SABABU ZA KUACHWA NDEMLA SAFARI YA UTURUKI HIZI HAPA, NDUDA NA WENGINE PIA ZIMO

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara Simba SC imesafiri alfajiri ya leo hii kuelekea nchini Uturuki ambapo itakaa huko kwa majuma mawili kabla ya kurejea kwa ajili ya tamasha lao la Simba Day litakalofanyika Agosti 8.

Simba imeondoka na wachezaji wake wote iliowasajili hivi karibuni pamoja na kocha wake mkuu Mbelgiji Patrick Aussems, kikosi kilichoenda kina jumla ya nyota 26 lakini wengine imeripotiwa kuachwa katika safari hiyo.

Mmoja kati ya walioachwa ni kiungo mshambuliaji Said Ndemla ambaye inasemekana amegoma kuongeza mkataba mpya na ndio maana ametoswa katika safari hiyo, pia beki Erasto Nyoni ametemwa katika safari kwakuwa ana matatizo ya kifamilia.

Nyoni ataungana na kikosi hicho keshokutwa, Said Mohamed Nduda,Emmanuel Mseja, Ally Shomari, Jamal Mwambeleko wameachwa kwa vile wanapelekwa kwa mkopo kwenye klabu nyingine wakati Moses Kitandu anatarajia kujiunga na Lipuli ya Iringa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA