ila sisi bado tunaendelea na mapambano yetu ili tufanye vizuri na kuchukua ubingwa kwa msimu huu.” Timu hiyo inaendelea kushika nafasi ya pili baada ya michezo ya raundi ya sita huku JKT Queens ikiendelea kuongoza na pointi 18. . Musa Mgosi kocha msaidizi Simba Queens

CAPE VERDE KUMNGOJA SENEGAL AU IVORY COAST

Picha
Bao pekee lililofungwa na nahodha wa timu ya taifa ya Cape Verde, Mendez limeiwezesha kutinga robo fainali baada ya kuilaza Maurtania bao 1-0 kwenye mchezo uliomalizika muda huu hatua ya 16 bora Afcon zinazofanyika Ivory Coast. Jana usiku DR Congo iliifuata Guinea baada ya kuiondosha kwa matuta Misri baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, DR Congo ilipata penelti 9 dhidi ya 8 za Misri. Mechi itakayofuata usiku huu ni kati ya wenyeji Ivory Coast na mabingwa watetezi Senegal

WACHEZAJI WATATU NIGERIA WADAIWA KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU DHIDI YA CAMEROON

Picha
Zaidi ya wachezaji 3 Wa timu ya Taifa ya Nigeria akiwemo Victor Osimhen watafanyiwa vipimo vya Afya baada ya kuhisiwa kuwa walitumia dawa za kuongeza Nguvu katika mechi dhidi ya Cameroon Ambapo timu ya taifa ya Nigeria ilipata ushindi Wa magoli 2.

NEVER TIGERE AREJEA KWAO ZIMBABWE

Picha
Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Never Tigere Amejiunga na klabu ya Ngezi Platinum Stars ya Zimbabwe kwa Kandarasi ya mwaka mmoja nusu Akitokea klabu ya Ihefu SC ya Tanzania kwa Uhamisho Huru Baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Ihefu SC. Tigere atakumbukwa kwa assist zake za mabao ya Ihefu dhidi ya Yanga ambapo timu hiyo ilipekeka salamu za ushindi mara mbili mfululizo huku pia akiweza kuifunga Yanga kwa mipira ya adhabu ndogo

KIDUKU AMJIBU MWAKINYO

Picha
Vita ya maneno kati ya mabondia Twaha Kiduku na Hassan Mwakinyo imezidi kushika kasi, baada ya Kiduku kuandika ujumbe kwenye Instagram ukionekana ni ujumbe uliomlenga Mwakinyo. Baada ya Bondia Hassan Mwakinyo kumtwanga kwa TKO bondia Elvis Ahorgah kutoka Ghana katika raundi ya Saba ya Pambano la ubingwa wa WBO Afrika. Kufuatia ushindi huo Mwakinyo aliweka wazi kuwa ametuma salamu Morogoro kuwa yupo tayari kupigana. “Nilikuwa nataka kutuma salamu Morogoro kwa watu ambao walikuwa wanaamini naogopa zile Piko kama mabibi harusi wa huku nilikuwa nataka kutumia hii Fursa kama mfano kuonesha kwamba dau likifikiwa ambalo lipo katika nakubaliano yangu mimi na timu yangu pambano litapigwa hata la kirafiki ili tuone nani ni nani.” amesema Mwakinyo. Nae Twaha Kiduku bondia kutoka Morogoro kupitia mtandao wa Instagram kwenye ukurasa wake ameandika . ‘’Mwenye hasira nyingi,ana hekima chache.” Twaha Kiduku

NANDY AMFANYIA KITU MBAYA BRIGHT

Picha
Mwimbaji wa Bongofleva, Bright amedai kuwa Nandy kwa sasa hapokei simu zake licha ya huko nyuma kumsaidia kupitia kolabo yao, Umebadilika (2017) ambayo ilimtangaza zaidi African Princess huyo. "Watu hawana shukrani, nilimsaidia Nandy wakati hajajulikana vizuri, tukafanya nae wimbo watu wakamjua kwa ukubwa lakini baada ya kupata mafanikio zaidi yangu hataki tena kusikia habari zangu na hata simu zangu hapokei. Umri wangu bado mdogo ipo siku nitafanikiwa"- Bright.

YANGA KUIVAA HOUSING FC FA CUP

Picha
Baada ya takribani mwezi mzima kwa mashabiki wa Yanga kukosa burudani ya timu yao, hakuna tena muda wa kusubiri kwani keshokutwa Jumanne, Januari 30 Yanga itakuwa uwanjani kumenyana na Housing Fc katika mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) raundi ya pili Yanga tayari imeweka hadharani vingilio vya mchezo huo ambapo VIP A ni Tsh 20,000/-, VIP B ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/- Mtanange utapigwa saa 1 usiku Katika Uwanja Wa Azam Complex Chamazi

GUINEA YAICHAKAZA EQUATORIAL GUINEA LALA SALAMA

Picha
Dakika za jioni kwbisa zimeifanya Guinea kutinga robo fainali ya kombe la mataifa Afrika, AFCON baada ya kuilaza Equitorial Guinea bao 1-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora. Bao pekee lililofungwa dakika ya 90+8 na Mohamed Lamin Bayo limeifanya timu hiyo kuisubiria Misri au DR Congo ambazo baadaye zitashuka uwanjani. Jana usiku Nigeria iliilaza Cameroon mabao 2-0 na kutinga robo fainali, saa 5 usiku Misri itaumana na DR Congo

BALEKE AENDE LIBYA KWA MKOPO

Picha
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Jean Othos Baleke (23) amejiunga na Al Ittihad ya Libya kwa Mkopo wa mwaka mmoja hadi Januari 30, 2025, Baleke alieifungia Magoli (8) Msimu huu akiwa na Simba amejiunga na Al Ittihad baada ya kuachana na Simba SC na kumrudisha TP Mazembe ambapo imemtoa tena kwa mkopo mwingine. Jean Baleke amesajiliwa kwa mkopo Libya

MWAKINYO ATWAA MKANDA WA WBO KWA KO

Picha
Bondia kutoka Tanzania Hassan Mwakinyo amefanikiwa kunyakua Mkanda wa WBO baada ya kumtuanga Bondia kutoka nchini Ghana Elvis Ahorgah kwa KO raundi ya 7. Mwakinyo amefanikiwa kuubeba mkanda huo katika pambano lililifanyika Zanzibar..

MAMELOD YANASA KIUNGO WA ORLANDO PIRATES

Picha
Klabu ya Mamelodi Sundowns FC imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Thembinkosi Lorch (30) kutoka Orlando Pirates FC, Lorch aliyeitumikia Pirates kwa miaka 8 akicheza michezo 176, akifunga magoli 34. Huu Unakuwa Usajili wa nne kwa "Masandawana" katika dirisha ili Usajili mwezi Januari baada ya kuwasajili Tashreeq Mathew kutoka IK Sirius ya Sweden, Matias Esquivel kutoka Club Atletico Lanus ya Argentina na Zuko Mdunyelwa kutoka Chippa United.

SIMBA YAMWANGUKIA CHAMA, YATAKA AREJEE KIKOSINI

Picha
Klabu ya soka ya Simba imemtaarifu Clatous Chama kuwa arejee kambini kwaajili ya kutumikia mkataba wake wa miezi mitano uliobaki. Klabu itazungumza nae kuhusu suala lake la nidhamu kisha itamruhusu aanze mazoezi na wachezaji wenzake Clatous Chama .

ANGOLA WANAKWENDA ROBO FAINALI

Picha
Mabao matatu yaliyowekwa kimiwni na Delson Dala dakika ya 38 na dakika ya 42 huku lingine likiwekwa wavuni na Mabululu dakika ya 66 yametosha kabisa kuilaza Namibia mabao 3-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya kombe la mataifa Afrika, AFCON nchini Ivory Coast. Kwa ushindi huo sasa Angola watacheza na mshindi wa mechi ya baadaye kati ya Nigeria na Cameroon Hata hivyo kipa wa Angola Neblu alionueshwa kadi nyekundu wakati Luneni Haukongo naye alionyeshwa kadi nyekundu

DITRAM NCHIMBI AIBUKIA LIGI KUU RWANDA

Picha
Nyota wa zamani wa Polisi Tanzania, Young Africans na Taifa Stars Ditram Nchimbi 'Duma' amejiunga na Klabu ya Etincelles FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Rwanda kwa mkataba wa nusu msimu hadi June 2024. Mshambuliaji huyo anajiunga na Etincelles Club kama mchezaji huru baada ya kusitishwa kwa mkataba wake na FGA Talents FC ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, Nchimbi amewahi kutamba pia na Vilabu vya Majimaji FC, Mbeya City, Njombe Mji na Polisi Tanzania. Ditram Nchimbi

YANGA YAWEWESEKA KWA KILANGALANGA

Picha
Mabosi wa Yanga wametua kwa straika wa timu ya Bisha FC ya Saudi Arabia, Glody Kilangalanga ambaye alijiunga na klabu hiyo msimu huu inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini humo ambaye wanaamini atawafaa. . Kilangala (23) ana mkataba na timu hiyo ambayo alitua akitokea CS Chebba ya Tunisia, ambapo Yanga inataka kufanya biashara moja kati ya mbili, ama kuuziwa au kupewa kwa mkopo.

SIMBA KUWAACHA BALEKE NI PHIRI NI KUJIMALIZS AU KUJIJENGA UPYA?

Picha
Na Prince Hoza KLABU ya Simba SC maarufu Wekundu wa Msimbazi imewaacha washambuliaji wake hatari Moses Phiri raia wa Zambia na Jean Baleke raia wa DR Congo, Simba imeamua kuwaacha washambuliaji hao baada ya kutoridhishwa na viwango vyao. Mbali na kuwaacha washambuliaji hao, pia imewaacha na wachezaji wengine wazawa, klabu hiyo imeamua kufanya mabadiliko kwa kuwasajili wachezaji wapya wakiwemo washambuliaji na wa maeneo mengine. Baada ya kutangaza kuwaacha washambuliaji hao, zimetoka lawama kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake na wadau wa soka wakishangaa kuwaacha Baleke na Phiri ingawa takwimu ziliwabeba.  Nikianza kwa Phiri, takwimu zilimbeba mshambuliaji huyo aliyejiunga na Simba msimu uliopita akitokea Zanaco ya Zambia. Mshambuliaji huyo alifanikiwa kufunga mabao 10 kwenye Ligi Kuu bara akiongoza kwa mabao kwenye timu yake na pia akishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu bara akiwa nyuma ya Fiston Mayele aliyekuwa anaichezea Yanga SC.  Hata hivyo Phiri aliumia katika ligi ik

CISSE KOCHA BORA HATUA YA MAKUNDI AFCON

Picha
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Senegal Aliou Cissé amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa hatua ya makundi katika michuano ya AFCON 2023. Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Senegal Lamine Camara amechaguliwa kuwa Mchezaji bora Chipukizi wa Michuano ya AFCON 2023 hatua ya makundi. Na Golikipa wa Timu ya Taifa ya Equatorial Guinea Jesús Owono amechaguliwa kuwa Golikipa Bora wa Michuano ya AFCON 2023 hatua ya makundi.

MUSONDA KUREJEA YANGA NA MOTO WA AFCON

Picha
Mshambuliaji wa Yanga Kennedy Musonda alikuwa na wakati mzuri kwenye michuano ya Afcon 2023 akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia Musonda alipata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kocha Avram Grant akianzishwa katika mchezo wa mwisho dhidi ya Morocco, mchezo uliohitimisha ushiriki wa Zambia baada ya kipigo cha bao 1-0 Ni wazi michuano hiyo imemuongezea Musonda ari, morali na kujiamini. Pengine Wananchi watarajie kuona analeta kasi hiyo katika ligi kuu ya NBC Yanga imeongeza ushindani eneo la ushambuliaji baada ya kumsajili Joseph Guedo katika dirisha dogo

MASAU BWIRE ADAI STARS INA USIMBA NA UYANGA

Picha
Na Shafih Matuwa MSEMAJI wa timu ya JKT Tanzania, Masau Bwire amedai tatizo la timu ya taifa, Taifa Stars ambalo linaitafuna siku hadi siku ni kuwa na Usimba na Uyanga kila ambapo inateuliwa kushiriki mashindano.  Bwire ameyasema jana mara baada ya timu ya taifa, Taifa Stars kuondoshwa kwenye michuano ya mataifa Afrika, AFCON inayoendelea nchini Ivory Coast.  Msemaji huyo aliyepata umaarufu akiwa na Ruvu Shooting iliyoshuka daraja, amesema timu hiyo imejaa Usimba na Uyanga na kama tabia ikiendelea itakuwa ngumu kukubalika na watu wengine wasiozipenda timu hizo

WAZIRI WA MICHEZO IVORY COAST ADAI PACOME HAWAMJUI

Picha
Waziri wa michezo nchini Ivory Coast amesema hajui kama mchezaji Pacome Zouzoua anakiwasha kwa kiwango cha kuogopesha kwenye ligi ya Tanzania. Ndio maana hajashangaa kutomuona kwenye timu ya taifa. Hayo ameyasema alipozungumza na waziri Dr. Damas Ndumbaro alipomuuliza (kwa utani)- Kwanini nyota huyo wa @yangasc hajajumuishwa kwenye kikosi cha taifa?

GADIEL MICHAEL ATAMBULISHWA CAPE TOWN SPURS

Picha
Nyota wa Zamani wa Klabu ya Azam FC , Yanga , Simba na Singida Big Stars amejiunga rasmi na Kikosi cha Cape Town Spurs inayoshiriki ligi Kuu ya South Africa. Gadiel anaungana na Kocha wake wa Zamani wa Singida Fontaine Gate Ernst Meddendorp pale

BENCHIKHA ATAJWA KUMRITHI KOCHA WA ALGERIA

Picha
Kocha wa Simba SC Abdelhak Benchikha ni moja ya makocha wanaopewa nafasi ya kwenda kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Algeria. Kocha huyo raia wa Algeria anapewa nafasi hiyo baada ya Tetesi zinazoeleza kuwa Kocha Mkuu wa Algeria Djamal Belmad anataka kujiweka kando na timu hiyo. Benchikha anatajwa kutokana na mafanikio aliyoyapata akiwa na USM Alger mwaka jana Kwa kutwaa Kombe la Shirikisho na CAF Super Cup.

IVORY COAST YAMUOMBA KOCHA WA WANAWAKE UFARANSA AWAFUNDISHE KWA MUDA AFCON

Picha
Imeripotiwa kuwa Shirikisho la soka nchini Ivory Coast limewasilisha ombi kwa Shirikisho la soka nchini Ufaransa la kutaka kumuazima kwa mkopo kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Ufaransa, Hervé Renard (55) kwa ajili ya kuja kuifundisha timu ya taifa ya Ivory Coast kwa muda hadi pale michuano ya AFCON itakapomalizika. Hervé Renard amewahi kuiongoza Ivory Coast kwenye michuano ya AFCON mwaka 2015 na kufanikiwa kutwaa kombe hilo, kwa Sasa Herve Renard ni Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake wa Ufaransa, ikumbukwe Kocha huyo ameshawahi kutwaa mataji mawili ya AFCON akiwa na Zambia Chipolopolo

YANGA KUJIPIMA NA JKU

Picha
Na Tom Cruz Kikosi cha Yanga siku ya Jumamosi kinatarajiwa kucheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya JKU ya Zanzibar katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kwa ajili ya michuano ya Afcon 2023 inayoendelea huko lvory Coast Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi aliwaagiza viongozi wa Yanga kuhakikisha wanapata angalau mechi mbili kila wiki ili kuhakikisha kikosi chake kinaendelea kubaki katika hali ya ushindani Uongozi wa Yanga pia unatafuta timu nyingine kutoka nje ambayo itatoa upinzani unaoendana na mechi ambazo Yanga itakwenda kucheza pale michuano ya Afcon 2023 itakapomalizika Gamondi amesema ni muhimu kwa vijana wake kupata mechi za kujipima nguvu ili kuona wamefanikiwa kwa kiasi gani katika maandalizi wanayoendelea nayo Yanga kujipima na JKU "Tumerejea mapema kwenye mazoezi kuweza kujijpanga kwa muda huu ambao upo kwa sasa, unajua tuna wachezaji wapya ambao wamesajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo la usajili, tupo nao kwenye mazoezi hivyo ni vizuri kupata michezo ya kiraf

BABACAR SARR ATABIRIWA MAKUBWA SIMBA

Picha
Kocha wa viungo wa timu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, Junior Robertinho ambaye ni mtoto wa aliyekuwa kocha wa Simba, Robertinho Oliviera amesema kiungo mpya wa Msimbazi, Babacar Sarr ni mtu wa kazi Sarr aliyesajiliwa msimu huu kutoka US Monastir tayari amecheza mechi mbili, kwani aliposajiliwa tu alikuta timu ikiwania ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Zanzibar. Japokuwa Wekundu hao hawakutwaa kombe hilo mbele ya mabingwa watetezi Mlandege, Sarr ni miongoni mwa wachezaji walioingia kipindi cha pili walipocheza dhidi ya Singida Fountain Gate, na fainali kocha alimpanga kikosi cha kwanza ingawa inaonekana bado kuna mashabiki hawajamuelewa Junior amesema amewahi kumuona kiungo huyo kwa muda wa dakika 90 walipocheza na US Monastir na alikuwa mchezaji hatari. Alieleza kuwa, hakuna mchezaji ambaye hana matokeo kwenye timu halafu akachezeshwa mechi nzima na hiyo tu inaonyesha ni aina gani ya mchezaji Simba wamempata. "Niliwasikia makocha wake wakisema ni mchezaji mwenye nidhamu ya ukabaji na t

CAF YAKOSOLEWA KISA KISWAHILI

Picha
Mtandao wa African Football Greats imetoa taarifa kuwa CAF imekosolewa baada ya kumzuia kocha na nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta, kutumia lugha ya Kiswahili kwenye mikutano ya waandishi wa habari, wameagiza kuwa lugha zinazotakiwa kutumika ni Kifaransa, Kingereza, Kireno na Kiarabu. Mbwana Samatta

JOSEPH GUEDE KUTUA WIKI HII

Picha
Wiki hii mshambuliaji mpya wa Yanga Joseph Guede anatarajiwa kutua nchini kuungana na wenzake ambao wanaendelea na mazoezi Avic Town kujiandaa na mechi za Ligi Kuu, kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Baada ya kukamilisha usajili wake, Guede alipewa ruhusa maalum ili akamilishe masuala binafsi kabla ya kutua nchini kuanza majukumu mapya na mabingwa hao wa nchi Yanga inarejea mazoezini leo baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki ambapo wiki hii vijana wa Kocha Miguel Gamondi wanatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki Katika moja ya mahojiano yake, Gamondi alisema amemuagiza Guede akatishe mapumziko na kutua nchini haraka ili aanze mazoezi na wenzake Gamondi alisema Guede anatakiwa kuja kufanya maandalizi haraka na wenzake ambayo yatamrahisishia kuwa na mwanzo mzuri ndani ya timu hiyo wakati wa mashindano utakaporejea "Tunaendelea na mazoezi yetu, wikiendi tulipumzika kidogo kazi zaidi itaendelea Jumatatu ni muhimu kuwa tayari mapema nafurahia jinsi wachezaji wanavyojituma licha ya ug

GIFT FRED APEWA NAFASI NYINGINE NA GAMONDI

Picha
Mlinzi wa kati wa Yanga Gift Fred raia wa Uganda amepewa nafasi nyingine ya kupigarnia nafasi yake katika kikosi cha kwanza Gift aliyetua Yanga katika dirisha kubwa la usajili lililopita akitokea SC Villa ya Uganda, alimanusra apewe mkono Wa kwaheri katika usajili wa dirisha dogo Hata hivyo kiwango alichoonyesha katika michuano ya kombe la Mapinduzi kikabadili upepo kwani Kocha Miguel Gamondi akapendekeza Mganda huyo aendelee kusalia katika kikosi chake Ni wazi bado atakuwa na kazi ya kupigania nafasi yake mbele ya nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Dickson Job Wakati yeye akiendelea na mazoezi Avic Town, wenzake wako kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars' wakishiriki michuano ya Afcon 2023. Hatma ya Tanzania kuendelea kubaki lvory Coast au kurejea nchini itaamuliwa Leo kwenye mchezo wa tatu hatua ya makundi dhidi ya DR Congo Tanzania inahitaji kushinda mchezo huo ili kukata tiketi ya hatua ya mtoano Gift Fred

RIYAD MAHREZ ATUNDIKA DARUGA ALGERIA

Picha
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Algeria Riyad Mahrez mwenye umri wa Miaka (32) Ametangaza rasmi Kustaafu kuitumikia timu yake ya Taifa ya Algeria baada ya kuondolewa kunako michuano ya AFCON 2023 huko Nchini Ivory Coast hatua ya makundi. Mahrez Alianza Kuitumikia timu ya Taifa ya Algeria mwaka 2014 na mpaka anastaafu Kuitumikia Timu hiyo ya Taifa Baada ya Kuhudumu miaka (10) amecheza mechi (93) na Kufunga Magoli (31) na Kafanikiwa kushinda ubingwa AFCON Mwaka 2019 nchini Egypt.

NOVATUS DISMAS NDANI, STARS IKIIVAA DR CONGO

Picha
Kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars” kitakachoanza katika mchezo wa AFCON Kundi F dhidi ya DR Congo kwenye uwanja wa Amadou Gon Coulibaly, Ivory Coast. Katika kikosi hicho kiungo mkabaji Novatus Dismas anayecheza Ukraine katika klabu ya Shakhtar Donesk ambaye alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Zambia, ataanza leo dhidi ya DR Congo na kwa vyovyote matumaini ya ushindi kwa Tanzania ni makubwa

MJUE Z ANTON; HIT MAKER WA BINTI KIZIWI

Picha
Ally Mohamed Ahmad, almaarufu Z. Anto, alizaliwa jijini Dar es Salaam mwaka 1988. Mwaka 2004 aliwasiliana na Tiptop Connection, watayarishaji wa wasanii wapya wa bongo flava nchini, ili kumpa nafasi ya kurekodi. Walimtaka afanye freestyle hapohapo lakini alishindwa majaribio. Baada ya muda alirejea akiwa amekaa nyumbani akitunga wimbo wa Mpenzi Jini. Wimbo huo ulirekodiwa na kuwa wimbo wa papo hapo nchini kote. Wakati huo aliweza kurekodi albamu nzima, yenye nyimbo nane zikiwemo 'Binti Kiziwi', 'Mapenzi Spesho', 'Diskovumbi', 'Imani Sina', 'Chakula Changu' na 'Chake Time'. Albamu hii inaendelea kuuzwa vizuri kote nchini Tanzania na Kenya, hasa ukanda wa pwani ambapo mtindo wa wapenzi wa bongo flava unaonekana kuvuma sana miongoni mwa mashabiki wa vijana wa kike na wa kiume. Z Anto amelazimika kufanya kazi kwa bidii katika muziki, akiwa anatoka katika familia maskini ambayo inampasa kuitunza, hasa tangu baba yake alipofariki. Anamshukuru M

TSHABALALA USO KWA USO NA SIPHIWE TSHABALALA

Picha
Mohamed Hussein 'Tshabalala' kutoka Tanzania na Siphiwe Tshabalala kutoka Afrika kusini wamekutana huko Nchini Ivory Coast  ambako inafanyika Michuano ya #TotalEnergiesAFCON2023 Siphiwe Tshabalala ndiye mmiliki halisi wa jina la Tshabalala huku Mohamed Hussein akitumia jina la Tshabalala kama jina lake la Utani.

IHEFU YAPORA NYOTA WAPYA WA SINGIDA FOUNTAIN GATE

Picha
Katika hali ya kushangaza, mabadiliko ya umiliki katika lango la Singida Fountain yakitokea huku pesa za Waarabu zikibadilisha kila kitu. Beki wa kushoto wa Zebras Benson Mangolo amesajiliwa Ihefu SC, si Singida! Ihefu ni klabu inayomilikiwa na Waarabu nchini Tanzania Ligi Kuu. Baadhi ya wakurugenzi wa Singida nao wakihamia Ihefu FC. Ihefu itaweka kambi mpya Arusha. Ihefu imesajili wachezaji 9 ghali kutoka Singida. Mkurugenzi Mtendaji wa Singida, Sikwane aliteuliwa kuwania nafasi ya juu katika Ihefu SC. Mshambulizi wa Gaborone United, Thatayaone Kgamanyane amehamia Ihefu Sc mwezi Juni.

MATAIFA YALIYOFUZU HATUA YA 16 AFCON

Picha
Mataifa yaliyofuzu hatua ya 16 BORA ya AFCON mpaka sasa. 🇦🇴 Angola 🇧🇫 Burkina Faso 🇨🇻 Cape Verde 🇪🇬 Egypt 🇬🇶 Equatorial Guinea 🇬🇳 Guinea 🇲🇱 Mali 🇲🇦 Morocco 🇳🇬 Nigeria 🇸🇳 Senegal

MANENO YA SAMUEL ETO' O YAWE FUNZO KWA TANZANIA

Picha
"Kitu nachokiona, tulifanya makosa kuwakabidhi bendera watu waliozaliwa nje ya Cameroon. Uzalendo kwa taifa upo mbali na hisia za mioyo yao. Hawana DNA na udongo wa Cameroon. Lakini baada ya Afcon kila kitu kitabadilika". "Tutahakikisha tunafanya kipimo cha uzalendo kwa kila kijana kabla ya kumvalisha jezi ya nchi yetu." - Samuel Eto'o, Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Nchini Cameroon . Chukua hiyo kauli ya Eto'o ilete kwa kikosi cha Taifa stars cha kocha Adel kisha ilete kwenye kikosi cha Stars cha kocha Morocco

KAIZER CHIEF YAFUFUA MATUMAINI YA KUMNASA TSHABALALA

Picha
Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imefufua matumaini ya kumsajili mlinzi wa kushoto wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala'. Wababe hao wa Afrika Kusini wanajiandaa kutuma ofa kwenda Simba SC kwa ajili ya mlinzi huyo.

IVORY COAST YATOLEWA KWA AIBU AFCON, YAWEKA REKODI TANGU 1984

Picha
Baada ya kuondolewa hii leo kwenye Michuano ya AFCON 2023,Ivory Coast anaweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza mwenyeji kupoteza michezo miwili ya hatua ya makundi ya #TotalEnergiesAFCON tangu mwaka 1984. Ivory Coast leo imepokea kichapo cha mabao 4-0 toka kwa Guinea Ikweta katika mchezo wa mwisho huku ikiwa mwenyeji. Timu ya mwisho kufanya hivyo pia ilikuwa ni Timu ya Taifa ya Ivory Coast