Kipre Tchetche kurejea Azam FC
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Brice Herman Tchetche muda wowote kuanzia sasa anakuwa mchezaji mpya wa Azam Fc baada ya makubaliano kati ya Azam Fc na klabu anayoitumikia kwa sasa ya Terengganu Fc ya Malaysia.
Taarifa za kurejea Tchetche katika kikosi cha Azam Fc ni baada ya mmoja kati ya wakurugenzi wa timu hiyo, Yusuf Bakhresa kuelekea Malaysia na kukutana na viongozi wa Terrengganu Fc ambapo wameonesha kukubali kumwachia.
Mchezaji huyo amebakiza mkataba wa miezi mitatu hivyo haitaizuia Azam Fc kumrejesha nyumbani mshambuliaji huyo aliyejiunga na Azam Fc akitokea timu ya taifa ya vijana ya Ivory Coast iliyokuja nchini kushiriki michuano ya Chalenji