YANGA KULIPA KISASI KWA GORMAHIA LEO?
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga SC usiku wa leo wanatelemka uwanja wa Taiga kuumana na For Mahia ya Kenya mchezo wa kundi C kombe la Shirikisho barani Afrika.
Huo ni mchezo wa nne kwa Yanga na wa pili kwa timu hizo kwani ziliumana hivi karibuni katika uwanja wa Moi Kasarani mjini Nairobi nchini Kenya na Yanga kubamizwa mabao 4-0 lakini iliemda kucheza ikiwa na mgomo wa wachezaji wake wakishinikiza kulipwa stahiki zao.
Hata hivyo uongozi wa Yanga umeonekana kumalizana na wachezaji wake na mambo sasa yanekuwa shwari, kikosi kamili cha Yanga kiliingia kambini kujiandaa na mchezo huo na huenda Leo ikalipa kisasi.
Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga umejinasibu kushinda I'll kufufua matumaini ya kusonga mbele Yanga pekee iko mkiani ikiwa na pointi moja wakati MC Alger ya Algeria ikiwa kileleni na pointi 7 Gor Mahia ya Kenya ina pointi 5 huku Rayon Sports ya Rwanda ikiwa na pointi 2 Kila la kheri Yanga SC