TARIMBA AZUIA USAJILI WA YONDANI SIMBA, AMBAKIZA JANGWANI

Na Asha Maliyaga. Dar es Salaam

Mwenyekiti wa zamani wa kamati ya mpito wa Yanga Sc, Tarimba Abbas Tarimba jana usiku alikuwa na kikao kizito na beki kisiki Kelvin Patrick Yondani na kuweza kumshawishi abakie katika kikosi cha Yanga.

Yondani alikuwa katika rada nzito za kujiunga na mabingwa wa soka nchini Simba Sc ambao inasemekana walikuwa tayari kumtumbukizia shilingi milioni 80 kwenye akaunti yake ya benki, lakini dakika za lala salama kigogo huyo akaingilia kati ma kuokoa jahazi.

Pia Tarimba aliweza kumtuliza na beki mwingine Hassan Ramadhan Kessy ambaye naye alikuwa katika rada za kutoweka Yanga kwani naye aligoma kama Yondani

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA