NIYONZIMA AWAZIMIA SIMU VIONGOZI WA SIMBA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kiungo wa kimataifa wa Kinyarwanda Haruna Niyonzima "Fabregas" ameamua kuikacha ziara ya Uturuki na kuzima simu yake ama kutopokea simu pindi anapopigiwa na viongozi wa klabu yake ya Simba.
Niyonzima kwa sasa amerejea nyumbani kwao Rwanda na iliripotiwa angesafiri juzi na wenzake wanne ambao ni Meddie Kagere naye Mnyarwanda, Hassan Dilunga, Said Ndemla na Erasto Nyoni kuelekea kwenye kambi ya klabu hiyo iliyopo jijini Istambul, Uturuki lakini hakuweza kuungana nao.
Mpaka sasa Niyonzima hajazungumza lolote juu ya kurejea kwake Simba kwani mwanzo alipozungumza na viongozi akawaambia pasipoti yake imeisha muda hivyo aliwaahidi angekuja mapema ili kushughurikia hilo na kuanza safari, lakini alipopigiwa tena simu hakupokea na pia kuna wakati akipigiwa anakata simu ama kuizima kabisa.
Niyonzima alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea kwa mahasimu wao Yanga SC na tangu alipojiunga na kikosi hicho cha Msimbazi ameweza kufunga mabao mawili tu yote kwa penalti dhidi ya Majimaji FC ya Songea