Biashara United hawatanii aisee, yatambulisha majembe
Na Paskal Beatus. Mwanza
Klabu ya Biashara United ya Mara jana imewatangaza wachezaji wanne ambao imewasajili kutoka vilabu tofauti ili kuendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara .
Wachezaji hao ni Lambele Jerome kutoka Lipuli, Yohana Moris aliyekuwa Mbeya City, Frank Sekule kutoka Dodoma FC na Daniel Manyenye kutoka Toto Africans.
Biashara United imepanda Ligi Kuu bara kwa mara ya kwanza na itashiriki msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 22 tayari imeshakamilisha ujio wa kocha mpya wa kigeni na kusajili baadhi ya wachezaji pia wa kigeni ikijiandaa kutoa ushindani kwenye ligi hiyo