CHEGE ASHANGAA MUZIKI KUHAMIA ISTRAGRAM

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyepata kutamba na kundi la TMK Wanaume Family lililokuwa na maskani yake Temeke jijini Dar es Salaam, Said Chege Chigunda "Chege" ameshangazwa na muziki wa sasa kuhamia Istragram badala ya steji.

Akizungumza jana na kituo cha Efm cha jijini Dar es Salaam amesema wasanii wanaotamba sasa wameshindwa kuusimamisha muziki huo na badala yake wamekuwa wakishindana katika mitandao badala ya stejini, Chege ameshangazwa mno kuona wasanii hao kujitamba wana viewers wengi mitandaoni.

Akielezea upande wake kimuziki Chege amedai bado yuko vizuri na amewataka wale wasanii wanaojiona wana majina makubwa kwa sasa kushindana naye, amesema yuko tayari kuchuana nao na atawashinda, kulingana na maneno yake ya mafumbo ni kama amemlenga Diamond Platinum ambaye hivi karibuni alitangazwa kuongoza Istragram kwa viewers wengi kuliko msanii yeyote yule katika ukanda huu wa Afrika mashariki

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA