Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2017

Baada ya kupata ushindi wake wa kwanza Ligi Kuu, Mexime aanza kuchonga

Picha
Na Mwandishi Wetu. Bukoba Baada ya kikosi chake cha Kagera Sugar kujikongoja na kupata ushindi wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara, kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime ameanza kuchonga. Kocha huyo bora wa VPL msimu uliopita ameanza kutamba akisema kikosi chake kimeanza ligi na Jumamosi ijayo kitaendeleza mauaji kwa maafande wa Tanzania Prisons katika uwanja wao wa Kaitaba mjini Bukoba. Kagera Sugar itawakaribisha maafande wa Prisons ambao jana Jumatatu wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani, lakini Mexime amedai ushindi ni lazima na ameahidi kikosi chake kitasogea hadi nafasi za juu kuwania ubingwa Kocha bora msimu uliopita,Mecky Mexime ameanza kuchonga

WACHEZAJI MBEYA CITY WAAPA KUFA NA SIMBA JUMAPILI

Picha
Na Exipedito Mataruma. Mbeya Wachezaji wa kikosi cha Mbeya City wamesema watakula sahani moja na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC watakapokutana Jumapili ijayo mchezo wa ligi raundi ya tisa. Mbeya City ambayo ilifingwa bao 1-0 na Azam FC katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam wameapa kufia uwanjani ili wasifungwe na Simba na kugeuzwa ngazi ya ubingwa. Simba ambayo Jumamosi iliyopita ililazimishwa sare ya 1-1 na watani wao wa jadi, Yanga SC katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, nao hawatakubali kupoteza mchezo huo hivyo itazifanya nyasi za uwanja wa Sokoine kuwaka moto. Kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Mrisho Ngasa ameiambia Mambo Uwanjani kuwa wanaisubiri kwa hamu kubwa mechi hiyo ili wathibitishe kile wanachokisema Wachezaji wa Mbeya City wameahidi kuikomalia Simba, Jimapili

Sare dhidi ya Yanga, Simba wambebesha lawama mwamuzi

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Baada ya kushindwa kulinda goli lao na hatimaye Yanga kusawazisha na matokeo kuwa 1-1 , vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC wamemtulia lawama mwamuzi aliyechezesha mechi ya watani Simba na Yanga, Jumamosi iliyopita uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Heri Sasii kwa kushindwa kuwazawadia penalti mbili wakati wachezaji wawili wa Yanga waliunawa mpira kwenye maeneo hatari. Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Sunday Manara 'Computer' amesema mwamuzi Heri Sasii aliwabeba Yanga waziwazi kwa kushindwa kuwapa penalti, anasema beki wa Yanga, Kevin Yondan na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi walinawa mpira kwa nyakati tofauti na video imeonyesha matukio. Manara analalamikia kitendo cha mwamuzi huyo kuwanyima waziwazi Simba penalti akidai imekuwa kawaida Yanga kupendelewa na waamuzi, hata hivyo Yanga ilisawazisha goli katika dakika ya 60 likifungwa na Obrey Chirwa baada ya Simba kutangulia kufunga. Simba ilijipatia bao

MILAMBO YAKIONA CHA MOTO KWA WANAJESHI WA MSANGE

Picha
Na Emil Kasapa. Tabora Timu ya soka ya Msange JKT ya TABORA  imewatandika ndugu zao  MILAMBO FC ya TABORA katika mchezo wa ligi daraja la pili TANZANIA BARA mchezo ukipigwa katika dimba la Mwinyi mjini hapa. Goli pekee la dakika ya 46 likifungwa na Hamad Yahaya lilitosha kuwapa ushindi wageni hao wa soka wanaochipukia mkoani hapa na kufuta matumaini ya Milambo ya kushinda mchezo huo Mchezo huo ni wapili mfululizo kwa MILAMBO kupoteza baada ya kufungwa bao moja kwa bila na MASHUJAA ya Kigoma wiki iliyopita wakati MSANGE JKT wao waishinda bao tano kwa mbili dhidi ya NYANZA ya Manyara. Baada ya Mchezo huo mwalimu wa Msange JKT,Gift Emmanuel amesema timu yake haikuanza vizuri mwanzoni mwa ligi kwa hakuwepo na kwa sasa mambo yataendelea kuwa mazuri na kuwasihi wanatabora kuhamishia mapenzi kwa timu hiyo. Kwa upande wake mwalimu Andrew Zoma wa Milambo amesema ni moja ya matokeo ya mpira na anajipanga kwa mzunguko wa pili. Kwa matokeo hayo MSANGE JKT wamefikisha alama nane na kuwapumuli

Prisons yazidi kuikandamiza Ruvu Shooting ya Masau Bwire

Picha
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya Timu ya Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine. Bao pekee lililoizamisha Ruvu Shooting ya Masau Bwire lilifungwa na straika Mohamed Rashid mapema kabisa dakika ya 19 kipindi cha kwanza, na kwa ushindi huo Prisons imefikisha pointi 13 sawa na Singida United na ikishika nafasi ya tano nyuma ya Simba SC, Yanga, Azam na Mtibwa zenye pointi 16. Kipigo hicho kinahatarisha uhai wa  Ruvu Shooting kwenye ligi hiyo hasa kutokana na nafasi yao, kwa sasa kikosi hicho kinashikilia mkia baada ya jana Kagera Sugar iliyokuwa mkiani kwa muda mrefu kushinda 2-1 dhidi ya Ndanda FC na kupanda hadi nafasi ya 13 Kikosi cha Prisons ambacho leo kimeizamisha Ruvu Shooting

Saa za Omog zinahesabika Simba, apewa mechi mbili

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kocha mkuu wa Simba SC, Mcameroon, Joseph Marius Omog yuko shakani kusalia kikosini na muda wowote anarejea nyumbani huku Mrundi Masoud Djuma akichukua nafasi yake. Omog amepewa mechi mbili tu na ikitokea bahati mbaya Simba ikapoteza mechi moja kati ya hizo ama kutoka sare basi kibarua chake kitafutwa rasmi, Simba ililazimishwa sare ya 1-1 na mtani wake Yanga lakini ilielemewa na kuomba mpira uishe. Vigogo wa Simba hawakufurahishwa na matokeo hayo isitoshe Simba msimu huu imefanya usajili mkubwa kuliko timu zote, mashabiki wa Simba pia hawamtaki kocha huyo wakidai ameshusha kiwango cha Simba. Simba iko kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga huku timu nne Simba, Yanga, Mtibwa na Azam zote zina pointi sawa 16 kila moja na mechi 8, Omog sasa amepewa mechi mbili dhidi ya Mbeya City na Prisons zote itacheza ugenini jijini Mbeya Kocha wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog kutupiwa virago

KISPOTI:

Picha
KWA HILI SIMBA NA YANGA MMEPATIA AISEE. Na Prince Hoza ACHANA na matokeo ya juzi Jumamosi ambapo mahasimu Simba na Yanga waliumana vikali uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kumaliza dakika 90 za mchezo kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1. Sare hiyo ilitokana kwa magoli ya Shiza Kichuya wa Simba aliyefunga kunako dakika ya 57 na Obrey Chirwa wa Yanga aliyefunga dakika ya 60, timu zote sasa zimefikisha pointi 16 huku Simba ikiongoza na Yanga ikifuatia. Na hiyo yote imetokana na jana Mtibwa Sugar kushindwa kuchomoza na ushindi dhidi ya Singida United ambapo timu hizo zilitoka suluhu 0-0 mechi ikipigwa uwanja wa Manungu Complex Arena mjini Morogoro. Sare hiyo imewafanya Mtibwa nao kufikisha pointi 16 lakini utasimama katika nafasi ya tatu kwakuwa imezidiwa mabao ya kufunga na vinara Simba waliofunga magoli 20, Yanga waliofunga magoli 11 na wao wenyewe wana magoli 7 tu. Na sasa narudi kwenye mada yangu ya leo Jumatatu tulivu wenyewe wanaiita 'Blue Monday', Leo nimeamua k

Kesho ni "Derby" ya Tabora, Milambo na Msange JKT

Picha
Na Emil Kasapa. Tabora Timu ya soka ya  Milambo FC maarufu kama wanazuke mselebende wanatarajia kushuka dimbani kesho katika uwanja wa Mwinyi mkoani hapa kucheza mchezo wao wa watano wa ligi daraja la pili dhidi ya Msange JKT zote kutoka mkoani Tabora. Timu hizo zinakutana huku Milambo ikiwa katika nafasi ya pili ikiwa na alama 9 wakati Msange Jkt (mabingwa wa mkoa huu msimu uliopita) wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 5. Kuelekea mchezo huo mwenyekiti wa Msange JKT Pascal Francis amesem wamejipanga kuhakikisha wanapunga gape pa pointi kati yao na ndugu zao Milambo. Kwa upande wake msemaji wa kikosi cha wanazuke mselebende-Milambo Fc ,Ramadhan Faraji amesema makosa waliyoyafanya katika mchezo dhidi ya mashujaa na kuppteza hayatajirudia tena kesho. Milambo FC kesho wanaumana na Msange JKT

Kagera Sugar waona mwezi, Mtibwa yang' ang' aniwa nyumbani

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara leo imeendelea kwa mechi tano ambapo Kagera Sugar kwa mara ya kwanza imeona mwezi baada ya kuilaza Ndanda FC mabao 2-1 katika uwanja wake wa nyumbani wa Kaitaba mjini Bukoba na kufikisha pointi sita. Ndanda walikuwa wa kwanza kupata bao likifungwa na mshambuliaji wake Omary Mponda lakini Venance Ludovic aliisawazishia Kagera bao kabla ya Christopher Edward kuifungia bao la ushindi. Matokeo mengine ni kama ifuatavyo: Mtibwa Sugar 0 Singida United 0, Lipuli FC 2 Mbao FC 1, Majimaji FC 1 Mwadui FC 1,  Njombe Mji 0 Stand United 0, Ligi hiyo itaendelea tena  kesho kwa mchezo mmoja kati ya Prisons na  Ruvu Shooting Kagera Sugar wakishamgilia ushindi wao wa kwanza

Kichuya adhihirisha Yanga hawana mabeki wa kumzuia asifunge

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Ukuta wa Yanga bado unaendelea kudhalilishwa na Shiza Ramadhan Kichuya ambaye jana ameweza kufunga bao lake la tatu dhidi ya Yanga, na yote amefunga katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Shiza Ramadhan Kichuya ambaye ni mtoto wa shabiki wa Yanga anayeishi mkoani Morogoro, amethibitisha kuwa Yanga hawana beki wa kuweza kumzuia kwani amefunga katika mechi tatu na kuifikia rekodi ya Amissi Tambwe ambaye naye ameitungua Simba mara tatu mfululizo. Kichuya alifunga goli msimu uliopita Oktoba 1 mwaka jana wakati miamba hiyo ilipotoka sare ya 1-1, goli lake lilikuwa la kusawazisha alifunga kwa mpira wa kona, pia akafunga goli la kusawazisha, Simba ikiifunga Yanga 2-1 Aprili mwaka huu na tena amefanya hivyo jana Shiza Kichuya (Kushoto akimtoka beki wa Yanga, Andrew Vicent "Dante"

HUYU TSHISHIMBI ALIWAVURUGAVURUGA SIMBA JANA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Inaaminika kwamba Papy Kabamba Tshishimbi ndio mchezaji bora wa mechi ya jana ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na timu hizo kufungana bao 1-1. Tshishimbi jana alikuwa akionekana kila ulipo mpira kwa maana alizunguka uwanja mzima, na pia yeye alifanya kazi ya ziada kukata umeme na kuwapoteza viungo wote wa Simba. Kama si uhodari wa kipa wa Simba Aishi Manula, basi jana Tshishimbi alikuwa anafunga mabao yake mawili saafi, Tshishimbi aliwavurugavuruga Mzamiru Yassin, James Kotei na kufanya wasionekane kabisa uwanjani mpaka kocha wa Simba, Mcameroon Joseph Omog akaamua kuwatoa Papy Kabamba Tshishimbi aliwavurugavuruga viungo wa Simba jana

Bila Aishi Manula, Mnyama alikuwa anachinjwa kirahisi jana

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam #Michezo: BILA AISHI MANULA MNYAMA JANA ALIKUWA ANACHINJWA KIRAHISI. Mlinda mlango namba moja kwa sasa hapa nchini, Aishi Salum Manula jana amefanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya wachezaji wa Yanga iliyokuwa inaelekea moja kwa moja wavuni. Yanga jana ilikutana na hasimu wake Simba katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kumaliza dakika 90 kwa kufungana bao 1-1, Simba walitangulia kupata bao likifungwa na Shiza Kichuya lakini dakika mbili baadaye Yanga wakakomboa kupitia kwa Obrey Chirwa. Lakini kama si juhudi za Aishi Manula ambaye alikuwa golikipa wa Simba basi huenda mnyama angelala mapema tena si chini ya bao nne, kwani wachezaji wa Yanga walikuwa wanalenga langoni kwa kupiga mashuti makali. Papy Kabamba Tshishimbi raia wa DRC jana alikuwa hatari kwa Simba baada ya kufanikiwa kupiga mashuti mawili makali ambayo yaliokolewa na Manula, Manula anatajwa kama mchezaji bora wa mechi hiyo kwa upande wa Simba, wachezaji wengine waliomjaribu ni Geo

MTIBWA SUGAR KURUDI KILELENI LEO?

Picha
Na Ikram Khamees. Morogoro Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inaendelea tena kwa nyasi za viwanja sita kuwaka moto baada ya juzi na jana kufanyika mechi moja moja, Katika uwanja wa Manungu Complex mjini Morogoro shughuri itakuwa pevu pale Mtibwa Sugar itakapowaalika Singida United. Mchezo huo licha kwamba utakuwa mgumu lakini rekodi zinaibeba Mtibwa Sugar inayonolewa na mwanasoka wake wa zamani, Zuberi Katwila kuibuka na ushindi na kukamata usukani, Mtibwa ina pointi 15 kwa mechi 7 hivyo ikishinda itafikisha pointi 18 itaziacha Simba, Yanga na Azam zenye pointi 16 kila moja. Simba na Yanga jana zilishindwa kutambiana Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam baada ya kumaliza dakika 90 zikitoka sare ya 1-1, na juzi Azam FC iliifunga Mbeya City bao 1-0 katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi. Mechi nyingine tano zitapigwa leo ambapo Majimaji itawaalika Mwadui FC, uwanja wa Majimaji Songea, Kagera Sugar na Ndanda zitaumana Kaitaba pale Bukoba, Tanzania Prisons na Ruvu Shooting, Sokoine Mbey

Chirwa ainusuru Yanga kulala kwa Simba

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Goli la kusawazisha lililofungwa kunako dakika ya 60 jioni ya leo uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, limetosha kabisa kuipa sare ya bao 1-1 na mahasimu wao Simba SC. Hadi mapumziko timu hizo zimeenda vyumbani zikiwa hazijafungana hata bao, kwa hakika leo mpira umepigwa mwingi karibu timu zote mbili lakini Papy Kabamba Tshishimbi ameendelea kuwa nyota wa mchezo kwa mara ya pili. Yanga watajilaumu sana kwa kushindwa kuchomoza na ushindi kufuatia mashambulizi yao ya kushutukiza, Shiza Kichuya aliifungia Simba bao la uongozi dakika ya 58, timu hizo sasa zote zikifikisha pointi 16. Ligi hiyo itaendelea tena kesho ambapo viwanja sita vitawaka moto lakini mchezo utakaozikutanisha Mtibwa Sugar na Singida United utakaofanyika uwanja wa Manungu Complex mjini Morogoro unatajwa kuwa mkali na wa kusisimua Obrey Chirwa (Wa kwanza kushoto akishangilia moja ya magoli

Mitanange ya Ligi Kuu Bara wikiendi hii

Picha
Oktoba 28 Jumamosi Ni Yanga SC vs Simba SC, (Uhuru Stadium, Dar es Salaam). Oktoba 29, Jumapili. Lipuli FC vs Mbao FC (Samora Stadium, Iringa) Mtibwa Sugar vs Singida United (Manungu Complex, Morogoro) Majimaji FC vs Mwadui FC (Majimaji Stadium, Songea) Njombe Mji FC vs Stand United (Sabasaba Stadium, Njombe) Ruvu Shooting vs Tanzania Prisons. Moja kati ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara

YANGA NA SIMBA NI MECHI YA KUCHANA MIKEKA LEO

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Leo ndio leo ambapo Jamhuri ya muungano wa Tanzania itasimama kwa muda kupisha mpambano wa watani wa jadi Yanga na Simba utakaofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni. Mechi hiyo ya raundi ya nane Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatajwa itakuwa ya kuchana mikeka kwani kuna watu wamebeti matokeo lakini huenda isiwe hivyo walivyobeti wao kwani matokeo yataamuliwa na dakika tisini. Katika mchezo huo Yanga huenda ikawategemea zaidi wachezaji wake ambao ni kipa Youthe Rostand, walinzi Juma Abdul na Gardiel Michael, lakini pia itamtumainia kiungo wake Papy Tshishimbi na washambuliaji Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu. Wakati Simba nao itawategemea zaidi Aishi Manula, Erasto Nyoni, James Kotei, Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya, yote kwa yote tusubiri muda ufike kwani mshindi wa leo atakaa kileleni. Simba wao waliingia Dar es Salaam jana asubuhi wakitokea visiwani Zanzibar kwa ndege ambapo walikaa wiki moja kujiandaa

Azam FC yaishusha Simba kileleni usiku huu

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mabingwa wa Afrika mashariki na kati, Azam FC usiku huu wamefanikiwa kukamata usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, baada ya kuilaza Mbeya City ya mkoani Mbeya bao 1-0 uwanja wa Azam Complex usiku huu. Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafungana hata bao, kipindi cha pili timu zote zilishambuliana kwa zamu lakini Azam FC wakafanikiwa kujipatia goli la ushindi. Goli hilo lililofungwa kunako dakika ya 59 na mshambuliaji wake Mbaraka Yusuf aliyeitendea haki pasi nzuri ya Mghana, Enock Atta Agyei, kwa ushindi huo Azam sasa inakuwa kileleni kwa kuishusha Simba iliyokuwa inaongoza ligi, Azam wamefikisha pointi 16 lakini wamecheza mechi nane. Hata hivyo Azam FC itakaa kileleni kwa masaa tu kwani kesho inaweza kuondolewa kileleni na Simba, Yanga au Mtibwa ambazo zitashuka dimbani Azam FC wamekaa kileleni usiku huu

Yanga nao watua Dar na kuelekea hotelini tayari kuua mnyama kesho

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC wamewasili mchana wa leo wakitokea mkoani Morogoro ambapo waliingia kambini tangu Jumanne iliyopita wakitokea Shinyanga ambako waliishinda Stand United mabao 4-0 Jumapili iliyopita mchezo wa Ligi Kuu bara. Machampioni hao wa kandanda wametua mchana ea leo kwa basi na moja kwa moja wameelekea hotelini ambapo watakaa hadi kesho na saa wataelekea uwanja wa Uhuru jijini kwa ajili ya kuua mnyama, Yanga inakutana na hasimu wake Simba na kikubwa kwao ni kulipiza kisasi baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti Agosti 23 mwaka huu mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii. Hata hivyo msemaji wa Yanga Dissmas Ten,hakuweka wazi hoteli gani waliyofikia akidai wanahofia hujuma kutoka kwa watu wasiowatakia mema, katika mchezo wa kesho Yanga inaweza kuwakosa nyota wake watatu Wazimbabwe  Thabani Kamusoko na Donald Ngoma lakini pia itamkosa na Mrundi Amissi Tambwe Wachezaji wa Yanga wakirejea mchana wa leo

SIMBA WATUA KIBABE DAR, WAENDA KUJIFICHA SERENA, KESHO KUIFYEKAFYEKA YANGA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC wamewasili asubuhi ya leo katika uwanja wa kimataifa wa ndege (JNIA) wakitokea Zanzibar ambako waliweka kambi ya wiki moja tayari kabisa kumkabili mtani wake wa jadi Yanga SC mchezo wa Ligi Kuu bara utakaofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mchezo huo utapigwa kesho utaanza saa 10:00 jioni na mwamuzi wa kati atakuwa kijana Heri Sasii ambaye ana beji ya Fifa, wachezaji wa Simba walipotua moja kwa moja wakaingia kwenye basi lao na kuelekea katikati ya jiji ambapo watakaa katika hoteli ya kifahari ya Serena na kesho wataenda kuifyekafyeka Yanga. Wachezaji wa Simba wametua kwa shauku kubwa uwanjani hapo leo na kila mchezaji ameonekana katika hali ya kujiamini, Simba inakwenda kuendeleza ubabe kwani ikumbukwe tangia Februali 20 mwaka 2016 hawajafungwa tena Yanga na wameweza kushinda mechi tatu mfululizo na zote za mashindano Wachezaji wa Simba wakitpkea Zanzibar, leo

Mwanasoka Ghana aanzisha shirika lake la ndege

Picha
Mwanasoka wa zamani wa timu ya Sunderland ya Emgland na timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan amepatiwa kibali na serikali ya Ghana kuanzisha shirika lake la ndege. Gyan amenunua ndege aina ya Jet ambazo zitafanya safari na serikali imeamua kumruhusu mwanasoka huyo kuanzisha shirika ambalo litasimamia usafiri huo, chakushangaza, Gyan ameamua kuliita shirika hilo jina lake la utani la Baby Jet Airline. Hiyo ni hatua kubwa kufikiwa na mwanasoka huyo wa Kiafrika ambaye ameweza kuwafikia ama kuwavuka nyota wengine wa Kiafrika waliotikisa duniani Asamoah Gyan ameanzisha shirika lake la ndege

STAA WETU:

Picha
JOHN RAPHAEL BOCCO ANAWEZA KUWA MWIBA KWA YANGA KESHO. Na Prince Hoza HAYUPO katika mahesabu ya mchezo wa mahasimu Simba na Yanga unaotazamiwa kufanyika jioni ya kesho mishale ya saa 10:00 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambao unaweza kuamuliwa na matokeo ya aina mbili pekee. Mwamuzi chipukizi Elly Sasii ameshapangwa kuamua 'Derby' hiyo inayowakutanisha watoto wa Kariakoo, ni mechi ya 98 tangu miamba hiyo ikutane katika historia yao, lakini ni mechi ya nne kwa wakufunzi Mcameroon Joseph Marius Omog wa Simba na Mzambia George Lwandamina wa Yanga. Na katika mechi hizo zote, Omog ameonekana kuibuka mbabe kwa kufanikiwa kushinda mechi tatu mfululizo huku Lwandamina akitoka kapa, na mchezo wake pekee ambao unaweza kumpa ahueni ni huo wa kesho. Desemba mwaka jana miamba hiyo ilikutana katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi iliyofanyika visiwani Zanzibar katika uwanja wa Amaan, na katika mchezo huo Yanga ili

Stand United kwachafuka, kocha mkuu asimamishwa

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Baada ya kupokea vichapo mfululizo, Stand United imeamua kumsimamisha kocha wake mkuu, Athuman Bilal maarufu Bilo kwa utovu wa nidhamu, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Stand United imesema kuwa wamemsimamisha kocha wao kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Hali si shwari kwa timu hiyo yenye maskani yake mjini Shinyanga kwani hadi sasa inakamata nafasi ya 15 ikiwa ya pili kutoka mkiani, Stand United ilipokea kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya mabingwa watetezi Yanga wiki iliyopita na hadi sasa nidhamu kwa wachezaji imeshuka mpaka kumsimamisha kocha huyo. Katibu mkuu wa timu hiyo Kennedy Mwangi amedai Bilo amesimamishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja na tayari wamemwandikia barua ili aweze kujibu tuhuma zake kabla hawajatoa maamuzi mengine, kwa udadisi wa Mambo Uwanjani imegundua matokeo mabaya ndio chanzo cha kumsimamisha na huenda akafutwa kazi Stand United ilipocheza na Yanga na kufungwa mabao 4-0

KUELEKEA MPAMBANO WA WATANI, SIMBA WAMUHOFIA AJIBU

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kuelekea mpambano wa watani wa jadi Jumamosi ya keshokutwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, baadhi ya viongozi, wanachama na wapenzi wa Simba wameanza kumuhofia mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu Migomba. Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hanspoppe alisikika akisifu uwezo wa Ajibu na akawahi kusema katika kikosi cha Yanga anayemnyima usingizi ni Ajibu peke yake, wakati Hanspoppe akimlilia Ajibu, mwanachama na shabiki lialia wa Simba, Said Muchacho naye amesema Ajibu ndio anamyima raha. Na leo hii aliyekuwa mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage naye ameonyesha hisia zake kwa Ajibu akisema anaweza kuwalaza mapema ingawa Rage ameenda mbali kwa kusema Yanga si lolote kwao na watawafunga na Ajibu wao. Ajibu alikuwa mchezaji wa Simba  na tangu ajiunge na Yanga amekuwa na mwanzo mzuri ambapo mpaka sasa amekuwa akiifungia timu yake hiyo mabao muhimu, mpaka sasa Ajibu amefunga magoli matano akiwa nyuma ya kinara wa mabao Emmanu

BOCCO, MO FITI KUIVAA YANGA, JUMAMOSI

Picha
Na Mwandishi Wetu. Zanzibar Washambuliaji John Raphael Bocco "Adebayor" na Mohamed Ibrahim "Mo" sasa wako fiti na Jumamosi ijayo wataiongoza timu yao ya Simba katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya mahasimu wao Yanga, uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Simba kwa sasa wapo Zanzibar wameweka kambi kujiandaa na mchezo huo na wachezaji hao ambao walikuwa majeruhi wamepona na walianza mazoezi tangu jana na kuendelea leo na kwa mujibu wa daktari wa timu Yassin Gembe amesema wako fiti. Gembe amesema Simba itaendelea kuwakosa Shomary Kapombe, Said Mohamed Nduda na Salim Mbonde ambao ni majeruhi wa muda mrefu, kupona kwa Bocco na Mo kunaweza kukaipa ahueni kubwa Simba ambayo itajivunia uwepo wa nyota hao John Bocco yuko fiti kwa mpambano wa watani Jumamosi ijayo

Goli la tatu lasababisha kipa wa Simba kufariki dunia

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Goli la tatu na timu ya Changanyikeni dhidi ya Abajalo FC mchezo wa Ligi Daraja la pili (SDL) limesababisha kifo cha aliyekuwa mlinda mlango wa zamani wa CDA ya Dodoma, Sigara na Simba SC zote za Dar es Salaam, Rashid Omary Mahadhi (43). Kipa huyo ambaye pia kaka wa Habibu Mahadhi na Waziri Mahadhi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na kwa mujibu wa familia mazishi yanatarajia kufanyika kesho mkoani Tanga na msiba upo Kimara jijini Dar es Salaam. Rashid Mahadhi enzi za uhai wake. Taarifa za kifo chake zinasema kwamba, marehemu ambaye ni kocha msaidizi wa Abajalo FC ya Sinza ambayo ilikuwa inacheza na Changanyikeni mchezo wa Ligi Daraja la pili, ambapo timu yake ililalakwa mabao 3-0. Wakati timu yake ikifungwa goli la tatu,hali yake kiafya ilibadilika ghafla na ikabidi apelekwe katika hospitali ya Palestina iliyopo Sinza ambapo mauti yalimfika saa 7 usiku. Kipa huyo wa zamani wa Simba, ni mtoto wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu y

YANGA YAIENDEA SIMBA, MORO

Picha
Na Ikram Khamees. Morogoro Klabu bingwa ya soka Tanzania bara, Yanga SC imeingia kambini rasmi jana mjini Morogoro ikiwa tayari kabisa kuchuana na mahasimu wao Simba SC, Jumamosi ijayo uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Msemaji wa Yanga, Dissmas Ten amethibitisha kikosi hicho kuwasili jana Morogoro kikitokea Shinyanga na basi lake, hata hivyo Ten amedai wavhezaji wake watatu ambao iliwaacha Dar es Salaam kwa maana Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko nao wameungana na wenzao kambini hapo. Yanga yenye pointi 15 na mechi saba sawa na mahasimu wake Simba SC ambao wako kileleni kwa tofauti ya magoli ya kufunga, itangia uwanjani ikitaka kulipiza kisasi baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti katika mchezo wa Ngao ya Jamii uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Agosti 23 mwaka huu Kikosi cha Yanga kimeingia kambini jana mjini Morogoro

Kocha mpya Simba apata kibali cha kazi

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Hatimaye kocha mpya msaidizi wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, Masoud Djuma raia wa Burundi amepata kibali cha kufanya kazi nchini ambacho kimetolewa na idara ya uhamiaji. Djuma aliyejiunga na kikosi hicho Alhamisi iliyopita akichukua mikoba ya Jackson Mayanja aliyejiuzuru kwa matatizo ya kifamilia, alishindwa kukaa benchi na kuishia jukwaani Jumamosi iliyopita Simba ilipocheza na Njombe Mji FC uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Kocha huyo aliyewahi pia kucheza soka kama mshambuliaji akiwa na vilabu vya Rayon Sports na APR zote za Rwanda kabla hajavifundisha vyote viwili, sasa ataanza kazi rasmi Jumamosi ijayo wakati Simba ikicheza na hasimu wake Yanga uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Masoud Djuma (Wa kwanza kulia) ataanza kazi rasmi Jumamosi Simba na Yanga

MKALI FIZO AACHANA NA UKAPERA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyetamba na wimbo wake "Mapenzi ujinga", Fadhili Kimbendela "Mkali Fizo", Jumamosi iliyopita aliuaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mchumba wake, Bi Mariam Khalifa iliyofanyika nyumbani kwake Tabata Dar es salaam. MKALI FIZO (KULIA) NA MKEWE BI MARIAMU KHALIFA (KUSHOTO) WAKIWA KATIKA FURAHA ILIYOJE BAADA YA KUFUNGA NDOA Akizungumza na Mambo Uwanjani, Mkali Fizo amefurahia harusi yake hiyo na kudai mwenyezi Mungu amemjaalia mpaka kuitimiza ndoto yake ya muda mrefu. Fizo ambaye ni msanii wa bongofleva akiwa tayari ameshaachia nyimbo nne hewani, amedai kikubwa kwake anachokisubiria katika ndoa yake ni kuishi kwa amani na upendo na kupata familia bora, naye mke wa msanij huyo Bi Mariamu Khalifa amemsifu mumewe kuwa ni mume bora kwake kwani anampenda na ndio maana amekubali kuolewa naye

Mayanja ataja kikosi cha Stars kitakachoivaa Benin, Novemba 11

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Shaaban Mayanga ametangaza kikosi kamili cha timu ya taifa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa mapema mwezi ujao. Baada ya kucheza nyumbani mfululizo mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars sasa itatoka mwezi ujao kwenda nchini Benin kucheza na wenyeji Novemba 11 mwaka huu. Na leo kocha Mayanga ameita kikosi cha wachezaji 24 ambacho kitaingia kambini Novemba 5 mjini Dar es Salaam kabla ya kusafiri Novemba 9 kwenda Benin tayari kwa mchezo huo. Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo kinaundwa na makipa, Aishi Manula, (Simba SC), Peter Manyika, (Singida United) na Ramadhan Kabwili (Yanga SC), Mabeki ni Boniface Maganga, (Mbao FC), Abdi Banda, (Baroka FC, Afrika Kusini), Gardiel Michael (Yanga SC), Kevin Yondan, (Yanga SC), Nurdin Chona (Prisons), Erasto Nyoni, (Simba SC) na Dickson Job, (Mtibwa Sugar). Viungo: Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar, Kenya), Mzam

Buffon aula kikosi cha FIFA

Picha
SHIRIKISHO la soka duniani, FIFA limetangaza kikosi bora cha soka ya wanaume duniani mwaka 2017 ambapo kuna mabadiliko matatu kutoka kwa kikosi kilichotangazwa mwaka jana 2016. Kwenye kikosi hicho, maarufu kama Fifpo World xi, Mlinda mlango Gianluigi Buffon amechukua nafasi ya Manuel Neuer, naye beki wa AC Milan ya Italia, Leonardo Bonucci akachukua nafasi ya mkongwe wa Barcelona, Gerard Pique kwenye safu ya ulinzi. Mshambuliaji mpya wa PSG, Neymar Jr raia wa Brazil, ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi kwa sasa hapa duniani naye ameingia kuchukua nafasi ya Luis Suarez katika safu ya ushambuliaji ndani ya kikosi hicho bora cha ulimwengu. Hakuna hata mchezaji mmoja wa ligi ya premia (EPL) aliyefanikiwa kujumuhishwa katika kikosi hicho. KOCHA BORA DUNIANI Zinedine Zidane amemshinda meneja wa Chelsea, Antonio Conte baada ya kuiongoza Real Madrid kushinda La liga msimu uliopita kwa mara ya kwanza tangu 2012 na kushinda Ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili mfululizo. Conte alishinda

CRISTIANO RONALDO AWA MWANASOKA WA DUNIA

Picha
CRISTIANO Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka duniani, FIFA la mchezaji bora wa kiume wa kandanda mwaka huu 2017 ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo. Mchezaji huyo kutoka Ureno amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki kwa mwaka kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliyochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La liga, na Ligi ya Klabu bingwa barani Ulaya. Ronaldo alipokea tuzo yake mjini London  na aliwashukuru mashabiki wake na wa Real Madrid, wachezaji wenzake na rais wake. Tuzo kwa mchezaji bora mwanamke ilinyakuliwa na mchezaji wa Uholanzi Lieke Martiens, anayeichezea Barcelona, Martiens aliwahi pia kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi iliposhinda mashindano ya Euro 2017 Cristiano Ronaldo mshindi wa Ballon D' Or

Simba yatangulia Zenji kuifanyia ukatiri Yanga

Picha
Na Mwandishi Wetu. Zanzibar Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC leo asubuhi wameelekea visiwani Unguja kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na pambano la mahasimu litakalofanyika Jumamosi ijayo uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara amesema, Simba imewasili Zanzibar mapema na itakaa huko kwa juma moja kabla ya kucheza na mtani wake Yanga mchezo wa Ligi Kuu Bara, vinara hao waliishinda Njombe Mji mabao 4-0 Junamosi iliyopita. Huo utakuwa mchezo wao wa tatu mwaka huu kukutana mahasimu hao na mara mbili Simba imeibuka mbabe, mara moja ikishinda 2-1 uwanja wa Taifa mchezo wa marudio wa Ligi Kuu bara na maya ya pili mchezo wa Ngao ya Jamii, Simba pia ikishinda kwa penalti 5-4 baada ya sare tasa 0-0 dakika tisini za mchezo Simba wakiingia Unguja

Yanga yazaliwa upya, Manji awatisha Simba

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kuelekea mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaofanyika Jumamosi ijayo uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mabingwa watetezi Yanga SC wanaingia katika mchezo huo wakiwa na ari na kasi mpya hasa baada ya aliyekuwa mwenyekiti wao na mfadhili mkuu, bilionea Yusuf Manji kuungana na wachezaji wa kikosi hicho na akiwaahidi neema endapo watashinda mechi zao zote za mzunguko wa kwanza ukiwemo dhidi ya Simba. Manji amewaambia wachezaji hao kuwa yeye ni Mwanayanga na anahitaji furaha hivyo wapambane walete ushindi Jumamosi ijayo watakapoumana. Kibopa huyo aliyefutiwa kesi zake zote mbili, kwa sasa yuko huru na amejitolea kuwalipa mishahara wachezaji wote na wale wanaoidai klabu hiyo huku akisema bado yupo Yanga, hayo ni maneno ya kuudhi kwa wapenzi wa Simba. Yusuf Manji alipowatembelea wachezaji wa Yanga hivi karibuni

KISPOTI:

Picha
SIKUBALIANI NA LIGI KUU KUWA NA TIMU 20 MSIMU UJAO. Na Prince Hoza KWANZA kabisa nianze kwa kuupongeza uongozi mpya wa Bodi ya Ligi (TPLB) uliochaguliwa Oktoba 15 mwaka huu, pongezi sana Kaimu mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Andrew Sanga kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Bodi hiyo. Lakini pia shukrani zangu nyingine nazielekeza kwa makamu mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Shani Christoms Mrigo pamoja na wajumbe waliochaguliwa kuunda kamati ya Bodi hiyo ambayo itakuwa ikisimamia kutoa maamuzi mbalimbali yanayohusu ligi. Ikumbukwe Bodi ya Ligi inasimamia Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL), Ligi Daraja la kwanza Tanzania bara (FDL) na Ligi Daraja la pili Tanzania bara (SDL). Kupatikana kwa uongozi huo mpya wa Bodi ya Ligi kunakamilisha mchakato mzima wa uchaguzi na pia kunadhihirisha sasa kuwa mambo mapya yanaanza, tayari Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) limeshapata viongozi wake wapya baada ya Jamal Malinzi na wenzake kukamilika kwa kipindi chao cha uongozi. TFF ilipata

Yanga yaijibu Simba, nayo yaigonga Stand United 4-0

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga SC jioni ya leo wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, ushindi huo ni majibu kwa mahasimu wao Simba ambao jana waliichapa Njombe Mji FC magoli 4-0 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Simba na Yanga zitaumana Jumamosi ijayo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara hivyo kila timu imejaribu kushinda kwa kumtumia salamu mwenzie. Ibrahim Ajibu Migomba alikuwa mwiba kwa vijana wa Stand United akifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kuifanya Yanga iende mapumziko ikiwa vinara, kipindi cha pili Yanga waliongeza mabao mengine mawili, Pius Buswita akifunga la tatu na Mzambia Obrey Chirwa akiongeza la nne. Kwa matokeo hayo Yanga inafikisha pointi 15 sawa na Simba lakini inaangukia nafasi ya pili na kuishusha Mtibwa Sugar, Yanga sasa inakamata nafasi hiyo kwa wingi wa mabao dhidi ya Mtibwa

BAADA YA GEORGE WEAH KUSHINDA URAIS LIBERIA, ATHUMAN CHINA NAYE KUWANIA URAIS TANZANIA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mwanasoka wa zamani nchini, Athuman China ambaye aliwahi kuzichezea Yanga na Simba pamoja na Taifa Stars anayeishi nchini Uingereza ametangaza azma yake ya kugombea urais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa nyakati zijazo. China anafuata nyayo za mkongwe Leodegar Tenga ambaye amewahi kuliongoza shirikisho hilo, Tenga naye aliwahi kuzichezea kwa nyakati tofauti, Yanga, Pan Africans na timu ya taifa. Akizungumza kutoka Uingereza, China amesema nia yake kuja kuukomboa mpira wa Tanzania ambao unazidi kudidimia, kiungo huyo wa zamani aliyetamba vilivyo amesema watu wa mpira kama yeye ndio watakaoweza kuuokoa Athuman China (wa katikati aliyeshika kiuno)

Yanga na Stand ni kufa au kupona, Ajibu kuongoza safu ya ushambuliaji

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Leo ndio leo katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga wenyeji Stand United wakiikaribisha Yanga SC mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Yanga leo itamtegemea zaidi mshambuliaji wake Ibrahim Ajibu (Aliyeshikilia jezi namba 10) hasa baada ya kuwaacha Dar es Salaam mastaa wake watatu, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko. Msimu uliopita katika uwanja huo huo wa Kambarage timu hizo zilipokutana Stand ilishinda bao 1-0 hivyo leo ni zamu ya Yanga kushinda ama laah. Yanga iliwasili Shinyanga juzi ikitokea Tabora ambako ilicheza mechi ya kirafiki na Rhino Rangers na kulazimishwa sare tasa ya 0-0 lakini ilichezesha kikosi cha pili Ibrahim Ajibu aliyeshikilia jezi namba kumi, ataongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga leo

Matokeo yote ya VPL leo hii, haya hapa

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam. Simba SC 4 Njombe Mji FC 0, (Uhuru Stadium Dar es Salaam).  Ndanda FC 0 Singida United 0, (Nangwanda Sijaona, Mtwara),  Mbao FC 0 Azam FC 0, (CCM Kirumba, Mwanza)  Mtibwa Sugar 1 Tanzania Prisons 0 (Manungu Complex, Morogoro)  Lipuli Fc 1 Majimaji Songea 0, (Samora Stadium, Iringa)  Mbeya City 2 Ruvu Shooting 0 (Sokoine Stadium, Mbeya)  Kesho Jumapili Stand United vs Yanga SC (CCM Kambarage, Shinyanga) Wachezaji wa Azam FC wakipasha kabla ya kuingia mchezoni

SIMBA YAITUMIA SALAMU YANGA, YAIGONGA NJOMBE 4-0

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Simba SC jioni ya leo imewatumia salamu mahasimu wao wakuu Yanga SC, baada ya kuilaza Njombe Mji FC mabao 4-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Ushindi huo mkubwa unazidi kuisogeza zaidi kileleni kwa kufikisha pointi 15 na mabao ya kufunga 17 huku mshambuliaji wake Emmanuel Okwi ambaye leo ametupia goli moja na kuseti mawili akizidi kuongoza kwa kufunga mabao manane. Simba leo ilicheza vizuri kwa maelewano makubwa na kufanikiwa kupata bao moja hadi filimbi ya kuelekea mapumziko ilipopulizwa, kipindi cha Simba ilirejea na makali zaidi ikifanikiwa kufunga magoli matatu na kuondoka na pointi tatu muhimu. Magoli mengine ya Wekundu hao wa Msimbazi, yalifungwa na Muzamir Yassin (mawili) na Laudit Mavugo aliyemalizia goli la nne, kikosi hicho cha Simba kesho kitaelekea Zanzibar kuweka kambi kujiandaa na mpambano wa watani dhidi ya Yanga, Jumamosi ijayo Emmanuel Okwi ameiongoza vema Simba leo katika ushin

YANGA KUUTUMIA UWANJA WAKE WA KAUNDA MSIMU UJAO

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Yanga SC imepanga kuutumia uwanja wake wa Kaunda ifikapo msimu ujao kwa mechi mbalimbali za kirafiki na mashindano. Pia imebainika kwamba mjumbe mmoja wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe bayana kwakuwa si msemaji wa klabu, ameiambia Mambo Uwanjani kuwa maendeleo makubwa ya uwekezaji yanayofanyika sasa, yanaupa hadhi uwanja huo wa Kaunda. Na msimu ujao Yanga itautumia uwanja huo kwa mazoezi na mechi za kirafiki, lakini pia timu za madaraja mengine kama Daraja la kwanza, daraja la pili na daraja la tatu zitaumia kwa mashindano. Uwanja wa Kaunda upo katika marekebisho makubwa ili utumike msimu ujao

Bocco kuikosa Njombe Mji

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba SC leo wataendelea kumkosa straika wake hatari John Bocco 'Adebayor' ambaye ana maumivu na atakaa nje kwa wiki moja, taarifa iliyotolewa na msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara hivi karibuni imesema straika huyo atakaa nje. Simba inakutana na Njombe Mji jioni ya leo ya leo katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kukosekana kwa straika huyo kunafifisha ndoto za vinara hao kuendelea kukaa kileleni kwani kama itateleza kwa kutoka sare tena ama kufungwa basi itaondolewa kileleni. Katika siku za hivi karibuni Simba imekuwa ikipata ushindi mwembamba kutokana na washambuliaji kushindwa kuzitumia vema nafasi John Bocco atakosekana katika mchezo wa leo

Ligi Kuu Bara mechi sita kupigwa leo

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Leo Jumamosi ya Oktoba 21, 2017 Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea kwa mechi sita kupigwa viwanja tofauti. Mbao FC vs Azam FC, (CCM Kirumba, Mwanza) Lipuli FC vs Majimaji Songea, (Samora Stadium, Iringa) Mbeya City FC vs Ruvu Shooting, (Sokoine Memoriel Stadium, Mbeya) Ndanda FC vs Singida United, (Nangwanda Sijaona, Mtwara) Simba SC vs Njombe Mji FC, (Uhuru Stadium, Dar es Salaam) Mtibwa Sugar vs Tanzania Prisons, (Manungu Complex, Morogoro) Jumapili Oktoba 22, 2017 Stand United vs Yanga SC, (CCM Kambarage, Shinyanga) Ligi Kuu kuendelea leo

Jeshi la Simba kamili gado kuiangamiza Njombe Mji kesho

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC kesho wanashuka uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuumana na Njombe Mji FC ya mkoani Njombe mchezo unaotazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua. Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kesho jeshi la Simba litaendeleza mauaji yake kama kawaida na wala hakutakuwa na sare ama kupoteza mchezo. Manara amedai ujio wa Mrundi, Masudi Juma ambaye amekuja kuchukua mikoba ya Jackson Mayanja aliyejiuzuru juzi, inaipa jeuri Simba kushinda mchezo huo wa kesho, Simba ikimaliza mchezo huo itaelekea Zanzibar ambapo inaenda kuweka kambi kujiandaa na mpambano wa watani dhidi ya Yanga SC Wachezaji wa Simba wakimalizia proglamu ya mwisho, kesho wanaivaa Njombe Mji

Kagera Sugar yanusurika kichapo kwa Mwadui

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Timu ya Kagera Sugar inayonolewa na kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita wa 2016/17, Mecky Mexime jioni ya leo imenusurika kipigo toka kwa wenyeji wao Mwadui FC ya bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu bara uliofanyika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga. Mwadui walitangulia kupata bao lililofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Poul Nonga aliyeunganisha krosi ya Malika Ndeule na kumpita kirahisi kipa mkongwe Juma Kaseja. Vijana wa Kagera Sugar walionyesha hasira ya kutaka kusawazisha goli hilo lakini iliwachukua hadi kipindi cha pili dakika ya 87 iliposawazisha bao kupitia kwa Jaffari Salum Kibaya ambaye alitumia vema makosa ya beki wa Mwadui, David Luhende. Kwa matokeo hayo sasa Kagera wanafikisha pointi tatu bado wanaendelea kubaki mkiani huku hatma ya kocha wao Mecky Mexime iko shakani na inawezekana naye akaondoshwa mapema Kagera Sugar wakipongezana baada ya kupata bao

Tutaisimamisha Simba kesho, asema kocha wa Njombe Mji

Picha
Na Ikram Khamees. Mlandizi Kaimu kocha mkuu wa timu ya Njombe Mji, Mrage Kabange amesema vijana wake wataingia uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kesho kwa kazi moja tu ya kuisimamisha Simba katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Njombe Mji tangu ilipomtimua kocha wake mkuu Hassan Banyai, haijapoteza mchezo wowote na kesho imepania kuondoka na pointi, Kabange amesema anaijua vizuri Simba hivyo kazi yake itakuwa moja tu, kuizuia. Njombe Mji wameweka kambi yao Mlandizi mkoani Pwani, lakini kesho watachuana na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC mchezo ambao utatoa mwelekeo wa vilabu vyote viwili. Kocha msaidizi wa Simba Mganda Jackson Mayanja alibwaga manyanga juzi Jumatano na nafasi yake ilichukuliwa na Mrundi, Masudi Juma ambaye zamani alikuwa akiinoa Rayon Sports ya Rwanda,  kwa maana hiyo mechi hiyo itakuwa na rekodi za kipekee kwa timu zotembili Kikosi cha Njombe Mji ambacho kesho kitaumana na Simba

STAA WETU:

Picha
IBRAHIM CLASS. MTANZANIA WA KWANZA KUTWAA UBINGWA WA NDONDI WA GBC WA DUNIA. Na Prince Hoza NAKUMBUKA kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilipata mapokezi makubwa wakati kilipowasili nchini kikitokea Afrika Kusini ambako kilienda kushiriki michuano ya COSAFA Castle Cup. Taifa Stars ilikamata nafasi ya tatu ambapo ilitunukiwa medali ya shaba na kitita cha fedha, Dola 10,000 za Kimarekani, Stars ililakiwa na waziri wa habari, michezo, sanaa na utamaduni, Dk Harrison Mwakyembe kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Mwl Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. Na pia aliweza kuzungumza na wachezaji wa timu hiyo akiwapongeza kwa hatua hiyo waliyofikia huku pia akiwataka waongeze bidii na waweze kuishinda Rwanda katika mchezo wao uliofuata wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani, maarufu CHAN. Mwakyembe amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha timu yetu ya taifa inafanya vizuri kwani hiyo si mara yake ya kwanza, alishafanya hivyo mara kadhaa z

LIGI KUU KUENDELEA TENA KESHO, MWADUI NA KAGERA KAZI IPO

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Kesho Ijumaa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inaendelea tena kwa mchezo mmoja tu utakaozikutanisha Mwadui FC na Kagera Sugar katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga. Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi ambapo Mbao FC vs Azam FC, CCM Kirumba Mwanza, Lipuli vs Majimaji Songea, Samora Stadium, Iringa, ilihali Ruvu Shooting vs Mbeya City, Sokoine, Mbeya na Simba vs Njombe Mji uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Ndanda FC vs Singida United, Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Mtibwa Sugar vs Tanzania Prisons, Manungu Complex Morogoro. Wakati Jumapili Stand United vs Yanga SC, CCM Kambarage  mjini Shinyanga, Simba ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 12 wakifuatiwa na Mtibwa Sugar, Yanga na Azam zote hizo zina pointi 12 Mwadui FC kesho wataumana na Kagera Sugar

MRITHI WA MAYANJA AWASILI MSIMBAZI

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Hatimaye mrithi wa Jackson Mayanja ambaye alikuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba amewasili nchini tayari kabisa kujiunga na machampion hao wa kombe la FA na Ngao ya Jamii, Simba SC. Masudi Juma mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Burundi na kocha mkuu wa Rayon Sports ametua na ameshafanya mazungumzo na uongozi wa Simba na muda wowote kuanzia sasa anamwaga wino kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo akisaidiana na Mcameroon, Joseph Omog. Kocha huyo amewasili katika uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere mapema leo na amefurahi kuja kufanya kazi katika klabu hiyo akisema Simba ni klabu kubwa barani Afrika hivyo anajiona ni mtu muhimu sana. Aidha kocha huyo amedai amekuja kuipa mataji Simba ambayo mpaka sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 12 ikicheza mechi sita Masudi Juma kocha msaidizi mpya wa Simba Masudi Juma akitua Mwl Nyerere International leo