Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2015

BRAZIL YALIPIZA KISASI KWA UFARANSA, YAIDUNGUA 3-1

Picha
Brazili jana aliikimbiza mchamchaka Ufaransa baada ya kuichabanga magoli matatu kwa moja. Haikuwasaidia Ufaransa kuanza kuona lango la Brazil katika dakika ya 21 kwa goli lililofungwa na Raphael Varane kwani ni kama waliichokoza kundi la nyuki kwani goli hilo lilirudishwa na Oscar dos Santos Emboaba Júnior katika dakika ya 40, na hatimaye kushindiliwa magoli mengine mawili kupitia kwa Neymar da Silva Santos, Júnior, na Luiz Gustavo na hivyo hadi mechi hiyo inamalizika Brazil 3 Ufaransa 1.

OZIL AITAMANI TUZO YA RONALDO

Picha
Kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil amesema miaka ijayo anaamini atashinda tuzo ya Ballon d’or na jinsi wachambuzi wanavyozidi kumkosoa ndiyo anapata nguvu ya kujituma zaidi. Mjerumani huyo ameichezea Arsenal mechi 14 tu katika ligi kuu msimu huu kufuatia kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha lakini tangu arudi tena uwanjani amekuwa katika kiwango bora. Mchezaji huyo aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea Real Madrid anaonekana kuizoea ligi ya Uingereza tofauti na hapo awali. “Nikiendelea kufanya vizuri, afya yangu ikawa imara basi miaka michache ijayo Ballon d’or itakuwa mikononi mwangu” alisema Ozil. .”Ninajisikia vizuri. Mimi ni mchezaji mkubwa duniani,ninacheza katika klabu kubwa. Pia hii ligi tunatumia nguvu nyingi kuliko kule La Liga kwa hiyo ninazidi kuimarika zaidi kuliko mwanzo ” aliongeza Ozil.

MAKALA: SIMBA HAIWEZI KUTWAA UBINGWA WA BARA MSIMU HUU

Picha
Ni dhahiri kuwa ikiwa na pointi 32 kibindoni, Simba itamaliza msimu wa tatu bila taji la Ligi Kuu Tanzania Bara. Kimahesabu, Simba ambayo tayari imecheza mechi 20 ikilinganishwa na 19 za Yanga yenye pointi 40 na 18 ya Azam yenye pointi 36 haiwezi kutwaa ubingwa, isipokuwa kama Yanga au Azam zitapoteza mechi nne kati ya zile walizobaki nazo. Endapo Azam yenye mechi nane ikipoteza mechi nne itamaliza ligi ikiwa na pointi 48, huku Yanga yenye mechi saba ikipoteza nne, itakuwa na pointi 49 na Simba ikishinda mechi zake zote sita ilizobakiwa nazo, itakuwa na pointi 50, hivyo itaibuka bingwa.

NI VITA KATI YA MZEE YUSUF NA ISHA MASHAUZI TRAVERTINE JUMAPILI

Picha
Keshokutwa jumapili ktk ukumbi wa Travertine uliopo Magomeni jijini Dsm patakuwa hapatoshi wakati bendi mahasimu za muziki wa taarabu zitakapochuana vikali kwa kiingilio cha shilingi 10, 000. Mashauzi Classic inayoongozwa na mkurya wa kwanza kuimba taarabu mwanadada Isha Ramadhan na kundi la Jahazi Modern Taarabu chini yake mfalme Mzee Yusuf. Tayari Isha Mashauzi ameshatangaza kumgaragaza bosi wake wa zamani Mzee Yusuf na amewataka wapenzi na mashabiki wake kujitokeza kwa wingi ndani ya Travertine.

PLUIJM ASEMA YANGA ITAKUWA MABINGWA WA BARA MSIMU HUU

Picha
Baada ya timu yake kuendelea kupata ushindi mfululizo katika mechi za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm, ametamba kuwa sasa njia ni nyeupe kwa kikosi chake kutwaa ubingwa wa ligi hiyo. Yanga juzi ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wa mchezo huo 'Maafande' wa JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani na kufikisha pointi 40, hivyo kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi. Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm, alisema ushindi wa kila mechi huifanya timu yake kujiweka katika mazingira mazuri ya kuunyakua ubingwa wa ligi na pia kufanya vyema kwenye mashindano ya kimataifa wanayoshiriki.

THE GUNNERS WATUPWA NJE ULAYA

Picha
Pamoja na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini katika mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia leo, washika bunduki wa jiji la London Arsenal wameshindwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa kosa la kuruhusu magoli mengi wakiwa nyumbani katika mchezo wa awali, ambapo Monaco iliwabamiza wenyeji wao hao Arsenal kwa jumla ya mabao 3-1. Arsenal ilijipatia goli la kwanza dakika ya 36 ya mchezo huo kupitia mchezaji wake Olivier Giroud kabla ya Aaron Ramsey kuongeza la pili katika dakika ya 79 ya mchezo huo. Matokeo ya jumla kwa timu hizo ni 3-3 japo Monaco inasonga mbele kwa faida ya kuwa na magoli mengi ya ugenini na kuwaacha vijana wa mzee Wenga wakikosa kufika robo fainali kwa mara ya tano mfululizo.

SIKIA HII:- KIBIBI YAHYA AMPOKONYA WIMBO WA "NO DISCUSSION" SALHA WA HAMMER Q!!.

Picha
Na Kais Mussa Kais Kibibi Yahya ni muimbaji wa kutegemewa wa bendi ya Maja's Modern Taarab iliyo na maskani yake manzese jijini Dar!, katika siku za nyuma kabla Salha wa Hammer hajatimka zake Five stars modern taarab alifanikiwa kurekodi wimbo uitwao "No discussion" ambao tayari upo katika vituo mbalimbali vya redio ukichezwa. Lakini mtandao huu makini wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Umegundua ama umebaini kwamba wimbo huo umerekodiwa tena upya na muimbaji Kibibi Yahya katika studio za soundcrafters temeke kwa producer bora kwa sasa katika taarab nchini Mr Enrico, na hii ni baada ya Salha wa Hammer Q! kuamua kuhama bendi na kuelekea zake Five stars modern taarab. Mtandao huu unazo nakala zote mbili za nyimbo hiyo ambayo moja imeimbwa nae Salha na ya pili imeimbwa nae Kibibi

CHANONGO RUKSA KWENDA YANGA

Picha
Uongozi wa klabu ya Simba ya jijini umetangaza rasmi kuachana na winga wake Haroun Chanongo ambaye alikuwa amepelekwa kwa mkopo Stand United ya Shinyanga, Chanongo anahusishwa na mipango ya kujiunga na Yanga SC ambao ni watani wa jadi wa wekundu hao wa msimbazi. Mwenyekiti wa kamati ya kamati ya usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hanspoppe amesema juzi kuwa Simba haina mpango wa kumrejesha tena katika kikosi chake kiungo huyo aliyeibuliwa kutoka kikosi cha pili sambamba na nyita wengine wanaong' ara katika kikosi hicho. Hanspoppe alisema klabu yake iko mbioni kuwarejesha nyota wake wote waliotolewa kwa mkopo isipokuwa Chanongo ambaye inadaiwa aliisaliti timu hiyo na pia amekuwa na mapenzi makubwa na Yanga, Chanongo hivi karibuni alitangazwa kwenda kufanya majaribio katika klabu ya TP Mazembe ya DRC.

MGAMBO SHOOTING YAAPA KUSIMAMISHA SIMBA, MKWAKWANI LEO

Picha
Kocha mkuu wa Mgambo Shooting Stars, Bakar Shime, ametangaza vita dhidi ya Simba kuelekea mechi yao ya leo jioni. Simba itakuwa na kibarua kigumu mbele ya 'maafande' hao kutoka kitongoji cha Kabuku wilayani Handeni, timu hizo zitakapochuana katika mechi ya kiporo ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa. Mechi hiyo Na. 62 ya raundi ya 9 ya VPL, ilipaswa kuchezwa Januari 4, lakini ikapigwa kalenda kutokana na kufinyangwa finyangwa kwa ratiba ya ligi hiyo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) sanjari na ushiriki wa Simba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar mwanzoni mwa mwaka.

NGASA AIPA MKONO WA KWAHERI YANGA

Picha
Winga hatari wa Yanga na Taifa Stars, Mrisho Ngasa, amewaaga na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumpa sapoti katika kipindi chote alichokaa kwenye klabu hiyo ya Jangwani. Ngasa, mfungaji bora wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwaka jana na mfungaji bora wa Yanga msimu uliopita, mwishoni mwa wiki alikisaidia kikosi cha wanajangwani kupata ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Platinum FC ya Zimbabwe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mechi hiyo ya hatua ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Ngasa alifunga mabao mawili na kupika mengine mawili, lakini muda mfupi baada ya mechi hiyo aliandika maneno kwenye ukurasa wake wa Instagram yanayoashiria kuondoka Yanga.

CHAMA CHA WAZIRI MKUU ISRAEL CHASHINDA TENA UCHAGUZI

Picha
Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israel wa chama cha Likud kilichoshinda uchaguzi mkuu wa tarehe 17 Machi 2015 Chama cha Likud cha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kimepata ushindi wa kushangaza katika uchaguzi mkuu wa Israel. Vimeripoti vyombo vya habari vya Israel. Matokeo ya awali yalionyesha chama cha mrengo wa kushoto cha Zionist Union kupata mshitiko.

YANGA YATAMBA KUTWAA POINTI 3 ZA SIMBA JUMAPILI

Picha
Katika kuhakikisha timu yao inafanya mazoezi kwenye hali tulivu na salama, Yanga wamejificha kwenye eneo lenye msitu mkubwa huku kukiwa na siafu wengi. Yanga wanajiwinda na mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili ijayo. Yanga yenyewe iliyoweka kambi yake kwenye hoteli moja Bagamoyo huko Pwani, inatoka umbali mrefu kuufuata uwanja ambao umezungukwa na pori kubwa huku kukiwa na milio ya ndege tu.