Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2023

AYOUB LAKRED KICHEKO UJIO WA BENCHIKHA SIMBA

Picha
Ayoub Lakred ni moja ya wachezaji wenye furaha zaidi katika kikosi cha @simbasctanzania baada ya ujio wa kocha mpya Abdelhak Benchika . Golikipa huyu mtoa michomo leo ameonekana akifanya mazoezi kwa juhudi kubwa huku akiwa na tabasamu muda wote .....Ni wazi ujio wa Benchika umemfurahisha sana Golikipa huyu . Mwamba ataendelea kulinda lango la Simba wakiwa ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy .....wakati Manula anaendelea kuuguza majeraha yake .

WASHINDANI WA YANGA WALIVYOWASILI DAR

Picha
Klabu ya Al AlhlyTayari imewasili Tanzania Kwa ajili ya Mchezo Wa Hatua ya Makundi Ya Klabu Bingwa Afrika Dhidi ya Yanga SC Mchezo Huo Utapigwa Jumamosi Hii Katika Dimba la Benjamin Mkapa

INJINIA HERSI AWA RAIS WA VILABU AFRIKA

Picha
Na Prince Hoza Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amechaguliwa kuwa RAIS wa kwanza wa Chama cha Vilabu vya Afrika (ACA) huku Makamu wake akiwa ni Jesca Moutang Kutoka Kaizechief Ya Africa Kusini . Makao Makuu Ya Chama Yatakuwa Nairobi Nchini Kenya . Mkutano wa kuanzishwa chombo hicho umefanyika Leo jijini Cairo nchini Misri na Hersi anakuwa Rais wa kwanza kwenye historia ya taasisi hiyo.

SIMBA YAACHANA NA BOCCO

Picha
Mshambuliaji wa klabu ya Simba, John Bocco anamaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi mwishoni mwa msimu huu na atakuwa Mchezaji huru (Free agent) ambapo hakuna mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya. Kapteni John Bocco inatajwa hayupo kabisa kwenye mipango ya klabu ya Simba baada ya mkataba wake kumalizika, na mpaka hivi sasa tayari klabu imempa taarifa kuwa itaachana nae hivi karibuni. Simba inamtazama John Bocco kuwa miongoni mwa washauri wa timu hiyo baada ya mkataba wake wa utumishi kwa Wekundu wa Msimbazi kumalizika, Simba inasubiri ripoti ya Bocco mwishoni mwa mwezi ujao kama atakubali wadhifa huo.

TABIA BATAMWANYA ATUA RADA ZA EXTRA BONGO

Picha
Na Said Mdoe Mwimbaji wa kike Tabia Jumbe Batamwanya amenasa kwenye rada za Extra Bongo. Tabia anayetamba na wimbo wake "Narudi Nyumbani" atatambulishwa kama msanii wa Extra Bongo Jumamosi hii pale Andrew's Lounge, Sinza jijini Dar es Salaam. Extra Bongo ipo kambini ikijifua na onyesho lao la uzinduzi wa bendi litakalofanyika Jumamosi hii ambapo kikosi chao chote kitawekwa hadharani. Saluti5 imehakikishiwa kuwa Tabia Batamwanya atakuwa sehemu ya wasaniii wa Extra Bongo watakotambulishwa Jumamosi. Hata hivyo, Batamwanya si sehemu ya wasanii waliopo kambini bali yeye atajiunga na kambi ya Extra Bongo baada ya onyesho la Jumamosi. Kusajiliwa kwa Tabia Batamwanya, kunafanya Extra Bongo iwe na waimbaji wawili wa kike.

KOCHA TWIGA STARS ATOBOA MAKUBWA YA CLARA LUVANGA

Picha
KOCHA Mkuu wa Twiga Stars, Bakar Shime amevunja ukimya juu ya ishu ya mshambuliaji wa kimataifa wa timu hiyo, Clara Luvanga kutoitwa kikosini akisema anaumizwa na kitendo cha watu kulalamika ilihali yeye ndiye aliyemtengeneza nyota huyo anayecheza soka la kulipwa Saudi Arabia. . “Hakuna aliyekuwa anamjua Clara, mimi ndio nilimuibua nilipomtoa nikaamini uwezo wake na kumfundisha hadi akawa vile na kuisaidia timu kukata tiketi ya Kombe la Dunia U17 zilizopota. Mimi ndiye najua ninachohitaji katika timu ili kupata matokeo, naumia nikisikia watu wanaongelea ishu hiyo, halafu watu hawajui, mie ndiye nilimpeleka Saudia,” alisema Shime bila kufafanua kilichomfanya asimuite kwa sasa. . Clara anayekipiga Al Nassr ya Saudia inayoshiriki Ligi Kuu, hadi sasa amefunga mabao sita kwenye mechi tano akiwa ni mmoja ya nyota tegemeo wa timu hiyo, lakini jina lake halipo kwenye kikosi cha Twiga kilichoitwa juzi kuingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Afrika (WAFCON) dhidi ya Togo

SIMBA YANOGEWA NA SARE MAUA

Picha
Saido Ntibanzonkiza aliwapa Uongozi Simba kipindi Cha kwanza Kwa mkwaju wa Penalty. Asec Mimosas wakaja juu kipindi Cha pili na kuwapiga mafuriko ya kutosha Simba, ndipo Karamoko Sankara akawatoa nduki mabeki wa Simba Kisha kupiga krosi ya chini Serge Poku anaweka Mpira kambani. Poku anafunga bao mbele ya walinzi wa Simba watatu hii ni aibu kubwa sana kwao . Sankara Karamoko bonge la kiungo mshambuliaji huyu akiwa na Mpira mguuni wwe msindikize tuu .

CV YA KOCHA MPYA SIMBA HII HAPA

Picha
Kocha mkuu wa Simba SC Tanzania ndiye mwenye profile iliyoshiba zaidi ndani ya Ligi Kuu ya NBC. Abdelhak Benchika amewaacha mbali sana wenzake Kwa mafanikio katika michuano iliyo chini ya CAF. Benchika ameshavaa Medal tatu za CAF Hadi sasa ....alitwaa Africa Super Cup baada ya kuwachapa Wydad Athletic Club fainali akiwa na RS Berkane. Msimu Uliopita alitwaa CAF Confederation Cup baada ya kuwakanda Yanga katika mchezo wa fainali. Na siku Chache zilizopita alitwaa Africa Super Cup baada ya kuwapa kisago Al Ahly Sporting Club katika mchezo wa fainali akiwa na USM Alger. Hakuna kocha yoyote anayeweza kaaa meza Moja na Abdelhak Benchika ndani ya Ligi Kuu ya NBC Kwa mafanikio. Gamondi Kombe lake kubwa ni kufika Nusu fainali CAF Champions League akiwa Wydad Casablanca

CHE MALONE AWAANGUKIA MASHABIKI SIMBA

Picha
Baada ya jioni ya leo Simba kulazimishwa sare na Asec Mimosas ya Ivory Coast katika uwanja wa Mkapa jijini Dar ea Salaam ya 1-1 mchezo wa makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika, beki wa kati Che Fondoh Malone amewaangukia mashabiki wa timu hoyo. “Tunacheza kwaajili ya Simba Sc, tunaiwakilisha Simba Sc, kwahiyo tunawaomba mashabiki watusapoti". Mashabiki waungane na sisi na sio kututelekeza wenyewe kwani Mashabiki wetu ni familia yetu hivyo wakituacha watakuwa sio miongoni mwetu” Amesema Che Malone. 

YANGA NA WHIZPAY YAINGIA MKATABA MNONO

Picha
Klabu ya Yanga imeingia Mkataba na Kampuni ya Whizpay Technology LLC yenye Makao Makuu yake huko Abu Dhabi,Dubai kwaajili ya kutangaza kwenye mechi zao za Klabu Bingwa kampuni yao tanzu ya Whizmo ambayo inashughulika na huduma za kifedha kutoka UAE na duniani kote.

ASEC KAMILI KUIVAA SIMBA KESHO

Picha
Kikosi cha Asec Mimosas kimefanya mazoezi ya kwanza katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar Es Salaam kuelekea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Simba Sc Jumamosi hii Novemba 25 katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

HUYU HAPA HAJI SULEIMAN MNOGA, BABA MZANZIBAR MAMA MUINGEREZA

Picha
Anaitwa Haji Suleiman Mnoga wengi wanajiuliza huyu mwamba ana asili ya wapi huyu mwamba baba ni Mzanzibar na upande wa mama ni Uingereza yaani ni chotara la Zaneng Kiasili huyu mwamba uwanjani ni CB yaani Centre Back pia anaweza kucheza kama RB yaani right back na DM yaani Defence Mildefid, uwanjani kama hayumo hivi haimbwi sana lkn anapiga kazi kama punda wa muembe makumbi. Anatoka klabu ya Aldershot Town FC inayoshiriki ligi daraja la 5 pale England ni mchezaji mmoja mzuri sana mwenye umri mdogo na ni Hazina na kubwa Sana kwa Taifa la Tanzania

KOCHA USM ALGER AWA KOCHA MKUU SIMBA

Picha
Kocha mpya wa Simba, Abdelhak Benchika aliiongoza USM Alger kuchuka Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Yanga, pia aliiongoza USM Alger kuchukua CAF Super Cup baada ya kuifunga Al Ahly. Pia amezifundisha Raja Casablanca, RS Berkane, CR Belouizdad, Club Africain.

ASHA MASAKA ASHANGAZA HUKO ULAYA

Picha
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Princess ya Tanzania na pia mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Twiga Stars Aisha Masaka amekuwa mchezaji wa kwanza mwanamke kucheza timu mbili za UEFA CL, dhidi ya Paris FC na Madrid.

SIMBA YAFUNGIWA KUSAJILI

Picha
Klabu ya Simba imefungiwa kusajili mpaka itakapolipa madai ya klabu ya Teungueth ya Senegal kuhusu mauzo ya mchezaji Pape Sakho. Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mara baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya nyota huyo.

MAKUBWA! SIMBA YAWAGEUKIA MAX, AZIZ KI

Picha
Na Salum Fikiri Jr Klabu ya SIMBA imeonesha nia ya kuwataka viungo hatari zaidi kwenye ligi ya Tanzania Max Nzengeli na Aziz Ki Simba wanaangalia uwezekano wa kumpata Aziz Ki ambaye anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu Lwa upande wa MAX Simba walizani yupo kwa mkopo hivyo walijaribu kuongea na klabu yake ya zamani lakini walijibiwa kua ashauzwa kwa YANGA hivyo kama wanamtaka wanatakiwa wakaongee na YANGA... Ngoma ndo imekua ngumu hapo

BALEKE KUSALIA MSIMBAZI

Picha
Na Salum Fikiri Jr Klabu ya Simba ipo kwenye hatua za mwisho za kumuongeza kandarasi Jean Baleke ambaye mkataba wake wa mkopo kutoka TP Mazembe unaelekea ukingoni. Makubaliano kati ya Simba na TP Mazembe ni kuwa Simba itamuongezea kandarasi ya kudumu Jean Baleke ana sio kusaini mkataba tena wa mkopo kutoka TP Mazembe Klabu ya Simba tayari imeshaandaa kiasi cha Milioni 420 Tsh! Kama ada ya uhamisho wa Jean Baleke kutoka klabu ya TP Mazembe ya nchini DR Congo.

KIPA WA TAIFA STARS AULA SWEDEN

Picha
Golikipa mwenye asili ya Tanzania,Kwesi Kawawa amejiunga na klabu ya Orebro Syrianska IF inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Sweden akitokea Hammarby Talang. Kipa huyo alisimama langoni wakati Taifa Stars ilipolala kwa mabao 2-0 dhidi ya Morocco katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam mchezo wa kufuzu kombe la dunia

YANGA IMEKAMILISHA USAJILI- ALI KAMWE

Picha
Msemaji wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara YOUNG AFRICANS Ally Kamwe amesema timu hiyo tayari imekamilisha kwa kiwango kikubwa usajili wa wachezaji wanaowahitaji katika mlango wa dirisha dogo. Ally Kamwe amewafahamisha mashabiki wa soka na wanazi wa klabu hiyo kuwa klichobaki ni kusubiri wakati ufike ili kuwatangaza wachazaji hao wapya ambao hakuja idadi yao, timu wanazotoka wala nchi.

YANGA YAACHANA NA CHIVAVIRO

Picha
Wananchi Wameachana na mbio za kumuwania Mshambuliaji wa klab ya Kaizer Chiefs raia wa Afrika Kusini Ranga Chivaviro (30) ambaye alitakiwa kuja kwa Mkopo na hii baada ya kufanikiwa kuipata saini ya Uhamisho wa kudumu wa Mshambuliaji mwingine Kinda, Pia imefahamika Mwalimu Gamondi amekuwa akihusudu sana soka la vijana na ndio maana akapitisha jina la Mshambuliaji huyo anayetumia mguu wa kulia.

HUYU NDIO MSANII MPYA WCB

Picha
Staa wa Singeli, D Voice Ginnii anakuwa msanii wa nane kutambulishwa na WCB Wasafi, Record Label yake Diamond Platnumz. Utakumbuka awali WCB iliwatambulisha Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Rich Mavoko, Lava Lava, Mbosso na Zuchu.

DOGO ANAYECHEZA AUSTRALIA AIZAMISHA NIGER KOMBE LA DUNIA

Picha
Na Mwandishi Wetu Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars usiku wa leo imeanza vema kampeni yake ya kufuzu fainali za kombe la dunia baada ya kuilaza Niger bao 1-0 katika mchezo mkali uliofanyika mjini Marrakesh nchini Mprocco. Bao pekee lililoifanya Taifa Stars ichomoze na ushindi limefungwa na mchezaji wake Charles M' mombwa anayecheza soka la kulipwa Australia. Stars itarejea mapema kesho kujiandaa na kukutana na Morocco mechi ambayo itafanyika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Novemba 21 mwaka huu

YANGA YAPIGWA FAINI YA MIL 5

Picha
Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Shilingi 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi katika mchezo wa Derby ya Kariakoo uliowakutanisha Simba na Yanga kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 5, 2023. Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kutoka nje ya chumba cha kuvalia, jambo lililosababisha mchezo huo kuchelewa kuanza kwa dakika nne (4).

ZAMALEK YAWAPELELEZA PACOME, NZENGELI

Picha
Klabu ya Zamalek itatuma maafisa wake nchini Algeria katika mchezo wa CR Belouizdad dhidi Yanga kwaajili ya kuwafuatilia kwa karibu Pacone Zouzoua na Maxi Nzengeli. Taarifa kutoka gazeti la Championi zinaeleza kuwa Maafisa hao inaarifiwa kuwa watatua pia Tanzania kuendelea kuwafuatilia wachezaji hao watakapokuwa wanacheza michezo ya kimataifa pekee katika michezo ya nyumbani ya Yanga..

KIBU, INONGA, DIARRA WAPIGWA FAINI YA LAKI 5

Picha
Kamati ya Undeshaji na Usimamizi wa Ligi imewatoza faini ya Tsh. Laki tano (500,000) Wachezaji wa Simba SC, Kibu Denis na Henock Inonga , pamoja na golikipa wa klabu ya Yanga Djigui Diarra kwa makosa tofauti waliyoyafanya wakati wakishangilia magoli yaliyofungwa kwenye mchezo wa NBC kati ya Simba dhidi ya Yanga SC. Kibu Denis ametozwa faini hiyo kwa kosa la kushangilia bao lake mbele ya jukwaa la mashabiki wa Yanga huku akionyesha ishara ya kuwafunga midomo wakati Inonga yeye ametozwa faini hiyo kwa kosa la kushangilia bao mbele ya Maafisa wa Benchi la Ufundi la Yanga SC. Pia kwa upande wa golikipa wa Yanga Djigui Diarra ametozwa faini hiyo kwa kosa la kwenda kushangilia mbele ya benchi la ufundi la klabu ya Simba mara baada ya timu yake kufunga moja ya mabao katika mchezo huo wa Kariakoo Derby.

TAIFA STARS YATEMBELEA UWANJA WA MARRAKESH

Picha
Timu ya Taifa “Taifa Stars” imetembelea uwanja wa Marrakech utakaotumika kwa mchezo wa kesho kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger.

STARS YAWASILI MOROCCO

Picha
Timu ya Taifa ya Tanzania,  “Taifa Stars” imewasili Morocco kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger utakaochezwa kwenye mji wa Marrakech Jumamosi Novemba 18, 2023. Stars iliondoka alfajiri ya leo na imewasili salama