Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2018

Yanga nao wafuata ndumba Moro

Picha
Na Mwandishi Wetu Homa ya mpambano we watani wa jadi katika soka la Tanzania imepamba moto ambapo tayari vilabu vikongwe vimeshaanza kulikimbia jiji la Dar es Salaam. Simba wao wameenda kujificha Zanzibar kwenye marashi ya karafuu wakati Yanga wameondoka zao kuelekea mji kasoro bahari Morogoro, Yanga na Simba zitaumana siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, katika mchezo uliopita Yanga iliifunga Singida United mabao 2-0

Simba yafuata uchawi Zanzibar

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Simba SC wameelekea Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya mahasimu wao Yanga SC utakaopigwa Jumapili ijayo kwenye uwanja wa Taifa. Simba itamkosa nahodha wake John Bocco "Adebayor" ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu bara dhidi ya Mwadui FC ambao Simba ilishinda mabao 3-1 uwanja wa Kambarage, inasemekana watani zao Yanga wameelekea mjini Morogoro