KMC YAMNASA HASSAN KABUNDA
Na Mqwandishi Wetu. Dar es Salaam
Uongozi wa timu ya soka ya Manispaa ya Kinondoni ya KMC Leo imemtambulisha kiungo mshambuliaji Hassan Salum Kabunda na kumpa mkataba wa mwaka mmoja.
Kabunda aliyekuwa akiichezea Mwadui FC ya mjini Shinyanga anakuwa miongoni mwa wachezaji wapya wa timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu, Kabunda amejiunga na KMC akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba.
Kabunda aliyevaa kanzu akiwa na viongozi wa timu hiyo ni mtoto wa beki wa zamani wa Yanga SC, Salum Kabunda "Ninja" ama Msudani ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uchezaji wake wa kibabe na rafu nyingi