SIMBA YAKUBALI KUZINDUA UWANJA WA MAJALIWA STADIUM

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Mabingwa WA soka Tanzania Bars, Simba SC maarufu kama Wekundu wa Msimbazi, wamekubali ombi la timu ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi kucheza nayo mechi ya kirafiki ikiwa na lengo la kusherehekea uzinduzi wa uwanja wa kisasa wa Majaliwa Stadium Agosti 11 mwaka huu.

Wekundu hao wa Msimbazi wamekubali maombi ya timu hiyo na sasa watashiriki kikamilifu katika uzinduzi wa uwanja huo wa mpira, Ruangwa ndiko anakotokea Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa ambaye pia ni mpenzi mkubwa wa Wekundu hao hivyo itakuwa ni burudani tosha kwa wakazi wa Ruangwa kuitazama klabu bingwa ya soka nchini.

Mheshimiwa Majaliwa ndiye aliyehakikisha uwanja unajengwa na kukamilika ambapo sasa vilabu vya jimbo lake la Ruangwa na maeneo jirani vinaweza kuutumia uwanja huo kujiendeleza, Simba imeahidi kupeleka wachezaji wake wote nyota pamoja na kocha wake mpya Mbelgiji Patrick Winand Aussems, Wekundu hao kesho Jumapili wanaelekea Uturuki kujiandaa na msimu ujao watarejea Agosti 5 kabla hawashuka dimbanj kuadhimisha Simba Day inayonyika Agosti 8

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA