Baada ya kipigo toka kwa Gormahia, kocha Yanga aishushia lawama TFF
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kocha msaidizi wa klabu ya soka ya Yanga SC, Mzambia Noel Mwandila amelishushia lawama Shirikisho la soka nchini TFF kwa kitendo cha kuwachukua wachezaji wao jana na kukaa nao kwa zaidi ya masaa 10 wakati wakifahamu walikuwa na mchezo mgumu dhidi ya Gor Mahia siku inayofuata.
Kwa mujibu wa Mwandila, TFF iliwatoa kwenye kambi ya Yanga nyota sita wa timu ya taifa kwa ajili ya kwenda kupiga picha saa 8 mchana ambapo amesema walirejea kambini saa 7 usiku.
Mwandila alikuwa akielezea umuhimu wa TFF kutoa ushirikiano kwa timu hasa zinapoliwakilisha taifa huku akisema kuwa tukio hilo linaweza kuwa limewaathiri kwavile wachezaji hawakupata muda wa kupumzika.
Yanga imepoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 3-2.