Danny Lyanga amwaga wino Azam FC kumrithi Chilunda
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam FC imeingia kandarasi ya mwaka mmoja na mshambuliaji Danny Lyanga wa Singida United akienda kuziba nafasi ya Shaaban Iddi Chilunda aliyeuzwa Hispania.
Taarifa zilizotolewa na uongozi wa Azam FC zinasema kuwa mshambuliaji huyo aliyewahi pia kuzichezea Coastal Union ya Tanga, Simba SC na Fanja FC anajiunga na Azam FC baada ya kucheza kwa kipindi kifupi sana Singida United.
Lyanga in mmoja kati ya washambuliaji bora kabisa hapa nchini ambao wana uwezo mkubwa wa kufunga na kuasist, kutua kwake Azam FC kunaweza kurudisha matumaini ya timu kufanya vema kwani tayari imeshaondokewa na nyota wake wawili ambao no tegemeo