Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2015

SIMBA YAJIAPIZA KUIBOMOA NDANDA LEO

Picha
MABINGWA wa soka wa kombe la Mapinuduzi Simba SC leo jioni inashuka kwenye uwanja wa Nangwanda sijaona mjini Mtwara kukabiliana vikali na wenyeji wao Ndanda FC 'wana kuchele' timu ambayo imeipania vilivyo Simba. Uongozi wa Simba kupitia kwa msemaji wake Humphrey Nyosia umetamba kuwa ni lazima Simba iifunge Ndanda lakini kuhusu idadi ya magoli hiyo itajulikana uwanjani, akiongea na mtandao huu leo, Nyosia amesema kikosi cha Simba kimeimarika na kinaweza kushinda katika mchezo huo kwani wapinzani wao hawana ubavu hata kidogo.

Equatorial Guinea walenga Kombe la Dunia

Picha
Esteban Becker Kocha mwenye ndoto kubwa wa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Equatorial Guinea, Esteban Becker amehimiza vijana wake watumie dimba hilo kama ngazi ya kufuzu Kombe la Dunia. Becker wa kutoka Argentina ambaye alichukua utawala wa Nzalang Nacional mapema mwezi huu, amekuwa na majuma mawili pekee kuandaa kikosi chake kujitosa uwanjani nyumbani wakati shindano hilo litakapongoa nanga Jumamosi dhidi ya Congo Brazzaville jijini Bata kwenye Kundi A. Ingawa kufuzu robo fainali ya awamu ya 2012 wakati nchi hiyo iliandaa kwa pamoja na Gabon ni lengo mufti, Becker anatizama mbele zaidi na azima yake ya kuwaongoza kuingia Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kwenye historia yao. “Naota kila wakati kushiriki Kombe la Dunia kwa hivyo bidii zangu zote zitaelekezwa kutayarisha kikosi chetu changa kuwa na nafasi ya kuwania tiketi ya kucheza dimba hilo lijalo la 2018,” Becker ambaye aliongoza

AFCON kuanza leo Equatorial Guinea

Picha
Timu kutoka kote Afrika zimewasili nchini Equatorial Guinea wakati ambapo mechi za taifa bingwa barani zitarajiwa kung'oa nanga hii leo ikiwa ni miezi miwili tangu taifa hilo la afrika ya kati likubali kuandaa mechi hizo. Morocco ndiyo iliyokuwa iandae kombe hilo lakini badala yake ikaomba kuahirishwa kwake kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.

LIGI KUU BARA KIVUMBI NA JASHO LEO, SIMBA, YANGA AU AZAM KUCHEKA?

Picha
BAADA ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, sasa kazi inarejea kwenye. Ligi Kuu Bara.Michuano ya wiki ya Kombe la Mapinduzi mjini Zanzibar tayari imepata mbabe wake, Simba na kombe liko jijini Dar es Salaam. Vita ya vinara Mtibwa Sugar, Azam, Yanga na Simba ambao wote wana viporo katika michuano ya ligi kuu, kutokana na kuwepo katika ushiriki wa michuano ya Mapinduzi, lakini wikiendi hii- leo na kesho wanaendelea kumsaka mwali wa Ligi Kuu Bara ambaye anahifadhiwa na Azam FC. Kila upande una hofu, inajulikana kwa kuwa matokeo hayana uhakika. Mechi za mwisho zinaonyesha Yanga na Azam waliambulia sare, hali kadhalika Mtibwa Sugar wakati Simba walikutana na kichapo.

WAJERUMANI WASIKITISHWA NA BALLON D'OR

Picha
Manuel Neuer Wajerumani, waliotumai wangefagia tuzo za Fifa na kubeba Ballon D'Or, walieleza masikitiko yao Jumanne baada ya kipa wao aliyeshinda Kombe la Dunia Manuel Neuer kuibuka wa tatu katika matokeo ya mchezaji bora wa mwaka duniani wa mwaka 2014. Mreno Cristiano Ronaldo alishinda tuzo hiyo kwa mara ya pili mtawalia Jumatatu na mara ya tatu kwa jumla. Fowadi huyo wa Real Madrid alipata kura maradufu kumshinda mpinzani wake wa jadi aliyeshinda tuzo hiyo mara nne Lionel Messi, ambaye alimpiku pembamba kipa wa Bayern Munich Neuer aliyemaliza wa tatu. Neuer, aliyewika sana katika Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka jana na pia alisaidia Bayern kushinda ligi na kombe nyumbani, amefungwa mabao manne pekee katika mechi 17 alizocheza ligini msimu huu.

GRANT NUSURA AMTIMUE AYEW

Picha
Dede Ayew  Avram Grant alikuwa nusura amtimue kiungo wa kati kutoka wa Ghana Andre Ayew kutoka kwa kambi ya timu hiyo nchini Uhispania. Kisa hicho, kilichofanyika wiki jana, kilipelekea bosi huyo wa Ghana wa miaka 59 kuanzisha shughuli ya kumfukuza mchezaji huyo kutoka Seville baada ya nyota huyo wa klabu ya Marseille kufika kambini akiwa amechelewa. Lakini naibu mwenyekiti wa kamati simamizi ya Black Stars, Kudjoe Fianoo, aliingilia kati na kumsihi kubadilisha uamuzi wake. “Mimi na [mwenyekiti wa kamati] George Afriyie tulilazimika kuingilia kati na kuomba radhi kwa niaba ya Andre Ayew kwa kufika kambini akiwa amechelewa kwa sababu Avram Grant alikuwa amekasirishwa sana na mchezaji huyo kufika Uhispania akwia amechelewa,” afisa huyo aliambia Happy FM mjini Accra.

PLUIJM APONDA MASTRAIKA WACHOYO YANGA

Picha
Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amewajia juu washambuliaji wa timu hiyo kutokana na kukosa magoli mengi na amewataka kuacha uchoyo baina yao kwa manufaa ya timu. Licha ya kushinda kwa idadi kubwa ya mabao (4-0) katika mechi zao mbili za kwanza za Kombe la Mapinduzi, wachezaji wa Yanga walikuwa wakikosa magoli mengi ambayo yangeweza kuwafanya kupata ushindi mnono zaidi. Yanga ilitolewa katika robo fainali ya mashindano hayo maalum ya kuadhimisha Mapinduzi ya Zanzibar kwa goli 1-0 la dakika za lalasalama la JKU ya Zanzibar huku miamba hao wa soka wa Tanzania Bara wakiwa tayari wamekosa magoli mengi kupitia kwa washambuliaji wao Amisi Tambwe na Kpah Sherman.

HAKUNA KAMA SIMBA TANZANIA

Picha
Timu ya Simba Sc imeibuka kidedea kwa kutwaa kombe la mapinduzi kwa mikwaju 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo ulipigwa kwenye dimba la Amaani Visiwani Zanzibar. Dakika tisini za mchezo za kawaida zilimalizika kwa timu hizi kwenda sululu ya bila kufungana ndipo changamoto ya mikwaju ya penati ikafuata . Penati za simba zilifugwa na Awadh Juma, Hassan Kessy, Hassan Isihaka na Dan Ssenrukuma wakati ya Shaaban Kisiga iliokolewa na Kipa Said Mohamed.

YAYA TOURE MCHEZAJI BORA AFRIKA

Picha
Kiungo wa Manchester City Yaya Toure amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya CAF ya mchezaji bora Afrika kwa mara ya nne mfululizo.

KOPUNOVIC AAHIDI KUTINGA FAINALI LEO NA POLISI ZANZIBAR

Picha
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema kikosi chake kimeimarika na kinampa matumaini ya kushinda mechi yao ya leo ya nusu-fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Polisi na kutinga fainali ya michuano hiyo. Mechi hiyo itatanguliwa na mechi ya nusu-fainali ya kwanza ya Mtibwa Sugar dhidi ya wababe wa Yanga, timu ya JKU, mechi zote zikichezwa kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa saa 10:00 jioni na saa 2:15 usiku. Goran alisema visiwani hapa jana kuwa: “Kikosi chetu kinazidi kuimarika, jana (juzi) tulianza mazoezi maalum kwa ajili ya mechi ya nusu-fainali na ninaona tuko katika hali nzuri." "Kuna vijana wazuri nimewakuta kikosini, ninaamini tutafanya vizuri na kusonga mbele,:" alisema zaidi Mserbia huyo. Simba ilifanikiwa kutinga nusu-fainali ikiiadhibu kwa kipigo hicho kikali timu ya Daraja la Pili visiwani hapa Taifa ya Jang'ombe katika mechi yao ya robo-fainali Jumatano, shukrani kwa mabao ya kiungo mshambuliaji Ibrahim Hajibu aliyepiga 'hat-trick' daki

KASEJA AWAAMBIA YANGA MSINITANIE MIMI BADO JANGWANI.

Picha
Mlinda mlango Juma Kaseja ameshtushwa na habari za kutimuliwa kwake na Yanga na kudai yeye hatambui maamuzi hayo kwani yametolewa nje ya muda muafaka wa usajili pili hajapewa barua ya kufukuzwa kwake. Kaseja amesema yeye bado mchezaji halali wa Yanga na hatambui suala la kutimuliwa kwake. Juzi uongozi wa Yanga ulitangaza kuachana na mlinda mlango Juma Kaseja kwa madai hajaripoti kwenye kituo chake cha kazi kwa muda mrefu na hajulikani halipo.

RWANDA YAJA KUIFUNZA STARS MABORESHO NAJUARI 22 MWANZA

Picha
Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN).

SIMBA KUVAANA NA TAIFA JANG'OMBE ILIYOSHINDA KWA SHILINGI

Picha
Wapinzani wa Simba katika hatua ya robo-fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani hapa wamepatikana kwa kurusha shilingi baada ya timu mbili za Kundi A, Polisi na Taifa ya Jang'ombe kumaliza katika nafasi moja. Polisi, wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka huu, na Taifa ya Jang'ombe jana walimaliza mechi zao za hatua ya makundi wakitoka suluhu kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung visiwani hapa. Matokeo hayo yaliwafanya wote wamalize nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi A linaloongozwa na Yanga wakiwa wamefanana kwa kila kitu baada ya wote kufungwa 4-0 dhidi ya Yanga kisha wote kuifunga Shaba FC ya Pemba bao 1-0.

KAVUMBAGU AIHOFIA MTIBWA SUGAR

Picha
Na Mwandishi wetu, Zanzibar Mshambuliaji Didier Kavumbagu wa Azam FC amesema timu za Yanga, Mtibwa Sugar na KCCA ya Uganda ndizo ziwapa wakati mgumu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar mwaka huu. Akizungumza na jijini hapa, Kavumbagu alisema timu hizo zinatisha. "Yanga, KCCA na Mtibwa wako vizuri, si timu za kutamani ukutane nazo katika michuano hii. Yanga wameimarika, Mtibwa bado wako katika kiwango chao cha Ligi Kuu. Hii timu kutoka Uganda inacheza kwa ushirikiano sana," alisema Kavumbagu. Mrundi huyo alitamba akiwa na Yanga, lakini aliruhusiwa kuondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake na akatua bure Azam.

PLUIJM ATAMBA KUREJESHA KIWANGO CHA NGASSA

Picha
Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema winga Mrisho Ngasa ameshuka kiwango lakini atarejea katika makali yake muda si mrefu kwa sababu winga huyo ni "mchezaji mwenye akili nyingi". Akizungumza jana visiwani hapa jana, Pluijm alisema tangu arejee nchini Desemba kuinoa timu hiyo ya Jangwani baada ya kutimuliwa kwa Mbrazil Marcio Maximo, amekuwa akimwacha benchi mchezaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar, Toto African, Simba na Azam FC kutokana na kushuka kiwango. "Ni kweli Ngasa ameshuka kiwango ndiyo maana akacheza dakika saba tu katika mechi yetu dhidi ya Azam na hapa Zanzibar anacheza dakika chache pia. Azam ni timu nzuri ambayo unapaswa kuwa na mbinu za uhakika kabla ya kuingia uwanjani kuikabili.