AZAM FC KUELEKEA UGANDA LEO
Na Ramadhan Pilen.
Klabu ya Azam FC yenye maskani yake Chamazi Jijini Dar es Salaam inatarajia kuondoka leo kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya kwenda kuweka Kambi ya wiki mbili ili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara .
Kikosi hiko ambacho kitasafiri leo kitaondoka pasipo mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa toka klabu ya Yanga SC Mzimbabwe , Donald Ngoma kutokana na mchezaji huyo kuuguza majeraha .
Ikiwa nchini Uganda klabu ya Azam FC itacheza mechi za kirafiki na vilabu vya Vipers SC , KCCA, na Express FC .