Kakule ruksa Simba
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Uongozi wa klabu ya soka ya Kiyovu Sports Club ya Rwanda imeridhia kiungo wake raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania Bars Simba SC.
Awali klabu hiyo iliweka mgomo nyota wake huyo kujiunga na Simba kwa madai hawajafanya naye mazungumzo yoyote, lakini mchezaji huyo baada ya kufaulu majaribio yake katika klabu ya Simba alifunga safari ya Rwanda kuteta na viongozi wake.
Kakule alifaulu majaribio katika mazoezi ya klabu ya Simba yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam , kocha msaidizi wa klabu hiyo Mrundi, Irambona Masoud Djuma ameridhishwa na kiwango cha kiungo huyo na kuwataka mabosi wake kumpa mkataba, Djuma alidai kiungo huyo ataisaidia sana Simba katika michuano ya kimataifa na ligi