Mwigulu aipa Yanga beki Mzimbabwe
Na Aisha Maliyaga. Dar es Salaam
Beki wa kimataifa kutoka Zimbabwe Erisha Muroiwa anayekipiga timu ya Singida United sasa ataitumikia Yanga SC kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa kama msaada uliotolewa na Dr Mwigulu Nchemba kwa klabu hiyo.
Huo ni msaada wa pili anautoa Mwigulu kwa klabu ya Yanga ambayo kwa sasa ipo katika mdororo wa kiuchumi, jana Mwigulu aliwapa Yanga kiungo waliyemsajili kutoka JKU, Feisal Salum "Fei Toto".
Hata hivyo Mwigulu aliwasilisha barua kwa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF ikiwataka kuthibitisha usajili wa Muroiwa kwa klabu ya Yanga, Mwigulu ambaye ni mbunge wa Iramba Magharibi amedai mchezaji huyo ataenda Yanga lakini fedha za usajili ililipa Singida United hivyo huo ni msaada wake na amedai timu yoyote itakayotaka msaada hatosita kuwapa