Hatimaye Clement Sanga ajiuzuru
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Makamu mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam Clement Sanga ametangaza kujiuzuru nafasi yake leo huku akitaja sababu kubwa iliyochangia ni kuhofia maisha yake.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Protea Courtyard mjini Dar es Salaam, Sanga amesema ameamua kujiuzuru nafasi yake kufuatia baadhi ya wanachama na wapenzi wa Yanga kutishia maisha yake pamoja na familia yake.
Sanga amedai amepata clip zinazoonesha maandalizi ya watu hao ambao ni wapenzi wa Yanga wamejipanga kuvamia nyumbani kwake na kuwazuru kwa kutumia mapanga,visu nk, hivyo ameona bora ajiweke kando na kuwapisha wengine, Yanga imekuwa na mwenendo mbaya tangia iwe chini yake kaimu mwenyekiti hasa baada ya kujiuzuru mwenyekiti Yusuph Manji.
Timu imetokea kuwaudhi mashabiki wake baada ya kufungwa mfululizo na kuvuliwa ubingwa wake wa bara pia ikichapwa mabao 4-0 na Gormahia katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika