MSUVA AREJEA DAR NA KUSAINI MKATABA KMC
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kiungo mshambuliaji wa Mbao FC ya jijini Mwanza, James Happygod Msuva amejiunga na timu iliyopanda daraja ya KMC yenye maskani take Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Msuva (James) ambaye ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anayeichezea timu ya Difaa El Jadida ya Morocco ameripotiwa kusaini mkataba WA mwaka mmoja.
Msuva anaungana na beki wa kati Yusuph Ndikumana raia wa Burundi ambao wrote hao wamemfuata aliyekuwa kocha wao wa Mbao FC Etienne Ndayiragije aliyejiunga na timu hiyo akichukua mikoba ya mzalendo Fred Felix Minziro ambaye mkataba wake ulimalizika