Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2023

Gyan: soka limenipa kila kitu maishani

Picha
Gwiji wa soka nchini Ghana Asamoah Gyan amesema utajiri alionao asilimia kubwa umetokana na mchezo wa soka. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 anajulikana kuwa mmoja wa wachezaji wachache matajiri zaidi nchini humo, ambapo anamiliki Biashara kadhaa ambazo zimetia ajira nyingi kwa waghana wengi. Akizungumza na Premier League Productions, mshambuliaji huyo alikiri kwamba soka ilimpa kila alichotaka maishani. "Nikiangalia maisha yangu ya Nyuma ya soka na yale ambayo nimeweza kufikia, namshukuru Mungu kwa sababu nilifanikisha kila kitu kupitia soka," alisema Gyan alikuwa mshiriki wa kikosi cha Black Stars kilichocheza Kombe la Dunia la 2006, 2010 na 2014 nchini Ujerumani, Afrika Kusini na Brazil mtawalia. Anasalia kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ghana akiwa na magoli 51. Gyan alichezea vilabu kama Stade Rennes, Udinese Calcio, Sunderland...

BARCELONA KUMRUDISHA MESSI

Picha
Klabu ya Barcelona kupitia kwa Makamu wake wa Rais, Rafael Yuste amekiri kuwa wapo katika mipango ya kumrejesha mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi kwenye klabu hiyo kutokea PSG. Yuste amesema wao (Barcelona) wamekuwa na mawasiliano ya karibu na wawakilishi wa Lionel Messi na kwamba hata yeye (Messi) anafahamu kwa jinsi gani Barcelona wanampenda na wangependa arudi. Unadhani itawezekana tena kwa Messi kurejea Barcelona?

Beki la Yanga latoa tamko

Picha
Beki wa kati wa Kimataifa wa Yanga Mamadou Doumbia amesema kuwa licha ya kushindwa kupata nafasi ya kucheza lakini atapambana ili apate nafasi hiyo kama ilivyo kwa mabeki wengine. Doumbia amesema kuwa "wakati mwingine Soka ni katili sana nimecheza michuano mikubwa na yenye ushindani wa hali ya juu lakini nimekuja huku sichezi. "Hilo haliwezi kuondoa malengo yangu,najua kwenye soka changamoto ni kawaida na inahitaji moyo wa ujasiri na kutokukata tamaa kwani kila jambo linawakati wake. "Ninachojua mimi ni beki mzuri ukifika wakati wangu nitacheza na watu wataniona," alisema beki huyo

Yanga wakijifua Stade TP Mazembe Stadium leo

Picha
Kikosi Cha Yanga kimefanya mazoezi yake ya kwanza nchini DR Congo kwenye uwanja wa Stade TP Mazembe ikiwa ni maandalizi ya mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe

Kagera Sugar kuigomea Yanga

Picha
"Kikubwa sisi tunajiandaa ili tuweze kupata alama tatu, tarehe 11 tunacheza na Yanga, tunajua tunacheza na timu ya aina gani, timu ambayo inaongoza ligi, timu ambayo inatetea ubingwa kwahiyo tunajua tunaenda kukutana na ugumu kiasi gani" Kocha Mexime-Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mchezo wa kwanza msimu huu uliochezwa katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, Kagera sugar alipoteza alama tatu kwa kufungwa na Yanga 1-0.

Simba kulipiza kisasi kwa Raja au kushindiliwa magoli?

Picha
Na Prince Hoza WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC usiku mnene itashuka dimbani saa 7:00 ya tarehe 1-4.2023 itarudiana na Raja Casablanca mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Afrika. Simba ikiwa ugenini itakuwa na kazi ngumu kulipiza kisasi cha kufungwa mabao 3-0 nyumbani katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Hivyo katika mchezo huo Simba inatakiwa kushinda ili kulipa kisasi, lakini vile vile inaweza kufungwa zaidi ya magoli 3 kwani itacheza mbele ya mashabiki wake. Simba ina kumbukumbu nzuri hivi karibuni iliifunga timu ya Horoya ya Guinnea mabao 7-0 ushindi ambao umeshitua Afrika nzima kwani imepata tiketi ya kuingia robo fainali

Yanga waelekea Lubumbashi

Picha
Msafara wa kikosi cha Young Africans Sports Club waondoka kwenda nchini DR Congo kuifuata TP Mazembe kwenye Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) hapo Jumapili ya Aprili 2, 2023

Mkata umeme wa Lupopo kutua Simba

Picha
Tayari mabosi wa klabu ya Simba wamepiga hodi katika klabu ya FC Lupopo ya DR Congo kumuulizia mkata umeme mmoja anayekipiga timu hiyo fundi wa mpira, Harvy Ossete ambaye juzi kacheza dakika 90 wakati chama lake la Congo likiibuka na ushindi katika mechi za kufuzu AFCON. . Ossete ambaye ni raia wa Congo , anatajwa kuwa kati ya viungo wanaotazamwa kwa sifa ambazo Robertinho anazihitaji kikosini, akiwa na uwezo wa kukaba, anachezesha timu na anaweza kucheza kama beki wa kati akihitajika japo si eneo lake halisi.

Simba safarini Morocco

Picha
Baada ya jana kushindwa kusafiri kutokana na ndege iliyopangwa kusafiria kupata hitilafu,hii leo asubuhi kikosi cha Simba kimeanza safari ya kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kucheza mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Raja Casablanca ambao utapigwa Jumamosi ya April 1,2023 kuanzia saa saba kamili usiku kwa majira ya Tanzania. Simba wanatarajia kufika hii leo nchini Morocco lakini watapita Qatari kabla ya kuunganisha safari hadi Morocco wachezaji waliokwenye Mataifa yao wanatarajia kutokea kwenye mataifa yao hadi Morocco
Picha
SIMBA WAIANZA SAFARI YA MOROCCO 🚀 Baada ya jana kushindwa kusafiri kutokana na ndege iliyopangwa kusafiria kupata hitilafu,hii leo asubuhi kikosi cha Simba kimeanza safari ya kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kucheza mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Raja Casablanca ambao utapigwa Jumamosi ya April 1,2023 kuanzia saa saba kamili usiku kwa majira ya Tanzania. Simba wanatarajia kufika hii leo nchini Morocco lakini watapita Qatari kabla ya kuunganisha safari hadi Morocco wachezaji waliokwenye Mataifa yao wanatarajia kutokea kwenye mataifa yao hadi Morocco 

Makambo kurejea tena Tanzania

Picha
Straika wa zamani wa Yanga, Heritier Makambo amesema amejipa muda wa kujifua bila ya kuwa na timu kabla ya msimu ujao hajarejea nchini kuja kukiwasha. Klabu za Singida Big Stars na Namungo zilizopo Ligi Kuu zinatajwa kuanza mazungumzo naye

Morrison, Ambundo waachwa Yanga

Picha
Winga mtukutu, Bernard Morrison ameachwa katika kikosi cha wachezaji wa Yanga waliondoka leo Alhamisi kuelekea Congo kwa mechi ya marudiano dhidi ya TP Mazembe itakayochezwa Jumapili saa 10:00 jioni. . Taarifa kutoka Yanga inasema kuwa, Bernard Morrisoni, Dickson Ambundo na Mshery hawatasafiri na timu.

Mshery aanza tizi

Picha
Golikipa wa Klabu ya Yanga,Aboutwalib Mshery ameanza mazoezi mepesi baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimkabili ambayo yalimlazimu kufanyiwa upasuaji wa goti. Mshery alitabiriwa kukaa nje ya Uwanja kwa zaidi ya Miezi sita na hali inavyoonekana anaweza kupona na kuwa fit kabla ya muda uliotarajiwa na madaktari.

Diarra na Aucho kuikosa TP Mazembe

Picha
Klabu ya Yanga SC imethibitisha itawakosa kiungo, Khalid Aucho na kipa Djigui Diarra katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi D dhidi ya TP Mazembe Katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Aucho na Diarra watakosekana katika mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano walizopata katika michezo iliyopita.

Rais Samia na makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris leo

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimuonesha Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris nakshi za michoro ya milango ya Zanzibar pamoja na madirisha yake katika ukumbi wa Kikwete mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  akimuonesha Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris nakshi za michoro ya milango ya Zanzibar pamoja na madirisha yake katika ukumbi wa Kikwete mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Cristiano Ronaldo na mkoko wake wa Bil 20

Picha
Cristiano Ronaldo hapo jana alionekana kwenye jiji la Madrid nchini Uhispania akiendesha gari lake aina ya Bugatti Centodieci. Unaambiwa kuna magari 10 tu ya aina hiyo ulimwenguni. ni wazi yake ilikuwa namba 7. Bei ya gari ni Euro milioni nane ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 20 za Kitanzania

Yanga yazindua tawi DR Congo

Picha
Historia Inaandikwa Kwa Wananchi: Klabu ya Yanga inaenda kuwa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kufungua matawi ya klabu hiyo Nchini Dr Congo, Wanachama wapya wa klabu hiyo Nchini DR. Congo wameiomba klabu hiyo ikazindue matawi hayo matatu watakapoenda kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Tp Mazembe, Kwa mujibu wa katiba mpya ya Yanga, pamoja na vitu vingine tawi litakidhi vigezo kusajiliwa ikiwa limefikisha Wanachama (100),Hivyo basi, matawi yaliyokidhi vigezo ambayo yatazinduliwa yatakuwa 3, Yanga Sc inakuwa klab ya Kwanza kutoka Afrika Mashariki na kati kuwa na matawi nje ya Nchi yao,Pia inakuwa Miongoni mwa Vilabu Afrika na Duniani vinavyoendeshwa kwa Mfumo wa Wanachama kuwa Matawi nje ya nchi yao, Klabu ya Yanga itaondoka Nchini Tanzania Leo Alhmisi saa 5 Asubuhi Kuelekea DR. Congo kwa kutumia ndege ya ATCL tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa 2 April 2023, Team of Citizens Tunasema Soka la Tanzania limekuwa sasa, Limekuwa Bora Mpaka kuwavutia raia wa Nc

Mo. Tukimtaka Mayele tutambeba

Picha
“Sifuatilii sana mechi za Yanga...Sijamuona Mayele kwenye mechi namsikia, namuona kwenye mitandao naona clip zake anavyofunga magoli nampongeza ni mchezaji mzuri sana na namuombea kila la kheri" “Simba tuko tayari kumpata mchezaji bora popote Afrika kwa hiyo kama Mayele atakuwa ameorodheshwa na mkataba wake yuko tayari kuuvunja na Yanga na kuja Simba basi simba itakuwa tayari,”

Baba yake Manara kumng' oa Feitoto Yanga

Picha
Mzee Sunday Manara amesema, kuna watu kutoka Ulaya wamemtafuta kumtaka Feisal Salum 'Feitoto', na wapo tayari kutoka milioni 300, mshahara wa milioni 24 kwa mwezi na gharama za tiketi ya ndege ili kwenda kucheza soka Ulaya.

Mayele amfunika Chama

Picha
MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Yanga SC Fiston Mayele Hapo Jana kwenye timu yake ya taifa ya DR Congo alicheza kwa dakika 32 akitokea sub akichukua nafasi ya mshambuliaji wa klabu ya Sochaux inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Nchini Ufaransa,Aldo Kalulu. Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya goli 1-1 ambapo DR Congo ilikuwa ugenini kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya AFCON . Henock Inonga wa Simba hakupata bahati ya kucheza mchezo huo licha ya kupangwa kwenye kikosi Cha DR Congo cha hapo jana.

Makala; Yanga imeweka historia Afrika

Picha
NA ABDUL MAKAMBO Call.  0787905328.  TAREHE  19-3-2023 siku ya Jumapili, tarehe na mwaka wa kihistoria kwa klabu ya Dar Young Africans au Yanga iliifunga wawakilishi wa Tunisia us Monastir magoli 2-0 kwenye uwanja wa Mkapa jijini. Kwa hakika Yanga imeleta furaha kubwa kwa wanachama, wapenzi na heshima kubwa kwa taifa la Tanzania. Ni baada ya miaka mingi-Yanga iliingia robo fainali kwa mara ya kwanza na ilikuwa ni michuano ya Klabu bingwa barani Afrika mwaka 1969 kule Addis Ababa kule nchini Ethiopia na Yanga ikatolewa kwa shilingi. 2.Tokea mwaka ule yanga haikufanya tena vizuri na mwaka 1998 yanga ndipo ilipofanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani afrika-ilicheza na apr ya rwanda ikaitoa na ikacheza na coffe ya ethiopia na ikaitoa na yanga ikaingia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani afrika.Na kwenye makundi ilikua kundi moja na raja casablanca ya moroco. Asec Mimosas ya Ivory Coast na Maning Rangers ya Afrika Kusini na Yanga ilikuwa chin

Bilionea kuinunua Man United

Picha
Bilionea kutokea England Sir Jim Radcliffe na Kampuni yake ya kemikali INEOS wametuma tena zabuni nyingine iliyoboreshwa kwa ajili ya kuinunua klabu ya Manchester United. Sheikh Jassim bin Hamad wa Qatar na Sir Jim Radcliffe wote waliwasilisha maombi ya kuhitaji muda zaidi wa kuyapangilia vizuri zaidi maombi yao. Ujumbe kutokea kampuni ya INEOS wiki iliyopita uliitembelea klabu hiyo na kufanya mazungumzo ya saa sita vilevile ulipata wasaa wa kuvitembelea viwanja vya Old Trafford na Carrington. Nao ujumbe kutokea Qatar ulitembelea klabu hiyo na kufanya mazungumzo kwa saa kumi. Wakati huohuo, Manchester United imetupilia mbali zabuni ya Mfanyabiashara wa Finland Thomas Zilliacus aliyekuwa na nia ya kuinunua klabu hiyo na kumiliki asilimia 50 huku akiiacha nusu nyingine imilikiwe na mashabiki. Klabu hiyo inayomilikiwa na familia ya Glazer iko sokoni tangu mwaka jana . Uamuzi huo umekuja baada ya miaka mingi ya malalamiko na kutoridhishwa kwa mashabiki juu ya umiliki wa klabu hiyo.

Kocha Monastir aitabiria Yanga kufika nusu fainali

Picha
Na Shafih Matuwa Kocha wa klabu ya US Monastir amesema Yanga ina mambo (2) mazuri yanayowabeba na wananafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali iwapo watayaongezea nguvu. "Ubora wa kwanza wa Yanga wanaoongoza kundi letu ni uwepo wa kocha Nasreddine Nabi ambaye ameiweka Yanga mahali salama kimbinu na kwamba hata ukiwa mbele unaongoza kwa bao (1) unahitaji ubora kulilinda bao lako kwa kuwa Nabi ni kocha anayebadilika badilika" "Tulipocheza na Yanga tukashinda (2-0) lakini muda wote hatukuwa na utulivu wa kuona kama tumemaliza mechi. Nawaheshimu sana (Yanga) kwa kuwa wanaonesha kuna kazi kubwa kocha wao amefanya.. Hata nilipokuwa nawafuatilia na kuangalia mechi zao sikuona kama kuna mchezo wamezidiwa umiliki wa mpira" "Napenda wanavyocheza, wanakulazimisha, wakati wote wanataka mpira uwe katika miliki yao. Tulipocheza nao kisha kucheza na Tp Mazembe tuliona tofauti kubwa ilitosha kuona kwamba Yanga watakuwa washindani wetu wakubwa katika kundi letu" "Silaha ya

Alikiba alia na mwtumizi makubwa ya kuandaa video

Picha
Staa wa mziki nchini @officialalikiba amesema video zinamaliza pesa nyingi kwa wasanii tofauti na audio ambazo zinaingiza pesa bila shida yoyote. "Ni kweli tunafanya video lakini ukweli video inachukua pesa nyingi sana kwa wasanii na wanasubiri pesa zirudi. Unajua mziki ni biashara maono yangu nimejaribu kufanya mwaka huu 'Lyrics Video' ili waone reaction yangu nilivyoimba na kudeliver mziki wangu kupitia lyrics or dancing video". "Wasanii wamekuwa wakipoteza pesa bila kujijua hiyo tafiti nimeifanya baada ya kutoa ' The Only One King' kuna video ambazo zimeingiza pesa zingine hazikuingiza pesa lakini audio ina penetrate na kuingiza pesa bila shida yoyote".

KILICHOMWONDOA NKOMA YANGA PRINCESS HIKI HAPA

Picha
Na Mwandishi Wetu INASEMEKANA uongozi wa klabu ya Yanga SC umeamua kumfuta kazi kocha wa Yanga Princess, Sebastian Nkoma ni kutokana na tabia yake ya kutoka kimapenzi na baadhi ya wachezaji wake. Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizopatikana zinasema kwamba tabia ya kocha huyo ya kuwataka kimapenzi wachezaji wake imechangia kushindwa kuwanoa vema na kupelekea kushika nafasi ya nne kwenye ligi ya wanawake Serengeti Lite. Uongozi wa Yanga, jana uliamua kumfuta kazi kocha huyo aliyejiunga na Yanga Princess msimu uliopita akichukua nafasi ya Edna Lema, sasa Fred Mbuna atainoa timu hiyo hadi mwisho wa msimu akisaidiwa na Esther Chabruma "Lunyamila"

Uganda yaibutua Tanzania nyumbani

Picha
Na Shafih Matuwa TIMU ya taifa ya Uganda, The Cranes usiku huu imelipa kisasi baada ya kuibutua timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa bao 1-0 lililopatikana dakika za mwishoni katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa kipigo hicho bado Stars inaendelea kukamata nafasi ya pili nyuma ya Algeria inayoongoza kundi lao lenye timu za Tanzania, Uganda, Niger na Algeria. Katika mchezo huo leo, Stars haikuonyesha cheche zake kama ilivyocheza Misri ambapo ilicheza na Uganda na kushinda 1-0. Licha kwamba Watanzania walijitokeza kwa wingi, lakini Uganda ilicheza kandanda safi na kupata ushindi, hata hivyo nahodha wa Stars, Mbwana Samatta alitolewa 

ALI KIBA AMTEMBELEA MAMA YAKE MAGU

Picha
Staa wa muziki hapa Tanzania Alikiba hivi kalibuni ameonekana kwenye picha akiwa na mama mzazi wa hayati Dkt Jonh Pombe Magufuri wakizungumza machache kwa undani zaidi hii Inaonesha bado alama za mzee huyo zipo kwa kila idara hasa katika muziki

NKOMA ABWAGA MANYANGA YANGA PRINCESS

Picha
Klabu ya Yanga imethibitisha kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake, Yanga Pirincess, Sebastian Nkoma kwa makubaliano ya pande zote mbili. Uongozi wa Yanga unamshukuru Kocha Mkoma kwa kazi yake kipindi chote alichokuwa akiifundisha timu yetu ya Wanawake. Kwa sasa benchi la ufundi la Yanga Princess litakuwa chini ya kocha Fredy Mbuna mpaka mwisho wa msimu huu.

SIMBA WAJIFUA VIKALI KABLA YA KUIVAA RAJA

Picha
Kikosi Cha Simba SC kimefanya mazoezi ya Mwisho asubuhi ya Leo kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena kabla ya kuanza safari ya kuelekea Nchini Morocco hapo baadae saa tisa alasiri.