Machapisho

Rekodi ya Peter Shalulile kuvunjwa Ligi Kuu Afrika Kusini

Picha
Kocha wa Stellenbosch FC, Gavin Hunt, amethibitisha kuwa mshambuliaji Bradley Grobler analenga kuvunja rekodi ya ufungaji mabao katika historia ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL). Grobler mwenye umri wa miaka 38, anahitaji kufunga mabao manne pekee ili kufikia rekodi ya mabao 134 iliyowekwa na Peter Shalulile. Gavin Hunt alisema: “Ni wazi kuwa analenga rekodi hiyo, nasi tunatumaini kumsaidia kuifikia. Anatuhitaji, nasi tunamhitaji.”

Spika wa Bunge amaliza bifu la MO Dewji na Haji Manara, sasa njia nyeupe kurudi Simba

Picha
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, akimtania Diwani wa Kata ya Kariakoo, Mhe. Haji Manara , kuchukua jukumu la kumaliza mgogoro wake na Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), baada ya Manara kufanikiwa kumaliza uhasama wa miaka 31 kati ya Madrasa mbili za Kariakoo. Zungu ameyasema hayo wakati wa hadhara ya Maulid iliyofanyika Msikiti wa Manyema, Ijumaa Oktoba 16, 2026, Jijini Dar es Salaam, huku akidai anaamini Manara ni Mwanasimba hasa na kuwa huko alipo sasa Yanga sio kwa Manara. .

Yanga yaamkia Ligi ya mabingwa

Picha
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika Dar Young Africans maarufu Yanga SC, jioni ya leo wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CFFA FC ya Madagascar raundi ya kwanza michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika. Mchezo huo wa mkondo wa kwanza ulifanyika ugenini ulishuhudiwa Yanga ikipata magoli yote manne ya ‘Wananchi’ wakiwa ugenini Azam Complex, Chamazi; wafungaji ni Cheikh Toure, Albert Kangwanda, Mudathir Yahya na Maxi Nzengeli.

Kocha msaidizi Kagera Sugar afariki

Picha
Uongozi wa klabu ya Pamba Jiji FC umetangaza kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Themi Felix, kilichotokea leo katika Hospitali ya Bugando alipokuwa akipatiwa matibabu. Kupitia taarifa yake ya leo Oktoba 17, 2026 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Pamba Jiji FC, ametoa pole kwa familia, ndugu, na mashabiki wote huku akieleza kuwa kifo chake ni pigo kubwa na pengo lisilozibika kwa klabu hiyo na soka kwa ujumla kutokana na mchango, weledi, na jitihada zake. Aidha uongozi wa klabu hiyo umeeleza kuwa taratibu za msiba na mazishi zitatangazwa baada ya kukutana na familia ya marehemu huku akiwaomba mashabiki, wadau, na wote walioguswa na msiba huo kuwa watulivu na kuiombea familia ya marehemu nguvu na uvumilivu.

Manqoba aanza visingizio kuhusu kipigo cha Simba

Picha
kocha mkuu wa Young Africans MANQOBA, anadai kuwa kama wachezaji wake wasingepigwa kadi nyekundu kwenye mechi za nyuma, pamoja na kuwa na majeraha, Simba walikuwa ni wachache sana. Anadai kuwa Aziz Ki hakuwa kwenye mfumo, Selemani Mwalimu hakuwa kwenye mfumo pia. Hata Yao Yao pia alicheza, ila kipindi cha pili alipotoka, pengo liliweza kuonekana. Anasema ubaya wa mchezo huu, tulitawala dakika za mwanzo tu, ila kipindi cha pili sababu zangu hazikwenda sawa. “Mchezaji kama Chuga Boy ni mchezaji mdogo sana kiasi kwamba alipata presha ya mchezo, jambo ambalo lilipelekea kuanza kulinda kuliko kushambulia. Mchezo umekamilika, lakini matokeo hayajanipa ushawishi kabisa. Tusubiri mechi zinazofuata, nitafanya makubwa zaidi. Asante.” — Kocha wa Young Africans, Manqoba Mngqithi

Yanga kutupa karata yake leo

Picha
​Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Young Africans SC (Yanga SC), wanatupa karata yao muhimu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League) kwa kuvaana na CFFA kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Raundi ya Pili ya Kufuzu leo hii majira ya saa 9:00 alasiri (15:00). ​Wananchi wanaingia kwenye mchezo huu ugenini wakisaka matokeo mazuri yatakayowaweka kwenye nafasi nzuri na kuwapunguzia presha kuelekea mchezo wa marudiano. Kikosi hicho kinaingia uwanjani kikiwa na maandalizi kabambe pamoja na hamasa kubwa ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika. ​Baada ya kupepetana katika mchezo wa leo, miamba hiyo miwili itarudiana tena katika mzunguko wa pili utakaopigwa siku ya Jumatano, Oktoba 21, majira ya saa 1:00 usiku (19:00) ili kumpata mshindi atakayesonga mbele.

Daudi Kanuti afariki dunia

Picha
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Lameck Nyambaya ametangaza kwa masikitiko kifo cha kiongozi mwenzao Mzee Daudi Kanuti, kilichotokea usiku wa Oktoba 17, 2026. Marehemu Mzee Daudi Kanuti alikuwa mtumishi wa DRFA kutoka Ofisi ya Sekretarieti, na pia alikuwa akihudumu kama Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ilala (IDFA). Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 17, 2026 na Ofisi ya Mwenyekiti ya DRFA imeeleza kuwa, enzi za uhai wake, marehemu alikuwa kiongozi, baba, na mlezi wa karibu na kueleza kuwa “Mchango wake mkubwa katika utumishi wa DRFA na maendeleo ya soka kwa ujumla utabaki kuwa kumbukumbu ya kudumu ya daima.” Taarifa zaidi kuhusu ratiba ya mazishi na taratibu nyingine za msiba huu zitatolewa rasmi kadri zitakavyopatikana kutoka kwa familia na uongozi wa DRFA.