KISPOTI

Simba ilipaswa kumuamini Masoud Djuma

KLABU ya Simba SC imemtambulisha rasmi beki wa zamani wa kimataifa wa Ubelgiji Patrick Winand J Aussems kuwa kocha mkuu wake mpya akichukua nafasi ya Mfaransa Pierre Lechantre aliyeondoka Mei mwaka huu.

Aussems aliyezaliwa Februali 6 mwaka 1965 mjini Moelingen, Ubelgiji ametambulishwa mchana katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam na Rais wa klabu hiyo Salim Abdallah "Try Again" akitokea timu ya taifa ya Nepal.

Try Again amesema kwamba wana imani na Aussems kwamba atailetea mafanikio klabu yao kutokana na rekodi yake nzuri, kocha huyo ana uzoefu wa kufundisha timu kadhaa barani Asia na Ulaya lakini amewahi kufundisha KSA ya Cameroon na AC Leopards ya Dolisie nchini Kongo, hizo zikiwa pekee za Afrika.

Aussems alikuwa jukwaani uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam wakati wa mchezo wa mwisho wa kundi C Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Kagame kati ya Simba SC na Singida United ulioisha kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kocha huyo aliyecheza soka la ushindani kuanzia mwaka 1974 katika timu ya RCS Vise aliyodumu nayo hadi 1981 alipojiunga na Standard Liege mpaka 1988 alipojiunga na KAA Gent na mwaka 1990 akatua RFC Seraing zote za Ubelgiji.

Aussems alienda kumalizia soka lake kwenye timu ya ES Troyes AC kuanzia mwaka 1990 akadumu nayo hadi mwaka 1993, akaanza ukocha katika timu hiyo hiyo ya Troyes mwaka 1992 lakini akahamia SS Saint Louisienne kuanzia mwaka 1995 hadi 1999 alipojiunga na Capricome Saint Pierre aliyokaa nayo hadi mwaka 2001.

Kocha huyo mpya wa Simb akaenda zake Stade Beaucairois mwaka 2002 hadi mwaka 2003 alipojiunga na Stade de Reims ambayo hii alikaa mwaka mmoja tu hadi 2003 mwishoni, mwaka uliofuatia akaenda kufunza KSA ya Cameroon ambapo alihudumu hadi mwaka 2005 alipojiunga na SCO Angels akakaa hadi mwaka 2006.

Aussems akapata kazi tena katika timu ya Evian Thonon Gaillard FC kuanzia mwaka 2009 hadi 2016 kisha akaenda kuinoa Shenzhen Ruby akakaa hadi 2012 alipotimkia Chengdu Blades akadumu mwaka mmoja kabla ya kwenda kuifundisha AC Leopards ya Kongo nayo akakaa mwaka mmoja hadi 2012 alipoenda nchini Nepal kuifunza timu ya taifa ya nchi hiyo mpaka 2015 na mwaka huu amejiunga na Wekundu wa Msimbazi, Simba SC.

Katika kipindi cha mwaka mmoja Simba imeonekana kubadili makocha watatu tofauti, ilianza kunolewa na Mcameroo, Joseph Marius Omog aliyesaidiwa na Mganda Jackson Mayanja na kuisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa kombe la FA ambalo liliwarejesha tena katika michuano ya kimataifa kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne.

Mcameroon huyo alifutwa kazi baada ya Simba kuondolewa katika michuano hiyo hiyo ya FA baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na vijana wa Green Warriors ya Mwenge mjini Dar es Salaam, timu hizo hazikufungana hadi zinamaliza dakika 90 za mchezo.

Lakini alianza kubwaga manyanga kocha msaidizi Jackson Mayanja ambapo baadaye Simba ikamleta Mrundi, Masoud Djuma Irambona, ujio wa Masoud Djuma ulileta matumaini mapya angalai kwani Simba ilionekana kubadilika na kucheza soka safi, lakini kocha mkuu Mcameroon Joseph Omog alipopewa likizo na kurejea kwao, kikosi cha Simba kilikuwa chini ya Mrundi huyo ambaye aliweza kukinoa vema.

Simba ilionekana kucheza vizuri tofauti na Omog na ikaanza kutia vipigo vikubwa na kupachikwa jina la utani la Simba 4G, na viongozi wa Simba wakaamua kumfurusha Omog aliporejea nchini na kuiongoza katika mchezo dhidi ya Green Warriors, Simba ilizidiwa maarifa na vijana hao wa Jeshi la Wananchi Tanzania na ndipo alipofutwa kazi.

Masoud Djuma akawa kaimu kocha mkuu na akaiongoza vema mpaka pale alipoletwa kocha mkuu Mfaransa, Pierre Lechantre, Mfaransa huyo alikuja na msaidizi wake Mtunisia Aymen Mohamed Hbibi na walianzia jukwaani wakiishuhudia Simba ikiitandika Singida United mabaon4-0 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Kwa hakika Pierre Lechantre alishuhudia soka safi na la kuvutia wakati huo timu ikiwa mikononi mwake Mrundi Masoud Djuma, wengi walidhani Simba itampa moja kwa moja mikobaya kuwa kocha mkuu Mrundi huyo lakini kwa sababu viongozi wa Simba walitolea ufafanuzi hilo na Wanasimba wakaridhika kiroho safi na mambo yakawa poa.

Siku si nyingi Mfaransa huyo licha ya kuipa ubingwa wa Bara baaa ya miaka minne, lakini ushindi wa Simba ulipungua na ukawa wa bao moja ama mbili pia Simba ilikuwa ikicheza kwa kujihami mno yaani kupaki basi badala ya soka lake la kushambulia kama ilivyokuwa kwa Djuma.

Kocha huyo mkuu  huyo alisusa wakati timu ilipoenda kushiriki kombe la Sportpesa Super Cup kule Nakuru nchini Kenya na akaondoka zake kurejea Dar es Salaam, Lechantre aliiacha Simba ikiwa inasaka tiketi ya kucheza nusu fainali, Masoud Djuma alikiongiza kikosi hicho na kukifikisha fainali ambapo kwa bahati mbaya ikalala 2-0 dhidi ya Gormahia.

Na pia akakiongoza tena kikosi cha Simba kufika fainali ya michuano ya Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe a Kagame na Simba kufungwa na Azam FC mabao 2-1 katika mchezo wa fainali, bika shaka Simba imeonekana kucheza vizuri tofauti na Simba ya Lechantre hivyo ilipaswa kabisa kumuamini Masoud Djuma na kumfanya awe kocha mkuu badaa ya kukaimu tu pindi makocha wakuu wenye CV nzuri wanaposhindwa kazi, Djuma namuaminia kabisa na anao uwezo wa kuifikisha mbali klabu hiyo

alamsiki

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA