GARDIEL MICHAEL AAGANA NA UKAPELA
Na Mwandishi Wetu. Tanga
Beki wa kushoto wa wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga SC, Gardiel Michael Mbaga amefunga ndoa na aliyekuwa mchumba wake Lovenes Haroun katika kanisa la Luthelen la usharika wa Kana jijini Tanga.
Gardiel sasa anaachana na klabu ya ukapela na kuwa mwanandoa, pia anaondoa fununu kuwa in miongoni mwa wachezaji walioweka mgomo katika klabu ya Yanga kama inavgosemekana kuwa wachezaji karibu wote wamegoma.