Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2018

SINGIDA UNITED YAWANG' OA WABABE WA SIMBA USIKU HUU

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Timu ya Singida United imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la FA baada ya kuifunga timu ya Green Warriors mabao 4-3 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penalti baada ya sare tasa 0-0 ndani ya dakika 90. Mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi usiku huu na kuifanya timu hiyo inayonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm kusonga mbele hatua ya 16 bora. Mbali na Singida United kutinga hatua ya 16 bora, timu ya Mtibwa Sugar nayo ilitinga hatua kama hiyo baada ya kuilaza Majimaji Rangers mabao 2-1 uwanja wa Ilulu mjini Lindi huku mabao yote ya washindi yakifungwa na Kevin Sabato "Kiduku". Matokeo mengine kama ifuatavyo Tanzania Prisons 5 Burkina Faso 4 (Penalti) baada ya sare 1-1, Sokoine Mbeya, Majimaji Songea 2 Ruvu Shooting1, Majimaji Stadium, Songea, Njombe Mji 4 Rhino Rangers 1 (Penalti) baada ya sare ya 2-2, Sabasaba Stadium, Njombe. Matokeo mengine ni Stand United

JULIO ACHEKELEA KUIADHIBU MWADUI FC

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kocha wa Dodoma Fc ya mkoani Dodoma, Jamhuri Kihwelu "Julio" amechekelea ushindi wa timu yake dhidi ya Mwadui Fc wa mabao 2-1 jana katika uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. Akizungumza mara baada ya kumalizika mchezo huo, Julio amesema amejisikia furaha kuifunga Mwadui kwani ni timu yake ya zamani ambayo aliwahi kuipandisha Ligi Kuu Bara hivyo anayajua mapungufu ya timu hiyo. Dodoma Fc inayopigania kupanda Ligi Kuu Bara, jana ilifanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA kwa kuilaza Mwadui 2-1, hata hivyo Julio amekisifu kikosi cha Mwadui kuwa kimecheza vizuri na kuipa ushindani Dodoma Fc Jamhuri Kihwelu "Julio" kocha wa Dodoma Fc

NI VITA YA WABABE NA VIBONDE WA SIMBA LEO CHAMAZI

Picha
#Michezo: NI VITA YA WABABE NA VIBONDE WA SIMBA LEO CHAMAZI. Michuano ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu FA Cup leo inaendelea kushika kasi katika viwanja tofauti hapa nchini, mtanange mkali na wa kusisimua utapigwa pale Azam Complex, Chamazi ikizikutanisha Green Warriors ya Mwenge jijini na Singida United ya mkoani Singida. Ugumu wa mchezo huo unakuja pale unapozikutanisha timu mbili ambazo zina rekodi tofauti, Green Warriors hawatasahaulika na wapenzi wa soka baada ya kuiondosha na kuivua ubingwa wa michuano hiyo Simba. Katika mchezo uliowakutanisha na Simba, ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na walipoenda kwenye penalti Green Warriors wakaibuka wababe kwa mikwaju 5-4. Singida United nao wanaingia uwanjani wakiwa vibonde wa Simba baada ya kulazwa mabao 4-0 mchezo wa Ligi Kuu Bara na hapo ndiyo kutatoa mbabe wa kweli hii leo. Mechi nyingine za michuano hiyo itapigwa kama ifuatavyo. Majimaji Rangers vs Mtibwa Sugar Ilulu Lindi, Majimaji Fc vs Ruvu Shoot

BEKI MPACHIKA MABAO APATA ULAJI KENYA

Picha
Na Mwandishi Wetu. Kenya Beki Mtanzania mwenye sifa ya kupachika mabao aliyepata kuchezea Azam Fc, Coastal Union na Majimaji ya Songea, Tumba Lyi Sued amejiunga na timu ya Wazito Fc ya nchini Kenya kwa mkataba wa miaka miwili. Sued ndiye beki aliyeanza kusifika kwa upachikaji magoli, ameamua kujiunga na timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kutimiza ndoto yake ya kucheza soka nje ya Tanzania. Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Majimaji mwanzoni mwa msimu huu baada ya kuachana na Coastal Union ya Tanga, amefurahia kutua Wazitp Fc ya Kenya na kudai ni hatua nzuri aliyoifikia kujiunga na timu hiyo. Tumba Sued ambaye aliibuliwa na kulelewa na kituo cha Azam Academy kilichopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam anaungana na Watanzania wengine wanaosakata soka la kulipwa nchini Kenya Tumba Sued Lui (Kushoto) amesajiliwa na timu ya Wazito

YANGA TIA MAJI TIA MAJI YATINGA 16 BORA YA FA CUP

Picha
Na Exipedito Mataruma. Mbeya Mabingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu FA Cup baada ya jioni ya leo kuiondosha Ihefu Fc kwa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90. Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, iliwabidi Yanga wasubiri hadi dakika ya 90 ya mchezo kusawazisha bao kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Obrey Chirwa. Mwamuzi Athuman Razi wa Morogoro aliipa Yanga penalti baada ya Obrey Chirwa kukwatuliwa na beki wa Ihefu ndani ya box, Ihefu walikuwa wa kwanza kufunga bao kipindi cha kwanza dakika ya 36 kufuatia beki wa Yanga, Andrew Vicent "Dante" kujifunga. Katika mikwaju ya penalti Yanga walipata nne zilizopigwa na Kevin Yondan, Hassan Kessy, Gadiel Michael na Raphael Daudi, wakati Papy Kabamba Tshishimbi na Obrey Chirwa walikosa. Penalti za Ihefu zilifungwa na Andrew Kayuni, Mhando Mkumbwa, na Jonathan wakati Abubakar Kidungwe, E

Azam Fc yawalambisha Ice Cream tano Shupavu Fc

Picha
Na Mwandishi Wetu. Morogoro Klabu bingwa ya soka Afrika mashariki na kati, Azam Fc mchana wa leo imefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA baada ya kuilaza timu ya Shupavu mabao 5-0 uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Huo ni ushindi mkubwa kwa vijana hao wa Said Salim Awadh Bakhresa ambao Jumamosi iliyopita walifungwa mabao 2-1 na Yanga mchezo wa Ligi Kuu Bara. Azam ilijipatia mabao mawili kipindi cha kwanza moja likifungwa kwa mkwaju wa penalti na Yahaya Zayd kabla ya Iddi Kipagwile, magoli mengine matatu yamefungwa na Paul Peter na kuwa hat trick yake ya kwanza kwenye michuano hiyo Azam Fc imeifunga Shupavu mabao 5-0

Simba yaihofia Azam, yataka mechi yake isogezwe mbele

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc imeanza kuingia mchecheto baada ya kuitaka Bodi ya Ligi (TPLB) kuisogeza mbele mechi yake dhidi ya Azam Sc itakayochezwa Februali 11 mwaka huu. Akizungumza jana, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Sunday Manara amesema ratiba yao inawapa ugumu kidogo kwani kwa sasa akili zao wanazielekeza kwenye michuano ya kimataifa ambapo Simba itacheza na Wadjibout. Manara amedai ratiba ya Ligi Kuu Bara inawabana kwani Simba itacheza na Ruvu Shooting Februali 4 kisha na Azam Fc halafu itaenda Shinyanga kucheza na Mwadui kabla ya kucheza kombe la Shirikisho barani Afrika. Manara amedai mipango ya Simba ni kufika mbali katika michuano ya Afrika na ndio maana wamemchukua kocha Mfaransa, Pierre Lechantre ambaye amewahi kuipa ubingwa wa Afcon, Cameroon mwaka 2000. Kwa maelezo ya Manara, Simba wanaiomba Bodi ya Ligi iwasogezee mbele mchezo wao dhidi ya Azam ikiamini itajipanga vizuri, laki

Yanga, Azam na Singida United zaingia vitani FA Cup

Picha
Na Exipedito Mataruma. Mbeya Baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uhondo umehamia katika michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu FA Cup ambapo miamba Yanga, Azam na Singida United zitaingia vitani kesho Jumatano na keshokutwa Alhamisi. Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc wao watasafiri hadi mkoani Mbeya ambapo watachuana na timu ya Ihefu Fc katika uwanja wa Sokoine, lakini klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam Fc wao wataifuata Shupavu Fc katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Pambano lingine la kusisimua litakuwa pale Azam Complex, Chamazi likihusisha kigogo Singida United dhidi ya wenyeji wao Green Warriors, huo nao unatajwa kuwa mchezo mgumu kwakuwa vijana wa Green Warriors waliiondoa Simba na kuinyang' anya ubingwa ilioutwaa mwaka jana Yanga watacheza na Ihefu Fc mjini Mbeya

Simba na Majimaji waingiza milioni 40

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kati ya Simba Sc na Majimaji Songea uliingiza shilingi milioni 40. Hayo ni mapato makubwa kuliko yale yaliyopatikana juzi Jumamosi katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara kati ya Azam Fc na Yanga Sc ambao waliingiza shilingi milioni 28. Katika mchezo huo wa jana, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 yaliyofungwa na John Raphael Bocco (Mawili) na Emmanuel Okwi pia mawili Simba na Majimaji zimeingiza milioni 40

Yanga na Azam waambulia milioni 28

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam Fc na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga Sc limeingiza shilingi milioni 28 za Kitanzania. Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Azam Complex,  juzi Jumamosi Chamazi na Yanga kushinda mabao 2-1 uliingiza kiasi hicho cha pesa ambacho kinatajwa ni kidogo. Katika mchezo huo Azam ilitangulia kupata bao katika dakika ya tatu na mshambuliaji wake chipukizi Shabani Chilunda, lakini Yanga wakasawazisha kupitia Obrey Chirwa na Gadiel Michael Mbaga kwa shuti kali Yanga na Azam wameingiza milioni 28

AUBAMEYANG KUTUA ARSENAL

Picha
Klabu ya Arsenal inataka kumnunua Pierre Emerick Aubameyang raia wa Gabon kwa kitita cha e60 m, kutoka kwa klabu ya Borrusia Dortmund ya Ujeruman. Aubameyang (28) ameishawishi Arsenal ambayo hivi karibuni iliondokewa na mshambulizi wake Alexis Sanchez raia wa Chile aliyejiunga na Manchester United. Sanchez alipishana na Henrick Mkhitaryan ambaye amejiunga na washika bunduki hao wa Amirates, ujio wa Aubameyang hautakuwa rahisi kwani Dortmund hawatamruhusu mpaka pale itakapofanikiwa kumnasa straika mwingine hatari lakini kuna uwezekano wa Olivier Giroud akaangukia kwao Pierre Emerik Aubameyang (Kushoto) yuko mbioni kujiunga na Arsenal

KISPOTI

Picha
ALICHOFANYA JUMA NYOSO ANGEKUWA SIMBA SC INGEKUWA POA. Na Prince Hoza JUMATATU ya wiki iliyopita beki wa Kagera Sugar Juma Said Nyoso alimpiga shabiki wa Simba Sc mpaka kuzimia, Nyoso alifanya hivyo baada ya shabiki huyo kumpulizia vuvuzela masikioni mwake. Tayari Nyoso alikuwa na hasira kufuatia timu yake ya Kagera Sugar kuchapwa mabao 2-0 na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Inasemekana shabiki huyo alianza kumuandamana Nyoso tangu dakika 90 za mchezo, na baada ya mpira kumalizika shabiki huyo aliingia uwanjani akiwa na vuvuzela lake na kumkaribia Nyoso kisha kumpulizia masikioni mwake kama sehemu ya kuwasilisha furaha yake. Ikumbukwe msimu uliopita mashabiki wa Simba walitoka vichwa chini katika uwanja huo baada ya timu yao kulala kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, hivyo furaha ya kupitiliza waliyokuwa nayo wapenzi na mashabiki wa Simba ilizidi mipaka baada ya timu yao kulipiza kisasi na kum

SINGIDA UNITED YAFUFUKIA KWA PRISONS

Picha
Na Mwandishi Wetu. Singida Wenyeji Singida United jioni ya leo wameamka usingizini baada ya kuichakaza Tanzania Prisons bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa uwanja wa Namfua Singida. Goli ambalo limeibeba Singida United limefungwa na mshambuliaji wake Mzambia Elinyesia Sumbi na kuifanya timu hiyo kukwea hadi nafasi ya nne. Vijana wa Singida United wanaonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm wamefikisha pointi 27 wakiwa nyuma ya Yanga yenye pointi 28, Singida sasa inajiandaa kucheza na Mwadui hapo hapo Namfua mwishoni mwa wiki ijayo Singida United imeilaza Prisons leo

SIMBA SIYO YA MCHEZO MCHEZO, YAIFANYIA KITU MBAYA MAJIMAJI

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Simba Sc imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya jioni ya leo kuifanyia kitu mbaya Majimaji ya Songea kwa kuifunga mabao 4-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mchezo huo wa kuhitimisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ilishuhudiwa Simba ikiongoza kwa mabao mawili hadi ingwe ya kwanza inamalizika kwa magoli yaliyofungwa na nahodha John Raphael Bocco. Kipindi cha pili Emmanuel Okwi akaongeza mengine mawili na kufanya Simba iibuke na ushindi mnono wa 4-0 na kuendelea kuchanua kileleni. Huo ni ushindi wa kwanza wa kocha Mfaransa, Pierre Lechantre aliyechukua mikoba ya Joseph Omog raia wa Cameroon, kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 35 na mechi 15 ikizidi kuiacha Azam Fc kwa zaidi ya pointi 5 Emmanuel Okwi (wa kwanza kulia) akishangilia sambamba na Said Ndemla

KUSUJUDU KWA GADIEL MICHAEL KWAZUA MSHANGAO, MWENYEWE AFAFANUA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Madhabiki wa soka nchini jana waliingia na mshangao kufuatia beki wa pembeni wa mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc, Gadiel Michael Mbaga kushangilia bao lake kwa kusujudu kama waislamu. Beki huyo wa upande wa kulia aliyesajiliwa na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Azam Fc, jana aliifungia Yanga bao la ushindi dhidi ya Azam Fc katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 2-1 na Azam Fc walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa dakika ya 3 kipindi cha kwanza na Shabani Chilunda, lakini Obrey Chirwa akaisawazishia Yanga kabla ya Gadiel kufunga la pili na la ushindi. Baada ya kufunga, Gadiel alikimbia pembeni na kuinama chini akiswali kwa mtindo wa kusujudu ambao unatumiwa sana na waumini wa dini ya Kiislamu, baada ya kufanya hivyo mashabiki wa soka walishangazwa huku wengine wakidai mchezaji huyo ni Muislamu na wengine wakidai hata Wakristo hufanya hivyo. Lakini baadaye Gadiel alitolea ufafanuzi kuwa aliamua kusuju

Simba na Majimaji ngoma inogile Taifa leo

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc jioni ya leo inaumana na Majimaji ya Songea katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mchezo huo ni muendelezo wa Ligi Kuu Bara kukamilisha mzunguko wa kwanza, Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na alama 32 ikifuatiwa na Azam yenye alama 30 na Yanga ikikamata nafasi ya tatu ikiwa na alama 28. Majimaji imekuwa ngumu kufungwa na vigogo msimu huu hasa ikicheza uwanja wake wa nyumbani Majimaji Stadium mjini Songea kwani iliweza kuzibana, Yanga Sc, Azam Fc na Singida United, na kwa mujibu wa kocha wao mkuu Habibu Kondo amesema hata Simba wataibania leo. Timu hiyo inajivunia safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Peter Mapunda, Marcel Boniventure, Seleman Kassim Selembe na Jerryson John wakati Simba yenyewe inatambia nyota wake Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi, Asante Kwasi, John Bocco na Jonas Mkude, mchezo mwingine utapigwa mjini Mbeya wakati wenyeji Tanzania Prisons wakiialika Singida United Simba

Yanga yaichinja Azam, Chamazi

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Hatimaye ule ubishi wa nani mbabe kati ya mabingwa wa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Kagame Azam Fc na mabingwa wa Tanzania bara Yanga Sc umemalizika kwa Yanga Sc kuilaza Azam Fc mabao 2-1 uwanja wa Azam Complex, Chamazi, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Azam Fc inayonolewa na Mromania, Aristica Cioaba, ilitangulia kupata bao la uongozi lililofungwa na mshambuliaji wake chipukizi, Shaaban Iddy Chilunda aliyepasiwa krosi na Mzimbabwe Bruce Kangwa. Baada ya kuingia goli hilo, Yanga walicharuka na kulishambulia lango la Azam kama nyuki na kufanikiwa kusawazisha kupitia Obrey Chirwa aliyepasiwa na Ibrahim Ajibu, kabla ya kwenda mapumziko Yanga wakaongeza bao la pili lililofungwa na Gardiel Michael kwa shuti kali. Hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele, kipindi cha pili kila timu ilishambulia kwa zamu lakini mwisho Yanga wakaibuka wababe na kufikisha pointi 28 wakiendelea kushikilia nafasi ya tatu, Azam wanabaki na pointi zao 30. Mch

Wenger amtetea Sanchez kukataa kupima

Picha
Mkufunzi wa Arsenal, Arsenel Wenger amemtetea mchezaji wake wa zamani Alexis Sanchez aliyejiunga na mashetani wekundu, Manchester United kwa kukataa vipimo. Sanchez amekataa kupima afya kama anatumia madawa ya kuongeza nguvu ama hatumii, raia huyo wa Chile alikataa kupimwa baada ya kutakiwa na madaktari. Katika taarifa yake. meneja wa Arsenal, Arsenel Wenger amedai hakuna ulazima wowote wa kupima kwani Sanchez hatumii dawa hizo na anajiamini kwa kile anachokiamini Alexis Sanchez amekataa kupima afya

Yanga na Azam hapatoshi Chamazi

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Jiji la Dar es Salaam litasimama kwa muda kupisha vita ya mafahari wawili mabingwa wa kombe la Kagame Azam Fc na mabingwa wa Tanzania Bara Yanga Sc katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi mchezo wa Ligi Kuu Bara. Azam Fc ikicheza nyumbani ina kila sababu ya kuweza kuzoa pointi tatu na kukaa kileleni ikiishusha Simba inayoongoza kwa sasa ikiwa na pointi 32, Azam yenyewe ina pointi 30 lakini ikishinda itafikisha pointi 33. Kwa upande wa Yanga watakaocheza bila makocha wao George Lwandamina na Shadrack Nsajigwa, pia ikiwakosa nyota wake wa kikosi cha kwanza ambao ni majeruhi, ila Obrey Chirwa ataiongoza safu ya ushambuliaji akishirikiana na Ibrahim Ajibu na Raphael Daudi. Azam Fc wao wako kamili wakiwa na nyota wao Himid Mao, Salum Abubakar, Frank Domayo, Benard Athur, Iddy Kipagwile na wengineo bila shaka mchezo utakuwa mkali. Mechi nyingine za ligi hiyo zitapigwa leo ambapo pale Sokoine Mbeya, wenyeji Mbeya City watawaalika Mtibwa Sugar, kule Mwadui C

Ruvu Shooting yainyoosha Mbao

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Masarange wa Ruvu Shooting ya Mlandizi Kibaha mkoani Pwani jioni ya leo imeutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Mabatini baada ya kuilaza Mbao Fc mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kwa ushindi huo Ruvu Shooting imefikisha pointi 14 na sasa imetoka mkiani nafasi ya 16 na kupanda hadi ya 11, Ruvu Shooting waliupania vilivyo mchezo huo hasa wakikumbuka kichapi walichokipata msimu uliopita kutoka kwa Mbao cha mabao 4-0. Hivyo leo wamelipiza kisasi kwa ushindi huo, mabao yote ya Ruvu Shootibg yamefungwa na Mcha Khamis, ligi hiyo itaendelea tena kesho viwanja vinne vikiwaka moto, Azam Fc vs Yanga, Mwadui Fc vs Njombe Mji, Mbeya City vs Mtibwa Sugar na Kagera Sugar vs Lipuli Fc Ruvu Shooting wameifunga Mbao 2-0

JPM NA MKEWE WACHANGIA SHILINGI MILIONI 15 KWA WASTARA

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wamemchangia shilingi milioni 15 msanii wa filamu nchini Wastara Juma ili arudi hospitali ya Sifael nchini India, kwaajili matibabu chini ya uangalizi wa hospital hiyo. Fedha hizo zimekabidhiwa kwake na katibu wa Rais Ngusa Samike ambaye pia amemkabidhi Wastara shilingi milioni moja na laki tisa zilizochangwa na wasaidizi wa Rais, makabidhiano yakifanyika nyumbani kwa Wastara, Tabata Dar es Salaam. Hivi karibuni msanii huyo alikuwa akiomba msaada wa pesa kupitia vyombo mbalimbali vya habari ili arudi hospitali na kufikia hatua ya kuandika na kusambaza mtandaoni waraka maalum kwa Rais Magufuli, akiomba msaada. Katibu wa Rais, Ngusa Samike (Kushoto) akimkabidhi Wastara Juma shilingi Milioni 15 leo nyumbani kwake Tabata

AZAM FC YAMSHITUKIA NKONGO

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Uongozi wa klabu bingwa ya soka Afrika mashariki, Azam Fc wameiandikia barua Bodi ya Ligi (TPLB) likimpinga mwamuzi wa kati Israel Nkongo. Nkongo atachezesha mechi yao dhidi ya mabingwa watetezo Yanga Sc itakayopigwa kesho mishale ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Katika madai yao Azam kwa TPLB wanataka mwamuzi huyo abadilishwe kwakuwa anapopewa dhamana ya kuchezesha mechi zao zimekuwa na malalamiko, Azam wanathibitisha kuwa Nkongo hafai kuchezesha pambano lao na Yanga kwani amewahi kushindwa mara kadhaa kwenye mechi zao. Mwamuzi huyo aliwahi kuchezesha mechi ya Yanga na Azam na Azam kushinda mabao 3-0 na wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Stephano Mwasika walimshambulia mwamuzi huyo, hivyo hawataki yatokee hayo hiyo kesho Mwamuzi Israel Nkongo (Katikati) amekataliwa na Azam Fc

MBAO FC KAZI WANAYO LEO KWA RUVU SHOOTING MABATINI

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena hii leo kwa mitanange miwili kupigwa katika viwanja tofauti, lakini mechi ambayo ni gumzo itapigwa Mlandizi. Ruvu Shooting iliyofanyiwa marekebisho kwenye safu yake ya ushambuliaji baada ya kukosa mabao mengi ya wazi dhidi ya Yanga Sc, itawakaribisha Mbao Fc ya Mwanza katika uwanja wake wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani. Kwa mujibu wa msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire leo Mbao Fc kazi wanayo kwani wamewaandalia misumeno ya kufa mtu kwa ajili ya kuikatakata jioni ya leo, mchezo mwingine utapigwa Mwadui Complex kati ya wenyeji Mwadui Fc na Njombe Mji Ruvu Shooting inaumana na Mbao Fc leo

STAA WETU

Picha
SHOMARI KAPOMBE. AMERUDI KUWASHIKA. Na Prince Hoza MCHEZAJI ambaye sikutaka asajiliwe na Simba msimu huu ni Shomari Kapombe, kitu pekee kilichonifanya nisipende asajiliwe ni majeruhi aliyonayo ambayo nilidhani kama yatamfanya asirejee katika ubora wake. Ama kweli nililaani sana usajili wa Kapombe mpaka kufikia kumshutumu mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Simba, Kapteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). Zacharia Hanspoppe, sikuona mantiki yoyote Simba kumuacha Mkongoman Janviel Bokungu na kumsajili kiungo huyo mwenye uwezo pia wa kucheza  kama beki. Kapombe ni mchezaji mzuri na ndio maana akapata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Ufaransa katika klabu ya Cannes inayoshiriki Ligi Daraja la nne. Lakini tatizo kubwa linalomsumbua maishani mwake ni maumivu ya nyonga, inafikia wakati Kapombe anatamani kuachana na soka na kufanya shughuri nyingine, Kapombe amekosa raha kwa kipindi kirefu hasa akiwa nje ya uwanja akiuguza majeraha yake. Nyota huyo alis

NDANDA FC YAIZAMISHA STAND UNITED

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Timu ya Ndanda Fc "Wanakuchele" jioni ya leo imeizamisha Stand United bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Matokeo hayo yanaifanya Ndanda Fc kuchupa hadi nafasi ya saba ikiwa na pointi 16 katika mechi 14 ilizocheza. Bao pekee lililoipa ushindi Ndanda inayonolewa na mchezaji wa zamani wa Mlandege, Malale Hamsini lilifungwa na straika wake matata Omari Mponda, Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mechi mbili kupigwa, Ruvu Shooting na Mbao Fc uwanja wa Mabatini Mlandizi, Mwadui Fc na Njombe Mji uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga Ndanda Fc imeifunga Stand United leo

Tambwe, Maftah wamtetea Nyoso, Waziri wa Ulinzi aonya

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kitendo kilichofanywa na beki wa Kagera Sugar, Juma Nyoso cha kumpiga shabiki wa klabu ya Simba hadi kuzimia, kimeungwa mkono na baadhi ya wachezaji na kukosolewa pia. Kipa wa zamani wa Villa Squad, Zimamoto ya Zanzibar na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Kitwana Tambwe ameunga mkono kitendo cha Nyoso kumpiga shabiki huyo kwani hata yeye amewahi kumpiga kichwa shabiki aliyemzomea baada ya kufungwa. Lakini beki wa zamani wa Yanga na Simba, Amir Maftah yeye amelaani vikali kitendo cha Nyoso kumpiga shabiki lakini akadai hata yeye alipokuwa na Yanga waliwahi kumpiga shabiki mjini Morogoro hadi akazimia kisa tu aliwatukana. Ila beki wa zamani wa Yanga na APR ya Rwanda, Hamis Yusuf "Waziri wa ulinzi" ameonya vitendo kama hivyo vya kupiga mashabiki kwani amedai siyo vizuri, Yusuf amedai mashabiki ndio wamekuwa wakiwaaapoti wachezaji hivyo kuwapiga si haki Juma Nyoso ametetea na wachezaji wenzake

Cannavaro asema vijana wanaiangusha Yanga

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Beki na nahodha wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga Sc, Nadir Haroub Ally "Cannavaro" amesema wachezaji vijana wanaiangusha Yanga na ndio maana hawatishi msimu huu. Akizungumza na gazeti moja la michezo linalotoka kila siku, Cannavaro amesema uwepo wa wachezaji wengi vijana kwenye kikosi hicho kwa sasa hakiwapi matokeo ya kuridhisha mashabiki wa Yanga tofauti na wao walivyokuwa wakiaminiwa. Amedai kukosekana kwa mastaa kama Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na wengineo kunawanyima matokeo na soka la kuvutia, beki huyo amedai vijana hawajitumi ingawa kwa sasa hawana jinsi. "Mpango wa Yanga kwa sasa ni kukaa na vijana na sababu kubwa vijana hawa watakuja kuwa mastaa hapo baadaye lakini tatizo lao hawajitumi ipasavyo, Yanga ni jina kubwa na ina mashabiki wengi na wanataka matokeo na soka la kuridhisha, lakini vijana wanajitahidi ila hawajitumi", alisema nahodha mwenye heshima kub

Man United klabu tajiri duniani

Picha
Manchester United imeongoza orodha ya klabu 20 tajiri zaidi duniani kwa mwaka wa pili mfululizo na mara ya 10 kwa jumla , kulingana na kampuni ya Deloitte. Mbali na msimu wa 2016-17 jumla ya mapato ya klabu hizo 20 imeongezeka kwa asilimia 6 hadi €7.9bn (£6.97bn), ikiwa ni rekodi mpya. Real Madrid ilioongoza kwa miaka 11 ilikuwa ya pili na Barcelona ikawa ya tatu. Kulikuwa na rekodi ya klabu 10 za Uingereza katika orodha hiyo ya 20 bora. Orodha hiyo inaangazia mapato yaliopatikana na haiangazii madeni ya vilabu. •1. Manchester United: €676.3m •2. Real Madrid: €674.6m •3. Barcelona: €648.3m •4. Bayern Munich; €587.8m •5. Manchester City: €527.7m •6. Arsenal: €487.6m •7. Paris Saint Germain: €486.2m •8. Chelsea: €428m •9. Liverpool: €424.2m •10. Juventus: €405.7m Duru: Deloitte, Mapato ya msimu wa  2016-17

Sibuka sasa kutangaza live Ligi Kuu England

Picha
Na Alex Jonathan. Dar es Salaam Kituo cha redio Sibuka cha jijini Dar es Salaam kimeanza kutangaza mechi za Ligi Kuu ya England (EPL) na kuwataka wapenzi wa soka kujitokeza kusikiliza kwani wanaweza kuibuka mamilionea. Akizungumza na Mambo Uwanjani, mtangazaji wa redio hiyo David Pasko (Pichani) amesema kituo chake kimeanza kutangaza live ligi ya EPL. Amedai Watanzania wamekuwa wakipenda kufuatilia ligi ya England hivyo wameamua kuwaletea matangazo hayo moja kwa moja, pia Pasko amesema kituo chake kitaendelea kurusha matangazo ya moja moja ya mpira wa Ligi Kuu Bara

Shamte atambia Halima wake

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Msanii anayechipukia wa muziki wa kizazi kipya maarufu Bongofleva, Shukuru Nassoro "Shamte" ametamba kufanya vizuri na wimbo wake mpya "Halima" ambao tayari ameshautambulisha kwenye Media. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Shamte amesema tayari wimbo wake ameshausambaza kwenye mitandao ya kijamii na amedai wimbo huo utamtoa kimuziki. Akielezea mahadhi aliyotumia katika wimbo huo alionshirikisha nyota wa muziki wa Singeli Side Kichwa amedai ametumia miondoko ya Singeli. Ameongeza kuwa Halima ni hadithi ya kweli kabisa na ameamua kufikisha ujumbe, wimbo huo umeanza kupa viewers wengi kwenye mtandao wa youtube na amewataka mashabiki wake kuuchangamkia ili kumpa nguvu ya kuachia ngoma nyingine, msanii huyo kwa sasa anaishi Temeke Dar es Salaam

ISMAIL SUMA AZIKWA BURUNDI

Picha
Na Mwandishi Wetu. Mlinda mlango wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ismail Suma amezikwa jana mjini Bujumbura, Burundi baada ya familia yake kushindwa kuusafirisha mwili nchini Tanzania. Suma aliyezichezea Kariakoo Lindi, Yanga, Simba na African Lyon, amezikwa jana katika makaburi ya Bujumbura, Burundi kufuatia kufariki dunia kwa maradhi Ini. Kipa huyo aliondoka Tanzania na kwenda DR Congo kucheza soka la kulipwa ambapo pia aliondoka na kuelekea Burundi pia kucheza soka la kulipwa ambapo mauti yakamfika. Baadhi ya wachezaji wenzake aliocheza nao nchini Tanzania wameonyesha kusikitishwa na kifo cha kipa huyo na kuliomba Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kusaidia kuuleta mwili nyumbani Tanzania kwa mazishi

KOCHA WA MWADUI AFARIKI DUNIA

Picha
Na Mwandishi Wetu. Shinyanga Kocha msaidizi wa timu ya Mwadui Fc ya Shinyanga, Jumanne Ntambi amefariki dunia usiku huu baada ya kuanguka bafuni wakati akioga. Kocha huyo ameanguka na kufariki papo hapo licha ya jitihada za kumwahisha hospitali zilipofanywa lakini madaktari wakathibitisha Ntambi kupatwa na mauti. Ntambi alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na alipewa likizo ingawa jana alienda kuwajulia hali wachezaji wake. Mungu ailaze mahara pema peponi, Amina

KIPA WA SIMBA NA YANGA AFARIKI BURUNDI

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mlinda mlango wa zamani wa Simba na Yanga na African Lyon, Ismail Suma amefariki dunia huko Bujumbura nchini Burundi. Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Salum Athuman amesema kuwa Suma amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya Ini. Kipa huyo aliyeibukia Kariakoo Lindi na kujiunga na Yanga Sc mwaka 2000 ambapo aling' ara na kujiunga na mahasimu wao Simba kabla ya kujiunga na African Lyon wakati huo ikiitwa Mbagala Market aliugua kwa muda mrefu kabla ya umauti kumfika. Suma (Pichani wa kwanza kushoto) alienda Burundi baada ya kuondoka DR Congo alikokuwa anacheza soka la kulipwa, mazishi ya mchezaji huyo yatafanyika Burundi baada ya familia yake kushindwa kuuleta mwili Tanzania

POLISI YASEMA SHABIKI ALIMPULIZIA VUVUZELA NYOSO

Picha
Na Paskal Beatus. Bukoba Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Agustin Ollomi amesema sababu ya mlinzi wa kati wa timu ya Kagera Sugar, Juma Nyoso kumpiga mshabiki ni kukerwa na maneno ya maudhi pamoja na kupuliziwa vuvuzela masikioni. Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kati ya Kagera Sugar na Simba ambao Wekundu hao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 uliofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba. Kamanda Ollomi amesema shabiki huyo alishuka jukwaani na kwenda kumpulizia vuvuzela masikioni wakati Nyoso akiwa ametoka kufungwa kitu kilichomfanya kupata hasira. "Yule shabiki alimfuata Nyoso na kumpulizia vuvuzela masikioni wakati akiwa ana hasira ya kufungwa ndio maana akampiga na kusababisha kuzimia," alisema Kamanda Ollomi. Taarifa zinasema hali ya shabiki huyo inaendekea vizuri lakini bado yupo hospitali baada ya kuzinduka saa 6 usiku. Nyoso amefunguliwa shitaka la shambulio wakati shabiki nae amefunguliwa shitaka la kutukana hadharani

KOCHA WA SIMBA B ACHEKELEA KUIPANDISHA FRIENDS RANGERS

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Kocha wa zamani wa kikosi cha Simba B, Said Msasu "Nagri" ameanza kuchekelea kikosi chake cha sasa cha Friends Rangers ya Magomeni Kagera jijini Dar es Salaam kuelekea kupanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Msasu ambaye amewahi pia kuzichezea Simba Sc, Lipuli Fc na Singida United amedai timu yake ya Friends Rangers itapanda Ligi Kuu Bara licha kwamba bado wana mchezo mkononi dhidi ya JKT Mgambo. Friends ipo kundi C ambalo tayari timu ya JKT Ruvu imeshapanda Ligi Kuu na ushindani sasa upo kwao na African Lyon, Friends Rangers ina pointi 22 wakati Lyon ina pointi 21 na zote zimecheza mechi 12 hivyo ana uhakika kabisa ya kuipandisha Ligi Kuu timu hiyo iliyosotea nafasi kwa misimu kadhaa

Mashabiki Yanga wamkumbuka Mwambusi

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kufuatia kiwango kibovu inachokionyesha Yanga kwa sasa, baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wamemkumbuka aliyekuwa kocha msaidizi Juma Mwambusi wakidai ni bora yeye kuliko Shadrack Nsajigwa. Wakizungumza tofauti kupitia mitandao ya kijamii, mashabiki hao wameelezea hisia zao na kudai kwa sasa Yanga haiwapi raha kwani soka wanalocheza haliwavutii na timu yao inazidi kuwapa presha. Wanadai Yanga inacheza soka ambalo hawajazoea kuliona kwani hata ushindi wake umekuwa wa bahati, Yanga iliifunga Ruvu Shooting bao 1-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam lakini Ruvu ndio waliutawala mchezo huo. Hivyo wameutaka uongozi wa Yanga kumrejesha haraka kocha msaidizi Juma Mwambusi ambaye amejiuzuru ili aweze kuinusuru timu yao, kwani Mwambusi amefanya vizuri alipohudumu kwenye nafasi hiyo

Nyosso ashikiliwa na polisi kwa kumpiga shabiki wa Simba

Picha
Na Paskal Beatus. Bukoba Beki wa Kagera Sugar, Juma Said Nyoso anashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Kagera baada ya kudaiwa kumpiga shabiki wa Simba anayesemakana kumdhihaki mchezaji huyo. Taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo kwa sasa, zinasema kuwa Nyoso alitaka kumchapa Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara lakini polisi waliingilia kati na kuwanusuru wawili hao. Lakini Nyoso akiwa anaelekea kwenye gari la timu yake ya Kagera Sugar akakutana na shabiki wa Simba aliyemshambulia mchezaji huyo ndipo alipoamua kumdunda shabiki huyo na kumuumiza vibaya. Shabiki huyo amekimbizwa hospitalini na mchezaji huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi Juma Nyoso anashikiliwa na polisi kwa kupiga shabiki

Singida United yashikwa shati Songea

Picha
Na Mwandishi Wetu. Songea Timu ya Majimaji Fc ya Songea jioni ya leo imeibana mbavu Singida United baada ya kwenda nayo sare ya kufungana bao 1-1 katika uwanja wa Majimaji mjini Songea. Kwa matokeo hayo Singida United imeshindwa kuchupa kutoka nafasi ya tano waliyopo sasa hadi ya tatu endapo wangepata ushindi dhidi ya Majimaji, katika mchezo huo wa leo Singida United walitangulia kupata bao la kuongoza lililofungwa dakika ya 28 kipindi cha kwanza na Papy Kambale. Lakini vijana wa Majimaji waliweza kujitutumua na kuweza kusawazisha bao hilo lililowapa pointi moja muhimu lilifungwa na mshambuliaji wake Peter Mapunda kunako dakika ya 83, Singida United bado wana kumbukumbu mbaya ya kuchapwa mabao 4-0 na Simba Sc Singida United imeshindwa kuifunga Majimaji

Bocco, Ndemla wairejesha Simba kileleni

Picha
Na Paskal Beatus. Bukoba Simba Sc imerejea tena kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya jioni ya leo kuilaza Kagera Sugar kwa mabao 2-0 uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Iliwachukua kipindi cha pili Simba kujipatia mabao hayo baada ya kucheza dakika 45 za mwanzo bila kufungana, Kagera Sugar walionekana kuimudu Simba baada ya kuizuia isipate bao hadi zilipoenda kupumzika. Kipindi cha pili Simba ilirejea uwanjani ikiwa na kasi mpya na kuanza kujipatia mabao yake yaliyoipa pointi tatu na kuishusha kileleni Azam Fc iliyokamata kiti hicho kwa muda, mabao ya Simba yamefungwa na Said Ndemla na John Bocco "Adebayor", kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 32 ikicheza mechi 13 na mwishoni mwa wiki itaumana na Majimaji Simba imeifunga Kagera Sugar 2-0

Habari njema kwa Wanayanga, kurejea kwa Chirwa na Yondani, Buswita mmh

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC jumamosi ijayo (January 27) watakuwa wageni wa Azam FC katika uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wa muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara. Pius Buswita ataukosa mchezo huo, mara ya hapo jana kuoneshwa kadi ya njano ambayo ni ya tatu kwake, lakini ahueni kubwa kwa kikosi cha George  Lwandamina ni kurejea kwa mshambuliaji wake Mzambia Obrey Chirwa. Chirwa na Kelvin Yondani wanarejea uwanjani baada ya kumaliza adhabu zao, Chirwa alifungiwa mechi tatu na Yondani alikuwa na kadi tatu za njano. Daktari wa mabingwa hao watetezi, Edward Bavu amethibitisha kupatikana kwa huduma ya kinda Yohana Oscar Nkomola  aliyeumia hapo jana akieleza kuwa hali yake imetengamaa. Habari njema kwa Yanga kurejea kwa Obrey Chirwa (Kulia)

KAGERA SUGAR VS SIMBA NI MECHI YA KISASI

Picha
Na Paskal Beatus. Bukoba Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa kuzikutanisha Kagera Sugar na Simba Sc katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Huo ni mchezo wa kisasi kutokana na kumbukumbu ya msimu uliopita ambapo Simba ililala 2-1 mpaka kuamua kukata rufaa TFF kisha kutishia kwenda Fifa kwa kile kilichodaiwa Kagera Sugar kumchezesha Mohamed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano. Kwa maana hiyo mechi ya leo itakuwa ya kisasi, Simba ikitaka kulipiza kisasi, lakini pia itakuwa mechi ya uhasama kwani inawakutanisha tena Juma Nyosso na John Bocco ambao walikuwa maadui hawapatani na hasa Nyosso alimtomasa makalioni Bocco hivyo hatujui leo kitatokea kitu gani Kaitaba, Simba ikishinda ama kutoka sare itarejea kileleni Kagera Sugar inaumana na Simba leo

KISPOTI

Picha
SIMBA SASA IMEAMUA KULETA KOCHA KIBURI NA JEURI ZAIDI YAO Na Prince Hoza NIMESOMA vizuri rekodi ya kocha mpya wa Simba Sc, Mfaransa Pierre Lechantre kuwa hakuwahi kudumu na timu zaidi ya mwaka mmoja, lakini klabu ya Simba nayo haijawahi kudumu na kocha kwa kipindi cha mwaka mmoja au zaidi. Joseph Omog peke yake ndiye aliyedumu kwa mwaka mmoja na zaidi na ameweza kwa sababu aliiwezesha Simba kurejea kwenye michuano ya kimataifa baada ya kukosa kwa miaka minne, Simba ilianza timua timua ya makocha tangu msimu wa 2011/12. Pamoja na uongozi wa Simba kutoweka bayana muda wa mkataba wa kocha wake mpya Pierre Lechantre wa kuitumikia klabu hiyo, takwimu zinaonyesha Mfaransa huyo hajawahi kukaa katika klabu moja zaidi ya mwaka. Uongozi wa Simba umemtangaza Mfaransa Lechantre kuwa kocha wa klabu hiyo akichukua mikoba ya Mcameroon Joseph Omog aliyetimuliwa hivi karibuni, ujio wa kocha huyo Mfaransa unaifanya Simba kuwa imefundishwa na makocha tisa tangu ilipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msi

AZAM FC YAISHUSHA SIMBA KILELENI

Picha
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc jioni ya leo imeifunga Tanzania Prisons mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Ikicheza nyumbani, Prisons waliweza kuibana Azam Fc kipindi cha kwanza na kufanya mashambulizi ya kushutukiza, lakini hadi mapumziko timu zote zilienda zikiwa hazijafungana hata bao. Kipindi cha pili dakika ya 77 Azam walijipatia bao la kuongoza likifungwa na kinda Yahya Zayd kabla ya dakika ya 83 kinda mwingine Paul Peter kufunga la ushindi, kwa matokeo hayo Azam wanakamata usukani wakifikisha pointi 30 wakifuatiwa na Simba wenye pointi 29. Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara timu ya Mwadui ililazimishwa sare ya  1-1 na Ndanda Fc uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Ligi hiyo itaendelea kesho kwa Simba Sc na Kagera Sugar uwanja wa Kaitaba na Majimaji na Singida United kule Songea Azam imeidunga Prisons 2-0 leo

YANGA YAWASHA ENDIKETA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imewasha endiketa zake baada ya kuilaza Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani bao 1-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Kwa uahindi huo Yanga imekwea kutoka nafasi ya tano hadi ya tatu ikifikisha pointi 25 sawa na Mtibwa Sugar lakini ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga, Yanga imecheza mechi 13 na iliingia uwanjani leo ikisaka ushindi kwa udi na uvumba. Goli ambalo limeipa ushindi Yanga limefungwa na mshambuliaji wake chipukizi Pius Buswita aliyepokea pasi ya Ibrahim Ajibu, hadi timu hizo zinaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo, timu zote zilishambuliana kwa zamu hadi mwisho matokeo ndiyo hayo Pius Buswita ameifungia Yanga bao pekee

NINJE AMPONZA MAYANGA STARS

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) limetangaza kuanzisha mchakato wa kusaka kocha mpya wa timu ya taifa, Taifa Stars akichukua mikoba ya Salum Mayanga anayemaliza mkataba wake. Taarifa ambazo Mambo Uwanjani imezinyaka ni kwamba mkataba wa Mayanga upo ukingoni na mipango ya TFF kwa sasa ni kuajili kocha mzungu. Lakini inasemekana kuwa kufanya vibaya kwa Tanzania Bara katika michuano ya Chalenji iliyofanyika Kenya ambapo karibu kikosi chote cha Bara ni kilekile cha Mayanga na hivyo  kimepelekea Watanzania kutokuwa na imani naye. Bara ilikuwa ikinolewa na Ammy Ninje, ambaye pia alikuwa msaidizi wa Mayanga kwenye kikosi cha Stars, kwa mujibu wa TFF mchakato wa kusaka kocha mpya walimu kutoka Zanzibar nao wametakiwa kutuma maombi Ammy Ninje 

Yanga na Ruvu Shooting ni machozi jasho na damu

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kipute cha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kinaendelea tena leo kwa viwanja vitatu nyasi kuwaka moto, kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam mabingwa watetezi Yanga Sc watakuwa wageni wa Ruvu Shooting ya Pwani. Huo ni mchezo mwingine kwa Yanga ambao wapo katika wakati mgumu kwa sasa hasa baada ya kuandamwa na majeruhi na nyota wake wa kikosi cha kwanza, hata hivyo wamejinasibu kushinda mchezo huo ingawa Ruvu Shooting nao si wa kubeza. Mechi nyingine leo zitapigwa mikoani, Tanzania Prisons itawaalika Azam Fc uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Mwadui Fc wataikaribisha Ndanda pale Mwadui Complex Shinyanga Yanga inacheza na Ruvu Shooting leo

Simba yaipashia Kagera Sugar

Picha
Na Mwandishi Wetu. Bukoba Unakumbuka ule mchezo wa msimu iliopita kati ya Simba Sc na Kagera Sugar ambao ulimalizika kwa Simba kufungwa mabao 2-1 mchezo wa Ligi Kuu Bara duru la lala salama. Kipigo kile kiliwafanya Simba wakose ubingwa wa Bara uliokwenda kwa Yanga, sasa timu hizo zinakutana tena Jumatatu ya wiki ijayo katika uwanja wa Kaitaba uliopo mkoani Kagera. Leo hii wachezaji wa Simba wakiwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma, waliipashia Kagera Sugar katika uwanja wa Tengamano Seminal School kabla ya kesho kupasha katika uwanja wa Kaitaba, Simba ndio vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 29 Simba wakipasha kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar

Nyosso amkaribisha Bocco Kaitaba

Picha
Na Mwandishi Wetu. Bukoba Kama umewahi kusikia Juma Nyosso alifunguliwa adhabu ya kufungiwa kucheza soka ndani na nje ya uwanja kwa kipindi cha miaka miwili ujue ni kwa sababu ya John Bocco "Adebayor". Sikia ilikuwa hivi, Nyosso alikuwa anaichezea Mbeya City akiwa nahodha, na John Bocco naye akiichezea Azam Fc naye nahodha, basi ilipigwa mechi uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi. Nyosso alimdhalilisha Bocco kwa kumwingiza kidole makalioni, hapo ndipo TFF iliponfungia kwa miaka mitatu, na mwaka jana alifunguliwa ndipo alipojiunga na Kagera Sugar na Jumatatu kwa mara ya kwanza Nyosso anakutana tena na Bocco. Mambo Uwanjani iliwasiliana kwa simu na beki huyo wa zamani wa Ashanti United, Simba Sc na Coastal Union na kusema anamkaribisha Bocco Juma Nyosso aliyevalia jezi ya kijani, na John Bocco mwenye jezi nyekundu, wanakutana Jumatatu

Stand United yaikatakata Mbao Fc CCM Kirumba

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Timu ya Stand United ya mjini Shinyanga, jioni ya leo imeitoa nishai Mbao Fc baada ya kuichapa bao 1-0 katika uwanja wake wa nyumbani wa CCM Kirumba jijini Mwanza, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kwa ushindi huo moja kwa moja Stand United imekwea hadi nafasi ya 11 ikifikisha pointi 14, goli pekee lililoipa ushindi Stand United limefungwa kwa mkwaju wa penalti kunako dakika ya 40 na Vitalis Mayanga. Penalti hiyo ilisababishwa na kipa wa Mbao Fc, Ivan Rugumandiye ambaye alimkamata miguu mshambuliaji wa Stand United, Landry Ndikumana na wote kuanguka wakiwania mpira kwenye box, Mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara ulifanyika katika uwanja wa Manungu Complex Morogoro ambapo Mtibwa Sugar ilitoka suluhu 0-0 na Njombe Mji Stand United imeifunga Mbao leo

Diamond Platinum atembelea yatima Rwanda

Picha
#BURUDANI: DIAMOND PLATINUM ATEMBELEA YATIMA RWANDA. Msanii wa kimataifa wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, bongofleva, Nasibu Abdul au Diamond Platinum ametembelea kituo cha watoto yatima nchini Rwanda na kutoa misaada mbalimbali. Mwanamuziki huyo aliamua kutua Rwanda baada ya safari zake za kimuziki ikiwemo kufuata tuzo yake aliyoshinda nchini Nigeria. Msanii huyo amekuwa akijitolea na kusaidia makundi mbalimbali ya wasiojiweza wakiwemo watoto, tayari msanii huyo anamiliki kundi kubwa la muziki WCB lililokusanya wasanii mbalimbali na ametambulisha biashara yake ya karanga zilizowapa ajira vijana wa Afrika mashariki Mwanamuziki Diamond Platinum akiwa na watoto yatima alipowatembelea nchini Rwanda