Nyota mwingine Azam FC apata ulaji Afrika Kusini
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Neema imeemdelea kuwaangukia wachezaji wa timu ya soka ya Adam FC ya mjini Dar es Salaam baada ya leo kiungo mshambuliaji wake Yahya Zayed kukwea pipa na kuelekea nchini Afrika Kusini kufanya majaribio katika klabu ya Bidvest Wits inayoshiriki Ligi Kuu maarufu ABSA.
Zayed aliyeisaidia Azam FC kutwaa ubingwa wa kombe la Kagame kwa kuilaza Simba SC mabao 2-1 katika fainali iliyofanyika uwanja WA Taiga mjini Dar es Salaam amesafiri kwa baraka zote na kama atafaulu majaribio ina maana Azam FC itakunja noti kwani tayari ilishamuongezea mkataba WA miaka miwili.
Kuondoka kwa Zayed kunaifanya Azam FC iwe imetoa karibu wachezaji wanne kucheza soka la kulipwa, tayari Farid Musa ametangulia Hispania na kujiunga na CD Tennerife inayoshiriki Sagunda Divion, lakini Humid Mao yeye amejiunga na Petrojet ya Misri na Shaaban Iddi Chilunda akiula kwa kumfuata Farid Musa katika klabu ya Tennerife ya Hispania, kila LA kheri Yahya Zayed